Tigo, Vodacom ni matapeli wa hali ya juu, hii ni baada ya kununua smart kitochi

yahoo

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
3,527
1,405
Baada ya kuskia matangazo ya smart kitochi, nikaenda zangu mliman city kushuhudia kitochi kikoje.nikaingia tigo kuzicheki zao then nikaingia voda, lakini nikagundua za Tigo ni bora zaidi ya voda, ingawa voda zinauzwa kwa bei ya chini na ofa zao ni nyingi ,yani wanakupa gb kibao dakika sms fb ya bure kwa miezi sita, yani kila mwezi ofa zinajirudia, lakini simu zao ni 3g tofauti na matangazo yao(Utapeli huo) ,tig wao simu zao 4g na ofa yao ni fb ya bure tu kwa miezi 6 yani kila mwezi unapewa mb za bure kwaajili ya fb.

Baada ya mwezi mmoja nikaenda mliman city nikiwa na cash nikapita maduka yote mawili, hatimaye nikavutiwa na kitochi ya tigo ambayo bei yake ni ya juu zaidi na ofa zao ni chache, hii ni kutokana na ubora wake niliouna.

Baada ya kuichukua nikagundua intanet yake upande wa tigo inakula mb nyingi kuliko kawaida haswa unapoangalia video you tube yani kavideo ka dk 2 tu unaweza kukuta kamekula mb hadi 50 na kadhaa, kuna mdau mmoja aliyenunua kitochi cha voda aliwah kulalamikia hilo kwa upande wa Voda.

FB ya bure niliitumia mwezi mmoja baada ya hapo sikuipata tena nilifatilia kwa kupiga cm tigo wakanambia niende nilikonunulia nikaenda mliman city nikazungushwa nikaambiwa nitaunganishwa niende tu nikapewa namba ya customer care , kila nikipiga ni badae badae hadi nikaamua kuacha, the same to na yule jamaa aliyekuja kulalamika kuhusu kitochi chake cha voda ambaye alisema alizungushwa vifurushi vyake kama mimi.

Nilichojifunza ni kwamba hawa jamaa wanaweza kuwa ni matapeli kama matapeli wa Manzese,
Lakini TCRA wamelala

Nashauri TCRA wazichunguze hizi simu upande wa ulaji wa mb, nawahakikisia mtakusanya fine kubwa kutoka kwa haya makampuni mawili.
 
Pole Mkuu...

Mi kwa kweli Vile visimu SIJAVIPENDA kimwonekano, user interface, Charge, Batan, n.k nilinunua cha Tigo pale k.koo Msimbazi, Nilikaa nacho siku tatu nikauza, Nikanunua ki samsung..

Hizo offa wala sikuziwaza, lengo langu ni experience hizo sifa zake, lakini nikaishia kua disapointed.

Simu za batani, hatokuja kutokea kama Nokia, Sizungumzii nokia hawa wababaishaiji.
 
Haya matangazo nimebaki kuyasikiliza na kupita kushoto vinginevyo ukisikia kila kitu ukataka kufanya ndiyo hilo lililokukuta.
 
Visimu vya ajabu vile kwanza hata muonekano wake wa kishamba sana bora kama unataka simu ya batani ukachukue zako nokia
 
Nimenunua hicho kisimu cha Tigo lakini line yangu ya tigo haisomi, tatizo litakuwa nini?
minilikanunua bhana ila dah kazuri jamani wala ckuwaza ofa zao tena nikawa nakatumia kukaunganisha na pc bac wecha2 wenye vitecno walinikoma maana full 4g ila nikiwa ktk pilika zangu nikaangusha bhana gari ikakikanyaga kioo kikavunjika mpakale bdo natafuta kma mtu chakwake kimezima ghafla kwangu pxa kapata
 
Back
Top Bottom