tiGO, VODA, ZAIN na ZANTEL KWA NINI IKO HIVI? SERIKALI INAHUSIKA HAPA

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,592
29,721
Kampuni za simu nilizotaja hapo juu zinagawana wingi wa wateja ktk soko la mitandao ya simu nchini.
Ili kuwamotisha wateja kampuni hizi zimekuwa zinaandaa na kuendesha bahati na sibu mbali mbali huku zikitoa zawadfi kubwa kubwa za kuvutia.

Nimekuwa nafuatilia tangu mwanzo wa gamming zao ambapo kila mshindi anayetajwa au kufikiwa live anaonesha dalili ya kuandaliwa ama kuarifiwa kabla kuhusu ushindi wake. Pia washindi hawa ni kama wameandaliwa maana most of washindi kama hawajatokea dar es salaam basi ni mikoa ya kati (wachache) na kaskazini. mikoa ya kusini ni kama hawatumii mitandao hii ambayo mashindano yake hujiendesha automatic kwa mteja kujiunga. Sijasikia mshindi wa nyumba, gari, hela kuubwa katoka mtwara, lindi, ruvuma, au kusini kusini. washindi wengi ni dar to kaskazini. Pia hivi karibuni hizi kampuni zimepunguza bei za mawasiliano lakini ndo zimezidisha lottery kwa mfumo wa kuuliza maswali na kujibu ili kujiongezea points. Maswali yao yanakujia pale tu simu yako ikiwa na vocha tu na si vinginevyo.

Nimejaribu kuuliza watu wengi kama wanawafahamu ndugu, jamaa au rafiki zao waliowahi kushinda hizi promosheni majibu yanakatisha tamaa kuwa hawafahamu. Ila pia hizi kampuni zimejiingiza ktk mtego wa matangazo ya promosheni zao. Wanaposema VIGEZO NA MASHARTI KUZINGATIWA mbona hawasemi ni vigezo gani au masharti gani yanayozingatiwa? kama wanaweza kutuma wito wa kujiunga na maswali lukuki kwa subscriber wanashindwa nini washindwe kutuma hivyo VIGEZO NA MASHARTI? kuna jamaa yangu alishawahi kufuatwa na meneja masoko wa kampuni moja ya simu akimtaka waingie mkataba wa kupitisha zawadi mikononi mwake kwa masharti ya kifisadi nashukuru jamaa alikataa baada ya kustukia hali halisi.

Kwa kuwa michezo hii husimamiwa na GAMMING BOARD (wakati wa uchezeshaji tu) inaleta picha kwamba serikali kupitia board hii inashiriki kuwahadaa na kuwaibia wateja wa mitandao hii. Kama Gamming Board inasmamia promosheni hizi kwa nini ishiriki mwishoni tu? nina dukuduku kadhaa

  • vigezi vipi na masharti vinahusika ktk promosheni hizi?
  • namba za washiriki zinapoingizwa kwenye kompyuta ya promosheni nani anathibitisha?
  • kwa nini washindi hawaoneshi kufurahia ama kuwa surprised na ushindi wao?
  • kwa nini promosheni hizi zisikabidhiwe wakala kuziendesha? maana fairness haipo endapo kampuni zitajiendeshea bahatinasibu zao ambazo hushawishi ufisadi.
Kama kuna mdau anafahamu lolote ktk hili atujuze hapa maana maswali ni mengi kuliko majibu.
 
hahahaha WOS angalia hapa chini
The Following 2 Users Say Thank You to WomanOfSubstance For This Useful Post:

Invisible (Today), Msanii (Today)​
 
Nimewakilisha maoni ya wadau wa mtandao ambao wameshanilalamikia kinachoendelea huko kwenye hiyo mishirika ya simu
 
Vyovyote ilivyo kuhusu hizo bahati nasibu, jambo jema zaidi kiushindani kwa kampuni za simu lingekuwa kuendelea kushusha bei. Bei za chini zaidi na zaidi zingetunufaisha wenye simu wote badala ya kutoa magari, nyumba, nk kwa watu kiduchu.
 
Nilishakata shauri kitambo ikijaga iyo mimesji yao ya kuninvite huwa naidelete bse imani yangu kwa hao washindi ni zero
 
Ninashawishika kuwashauri watu wasiingie ktk mitego mufilisi ya hizi kampuni za simu
 
Kweli kabisa haya makampuni ya simu hasa Vodacom kweli wanakula sana hela zetu na promosheni yao ya Shinda Mkoko. Kila siku nafuatilia kwenye TV, yaaaani we acha tu. Ninaposhangaa zaidi ni wale washindi wanapopigiwa simu kuwa wameshinda yaani utakuta wapo wapo hawajui kinachoendelea. Hawaoneshi furaha yoyote kitu ambacho kinatupa wasiwasi kuhusu hawa washindi, huenda kuna kamchezo fulani kanachezwa.

Halafu sijui kwenye bahati nasibu yao wana-select mkoa fulani ili mshindi atoke huko! Mimi mwenyewe toka nimeanza kucheza mchezo huu nina pointi zaidi ya 100,000 naona nimewachangia vya kutosha ngoja nitulize boli.

Washindi wa shinda mkoko hawa hapa
Week One
Week Two
Week Three
 
Ni usanii mkubwa unaofanyika.

Ninawasiwasi namba huwa zinakuwa fed kabla, ili kuepusha mtafaruku.
Tokea promotion hizi zianze plus bahati nasibu ya bingo, haijawahi kutokea coincedence waziri/mbunge/balozi wa nchi flani/maasko wakuu kabisa/wafanyakazi wa makampuni husika wakatajwa/wakapigiwa simu kuwa wameshinda, kama kweli hii kitu inachezeshwa na komputer.

Mbona kwenye makampuni ya simu hawaseme wafanyakazi(mameneja) hawaruhusiwi kushiriki, na hakuna hata mmoja aliyewahi kushinda???

Hao wote kweli hawana bahati??

Au vigezo na masharti ni pamoja na wanadiplomasia computer ita-select??
 
Ni uwizi mtupu. Kama Tigo hilo shindano lao la JIKOKi washindi hawatangazwi. Wengi wamepata laptop, blackberry,Sh mil 2 lakini sijawaona kwenye magazeti. Hawataji pia point zao walizofikisha. Mshindi wa shilingi milion 100 alionekana ameshinda zawadi zote. Je alikuwa na point ngapi? hawakusema!!
 
Ni usanii mkubwa unaofanyika.

Ninawasiwasi namba huwa zinakuwa fed kabla, ili kuepusha mtafaruku.
Tokea promotion hizi zianze plus bahati nasibu ya bingo, haijawahi kutokea coincedence waziri/mbunge/balozi wa nchi flani/maasko wakuu kabisa/wafanyakazi wa makampuni husika wakatajwa/wakapigiwa simu kuwa wameshinda, kama kweli hii kitu inachezeshwa na komputer.

Mbona kwenye makampuni ya simu hawaseme wafanyakazi(mameneja) hawaruhusiwi kushiriki, na hakuna hata mmoja aliyewahi kushinda???

Hao wote kweli hawana bahati??

Au vigezo na masharti ni pamoja na wanadiplomasia computer ita-select??

Imagine bwana Kikwete kashinda Hyundai i10,duh!Balaaa...
zengwe tu hilo tunawekewa hakuna cha bahati nasibu wala nini!
 
Wizi wa mchana kweupeeee.
Cha msingi ni kutuliza boli na kuacha kucheza hizo bingo zao
 
Ni usanii mkubwa unaofanyika.

Mbona kwenye makampuni ya simu hawaseme wafanyakazi(mameneja) hawaruhusiwi kushiriki, na hakuna hata mmoja aliyewahi kushinda???

Hao wote kweli hawana bahati??

Ninavyojua mimi kwenye promotion mbalimbali (si za makampuni ya simu tu) wafanyakazi wao hawaruhusiwi kushiriki na wengine huenda mbali zaidi na kusema wafanyakazi na ndugu zao hawaruhusiwi kushiriki.
 
I hate hizo promotion uchwara!Wizi mtupu,wanawakamua watu hela zao tu!

Tatizo la wabongo wengi ni kupenda vitu vya mteremko na ndo maana kila siku mnalizwa tu. Badala ya kuchakarika usake hela ununue gari lako mwenyewe, unataka ucheze bahati nasibu upate gari kwa shs.500. Sasa jiulize huyo anayechezesha bahati nasibu hilo gari kaliokota? Kwa mtaji huu lazima muendelee kulizwa tu. Na kama unaona hapa kuna wizi ACHA KUSHIRIKI. Period.
 
Ninavyojua mimi kwenye promotion mbalimbali (si za makampuni ya simu tu) wafanyakazi wao hawaruhusiwi kushiriki na wengine huenda mbali zaidi na kusema wafanyakazi na ndugu zao hawaruhusiwi kushiriki.


Mi ninachotaka hao wafanyakazi washinde, afu ushindi wao utenguliwe,,kudhihirisha kuwa kumputa inafanya uchakatuaji wa ukweli.

Hata ivyo lini ulisikia tangazo la kuwakataza wasishiriki?
 
Wizi wa mchana kweupeeee.
Cha msingi ni kutuliza boli na kuacha kucheza hizo bingo zao

nimefanya jitihada kubwa kushawishi baadhi ya watu wasishiriki kabisa hiyo mibahati nasibu,naamin nimefanikiwa kwa kias kikubwa..madogo hawaombi vocha ovyo ovyo siku hizi..JF Members jitahidini muache kucheza hiyo mibahati nasibu(uamuzi ni wako mwenyewe,ukiamua cheza)..Siku zote kumbuka rahisi ni ghali!Unachangia mpaka laki na zaidi lakini zawadi zinaenda kwa wengine(nahisi nyingine zinarudi kwa wenyewe,kama hela lazima kuna percent kubwa inarudi kwao)!
 
Back
Top Bottom