TiGO Usipime kwa lazima kutoka kwa Timu ya mauzo ya TiGO!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TiGO Usipime kwa lazima kutoka kwa Timu ya mauzo ya TiGO!!!

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Tusker Bariiiidi, Nov 11, 2009.

 1. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #1
  Nov 11, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  KAMPUNI ya simu za mkononi ya Tigo, ilizindua promesheni nzuri ya kutuma ujumbe mfupi kwenda mitandao yote nchini kwa gharama ya sh 400 inayojulikana kwa jina la ‘Usipime.’

  Mteja wa TiGO anatakiwa kujiunga ktk huduma ya Usipime kwa kutuma neno Usipime kwenda 15313 na baada ya muda mfupi atapokea ujumbe utakaomujulisha kukubaliwa kwa ombi lake.

  “Ukishajiunga mara moja na huduma hii utakuwa unaunganishwa moja kwa moja kila siku masaa 24 siku 365 za mwaka mzima, cha kuzingatia ni kuhakikisha unakuwa na huduma ya muda wa maongezi usiopungua sh 400,”

  Hivi karibuni kumezuka mtindo wa baadhi... kama sio wote wa timu ya mauzo kuwaunganisha kwa nguvu katika huduma hiyo ya usipime.... kumbuka kila uchao unakatwa Sh.mia nne kwa ajili ya SMS unlimited na vijana hao wamewaingiza mjini wateja ambao hawajui hili wala lile na hivyo kupelekea wateja wengi kujikuta wanakatwa hela bila ridhaa yao kisa wanalipwa comission ya asilimia kadhaa za MATUMIZI ya mteja kwa miezi mitatu ya mwanzo HUUU NI WIZI WA MCHANA!!!! ... Je TCRA mpo?.... TCRA mnafanya nini? Je wateja wote wa huduma hii ya TiGO Usipime wanajua kuwa ndio wamefunga pingu za maisha kukatwa mia nne kila siku??? Wanajua jinsi ya kujitoa katika huduma hii?????
  NAOMBA KUWASILISHA!!!
   
Loading...