Tigo-pesa, kunradhi toka kwangu kwenda kwa ndugu, jamaa, marafiki na wateja. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tigo-pesa, kunradhi toka kwangu kwenda kwa ndugu, jamaa, marafiki na wateja.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kitomai, Jun 29, 2012.

 1. Kitomai

  Kitomai JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2012
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,037
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Napenda kutumia nafasi hii kuwapatia pole ya usumbufu wale wote ambao waliotumiwa meseji za kuombwa kutumiwa pesa kwa njia ya tigo pesa wakati ambapo nambari yangu ya tigo ilipokuwa swaped na kupewa mtu mwingine bila ridhaa yangu. Nimeona itakuwa vema kulitoa hili jambo hadharani kwa sababu bado kuna wengine wanaweza kudhania kuwa mimi mwenyewe ndiyo niliyekuwa nikisambaza jumbe za kuomba kutumiwa pesa kwa njia ya tigo pesa.
  Kifupi tarehe 27/6/2012 line yangu ya tigo muda wa mchana ilisimama ghafla kufanya kazi.

  Wakati nikitafakari nini kimetokea muda wa karibu na jioni mtu wangu wa karibu akanipigia simu kwa kupitia nambari yangu ya voda akaniuliza kuna tatizo gani limetokea mbona nimemuomba anitumie pesa haraka nikamjibu sijakuomba anitumie pesa. Akasema nimemtumia ujumbe kupitia nambari yangu ya tigo’ nikamjibu nambari yangu ya tigo imekufa haifanyi kazi. Akanijibu, hapana inafanya kazi na ukiipiga inaita muda mrefu bila kupokelewa, baadaye unakuja ujumbe siwezi kuongea kwa sababu simu yangu ina tatizo la spika. Na nilipoipiga ili kuhakiki nilichoambiwa ikawa inaita bila kupokelewa baadaye ukaja ujumbe huu ‘’simu yangu imeharibika spika hatuwezi kusikilizana’’.

  Baada ya hapo, nikapiga simu customer care kuwajulisha nini kinaendelea wakaniambia niende kutoa taarifa katika kituo chochote cha huduma kwa wateja juu ya hicho ninachokidai. Mara nikapokea ujumbe kutoka kwa jamaa mwingine anasema kwani vipi kuna tatizo gani mbona unasema nikutumie pesa alafu upokei simu maana nilikipiga simu ili nijue kulikoni. Nikapiga tena simu, tigo customer care majibu yakawa yale yale niende katika kituo cha huduma kwa wateja kutoa taarifa. Kutoka na mazingira yalivyokuwa nilifanikiwa kufika katika kituo cha huduma kwa wateja kilichopo Manzese pempezoni mwa barabara ya Morogoro jana asubuhi. Nikawaeleza wakanijibu hayo mambo yapo yapo!. Wakanipatia namba nyingine. Nikawauliza maswali mawili: Kwanza inawezekana vipi kampuni yenu inampatia mteja mwingine nambari yangu ili hali inatumika na mimi? Pili, katika account yangu ya tigo pesa nikakuta kuna salio la sh 100. Ina maana huyu jamaa aliyefanya hivyo ameweza vipi kuzichukua hizo fedha ili hali hakuna mtu hata mmoja anayeijua password yangu? Hayo maswali hayakupatiwa majibu.

  Baada ya kupatiwa line mpya nikaanza kuwapigia wadau, nikagundua kuwa aliyekuwa amehujumu hiyo line ametuma ujumbe kwa watu tofauti tofauti akiwataka wamtumie ‘’salio’’ muda wa maongezi na ‘’salio’’ tigo pesa. Wengine kawaomba sh 4000, wengine 80,000, wengine 2,000,000, Kama vile anajua uwezo wao. Nikajiuliza namba zao kazipata wapi? Zaidi, kila aliyeombwa akikuwa katika uwezo wa kutoa kiwango hicho alichoombwa. Baaada ya kugundua kuwa wapo wengi wameombwa hivyo nikaona itakuwa vema nitumie jukwaa hili kuwafikiwa wale wote ambao watakuwa wamekutana na usumbufu huu, poleni sana sana kwa usumbufu sikuwa mimi bali huyo asiyejulikana , nimwite tapeli, sijui mwizi!

  Zaidi, kwa uongozi wa kampuni ya tigo lifanyieni kazi hili jambo kwa kuwa lina kera, linachafua hadhi, heshima na tahadhima ya wateja wenu na hadhi ya kampuni yenu na kuletea usumbufu na hasara.
   
 2. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  tigo pesa si salama kwa kuweka kiasi zaidi ya 50K kwani line za tigo ni rahisi kuzi swap tak care man!
   
 3. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #3
  Jun 29, 2012
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  Kwa mambo kama haya acha mtandao huu ufananishwe na vitu vya ajabu ajabu....
   
 4. Baba Mtu

  Baba Mtu JF-Expert Member

  #4
  Jun 29, 2012
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 881
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Pole sana kwa yalokusibu
   
 5. next

  next JF-Expert Member

  #5
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 601
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  pole sana,
  wamezidiwa akili na vijana wao. nadhan tunatakiwa kujilinda wenyewe kwa kutotumia line za simu kuhifadhi pesa.
   
 6. iron2012

  iron2012 JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 358
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  pole sana mkuu, suruhisho pekee ni kuwahama maana huduma yao mbovu hawajari wateja bora watu wote tukatae huduma yao tuone kama wataweza kusurvive
   
 7. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #7
  Jun 29, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,807
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  duh pole sana....
   
 8. aye

  aye JF-Expert Member

  #8
  Jun 29, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,989
  Likes Received: 250
  Trophy Points: 160
  jamaa wananusa balaa hao wakishirikiana na wafanyakazi ambao sio waaminifu kwa kutoa siri za wateja weka pesa unapotaka kutuma tu usifanye kama bank kuifadhi salio si salama kabisa
   
Loading...