Tigo nawahama kwa muda hadi mtapopunguza gharama zenu

Kapepo

JF-Expert Member
Aug 14, 2015
1,052
1,155
Too much sasa kila siku tunapandishiwa vifurushi asee nina laini ya Airtel wacha tu nitumie hiyo, siwezi kutoa elfu nane nipate Gb 4 na dakika kizembe hivi. Jirekebisheni sisi si wote tuna hela za mchezo mchezo embu jiangalieni.
 
Mnaotumia tigo nawapa pole.

Mtandao umegawanya vifurushi vyake mithili ya nywele za kipilipili.

Yaani ukitaka dakika za kueleweka uandae pesa yake.

Sms pesa yake.

MB za kutosha uandae pesa yake.

Yani limtandao la ovyo sijapata ona.
 
Mimi kwenye saizi yako wamenipunguzia mb toka gb1 hadi mb 500 na siungi tena kifurushi chochote kwenye tigo, nahamia voda kwenye GB 2.5 kwa buku mbili.
 
too much sasa kila siku tunapandishiwa vifurushi asee nina laini ya airtel wacha tu nitumie iyo siwezi kutoa elfu nane nipate gb 4 na dakika kizembe ivi jirekebisheni sisi si wote tuna hela za mchezo mchezo embu jiangalieni

Wewe vumilia tu huko huko, mitandao yote ni shida...kama mimi nipo airtel pamoja na kujisifia na 4g mtandao ni wa shida balaa...inatia uvivu mpaka kuperuzi!
 
Siwezi kutoa 15k kwa ajili ya vifurushi tu wanazingua sana hawa sikuizi
 
Mimi kwenye saizi yako wamenipunguzia mb toka gb1 hadi mb 500, na siungi tena kifurushi chochote kwenye tigo, naamia voda kwenye GB 2.5 kwa buku mbili.
Unapataje hiyo kwenye menu ipi maana mi voda napata gb 3 kwa 3000 hiyo na muda wa maongezi no. Msg
 
Unahamia wapi huko ambako unafikiri kuna unafuu?

Kama unafuu upo haitazidi week nao watapandisha bei zao.
 
Mimi kwenye saizi yako wamenipunguzia mb toka gb1 hadi mb 500, na siungi tena kifurushi chochote kwenye tigo, naamia voda kwenye GB 2.5 kwa buku mbili.
Huko washabadili utakuta🤣🤣🤣
 
sema wabongo wavumilivu sana
Hili ndio kosa nyerere alifanya, sijui alitambikia wapi aisee. Tuna uvumilivu wa kipumbavu sana 😂😂😂 mbaka sometime tunajionea imani. Tuna ile kumuachia mungu tu!!!
 
Too much sasa kila siku tunapandishiwa vifurushi asee nina laini ya Airtel wacha tu nitumie iyo siwezi kutoa elfu nane nipate Gb 4 na dakika kizembe hivi jirekebisheni sisi si wote tuna hela za mchezo mchezo embu jiangalieni
Huko Airtel nako internet speed yake utakereka mpaka utarudi Tigo mwenyewe..,.
 
Too much sasa kila siku tunapandishiwa vifurushi asee nina laini ya Airtel wacha tu nitumie iyo siwezi kutoa elfu nane nipate Gb 4 na dakika kizembe hivi jirekebisheni sisi si wote tuna hela za mchezo mchezo embu jiangalieni
Nenda Halotel mkuu Kuna unafuu kidogo, 1Gb kwa 1000 siku 7.

Pia kuna bando la usiku la bila kikomo kwa 1500 kuanzia saa sita kamili usiku mpaka saa kumi na mbili kamili asubuhi.
 
Too much sasa kila siku tunapandishiwa vifurushi asee nina laini ya Airtel wacha tu nitumie iyo siwezi kutoa elfu nane nipate Gb 4 na dakika kizembe hivi jirekebisheni sisi si wote tuna hela za mchezo mchezo embu jiangalieni
Hahah hao wajinga kila walivyoona kila wiki naunga bando kubwa, nao wakaanza kamchezo ka Kunipandishia Gharama za Bando, wakati huo wanapunguza GB na Dakika.

Nilawapandia hewan, jaman kulikon??

Wananiambia Ooohooo wee tumeona matumizi yako makubwa, ohoooo nini ,

Nkawauliza mtaa, wilaya niliyopo. Mbona Rafiki zangu Mabando na gharama viko vilevile

Wakajibu... Ohooo kama tulivyokuambia wewe una matumizi

Nilimtukana yule mtoa huduma...

Nikatoa hela yangu Tigopesa yote... Nikakopa Kifurushi.

Sijawah tena kuweka salio Tigo!
 
Nenda Halotel mkuu Kuna unafuu kidogo, 1Gb kwa 1000 siku 7.

Pia Kuna bando la usiku la bila kikomo kwa 1500 kuanzia saa sita kamili usiku mpaka saa kumi na mbili kamili asubuhi.
navijua ivyo sema hawa wajomba wako slow si poa yaani mtandao wao
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom