Tigo na Zantel kuuzwa kwa Axian group ya Madagascar, naona wanakimbia Socialist economy

MURUSI

JF-Expert Member
Jun 25, 2013
4,472
8,692
Millicom wameamua kuuza Tigo kwa kampuni ya Madagascar, hivyo tutarajie tigo kubadilisha jina muda si mrefu.

Jamaa naona wanakimbia uchumi wa kijamaa, uchumi usioangalia Market Force bali unaongalia wanyonge wanasemaje.

Habari zaidi:

Dar es Salaam. Kampuni ya Millicom International inayomiliki hisa za Tigo na Zantel, imepanga kuziuza kampuni hizo kwa ubia utakaoongozwa na Axian Group, kampuni ya mawasiliano yenye makao makuu yake jijini Antananarivo, Madagascar.

Kuuzwa kwa Tigo na Zantel, kunaifanya Millicom kukamilisha safari yake ya kujiondoa katika soko la Afrika ilikodumu kwa zaidi ya miaka 25 badala yake kuelekeza nguvu zake Amerika Kusini.

Axian Group, ni kampuni ya mawasiliano inayotoa huduma katika visiwa vilivyomo kwenye Bahari ya Hindi, Afrika na Ulaya. Huduma zake kwa sasa zinapatikana nchini Madagascar, Senegal, Togo, Visiwa vya Reunion na Mayotte pamoja na Comoro.

“Millicom inafuraha kumpata Axian ambaye ni mwekezaji wa kimkakati kuendeleza huduma za Tigo Tanzania pamoja na Zantel kupeleka huduma nafuu na za kibunifu kwa wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” imesema Millicom kwenye taarifa yake.

Mchakato wa kuhamisha umiliki utakapokamilika muda wowote ndani ya mwaka huu, Axian Group inatarajiwa kuwekeza dola 400 milioni (zaidi ya Sh920 bilioni) ndani ya miaka mitano ijayo.

“Tunapenda kuwahakikishia wateja wetu na umma kwa ujumla kwamba huduma zetu zitaendelea kuwa kama zilivyo mpaka tutakapopata uthibitisho kutoka mamlaka za usimamizi,” inasomeka sehemu ya taarifa ya Millicom.

Tigo ilianza kutoa huduma zake nchini mwaka 1995 na miaka 15 baadaye ikazindua huduma za fedha, Tigopesa. Mpaka mwishoni mwa Desemba 2020, Tigo ni kampuni ya pili kwa kuhudumia wateja wengi wa mawasiliano hata wa huduma za fedha ikiwa nyuma ya Vodacom

===

Millicom is selling its Tanzania operations to Madagascar’s Axian as the Nasdaq and Stockholm-listed emerging markets telecoms group pulls out of Africa to focus on Latin America.

With 13m customers, Tanzania is Millicom’s main operation in Africa, where it is among the top three telecoms operator by number of customers.

On Monday, Millicom agreed to sell its entire operations for an undisclosed amount to Axian, an Antananarivo-based pan-African group that was part of the consortium that snapped up Millicom’s operations in Senegal in 2018.

“We knew that asset for a while because Tanzania has huge potential,” Hassanein Hiridjee, the CEO of Axian, told the Financial Times. “When we found that Millicom was divesting from Africa we said: ‘we must go there, we must’.”

With $366m in revenues last year, Tanzania represents a meagre 6 per cent of Millicom’s total revenue. Africa, the Miami-based company said, has historically generated lower returns than Latin America, where it has very profitable operations, especially in Guatemala, El Salvador, and Panama.

Millicom, via its Tigo brand, counts more than 52m mobile subscribers across 11 countries in Latin America and Africa. Yet, over the past four years, it has sold its operations in the Democratic Republic of Congo, Rwanda, Senegal, and Chad. On Friday, it agreed to transfer its stake in AirtelTigo to the government of Ghana — where it had a joint venture with India’s Airtel — taking on a $25m charge. Now, the selling of Tigo in Tanzania means the emerging market telecoms will be fully exiting Africa this year.

“Millicom is a Latin American focused telecom company with 95 per cent of our revenues coming from that region. With the announcement today of the divestiture of our remaining African businesses we draw a close on a chapter in our history and open another solely focused on the Latin American region,” Mauricio Ramos, the CEO of Millicom, told the Financial Times.

For Axian, the entrance to the Tanzanian market comes at a time of great expectations after the east African country’s new president, Samia Suluhu Hassan, signalled that she would improve strained relations with investors and multinational companies following five years of growing anti-market isolation under her predecessor, John Magufuli, who died in March.

Axian owns Telma, a telecom firm operating in Madagascar, Comoros, Réunion Island and Mayotte, and has a presence in Senegal through its operator Free Senegal, formerly Tigo, and in Togo, through Togocom.

The company was the first to roll out 5G in Africa and is one of the biggest investors in the EASSy — 10,000km submarine cable system deployed along the east and south coast of Africa that services voice, data, video and internet. Tanzania will be Axian’s first venture into an anglophone country, where it plans to invest some $400m over the next five years.

“We already have shared infrastructure. We’re very much interested in this market, which is not far from our home market,” Hiridjee added.
 
Faida waliyokuwa wanapata labda imepungua sana, kiasi cha kuona ni kuendelea na biashara yenye kodi zisizo tabirika hailipi, na afadhali kwenda kwenye nchi zenye sera za biashara na uwekezaji rafiki na zinazoeleweka(zenye consistency), na kuwaachia nyie muendelee wenyewe Afrika mnaoelewana.....
Kwa akili yako tigo hawapati faida sababu ya ujamaa?
 
Taarifa kwa watumiaji na wateja mbalimbali wa mawasiliano ya simu.

Kampuni mbili za mawasiliano ya simu nchini Tanzania Tigo na Zantel sasa zipo mbioni kuuzwa kwa Kampuni ya Axian Group.
 
Back
Top Bottom