Tigo mtandao pekee unaotuma SMS ya kawaida leo inafika kesho

mirindimo

JF-Expert Member
Nov 2, 2009
892
1,709
TCRA mnajitahidi sana kuhakikisha wateja wanapatiwa huduma ipasavyo, mimi leo naomba niseme tu Tigo kweli wanaibia sana wananchi kwanza huduma zao ni mbovu.

Nlijaribu kudadisi sababu kuna Engineer wao aliniambia maboss hawataki kubadili vifaa ili viendane na ukuaji wa teknolojia pia ongezeko la wateja ni kama wamezidiwa ndio maana kuna saa unaweza mpigia mtu simu yupo jirani yako ukaambiwa haipatikani lakini pia umekua ukitumiwa sana na matapeli.

Matapeli wote ukiangalia wanatumia namba za Tigo huezi kuta mtandao mwingine nafikiri hata jeshi la Polisi linaweza thibitisha hili kwa kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu uhalifu mtandaoni achilia mbali watapoteza wateja lakini humu ndani ya Tigo ni kama uwanja wa fisi zamani kama tukipalinganisha na eneo yaani kuna uhalifu wa kila namna.

Naomba mdau unaesoma huu uzi najua upo Tigo pia share hili kwenye group lenu la ofisini na maboss waone namna mnavyoendesha mambo kimazoea kiswahili swahili kibabaishaji mnakua kama makanjanja wa mjini matapeli tapeli yaani ujanja ujanja mwingi.
 
kuhamisha salio sasa ndio usiseme umekaa zako nyumbani unatumiwa sms umefanikiwa kutuma laki 2 kwenda no flani salio lako jipya nii halafu no iliyopelekewa pesa huijui, chaaaa me nilihamishaga salio langu nikapeleka bank mapemaa
 
Tigo munakera. Mimi ni mteja wenu wa siku mingi tu likini tatizo linalosemwa hapa nishanikumba mara nyingi tu pia mtandao wenu unakatika sana, ghafla tu unashaangaa mtandao haupo yaa bar za mtandao zinaondoka zote kwenye simu kisha zinarejea. Musije mukasema simu yangu ni kimeo. Simu yangu ina laini mbili lakini laini yenu ndio inakata mtandao kwa nini na nipo mjini?
 
Tigo wamenikera sana, juzi jmosi iliyopita nilitaka niweke salio ilikuwa mida ya saa 5 usiku, nikaenda kwenye maduka yaliyo karibu ili ninunue vocha nikakuta yamefungwa na yaliyokuwa bado yapo wazi hawakuwa na vocha za tigo.
Sasa nikaamua niweke pesa kwenye Tigo pesa halafu nije ninunue muda wa maongezi kutoka tigo pesa kwa sababu alikuwepo rafiki yangu karibu ambaye anajishughulisha na uwakala wa Tigo pesa nikamwambia niwekee jero kwenye namba yangu. Nikampa namba akaanza kutuma, alipofika kwenye hatua ya kuthibitisha ili anitumiwe jina likaonekana la mtu mwingine kabisa, halafu akaniuliza mbona jina sio lako?(halafu akanionesha hilo jina nikaona kweli sio langu) nikamwambia kata usithibitishe kwanza. Nikamwambia jaribu kupiga hiyo yangu nione kama kweli itaita au la, akanipigia kwa namba yangu simu ikaita kama kawaida lakini tukawa tunajiuliza kwanini kwenye tigo pesa inaonesha jina lingine ambalo sikulisajilia?
Nikaamua nijilipue nione kama kweli akituma hiyo hela itakwenda kwenye hilo jina wakati namba ni yangu. Nikamwambia tuma hiyo jero, akaanza hatua za kutuma, kwenye kuthibitisha likaonekana hilo jina na akathibitisha jero ikaenda kwenye hilo jina.

Hadi sasa sitaki kuitumia Tigo pesa na sitaki kufuatilia hili tatizo labda nikipenda ndio nitafuatilia, maana wamenikera sana hadi sina hamu nao.


TIGO wanatuibia sanaaaa!!!
 
TCRA mnajitahidi sana kuhakikisha wateja wanapatiwa huduma ipasavyo , mimi leo naomba niseme tu tigo kweli wanaibia sana wananchi kwanza huduma zao ni mbovu nlijaribu kudadisi sababu kuna engineer wao aliniambia maboss hawataki kubadili vifaa ili viendane na ukuaji wa teknolojia pia ongezeko la wateja ni kama wamezidiwa ndio maana kuna saa unaweza mpigia mtu simu yupo jirani yako ukaambiwa haipatikani.....lakini pia umekua ukitumiwa sana na matapeli ...matapeli wote ukiangalia wanatumia namba za tigo huezi kuta mtandao mwingine nafikiri hata jeshi la Polisi linaweza thibitisha hili kwa kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu uhalifu mtandaoni achilia mbali watapoteza wateja lakini humu ndani ya tigo ni kama uwanja wa fisi zamani kama tukipalinganisha na eneo yaani kuna uhalifu wa kila namna !!!

Naomba mdau unaesoma huu uzi najua upo tigo pia share hili kwenye group lenu la ofisini na maboss waone namna mnavyoendesha mambo kimazoea kiswahili swahili kibabaishaji mnakua kama makanjanja wa mjini matapeli tapeli yaani ujanja ujanja mwingi
Babu mtandao wenyewe unaitwa tigo, jina tu linasadifu haya wafanyayo
 
Nanyinyi watu wazima kwa nini mnavamia mitandao ya wanachuo.karibuni vodacom mtandao wa wajanja
 
Dah tigo wananilostisha mbayaa.

Jana mamilooo kanitumia text kuwa atakuja kejo hivyo nijiandae, basi mtoto wa watu akajua nimeinyaka na nitafanya hivyo.

Nimetoka niko kwenye mishe zangu mbali kabisa ndio naona text zinaingia kwa spidi ya mwendokasi kama nne hivi, kuzisoma ipo hiyo ya huo mu appointment na nyingine za kuomba kupokewa.

Kumbe jumbe zimetumwa muda kweli kweli ila zilikutana na foleni sijui!!

Mmesababisha mwenzenu nimenuniwa sijui hatima yangu mpaka sasa
 
Back
Top Bottom