Malalamiko mbalimbali kuhusu mabadiliko ya vifurushi yaliyofanywa na mtandao wa Tigo kwa mwaka 2020

mashonga

JF-Expert Member
Nov 30, 2013
594
967
MALALAMIKO MBALIMBALI YALIYOTOLEWA NA WADAU:
Habari za mida hii wakuu, hivi haya mabadiliko ya bando za Tigo ni kwangu tu au kwa watu wote? Maana daah bando zimekuwa ghali sana kwa sisi Wananchi wanyonge.

1580370489952.png

=====
Nina kawaida ya kuweka vifurushi vya simu kila wiki. Leo naingia kwenye mtandao wa Tigo nakutana na mabadiliko ya ajabu ya bei za vifurushi.

Nikaamua niangalie na Voda nako kukoje? Balaa ni lile lile hakuna nafuu, nikajiuliza kulikoni mabadiliko ya ghafla hivi ya bei za vifurushi kama soko la Tandale?

Baada ya tafakari nikagundua kuwa kampuni za simu zimechukulia nafasi hii ya TCRA kushikamana na NIDA kama nafasi ya kujipigia pesa kukiwa na taharuki.

TCRA imejionyesha nayo ni taasisi dhaifu sana katika usimamizi, jee nani hasa kiongozi wa kisiasa anayepaswa kulisimamia hili? Ni Mwakyembe au nani?

TCRA imeshindwa mitandao ya simu na kampuni za ving'amuzi sijui kwa nini, hadi inadhaniwa kuwa wakuu wake wameingizwa kwenye payrolls za makampuni hayo yanayofanya biashara kimafia.
---
Kwa sa hivi kama hutumii TTCL au Halotel una wakati mgumu sana wa bando.

Tena nao hadi ujue vifurushi vyao vizuri vilipo kama Halotel wamevificha vifurushi vyao kwenye Halo Pesa, Tigo acha ibaki kwa Tigo pesa tu. Kwakweli Tigo ni kero; mtu najiunga unanipa meseji 5? sasa zina kazi gani? Et mia 5 unapata dakika 7 mitandao yote sijui na vimeseji vingapi. Wakati Halotel wanakupa 18.

Maisha ni kupanga na kuchagua.
---
Ni kawaida kampuni kuzaliwa, kuishi na kufa katika ulimwengu wa biashara hivyo Tigo ni sehemu ya hayo automatically.

Ninachojiuliza ni kweli kuwa kampuni ya Tigo imekubali Kufa kirahisi hivyo baada ya jitihada Zooote za kukupambana sokoni.

Bila shaka Tigo wanajua jinsi kampuni zao nyingine Africa zilivyoshindwa kufanya vizuri isipokuwa ya Tanzania imekuwa tofauti. Hapa Kuna watu wa masoko wanastahili pongezi kubwa. Mfano ni kina Kelvin Twisa, hongera kwao maana walifanya kazi nzuri kipindi chao.

Nije kwenye suala la msingi la kwa nini Tigo inaenda kufa:

Kwanza ieleweke, mpaka kufikia maamuzi ya kubadili vifurushi mchakato huo utakuwa na sababu zilizokubalika na menejimenti na kwa kuwa wao ni key players yawezekana wameona mbali na wana taarifa za kutosha.

Pamoja na hayo, haituzuii kutoa maoni yetu.

Sasa basi kwa maoni yangu kitendo cha Tigo kubadili vifurushi vyao itasababisha wateja wao wakimbie.

Tigo itakimbiwa na wateja sababu ya msingi wa ukuaji wake ulijengwa kwa vijana hasa wanafunzi na watu wenye kipato kidogo ambao kimsingi ni wengi. Ilifikia kipindi karibu wanafunzi 'wote' ama wengi wana laini za tigo. Hapo ndipo likatokea Jina kuwa ni mtandao wa wanafunzi. Wanafunzi hao walipomaliza waliendelea na sasa wapo vijana wa kutosha ni watumiaji wa mtandao huu.

Shida kubwa ni msingi uliotumika kuikuza tigo na kushikilia wateja wake ambao ni vijana kwa kuwapa ofa kubwa za muda wa maongezi na internet. Sasa unapoondoa vitu hivi vijana hawa ni rahisi kuhama na kuhamia mitandao mingine yenye huduma nafuu kwa sababu wanazo alternatives.

Vijana ni risk takers, hawana vya kupoteza wanapohama hama. Ni tofauti na wazee ama watu wa umri wa kati.

Yawezekana mnawaiga Voda ila angalieni wao wamepandisha vifurushi vyao lakini hausikii kelele mitandaoni sababu ni aina ya wateja ambao Voda waliwachagua na utamaduni walioweka tangu mwanzo.

Tigo nawaambia hivi wateja wenu hawa vijana wanawahama sababu ni kuwa wakati nyie mnawabana kuna mitandao imewafungulia milango.

Ikiwa lengo lenu ni kuua kampuni ama kuuza kwa mtu mwingine basi sawa. Ila kama mnataka kuendelea fanyeni utafiti vizuri muwajue wateja wenu.

---
Ukitaka kuona upuuzi wa hawa Tigo endelea kufululiza kununua hicho kifurushi kama hawakitoa basi utakinunua kwa Sh.3500

Mimi laini yangu ya Tigo sikuwahi kuiwekea vocha ndani ya miezi mitatu basi wakaanza kunitamanisha na offer zao kua weka jero upate MB500 kwa siku tatu. Mi nikawa nawapuuza kwasababu kipindi hicho Halotel nilikua napewa MB 600 kwa jero.

Siku moja nikastuka kuona meseji kwenye laini yangu ya Tigo kua ukiweka vocha ya 500 utapewa GB 30 zakutumia mwezi mzima. Nikasema acha nijaribu kama watanitapeli jero siyo kesi kwasababu siyo hela kubwa.

Nilivyoweka nikajiunga ikakubali aisee nilifurahi sana nikawapiga chini halotel kwa muda nikawa na download vitu heavy torrentz ikawa shangwe sana

Lakini baada ya mfululizo wa siku tatu kuunga bando hilo nikishangaa sana ile menu niliyokua napata lile bando ikageuzwa kua menu ya kukopea

Mi sina hili wala lile nimeweka jero langu nataka nijiunge nakuta hongera umefanikisha kukopa sh 600, aaah nilimaindi kisenge
---
Ama kweli mtandao wa Tigo ni mtandao wanafunzi. Inawezekana vipi waseme kifurushi cha week ni 2500/- unapata dk 250 kisha ukisha ukishajiunga wanakwambia dk 90 upige kuanzia saa 4 ucku mpka 11 alfajiri.

Sasa hawa jamaa wanadhani sisi tunakesha kwa kuongea badala ya kudumisha ndoa zetu. Ukisikia dhulma ndo hii kutoka Tigo.

Kwanini wasifafanue kabla mtu hujajiunga ili ukubali kujiunga au ukatae. TIGO TIGO TIGO MUNGU ANAWAONA NA MTALIPWA KWA HILI
---
Wakuu salam za asubuhi hope ziko poa kwenu na mmeamka salama ila mimi hapana nimelala kwa taabu sana jana na joto la jiji hili.

Kisa hawa Tigo wametubadilishia vifurushi na kuweka gharama juu isio mkidhi mlaji. Lakini bado hawajachoka sasa hivi wamekuja na mpya

Unanunua kitu kupitia Tigopesa na pesa ipo ila unaambiwa huna salio la kutosha nimenunua umeme jana asubuhi hadi leo kimya kikuu. Ukipiga numbers zao wapo busy kibaya taarifa za mabadiliko hawajatoa wala nini sasa kilichobaki sasa hivi.

Nikuja na #hashtag #ott operation tokomeza Tigo. Kama wana hasira na line zao kuwekwa ban ni jukumu la kudeal na Serikali sio Wananchi walalahoi.

View attachment 1339200

Sent using Jamii Forums mobile app
---
Habari

NB: uzi huu hauchochei/ kutangaza mtandao wowote bali ni maoni tu.

Nimekuwa mtumiaji pendwa wa mtandao wa simu wa Tigo kwa miaka mingi kutokana na huduma zao kuwa bora (kwa maeneo niliopo) ikiwa ni pamoja na internet yenye kasi ya kuridhisha vilevile kupitia vifurushi vyenye gharama rafiki (kwangu mimi) hivyo kuniweza kupata sms, dakika na bando za intaneti kwa nyakati husika.

Tukiachilia mbali sifa mbalimbali mtandao wa simu wa Tigo umejipatia kumetokea na sintofahamu kwa siku za hivi karibuni ambapo vifurushi mbalimbali vya Tigo kuongezeka bei tofauti na mwanzo

Mfano 1: GB 1 iliuzwa kwa shilingi 1000 hivi saaa ni 3000
Mfano 2: SMS 3000 ulipata kwa shilingi 1000 hivi sasa unapata sms 1000 kwa shilingi 1000

Na vifurushi vingine vingi zaidi kubadilika

Maoni yangu:

- Baada ya mtandao wa simu wa Tigo kuweka kifurushi cha combo chenye dakika nyingi pia wajaribu kupunguza bei Za vifurushi(bei sio rafiki)/kurejesha vifurushi vilivyokuwepo wiki kadhaa nyuma

- Kuboresha vifurushi vya internet kwani bei na vifurushi haviendani hata kidogo.

- Matumizi ya data yarandane na kifurushi (Nikiangalia data usage kwa siku husika kama ni 1GB na kifurushi changu kiwe kimeisha Kwa 1GB kwani muda mwingine utakuta tofauti data usage 1GB ila kifurushi cha 3Gb kimetumika)

All in all ni maoni tu sio kwa ubaya ni kwa uboreshaji tu...

=====

WADAU WENYE MTAZAMO TOFAUTI:

Mimi nina mtazamo tofaut kidogo. Mitandao ya simu ikipandisha vifurush hasa vya internet bei kuwa juu nadhani watumiaji wa internet hasa kwenye social networks huku watapungua kwa asilimia kubwa hvyo wakosoaji watapungua pia. Hvyo ni game ya Win-lose kwa wanene. Kwahyo unataka TCRA wapige kelele kweli hapo?


Sent from my iPhone using JamiiForums
---
Kwanza mimi niwapongeze Tigo kwa kuleta vifurushi vipya vya internet ambavyo hata hivyo bado haviko affordable in terms of gharama, japo vina wingi wa data. Kidogo wameongeza wingi wa data zao tofauti na wenzao Voda (sijajua mitandao mingine kama Halotel, TTCL n.k)

Nisiongee sana, naomba muangalie tofauti ya vifurushi kisha mfanye judgement nyie wenyewe. Hii ni list ya vifurushi vya internet ambavyo sio vya ofa yoyote.

Vifurushi vya Siku

Voda

5000/= ----> 2GB/48HRS
2500/= ----> 1.2GB
1200/= ----> 350MB
1000/= ----> 200MB
1000/= ----> 1GB/2HRS
500/= ----> 70MB
600/= ----> 100MB

Tigo
2000/= ----> 1.5GB
1000/= ----> 300MB
500/= ----> 75MB

Vifurushi vya Wiki

Voda

20000/= ----> 12GB + FB
15000/= ----> 5GB + FB
10000/= ----> 2GB + FB
5000/= ----> 800MB+ FB
3000/= ----> 500MB+ FB

Tigo
15000/= ----> 12GB
10000/= ----> 7GB
5000/= ----> 3GB
3000/= ----> 1.5GB

Vifurushi vya Mwezi

Voda

95000/= ----> 40GB + FB
50000/= ----> 20GB + FB
35000/= ----> 10GB + FB
20000/= ----> 4GB + FB
10000/= ----> 1GB + FB

Tigo
50000/= ----> 40GB
30000/= ----> 20GB
20000/= ----> 13GB
10000/= ----> 5GB
---
Honestly Tanzania makampuni ya simu karibu yote huwa hawana kitu kama kum-retain mteja, kumwongezea Bando au airtime kwa kuwa mara kwa mara ananunua airtime na bando.

Huduma zimekaa kinyonyaji tu; it's unthinkable mtu ilikuwa unapata 2GB kwa buku 2 in 3days over a sudden wanaondoa.
Kama ni investment cost walisharejesha, na huwa nawaza, hakunaga regulatory authority kama EWURA ku-regulate bei. Maama kwenye miamala nako balaa. Mtu unatoa elfu 40 unakatwa 2300. This is a lot.

Bank Atm laki 4 makato 700 mpaka 1000; inakuwaje mtu anatoa laki 1 anakatwa 2700.

BoT wanao-regulate taasisi za fedha, huduma za kifedha kwenye simu, wizi umezidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
---
Umeeleza mengi ambayo kwa maoni yangu naona kama ni mhemko tu,

Kwa mtumiaji wa tigo kama mimi nimefurarhia sana kifurushi cha 10,000\= cha mwezi mmoja, ambacho kina dk. 1150.
Kati ya hizo 6000 ni za mitandao yote na 550 hizi ni za kuanzia saa nne usiku hadi asubui!
NANI MWINGINE ANATOA DK. KAMA HIZO? tigo bado ni babalao kwa gharama nafuu kbsa ktk muda wa maongezi!

Yote ulioyaeleza bila kusema umeasirikaje, na bila kuangalia maslai ya wengi utapoteza watu!

Airtal wana wanatoa dk. 450 kwa mwezi kwa sh. 10,000/ ungeongea kwa vigezo ili tufananishe!


Sent using Redmi Y2
pia soma >
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom