stunnacarter2015
JF-Expert Member
- Apr 7, 2017
- 463
- 1,287
Habari
NB: uzi huu hauchochei/ kutangaza mtandao wowote bali ni maoni tu.
Nimekuwa mtumiaji pendwa wa mtandao wa simu wa Tigo kwa miaka mingi kutokana na huduma zao kuwa bora (kwa maeneo niliopo) ikiwa ni pamoja na internet yenye kasi ya kuridhisha vilevile kupitia vifurushi vyenye gharama rafiki (kwangu mimi) hivyo kuniweza kupata sms, dakika na bando za intaneti kwa nyakati husika.
Tukiachilia mbali sifa mbalimbali mtandao wa simu wa Tigo umejipatia kumetokea na sintofahamu kwa siku za hivi karibuni ambapo vifurushi mbalimbali vya Tigo kuongezeka bei tofauti na mwanzo
Mfano 1: GB 1 iliuzwa kwa shilingi 1000 hivi saaa ni 3000
Mfano 2: SMS 3000 ulipata kwa shilingi 1000 hivi sasa unapata sms 1000 kwa shilingi 1000
Na vifurushi vingine vingi zaidi kubadilika
Maoni yangu:
- Baada ya mtandao wa simu wa Tigo kuweka kifurushi cha combo chenye dakika nyingi pia wajaribu kupunguza bei Za vifurushi(bei sio rafiki)/kurejesha vifurushi vilivyokuwepo wiki kadhaa nyuma
- Kuboresha vifurushi vya internet kwani bei na vifurushi haviendani hata kidogo.
- Matumizi ya data yarandane na kifurushi (Nikiangalia data usage kwa siku husika kama ni 1GB na kifurushi changu kiwe kimeisha Kwa 1GB kwani muda mwingine utakuta tofauti data usage 1GB ila kifurushi cha 3Gb kimetumika)
All in all ni maoni tu sio kwa ubaya ni kwa uboreshaji tu...