Tigo mmebadilisha bei za vifurushi vya internet vya wiki?

Mnasihi

JF-Expert Member
Oct 9, 2013
7,659
6,910
Habarini wadau na wanajf wote. Hongereni kwa kuuzingatia ushauri wa wataalamu wa afya ili kuzuia maambukizi mapya ya covid-19.

Nauliza Bei mpya ya vifurushi vya internet vya wiki kwa mtao wa tigo vimebadilika kutoka sh 3000/=?

nimejaribu kumnunua lakini napata and ya kuwa Sina salio la kutosha ilihali nimejaza vocha za sh 4000/= Kama Kuna mwenye kuyajua mabadiliko anisaidie tafadhali.
 
Hivi TCRA wana-regulate haya makampuni au ndio basi tena? Ifike mahali malalamiko kama haya yasitokee, inakuwaje kila uchwao malalamiko kutoka kampuni za simu Tanzania hayaishi?

BTW: Wale mlio bongo mnashindwa nini kulalamika TCRA? Just thinking!
 
Umekuwa mtandao wa ovyo sana wanapunguza gharama za vifurushi bila taharifa wezi wakubwa,hawa ni kuwahama tu,tcra nao ni wadau tu wa kuibiwa watanzani hawana msaada wowote utafikiri wamelala usingizi,pumbav.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu mtandao wa kipopoma sana, ina maana watu bado mpo tigo tu hadi leo?🤣🤣🤣

Si muhamie mnakopendwa jamani.

Wateja wa Tigo nawafananisha na hamorapa anavyopigania penzi la wema bila mafanikio 🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Kuanzia mwezi uliopita internet kifurushi cha week ilikuwa 2000 kwangu GB 3,kuanzia jana wamebadili ni sh 3000 halafu GB 2,kuna mdau hapo juu amesema yeye amelipia jana ya week 2500.

Kifurushi hicho hicho ila bei tofauti
Kifurushi cha aina moja, lakini bei zake zipo zaidi ya tatu tofauti!

Sent using Jamii Forums mobile app

♡♤Life belongs to all who struggle for it♤♡♧
 
Huu mtandao wa kipopoma sana, ina maana watu bado mpo tigo tu hadi leo?🤣🤣🤣

Si muhamie mnakopendwa jamani.

Wateja wa Tigo nawafananisha na hamorapa anavyopigania penzi la wema bila mafanikio 🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Tatizo uchumi amigo

My life is mine to remember
 
Back
Top Bottom