Tigo, kwanini mnatulazimisha kukopa kwa kuweka kiasi kikubwa cha bando kwenye Tigo Niwezeshe?

stickvibration

JF-Expert Member
Feb 7, 2017
3,227
5,132
Mimi ni mteja wa hii kampuni kuanzia Tritel hadi kampuni kuuzwa kwenda Mobitel pia kampuni ikauzwa kwenda Buzz hadi leo hii kufikia kampuni kuitwa TIGO. Mimi yule yule nipo tu na hata namba ni ile ile tu.

Tatizo kubwa ni pale nikitaka kujiunga Siku Bonus ya Internet napata ofa ya 2000=1GB kwa siku lakini nikitaka kujiunga INTERNET kwa kupitia Tigo Niwezeshe ya Sh. 2000 hiyo hiyo napata 2.5 GB kwa siku kisha nalipa Sh. 2400(400 ni interest).

Sasa inakuwaje mnatulazimisha kujiunga kwa tigo niwezeshe? Je, ni ili tulipe hiyo riba?

Maana Tigopesa ninayo hela ya kutosha lakini bila kupitia Tigo Niwezeshe naambulia 1 GB tu.

Tuangalieni kwa macho ya tofauti sisi ambao imani zetu haziruhusu kukopa ama kukopesha kwa riba ukizingatia sisi ni wateja wenu wakongwe!
 
Miamala yote hio hapo
Screenshot_20210202-032110.jpg
Screenshot_20210202-031628-1.jpg
Screenshot_20210202-031654-1.jpg
Screenshot_20210202-032532-1.jpg
Screenshot_20210202-031724-1.jpg
 
Inanibidi nikope tu kwa kupata Gb 2500
Hali ya kuwa Tigo Pesa Yangu ina balance ya Elf 50
...hii inamaanisha kuwa tunalazimishana kulipa kwa Intrest. Unakopa 2000 kisha lipa 2400
Vingenevyo kama hutaki kulipa kwa RIBA basi nunua kwa pesa yako kifurushi cha INTERNET kwa elf 2000 upate GB1
 
Kwa hiyo riba ya 400 inakuongezea GB1.5 si haki na mda mwingine wanajua kabisa kwa mbongo wa kawaida kumaliza GB1 kwa saa 24 haiwezekani utapeli wa wazi wazi
 
Kwa hiyo riba ya 400 inakuongezea GB1.5 si haki na mda mwingine wanajua kabisa kwa mbongo wa kawaida kumaliza GB1 kwa saa 24 haiwezekani utapeli wa wazi wazi
Na muda huo huo niliongea na Customer Care na akanijibu...endelea tu kukopa2000 na ulipe 2400 ili upate GB 2.5 kwa kupitia TIGO NIWEZESHE unless utaishia kupata GB1 kwa elf2000
Maelezo na nimesnap shot juu
 
Mi sasahivi nimekua mdau mkubwa wa kukopa tigo niwezeshe, now nimefikia uwezo wananikopa hadi mfululizo hadi elfu 7.....hii ndi tigo bhana..live it love it
 
Back
Top Bottom