Tigo kwa nini mnatufanyia njama za wizi kiasi hiki?

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,635
7,005
Mwezi uliopita nilinunua kifurushi cha shilingi elfu 10 cha mwezi mzima.Lakini baada ya siku tatu tu,nikabiwa kifurushi kimeisha na kusema kweli sikuwa nimeongea hata dakika 30.

Nilikuwa na dharura ya kupiga simu,ilibidi ninunue kifurushi kingine cha elfu 10.Hata hivyo nilifanya hivyo baada ya kuwapigia bila mafanikio yoyote.Baadae nilieapata wakaniambia kuwa nina dakika zaidi ya 2300.Na kwamba kulikuwa na tatizo ila limeisha.Hata hivyo sikufanikiwa kupiga simu kwa muda wa siku 3.

Kifurushi hicho kwa mara ya kwanza hakikumaliza mwezi ijapo elfu 10 huwa natumia mwezi mzima.

Sasa leo nimejaribu kununua kifurushi kupitia tigo pesa imegoma.Nimehamishia kwenye Salio ninunue kifurushi bado imegoma.Maana yake wananilazimisha nipige bila kununua kifurushi.

Naamini hii mbinu wamegundua inawaingizia pesa nyingi sana lakini mimi naona huu ni wizi kama wizi mwingine
 
Back
Top Bottom