Tigo kuumbuka hadharani na unyanyasaji wao kwa wateja kuanzia leo

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,484
54,855
Mlimani Tv kimekuwa chombo cha habari tanzania kinachotoa mda mkubwa wa hewani kutangaza matatizo yanayo wakumba wananchi wa Tanzania.
Makampuni ya simu yamekuwa ni moja ya kampuni zinazo kanyaga haki za raia kwa kuahidi wasivyo tekeleza. kumekuwa na hali ya kukatwa hela kusiko na mpango kwa haya makampuni ya simu.
Katika mwendelezo wa habari saa moja na nusu usiku, mlimani tv watakuwa wakizungumzia na kujadili Huduma za tigo kwa ujumla. Vituo vingine viige hiyo.
Ni hayo tu. Mia
 
Tatizo la huduma mbovu na ghali kwa watanzania linasababishwa na serikali pamoja na watanzania wenyewe. Kwa sasa hukuna nchi yenye huduma mbaya za simu kama Tanzania. Serikali kwa kutumia maafisa wake mafisi wanaingia mikataba na matapeli wasio na mtaji zaidi ya kutaka kutumia nafasi hiyo kukopa kwenye benki zetu na kutulangua huku ikijua fika matokeo yake. Kwa vile wahusika wanapewa hisa au ten percent wanapeta wakijua serikali yao ni ya hovyo. Wananchi nao wanastahiki lawama kwa kukubali kugeuzwa shamba la bibi wasigomee wala kuandamana kudai huduma ziboreshwe. Haya yakifanyika kwenye nchi kama Misri makampuni ya simu yatakula hasara maana wananchi watayashambulia hasa vitega uchumi vyao huku wakiikaba serikali na kuitaka irekebishe uoza wake au ipishe.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom