Tigo acheni wizi wa kipuuzi, msitafute pesa kwa kuwaibia watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tigo acheni wizi wa kipuuzi, msitafute pesa kwa kuwaibia watanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by luckman, Oct 17, 2012.

 1. l

  luckman JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Nimesikitishwa na mtandao huu wa simu wa Tigo, nimekuwa kila siku najaribu kuangalia mwenendo wa huu mtandao hata siuelewi lakini sikujali, ila siku zilivyokuwa zinaendelea niliona tabia hii imeidi nikaamua kufanya research
  yafuatayo nimegundua ni wizi mkubwa unaofanywa na hawa jamaa

  1. Ukitumiwa pesa na mtu lazima ukatwe 30% ya pesa uliyotumiwa ingawa na mtumaji anakatwa pia, nimeshangaa sana kwa ni nakumbuka siku za nyuma simu zinaanza ulipokuwa unapiga unakatwa na aliyepigiwa anakatwa, tigo wamerudi kulekule
  2. Ukikopa mda wa maongezi, unakatwa asilimia kadhaa na mbaya zaidi salio lako linatumika isivyo kawaida na muda wa maongezi wa kawaida, yani salio linawahi sana kuisha , inawezeka wanakata Tzs 3/sec (vat exclusive)
  3.Wana tabia ya kukata pesa bila sababu za msingi imezidi, unapunguziwa salio lako na bado ukiwapigia simu hawakupi sababu ya msingio zaidi wanakwepa maswali.
  4.Not reliable at all kwani wanaoneka kubabaisha sana kwenye business hii,

  Tafadhali sana waonee watanzania huruma na mjitokeze mseme kwanini mnakata pesa ya wateja wenu hata kama umepunguziwa muda wa maongezi na mtu.tunataka kujua
   
 2. h

  habi Senior Member

  #2
  Oct 17, 2012
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  unachosema ni kweli mimi imenitokea kwenye muda wa kukopa salio unaisha haraka sana dawa ni kuhama tuu mitandfao ipo mingi
   
 3. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2012
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,170
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  mimi nimeuchoka huu mtandao ingaawaje bado naung'ang'ania. Najua yote iko hivi. So nowhere to run to. Nimekubali kuliwa lakini wakumbuke kua Ukikubali kula lazima na wewe utaliwa. Ipo siku moja nao wataliwa. Laana!
   
 4. l

  luckman JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  i m not sure ni strategy ipi wanaitumia kumarket mtandao wao, strategy ipi kupata mapato ndani ya kampuni! malalamiko haya si credit kwao bali ni image destruction, wasijifanye hawajari ipi siku watashutuka but it will be too late!take my words.
   
 5. capito

  capito JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 415
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Tigo inabidi kweli wabadilike, kuna vocha za simu walitengeneza za kiwango cha chini ukikwangua kidogo inachubuka na namba hazionekani vizuri. Ilinitokea mimi kama miezi mitatu iliyopita nilikwangua vocha ya 2000 vibaya namba zikachubuka nikashindwa kuingiza zile namba, nilipopiga customer service wakasema niende kwenye ofisi zao, nilipofika ofisini nikapewa form kujaza mpaka leo bado nasubiria hiyo refund sijaipata, nikipita pale ofisini kuulizia naambiwa kuna form nyingi na za wenzangu zinasubiri nimeamua kuacha.
   
 6. Paw

  Paw Content Manager Staff Member

  #6
  Oct 17, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 2,032
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Hivi customer care namba yao inapatikana kweli?

  TCRA wanajua hili na kama kawaida hawaoni ni tatizo.
   
 7. M

  MAMC Senior Member

  #7
  Oct 17, 2012
  Joined: Jan 3, 2012
  Messages: 140
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kwa kweli kwa sasa tigo ni kimeo balaa! Japo sishangai sana mana kama makao makuu ya kampuni yamezungukwa na Bar ( black point, Chagga bite, makumusho, face to face) unategemea nini toka kwa wafanyakzi wao!?

  Kimeo namba 2 ni voda, so wenye afadhali kwa sasa ni Airtel! Na kwa bahati nzuri mie nimefanya kazi technical dept za kampuni zote za simu hapa Tanzania.

  Baadhi ya wizi wa voda na Tigo uko hivi

  1. Network zimezidiwa wana tumia mtindo wa "half rate" ku-fikisha simu matokeo yake - wateja hawasikilizani, na in effect ni kuwa hela yako inaliwa sana mana unatumia musa mrefu kuongea.,

  2. Simu zina -drop au hata unampigia mu eti hapatikani wakati simu yake ipo hewani. Hii inapimwa kwa dBm haitakiwa kuzidi -90, wenye blackberry waangalie iko hadi -110dBm

  3. Tigo ukilipia internet package hupati na salio linakatwa

  4. Customer care ya Tigo ndo maiti kabisa yani hawapokei simu, na wakipokea hawatatui tatizo.Wanaishia kukuambia watakupigia baadae - utangoja mpaka ukome.

  Cha kusikitisha sidhani hata kama TCRA huwa wana monitor nini? Ingawa sishangai sana kwa kuwa they inherently have deep conflict of interest, na kwa kuhakikisha hebu cheki presha aliyo ingia nayo Januari Makamba imeishia wapi?
   
 8. E

  Echimbe Member

  #8
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hii hata mimi imenitokea mfululizo zaidi ya wiki 4 sasa kila siku ifikapo muda wa jioni wanakata/wanapunguza salio ktk cm yangu bila kupiga au kutumu ujumbe kwa simu yangu;siku moja customer care walinipigia nikawauliza sababu za kufanya hivyo hawakuwa na sababu za msingi;tcra sijui wako wapi,n/waziri januari aliyeingia ofcn kwa maneno mengi vitendo havionekani!
   
 9. Zamaulid

  Zamaulid JF-Expert Member

  #9
  Oct 17, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 16,357
  Likes Received: 6,699
  Trophy Points: 280
  msikope tigo wajameni nendeni kwenye mabenki ya kueleweka!!!
   
 10. s

  suli Member

  #10
  Oct 17, 2012
  Joined: Feb 13, 2012
  Messages: 57
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  ukijiunga kwenye xtreme yao ndo utakoma, dakika zinaanza kuhesabiwa hata kabla ya wewe kuanza kuongea (i.e wanahesabu dak wakat wanatangaza matangazo yao) huu ni wizi mkubwa....! nshaamia airtel sa iv!
   
 11. l

  luckman JF-Expert Member

  #11
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Mamlaka husika ziko wapi?au wanagawana nao?haiwezekani wakawa hawajui huu ufedhuri.
   
 12. morenja

  morenja JF-Expert Member

  #12
  Oct 17, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 3,534
  Likes Received: 1,054
  Trophy Points: 280
  hakika tigo ni wezi aliye karibu na chama cha kutetea walaji na huduma akaripoti huu wizi wa tigo au takukuru kama ikibidi
   
 13. S

  SWEET HUSBAND Member

  #13
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 97
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hamia airtel,mi nimewahama tigo fasta,hawafai kabisa!
   
 14. Utamaduni

  Utamaduni JF-Expert Member

  #14
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 1,198
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Mimi niliyaona hayo kwa wkeli, toka mwanzo wa mwaka huu nilinunua line ya zantel, kwa bei wapo nafuu zaidi na hawasumbui ktk network zao. imefikia mahali line ya tigo naitumia just incase wakati ndo ilikuwa my number 1, ndo biashara, ukiona wanazingua tafuta mbadala.

  Maana hata ukisema vipi hawatosikia kwani wana wateja wengi sana, sasa ukilalamika mmoja hata hawasikii
   
 15. Takalani Sesame

  Takalani Sesame JF-Expert Member

  #15
  Oct 17, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kuna mitandao mingine zaidi ya Tigo. Toa chip tupa kule tafuta mtandao mwingine sajili namba toa taarifa kwa contacts wako, maisha yanasonga. Kung'ang'ania kitu kinachokukera ni stress za kujitakia tu!
   
 16. toghocho

  toghocho JF-Expert Member

  #16
  Oct 17, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 1,177
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  hapo kwenye salio la kukopa kweli diziani kama linasha fassta mpka basi umeongea dk 2 eti sh 450 imebaki 30 duh, mi sikopi tena kwanz wamepandisha rate zao.
   
 17. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #17
  Oct 17, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Tigo hawana maana kabisa, wamekuwa wezi sana, unaweka pesa inakatwa bila kutumika wanakwambia watakurudishia mimi ni week sasa nimekatwa pesa kibao kwenyesim yangu na hao customercare ndio hawajui lolote.

  Wanajibu wanayo yataka na weredi wao mdogo kabisa.

  Hii kampuni hovyo hovyo sana!
   
Loading...