Tido na wenzake wang’olewa MDTF

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Tido na wenzake wang’olewa MDTF


na Mwandishi wetu


amka2.gif
MAMBO ndani ya Chama cha Maendeleo Muheza (MDTF), yamezidi kuharibika baada ya sekretarieti inayoongozwa na Tido Mhando, kupinduliwa rasmi na genge linalojiita wanachama wakereketwa.
Kupinduliwa kwa sekretarieti hiyo kumekuja mwezi mmoja baada ya wanachama hao chini ya uongozi wa, Halid Kibwana, kutoa kitisho cha kufanya mapinduzi hayo.
Waraka wa maandishi uliosambazwa kwa baadhi ya wakazi wa Muheza waishio jijini Dar es Salaam umetaja uamuzi huo unalenga kukinusuru chama ambacho kinaelekea kufa tangu kuingia madarakani kwa sekretarieti hiyo mwaka juzi.
“Tumeamua kuing’oa sekretarieti ya MDTF kutokana na kushindwa kazi kwani tangu iingie madarakani mwaka juzi chama hakina ofisi, hakina hata shilingi kwenye akaunti, shughuli za utawala zimesimama na mipango yote ya maendeleo ikiwemo kuanzisha saccos Muheza imekufa,” inasomeka sehemu ya waraka huo.
Inaeleza pia kuwa alipoondoka Balozi Adadi Rajabu, aliacha chama kikiwa hai kwani alijenga shule ya sekondari na kufanya mambo mengine ya maendeleo tofauti na iliyo sasa ambayo ni mzigo.
MDTF inaundwa na sekretarieti inayoongozwa na Tido akiwa ni Mwenyekiti, Marry Chipungahelo- Makamu Mwenyekiti, Albert Semng’indu – Katibu.
Wengine ni Nehemia Mchechu ambaye ni Mweka Hazina na Mkurugenzi Mkuu Shirika la Nyumba (NHC) na Ramadhan Semtawa, Katibu Mwenezi huku Mkurugenzi Mtendaji akiwa ni Clement Mang’enya.
Alipoulizwa jijini Dar es Salaam jana kwa njia ya simu, msemaji wa MDTF, Semtawa, alikiri kupata waraka huo na kuongeza kwamba bado anawasiliana na wenzake kuona namna ya kufanya.
 
PHP:
"Tumeamua kuing'oa sekretarieti ya MDTF kutokana na kushindwa kazi   kwani tangu iingie madarakani mwaka juzi chama hakina ofisi, hakina hata   shilingi kwenye akaunti, shughuli za utawala zimesimama na mipango  yote  ya maendeleo ikiwemo kuanzisha saccos Muheza imekufa," inasomeka  sehemu  ya waraka huo.
   Inaeleza pia kuwa alipoondoka Balozi Adadi Rajabu, ali

Waliwaweka wazito kwenye nafasi nyeti wakifikiri ndiyo watachangia zaidi shughuli za kikundi chao.......................walipoona siyo hivyo basi wameamua kuachana nao...............................it is like shedding the unwanted baggage....................
 
Tido na wenzake wapinduliwa rasmi


Na Mwandishi Wetu

MAMBO ndani ya Chama cha Maendeleo Muheza (MDTF) yamezidi kuharibika baada ya sekretarieti inayoongozwa na Bw. Tido Mhando kupinduliwa rasmi na genge
linalojiita wanachama wakareketwa.

Kupinduliwa kwa sekretarieti hiyo kumekuja takriban mwezi mmoja baada ya wanachama hao chini ya uongozi wa Bw. Halid Kibwana, kutoa kitisho cha kufanya mapinduzi hayo.

Waraka wa maandishi uliosambazwa kwa baadhi ya wakazi wa Muheza waishio jijini Dar es Salaam umesema kuwa uamuzi huo unalenga kukinusuru chama ambacho kinaelekea kufa tangu kuingia sekretarieti hiyo mnamo mwaka juzi.

"Tumeamua kuing'oa sekretarieti ya MDTF kutokana na kushindwa kazi. Tangu iingie madarakani mwaka juzi, chama hakina ofisi, hakina hata shilingi kwenye akaunti, shughuli za utawala zimesimama na mipango yote ya maendeleo ikiwemo kuanzisha SACCOS Muheza imekufa.

"Alipoondoka Balozi Adadi Rajabu, aliacha chama kikiwa hai, alijenga shule ya kidato cha sita, visima vya maji na sekondari, lakini sekretarieti hii ya sasa ni mzigo. Kwa hiyo, tumeamua kwa maslahi ya Muheza, kuindoa madarakani. Wakazi wote wa Muheza mnaaombwa kuunga mkono mapinduzi hayo matufuku."

MDTF inaundwa na sekretarieti inayoongozwa na Mwenyekiti Bw. Tido, Makamu Mwenyekiti, Bi. Marry Chipangahelo, Katibu Bw. Albert Semng'indu ambaye ni Mkurugenzi CHC, Mweka Hazina Nehemia Mchechu, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba (NHC) na Bw. Ramadhan Semtawa, Katibu Mwenezi huku Mkurugenzi Mtendaji akiwa ni Clement Mang'enya.

Alipoulizwa jijini Dar es Salaam jana kwa njia ya simu, msemaji wa MDTF, Bw. Semtawa, alikiri kupata waraka huo na kuongeza kwamba, bado anawasiliana na wenzake kuona namna ya kufanya.

Bw. Semtawa ambaye pia ni mwandishi wa gazeti la Mwananchi, alisema inawezekana wanachama wakawa na hoja za msingi lakini tatizo likawa njia wanayotumia kutaka kuung'oa uongozi kupingana na katiba.

"Nikiwa kiongozi mkweli, nakiri sekretarieti yetu ina upungufu mkubwa. Ni kweli hakuna mradi hata mmoja ambao tumefanya tangu tukabidhiwe madaraka na wenzetu lakini, hata kama ni hivyo zipo njia za kikatiba kuondoa uongozi madarakani," alisema Bw Semtawa.

Hata hivyo, aliweka bayana kwamba, tayari karibu wajumbe wote wa sekretarieti walionyesha dhamira ya kutotaka kuendelea na nafasi zao tangu wanachama hao walipotangaza mpango huo wa mapinduzi hapo Februari.

"Wiki moja iliyopita mwenyekiti aliitisha kikao cha kamati tendaji, lakini wajumbe karibu wote (isipokuwa yeye Tido tu), hatukwenda na tulisema tunachojua tayari tumepinduliwa tangu Februari, hivyo tumeachia taratibu nyingine za kupata sekretarieti mpya," alisema Bw. Semtawa.

MDTF ni chama ambacho kimeanzishwa kwa dhamira ya kusaidia juhudi za serikali kuleta maendeleo kwa wananchi wa Muheza, chama hicho kilipata mafanikio makubwa wakati sekretarieti ikiongozwa na Balozi Adadi.
 
Back
Top Bottom