Tido Mhando na Ubinafsishaji wa TBC kwa StarTimes

Hawa watu wasitudanganye kabisa na vijisentence vya ajabu,hapa iko wazi kuwa tbc imeuzwa.Kamahujauza hizo sharing za kazi gani 65% ni ya wachina na mchezo umekwisha.Na wadanganyika wataendelea kudanganyika una 35% halafu unasema hujauza.Ndio yaleyale Celtel ni mtoto wa TTCL sasa yako wapi.
You can full people sometimes but not all times-Bob Marley

Malindi, sidhani mambo nia kama hivyo unavyosema.
Hii 35:65 share haihusu TBC, na sio kwamba TBC imeuzwa. Ni kitu kipya ambacho kinaanzishwa na hawa wachina watakua wanauza set-top-boxes ambazo zitakuwa zinatumika kwa ajili ya kudecode broadcasted digital signals. TBC1 ni moja ya channels ambazo zitakuwa available, pamoja na TBC2 ambayo itafunguliwa hivi karibuni kwa ajili ya entertainment (kama Channel 5 hivi). Pia channel nyingine za Asia zitakuwepo pia.

Watakachokuwa wakifanya hawa wachina, na hasa ndio ambapo hiyo 35:65 share ina apply ni ku supply technology (everything including set-top-boxes, broadcasting equipments etc) kwa wateja na TBC.

Sehemu nyingine ni kwenye collection ya fees. Ni vyema kujua kwamba hii huduma haitakuwa bure, utakuwa unalipia kama vile Dstv, isipokuwa rate yake itakuwa ni ndogo sana. So tegemea in the future almost every channel itakuwa ina cost something.

This chinese guys will be suppling scratch cards (like voucher cards). You scratch the card and send hidden codes to a specific short code say 15010 to recharge your account.

TBC is looking into another way to boost their revenue, and that's it.

Kusema kuwa TBC imeuzwa hapa, si kweli! I have worked with TBC since Sep 08, and also with Star Mobile to work out the short code thing and this is what I can say.

I don't mean I am employed at TBC, nonetheless!
 
Mwanahalisi wamefulia tuu

SERIKALI YAUZA TBC KINYEMELA

SHIRIKA la Utangazaji Tanzania (TBC) limeingia ubia na kampuni ya China bila ya kushirikisha Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA), imefahamika.
Aidha, taarifa ambazo gazeti hili limepata zinasema si serikali wala menejimenti ya TBC aliyetangaza zabuni (Expression of Interest) ili makampuni mengine yaweze kupeleka maombi ya kushirikiana na shirika hilo katika mfumo mpya wa utangazaji.
Hivyo kupatikana kwa mbia wa TBC katika maombi ya kusimamia masafa ya kitaifa, kunaelekea kuvunja Sheria ya Manunuzi ya Umma Na. 21 ya mwaka 2004 inayoshurutisha utangazaji wa tenda ili kila anayetaka ashiriki.
TBC imeungana na kampuni ya Star Communication Network Technology Co. Ltd ya China na kuanzisha kinachoitwa sasa Star Media (Tanzania) Company Limited, kwa kuipatia hisa 6,500 huku yenyewe ikibaki na 3,500.
Kila hisa kati ya hizo ina thamani ya dola 100. Star Media imesajiliwa Wakala wa Usajili wa Makampuni na Biashara (BRELA) 26 Juni 2009 na kupewa hati Na. 71639. Imedhaminiwa kwa dola 1 milioni.
Kaimu Mkurugenzi wa PPRA, Ayubu Kasuwi amesema mamlaka yake haijashiriki kwa namna yoyote katika hatua za kuwezesha TBC kuuza hisa zake kwa kampuni hiyo.
TBC inamilikiwa na serikali kwa asilimia 100 na hatua ya kuingia ubia sharti ifuate mlolongo wa taratibu za kisheria, ikiwa ni pamoja na kutangaza tenda.
Kasuwi alisema ofisi yake haina taarifa za kuuzwa kwa hisa asilimia 65 za TBC na kwamba imeanza kufuatilia taarifa hizo.
TBC iko katika mchakato wa kubadilisha mfumo wa utangazaji kutoka analogi (analogue) unaotumika sasa kuingia digito (digital).
Kwa upande wake, Kaimu Msajili wa Hazina, ambaye alitambulishwa na Katibu Muhtasi wake kwa jina moja la Mbelwa, alisema hana taarifa za kuuzwa kwa hisa za TBC.
Hata hivyo, Mbelwa hakuingia kwa undani kuzungumzia suala hilo, badala yake alishauri aulizwe Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TBC, Wilfred Nyachia.
Nyachia ambaye aliteuliwa na Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni kushika wadhifa huo, hakupatikana ofisini kwake wala kwa simu yake ya mkononi.
Katika hali ya kawaida, Msajili wa Hazina ndiye mwenye jukumu la kutunza – kama mwakilishi wa serikali – kumbukumbu za mali na huduma za serikali, mashirika, wakala na makampuni.
Hata hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TBC, Tido Mhando alisema mamlaka zote zinazotakiwa kufahamu mchakato huo, zimejulishwa.
Mhando alisema, “Yeyote anayetaka kujua suala lolote kuhusu ubia wa TBC na kampuni ya kichina, aende kwenye mamlaka hizo.”
Alipong’ang’anizwa kueleza anachokijua, Mhando aling’aka, “Kwani wewe unataka kujua nini hasa? Kama unataka kufahamu jinsi tulivyoungana na kampuni hiyo nenda kwenye mamlaka zinazohusika. Zote zina taarifa… nenda TCRA, BRELA, utaelezwa.”
Taarifa za ndani ya serikali zinasema, kampuni hiyo ya Kichina iliwahi kuomba kuwekeza katika sekta ya habari katika nchi za Uganda na Kenya, lakini ilikataliwa.
“Kama wewe ni mwandishi wa habari kwa nini unafanya kazi kwa kutumia maneno ya mitaani? Tafuta ushahidi ndipo uulize. Kwa taarifa yako ninafahamu kuwa muda si mrefu mwekezaji huyu ataanza kufanya kazi na KBC (Shirika la Utangazaji la Kenya),’” alieleza Mhando.
Mhando aligoma kuelezea utaratibu uliotumiwa kumtafuta mbia, badala yake akasisitiza zifuatwe mamlaka zinazowajibika kusimamia masuala hayo.
“Kwa taarifa yako, hivi karibuni tulikuwa na mkutano Dodoma kujadili suala hilo. Mwenyekiti alikuwa Waziri Mkuu… Nakueleza hayo ili ufahamu kuwa yametekelezwa kwa level (kiwango) hiyo,” alisema.
Kwa mujibu wa nyaraka zilizopo, maombi ya Star Media ya kumiliki masafa ya digito, kati ya asilimia 100 ambazo imeomba kutoka serikalini kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), asilimia 65 zitakuwa za kampuni ya Kichina wakati asilimia 35 ndizo zitakuwa na TBC.
Kwa kadri mambo yalivyo, kampuni hizi mbili tayari zimejihakikishia kupewa masafa kwa pamoja.
Muungano wa Mawasiliano ya Kimataifa (International Telecommunication Union-ITU) unataka kila taifa mwanachama kuhakikisha matangazo yote ya televisheni na redio yanakuwa katika viwango vya digito ifikapo mwaka 2012.
TCRA imewataka wananchi wanaopinga mgawo wa masafa, wapeleke hoja zao kwa Mkurugenzi Mkuu katika siku 14 tangu kutolewa kwa matangazo haya.
Serikali, kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imetenga nafasi tatu tu za kampuni zitakazopewa leseni ya kuendeshea mitambo ya kurushia matangazo ya televisheni kwa viwango vya digito (Digital Television Multiplex Services).
Mpango wa kuhakikisha matangazo yote yanatolewa kwa njia ya digito ulianza kwa kufanya vikao na watangazaji wote mwaka 2005.
Kutokana na mchakato huo, TCRA imegawa leseni za kuendesha mitambo hiyo katika maeneo matatu: Serikali, sekta ya biashara na madhehebu ya dini.
Taarifa nyingine kutoka BRELA zinasema kampuni ya Star Media hisa zake zimesajiliwa kwa mfumo wa dola badala ya shilingi, jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Kaimu Mtendaji mkuu wa BRELA, Noel Shani alikiri kwamba Star Media imesajiliwa kwa kutumia dola badala ya shilingi, jambo ambalo amekiri kuwa ni kinyume cha taratibu.
“Ni kweli, lakini tutawajulisha ili waweze kuja kubadilisha,” amesema.
Taarifa zinasema kampuni waliyoingia nayo haikufanyiwa tathmini (due diligence). Mkataba wake haujachunguzwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wala hakuna Baraka za Baraza la Mawaziri.
Hata hivyo, TCRA inasema haina jukumu la kufuata taratibu za ndani za TBC katika kuunda kampuni au kuingia ubia na kampuni nyingine ya kigeni au ya ndani.
Hata hivyo, kwa TBC kubakiwa na asilimia 35 na kuachia asilimia 65 kwa wageni kumeelezwa kupingana na mapendekezo ya serikali katika sera mpya ya habari, ambayo kama ikipitishwa, wageni hawataruhusiwa kuwa na hisa kubwa katika sekta ya habari kuliko watu wa ndani.
Katika maombi yao ya awali, TBC waliomba peke yao, lakini baadaye wakaingiza wageni hao walioingia nao ubia.

http://www.mwanahalisi.co.tz/index.php?id=622
 
Nimeshindwa kuona uhusiano wa ubinafsishaji wa TBC na memorandum of association iliyowekwa hapo juu. TBC kama taasisi inaweza kuanzisha kampuni tanzu inayojitegemea tu na kwa nia tu ya kuongeza ufanisi katika shughuli zake na kuondokana na bajeti tegemezi kutoka serikali kuu. Na hivyo si dhambi kabisa kwa Tido kuingia in a joint venture na mbia mwingine. Hii ni taratibu za kawaida katika kada ya biashara na uongozi.
 
Nimeshindwa kuona uhusiano wa ubinafsishaji wa TBC na memorandum of association iliyowekwa hapo juu. TBC kama taasisi inaweza kuanzisha kampuni tanzu inayojitegemea tu na kwa nia tu ya kuongeza ufanisi katika shughuli zake na kuondokana na bajeti tegemezi kutoka serikali kuu. Na hivyo si dhambi kabisa kwa Tido kuingia in a joint venture na mbia mwingine. Hii ni taratibu za kawaida katika kada ya biashara na uongozi.


George Mkuchika juzi kaenda public unakumbuka kasema nini ? Kwanza ka kana kabisa juu ya habari hizi mwisho akasema Ubia TBC ina own majority of the shares lakini si hivyo ilivyo hapa kwenye doc.
 
Mkuu majibu yako hapa chini.

Public Multiplexor Operator ni kampuni yoyote ama binafsi ama ya umma ambayo itarusha matangazo ya digital ya taasisi za umma.
attachment.php

kaka kwa hiyo kuna tatizo lakini TCRA hawana tatizo
 
Wafanyakazi TTCL wawapa somo TBC

na Shehe Semtawa


BAADHI ya wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), wamewataka wafanyakazi wenzao wa Shirika la Utangazaji (TBC), kuwa makini na kitendo cha serikali kuanzisha Kampuni mpya ya Star Media (Tanzania) Limited kwa ubia na Kampuni ya Star Communication Network Technology ili kuepuka matatizo ambayo yanaweza kuwapata.
Wakizungumza na Tanzania Daima Jumapili jana, kwa sharti la kutotaka kuandikwa majina yao, wafanyakazi hao walisema imekuwa kawaida kwa serikali kufikia maamuzi mazito kama hayo bila kuwashirikisha wafanyakazi.
Walisema kutokana na uzoefu walionao unaonyesha migogoro hutokea baada ya wafanyakazi kudai haki zao huku menejimenti ikiendelea na mambo yake.
Walisema hawakubaliani na kauli ya serikali kuwa shirika hilo halijauzwa bali ni kuunda kampuni mpya ambayo itakuwa na uwezo wa kutekeleza mabadiliko ya ‘digital’ na kurusha matangazo yake nchi nzima.
“Kama kampuni inachangia 65 wakati TBC inachangia asilimia 35 ambayo inatokana na rasilimali zake na si fedha, unaweza kujiuliza ni kwa nini wasiwe na maamuzi ya kipi kifanyike,” walisema.
Walisema imekuwa ni kawaida kwa serikali kuwashawishi wananchi kwa maneno matamu huku utekelezaji ukiishia katika mazingira ya utatanishi.
Tanzania daima.today;

Pamoja na maelezo yako mazuri toka kwa mdau wa TBC ila sio mwajiriwa,hata TTCL walidanganyika hivyohivyo na baadae jamaa wakageuka na mpaka leo TTCL yabaki yalia.AAAAAAHHHH kumbe TBC atakuwa mteja kwenye kampuni hiyo.Yaani atachomeka chanel zake kama alivyofanya kuchomeka Dstv.
Jamani kuna maswali mingi kuhusu hii sharing na hawa wachina.
 
Sheria ya manunuzi imekiukwa kwa kuwa taratibu za kutangaza zabuni hazijafuatwa. Maafisa mbalimbali wanaotajwa na mh. Waziri sio sehemu ya matakwa ya sheria.
 
Wapo wapi Vyama vya Upinzani kulisema hili...?Wanasubiri GT aseme? au JF...we want them to be ahead ya mambo yanayoendelea.

Bahati Mbaya vyama vyetu vya Upinzani havina wasomi wa kutosha kuweza kukabiliana na kila uozo unaofanyika. Wanasubiri magazeti yaandike, lkn watakuwa hawana watu wa kufanya uchambuzi wa Kina au kufuatilia baada ya Magazeti kuanika uozo huo....!!!

Hii TBC ndio itakayokuja kuwaua Wapinzani kwa matangazo yao...na Hawa wachina ndio Waliocheza mchezo mchafu na CCM kuiba kura za watanzania...2005.."
Leo hii wachina wameiba samaki...Kesi haifanyiki..Ubalozi wa China umewaandikia Barua Wizara husika sheria ichukue mkondo wake...Serikali inapata hasara kuwahifadhi samaki...Kesi haijulikani lini itaisha...
So China tutawapa kila kitu....the so called Wabunge nao "Hovyo"
 
Wapo wapi Vyama vya Upinzani kulisema hili...?Wanasubiri GT aseme? au JF...we want them to be ahead ya mambo yanayoendelea.

Bahati Mbaya vyama vyetu vya Upinzani havina wasomi wa kutosha kuweza kukabiliana na kila uozo unaofanyika. Wanasubiri magazeti yaandike, lkn watakuwa hawana watu wa kufanya uchambuzi wa Kina au kufuatilia baada ya Magazeti kuanika uozo huo....!!!

Hii TBC ndio itakayokuja kuwaua Wapinzani kwa matangazo yao...na Hawa wachina ndio Waliocheza mchezo mchafu na CCM kuiba kura za watanzania...2005.."
Leo hii wachina wameiba samaki...Kesi haifanyiki..Ubalozi wa China umewaandikia Barua Wizara husika sheria ichukue mkondo wake...Serikali inapata hasara kuwahifadhi samaki...Kesi haijulikani lini itaisha...
So China tutawapa kila kitu....the so called Wabunge nao "Hovyo"
Hiyo kampuni sio ya wachina bali ni vigogo wa CCM WAMEGUNDUA kuna haja ya kuwa na chombo chao lakini kwa sababu gharama za kuwa na mtandao nin kubwa na wakati wao wanataka kula sahani moja na Mengi wameamua kudandia. Ujanja huo pia ulitumika wakati wanaanzisha Zain(zamani ilikwa Celtel) SISI tukomae kwani shirika linalomilikiwa na serikali 100% kuingia ubia si ni lazima baraza la mawaziri likae na kupeleka hoja bungeni!

Wajanja hao sie twawajua wataka kujificha kwenye Public Private Partnership(Ithink we dont need it in TBC) .
Hata hivyo inatakiwa Public procurement ili mshindi achue chote.

Nataka kikao cha novemba akina Anna Kilango walikomalie hili kwani maeneo ya PPP yangetakiwa kama vile kule Kiwira na kuchimba Uranium na sio TBC kwani we have people like Star Tv who could help TBC kama wanataka ubia, Mtangazaji wa Redio Tido Muhando huo ni ufisadi tumewabamba nyie na swahiba wako JMK acheni huo upuuzi pamoja na Mkuchika George !!
 
Kwakweli wanatia kichefuchefu, kama kile kipindi chao cha ze komedi ndiyo sikipendi kabisaa, taarifa ya habari yao ndiyo baya kabisa jamani ebu niambieni TV ya Star mimi nawafagilia hawa jamaa wako makini kimtindo
 
Pasco, mambo mengine kama ubunifu simpingi sana Tido pamoja na kuwapo kasoro za hapa na pale katika kubagua watumishi (tatizo hilo lipo sehemu nyingi) lakini kwa hili kuna tatizo kaka. Kwanza kwa chombo nyeti cha umma kama TBC hawakupaswa kwenda haraka haraka hivyo kusajili na kuingia ubia na kampuni nyingine ya nje kwa kisingizio tu cha kukosa mtaji.

Tatizo sisi Watanzania tumezoea kuchukulia kila jambo kirahisi rahisi tu hata mambo mazito kama hili. Tatizo hili linaanzia katika ngazi ya kaya hadi Taifa, inasikitisha sana.

..inashangaza kuona kwamba TBC wamesajili kampuni chapuchapu kwa ubia na Star jambo lililosababisha kufanya hata makosa ya kisheria
Nafanya tuu rejea, na haswa Maneno haya..
"Tatizo sisi Watanzania tumezoea kuchukulia kila jambo kirahisi rahisi tu hata mambo mazito kama hili. Tatizo hili linaanzia katika ngazi ya kaya hadi Taifa, inasikitisha sana".
Kusema ukweli, JF kiboko!.
P.
 

Tido Mhando ambaye alipewa nafasi aliyonayo baada ya kufanyakazi kule BBC SWAHILI aliingia TBC kwa manjonjo yasiyo na kifani na sasa kuna habari kuwa apart from UFISADI uliokuwa unaendelea chini yake pale TBC huyu mheshimiwa amekuwa akinfluence ajira UNFAIRLY na ufisadi ulioipelekea TBC kupoteza mabilioni ya shilingi na hakuna aliyechukuliwa hatua yoyote ile.
Duh!.
P.
 
Dah nilikuwa najiuliza hawa azam tv kwanini hawajui kiswahili, jibu nimelipata asante kwa huu uzi
 
Ahsante JF!
Ni ajabu waliokuwa kwenye uzi wanashabikia kuwa Tido anakosea, leo walivyosikia kapelekwa mahakamani wanasema ccm inamuonea!!!!
Hili kaburi zuri sana wala halinuki, fukueni na mengine tena ya kuhusu Tido et al
 
source The New Times | Rwanda



BY JOHN GAHAMANYI & ALEX NGARAMBE

Star Africa Media, a Chinese company which operates pay TV services in Rwanda is rolling out its operations across other East Africa Community (EAC) countries.

Leo Hao, the company’s Marketing and Sales Director for the Kigali unit said that Star Africa Media last week acquired an operating license to open units in Uganda.

According to Hao, the company has already signed partnership agreements with Kenya Broadcasting Corporation (KBC) and Tanzania Broadcasting Corp (TBC) to provide digital TV services in Kenya and Tanzania respectively.

“Our CEO was in Burundi and we expect to get a license to operate there soon,” he revealed in an interview with Business Times on Friday.

Star Africa Media started operations in Rwanda last year with an initial financial outlay of above $20 million (Rwf11.3 billion).

Hao said investments in each of the three EAC countries of Kenya, Tanzania and Uganda will be higher than what was committed in the Rwandan market.

The media in Uganda on Tuesday quoted Maggie Kigozi, Uganda’s investment Authority Executive Director saying that the company is planning an investment of over $100 million (Rwf56.6 billion) in the Ugandan market.

“We have to think about the whole EAC as one entity. The people strongly relate to each other in terms of culture,” Hao said.

The Shandong province (China)-based company said it will also start delivering broadband internet by wireless means in Rwanda starting next year.

Hao said in an interview that effective July 30, 2009 Rwandan clients will receive a discount of 20 percent on every product purchased including the digital TV sets and the decoder.

The one moth promotion will see clients enjoy a full month without paying subscription fees as well as paying for decoders and TV sets in installments.

However, existing clients have been complaining about poor signal they experience.

“That is sometimes due to the poor signal from channels we broadcast,” Hao explained.

The company covers the analog, digital network and digital TV technology, cooperating closely with world leading technology
providers, equipment manufactures and software developers.

Since the launch of their operations in Rwanda, Hao said Star Media has hit a subscription base of 10,000 clients with a target of 20,000 clients before the year ends.

Company officials say that provision of digital network and digital TV sets is inline with Rwanda’s vision of digitalizing the broadcast media by 2012. It is also partly aimed at fulfilling the agreement of digitalizing the media as agreed between the company and government of Rwanda.
Kumbe hawa wachina sio TBC peke yake...!

East Africa hatutuchomoki kwa hawa wanadamu...
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom