Halisi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2007
- 2,802
- 613
Halisi, kama sheria itakuwa kushoto kwao, je nani anaweza kutengua ubia huu.. TCRA, Bunge au Mahakama ndiyo wanaweza?!
Kwa ninavyofahamu ni kwamba kwa sasa tayari watu kadhaa wamewasilisha pingamizi TCRA kwa mujibu wa sheria, ambako siku ya mwisho ilikua Ijumaa iliyopita. Waliowasilisha malalamiko hayo ni Watanzania wakiwamo viongozi wa Kiislamu ambao nao wana hoja nzito ya kutengwa katika masafa na wengine walioona kasoro hizo.
Lakini kwa maelezo yangu hapo juu, sidhani kama kuna mtu mwenye kuitakia mema nchi hii atakayeendelea na zoezi hili labda iwe ile ile hali ya kusema "This is Made in Tanzania Only" hapo nitaelewa. Kuna mapungufu mengi ya kiutendaji, kisheria na kiusalama ambayo yanalifanya zoezi zima liweze kurudiwa na TBC watapata nafasi ya kujipanga upya kwa kuzingatia maslahi ya umma.
Hapo juu nimezungumzia Waislamu lakini sijasema ni kitu gani. Ukisoma waraka wa TCRA kuna masafa ya aina tatu, ya kwanza ni ya UMMA yaliyopewa TBC na mawili ni ya "KIBIASHARA" ambayo vyombo vya habari vimewakilishwa na MOAT iliyounda kampuni na taasisi za dini zimeunda kampuni chini ya Agape. Sasa Waislamu wameshituka maana walikuwa katika majadiliano na wenzao wa Kikristo lakini kwa bahati mbaya wamejikuta wenzao wamesajili kampuni kinyemela na kupewa masafa na TCRA kwa kigezo cha kuwakilisha taasisi za dini. Sasa Waislamu wamelalamika rasmi na kupinga mchakato mzima kisheria.