Tido Mhando na Ubinafsishaji wa TBC kwa StarTimes

Ukiuliza avaraje Juma wa mtaani kuhusu TBC atakwambia kuwa its useless and its not woth the public funds, cha ajabu for someone like Tido one would have thought kuwa anaeleewa the meaning of PUBLIC SERVICE BROADCASTING lakini wapi!

unatuambia ya kwamba akiulizwa ata averaje juma anaweza ona ni upuuzi mtupu yakuwa hela inachezewa tu, sasa kuna sababu gani ya kuendelea kuigaramia, wakati we mwenyewe kwa maneno yako vipindi vyenyewe havi kuridhishi kwa mtaji huo sio mmoja wa audience yao.

na huyo jamaa alieletwa sijui mtaalam wa media kazi imemshinda basi si ni bora waje watu watakao leta programee zako au wachina wataanza kutangaza kichina?

au tuambie ulikuwa na mapendekezo gani maana uko tayari ata kupelekana nao maakamani hawa jamaa kwa jinsi walivyo kukera ingawa vipindi vyenyewe avi-kuridhishi na avitakiwi kusajiliwa na hela ya serikali kwa kauli zako. unataka kuzua ugomvi tu au una ona ni jinsi gani inaweza kuboreshwa na utuambie wafanyaje?

ps. nasubiri post zako za bandari,ardhi naTRA maana nao pia wanakukera au its only a game to you.
 
Kwa ninavyofahamu ni kwamba kwa sasa tayari watu kadhaa wamewasilisha pingamizi TCRA kwa mujibu wa sheria, ambako siku ya mwisho ilikua Ijumaa iliyopita. Waliowasilisha malalamiko hayo ni Watanzania wakiwamo viongozi wa Kiislamu ambao nao wana hoja nzito ya kutengwa katika masafa na wengine walioona kasoro hizo.

Lakini kwa maelezo yangu hapo juu, sidhani kama kuna mtu mwenye kuitakia mema nchi hii atakayeendelea na zoezi hili labda iwe ile ile hali ya kusema "This is Made in Tanzania Only" hapo nitaelewa. Kuna mapungufu mengi ya kiutendaji, kisheria na kiusalama ambayo yanalifanya zoezi zima liweze kurudiwa na TBC watapata nafasi ya kujipanga upya kwa kuzingatia maslahi ya umma.

Hapo juu nimezungumzia Waislamu lakini sijasema ni kitu gani. Ukisoma waraka wa TCRA kuna masafa ya aina tatu, ya kwanza ni ya UMMA yaliyopewa TBC na mawili ni ya "KIBIASHARA" ambayo vyombo vya habari vimewakilishwa na MOAT iliyounda kampuni na taasisi za dini zimeunda kampuni chini ya Agape. Sasa Waislamu wameshituka maana walikuwa katika majadiliano na wenzao wa Kikristo lakini kwa bahati mbaya wamejikuta wenzao wamesajili kampuni kinyemela na kupewa masafa na TCRA kwa kigezo cha kuwakilisha taasisi za dini. Sasa Waislamu wamelalamika rasmi na kupinga mchakato mzima kisheria.

Mkuchika amethibitisha hili. Kwanza hakujibu hoja hata moja ya msingi, ametoa bla blah na kutaka kupotosha ukweli huku akilalamikia MwanaHalisi kupotosha ukweli huku yeye ndiye anayepotosha ama kupotoshwa
 
TBC haijauzwa-Serikali

Na Grace Ndossa – Gazeti Majira

SERIKALI imesema taarifa zilizotolewa na gazeti moja la wiki hivi karibuni kwamba Shirika la Utangazaji Taifa (TBC) limeuzwa kinyemela ni uzushi.

Hayo yalisemwa jana Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Bw. George Mkuchika ambaye alibainisha kuwa TBC halijauzwa na haitauzwa kamwe.

Alisema kilichofanyika ni kuunda Kampuni Mpya iitwayo Star Media (Tanzania) Limited kwa ubia na mwekezaji aliyeteuliwa kihalali ili kutekeleza mabadiliko ya dijitali (digital) na kuendesha mitambo ya kurushia matangazo yake nchi nzima.

Bw. Mkuchika, alisema kazi hiyo ambayo inatakiwa kukamilika mwaka 2012 ni ya gharama kubwa ambazo TBC isingeweza kuzimudu .

Bw. Mkuchika, alisema shirika hilo litaendelea kuwa la umma na kumilikiwa kwa asilimia 100 na Serikali na Star Media (Tanzania) Limited itakuwa ni kampuni Tanzu ya TBC.

Alisema katika mradi huo Star Media inachangia asilimia 65 na TBC asilimia 35 ambazo inatokana na rasilimia zake na siyo fedha.

"Mradi huu TBC itafanikisha kubadilisha mfumo mzima wa utangaza wa televisheni kuwa dijitali na kusambaza matangazo yake na watangazaji wengine kufika maeneo yote nchini ifikapo mwaka 2012 matangazo ya digitali yatafika kote nchini yakiwemo maeneo ambako hayafiki kwa sasa,"alisema Bw. Mkuchika.

Alisema uteuzi wa mbia ulifanywa na Bodi ya Wakurugenzi ya TBC baada ya tathimini ya kina iliyowashirikisha wataalam kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo Wizara ya mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Costech, Tume ya Mawasiliano (TCRA) na kituo cha Taifa cha Uwekezaji(TIC) kuchambua na kupendekeza mbia anayefaa.

Alisema tathmini ya uwezo halisi wa mwekezaji ilifanywa na wajumbe wataalam wa TBC wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo na kutembelea kampuni hiyo Beijing, China na kuhakiki uwezo wake kabla ya kusaini mkataba.

Mkataba wa ubia uliandaliwa kwa pamoja kwa kushirikisha mwanasheria kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa maandishi kabla ya kusainiwa na mchakato mzima umekuwa wazi na kuhusisha ngazi zote za Serikali Wizara ya Habari Wizara ya Fedha na Uchumi, Wizara ya Mawasiliano Sayansi na teknolojia, Ofisi ya Waziri Mkuu, TIC na TCRA

Alisema hali ya ushindani iliyopo katika sekta hii ndiyo inayosababisha taarifa alizoeleza kuwa zina lengo la kupotosha umma.

Swali langu ni "kama mkuchika anasema serikali itaendelea kumiliki TBC 100%, je, huyo mbia analipwa nini?"

Na je, kama star media ni kampuni tanzu ya TBC ubia ni wa nini? Kwa sababu mimi navyo elewa mbia ameingiza pesa zake na ni lazima apate faida je, faida itapatikana ktk shughuli zipi? matangazo au?

Naomba mwenye uelewa zaidi hii kitu itakavyofanya kazi atuelimishe.
 
Mh! Changa la macho hilo, Yaani anataka kusema serikali haina uwezo wa kubadili mfumo wa analogue kwenda digital mpaka kuwe na UBIA? Naona hii haijakaa vizuri kama watu binafsi wanaweza je serikali inayokamua KODI itashindwa???
 
Kweli bongo nchi tambarare.

Kila mtu anafanya anavyojua kwa kadri awezavyo, kwani nani wa kumuuliza?

Yaani mkuchika anajiuma uma tu, star media inakuwaje kampuni tanzu ya TBC wakati huo huo inatajwa kuwa ni mbia?

hapa bila shaka kuna kaharufu ka ufisadi, kila mwenye nafasi anaboronga tu, hana wasiwasi kwani nani atamuwajibisha? watanzania tumepigwa ganzi, JK mshikaji wake, na kibaya zaidi promota wa ufisadi!!
 
TCRA huko nyuma walitangaza Expression of Interest kualika makampuni kwa ajili ya kutoa huduma za Multiplexxer Operator for Digital Broadcasting. Hii ni Terrestrial transmission Technology ambayo itamfanya mtumiaji wa TV na baadaye radio kupata matangazo yake kwa njia ya Digital. Faida yake ni kuwa matangazo yanakuwa na ubora wa juu na pia masafa yanayotumika (spectrum) ni ndogo kuliko ilivyo sasa kwa Analogue Transmission.

Katika Category ya sasa ya License kuna Content License, katika category hii kuna Radio na TV na Vituo vyote vya Radio na TV wana leseni hii. Leseni hii inawawezesha wenye vituo kuandaa Content na Kuzirusha.

Katika Digital Broadacsting, kuandaa content na kuzirusha kutatenganishwa. Anyaeandaa content hataruhusiwa kuzirusha ili kutoa room kwa fair competition kwa wale wengine watakoataka kuanzisha TV na Radio.

Kwa taarifa tu ni kuwa kwa DSM sasa hivi masafa ya Radio yamejaa na kwa hiyo huwezi kuanzisha Radio Mpya. TV masafa yamebaki machache. Katika Digital Braodacsting masafa yatakuwa mengi na wengi wanaweza kuomba leseni na kufungua vitua vyao vya habari.

Sasa basi katika Digital Broadcasting, Technolojia ya transmission ni tofauti na ya sasa hivi na zaidi ya hayo kujenga Miundombinu (Infrastructure) za transmission ni gharama kubwa sana kwa NCHI NZIMA, hii ni mbali na uendeshaji wake. Ni dhahiri kuwa inahitajika kampuni yenye uwezo mzuri wa kiufundi na kiutendaji.

Katika mfumo wa Fair Play huwezi kuwa Refa na kisha Mchezaji. Hivyo Makampuni yote ya Utangazaji hayakutakiwa kuomba kuwa Multiplexer Operator. Basically kulikuwa kunatakiwa makampuni matatu:
1. One - Public Multiplexer Operator
2. Two - Private Multiplexer Operator.

Defintely kimikakati ingefaa TBC waunde kampuni nyingine ya kurusha matangazo ya Public Broadcastors. So, hii inaweza ikawa sababu ya wao kufanya expression ya kufanya hiyo kazi pamoja. However, this has got nothing to do with CONTENT ambayo ndiyo Core activity ya TBC.

Katika Expression of Interest iliruhusiwa kuwa na partners na katika partners local partner lazima alitain 35% minimum.

Utaona kuwa kampuni kama ITV na StarTV yameungana kuunda kampuni ya Basic Transmission.

Na vile vituo vya kidini kuunda Agape associates Limited

Na TBC na partners kuwa StarMedia Tanzania Ltd.

Sasa hapa kuuzwa kwa TBC kunakujaje wakuu.
 
Nijuavyo Mimi:

Superman you are now talking. However, if issues are not spelt out clearly or kept under capert, rumours are bound to occurs. Many thanx.
 
Jamani hapa wa kulaumiwa sio Tido Mhando ni serikali na viongozi wetu wa juu mafisadi jambo pekee ambalo tunaweza mumlaumu Tido ni kukubali kuingoza TBC katika utawala wa viongozi wetu ambapo wengi ni mafisadi hata uwe na kipaji gani na mipango gani katika utawala huu hutafanya lolote tumemuona Salva Reyemamu baada ya kwenda Ikulu sio yule tuliomzoea nawaurumia watu hawa Tido Salva na wengine wengi ambao wanania njema kwa nchi yetu.Ni imani yangu Tido alikua na malengo ambayo mtoa hoja ameyataja hapo juu kuhabarisha,Burudani na mafunzo n.k.Lakini kwa viongozi wa Serikali na CCM TBC ambayo inaendeshwa kwa kodi ya wananchi ni chombo cha kulinda na kuwasafisha viongozi hao propoganda hivyo vipindi vingi ni vya kuwadumaza wananchi.Ningelitoa ushahuri kwa watu hao kama Tido pamoja na Salva tunafahamu kwamba masilahi muhimu lakini kabala ya kupokea post unabidi ujiulize je naweza kuitumia taaluma yangu katika kulisaidia taifa langu ?Bila kujiuliza swali ili ni sawa nakujiaanda kwenda kuishi saibaria wakati wabaridi ukiwa umevaa fulana na mawazo ya kwamba hutovaa nguo za kujikinga na baridi milele,matokeo yake kufa kwa baridi au kukubali kuvaa nguo za kujikinga na baridi.Haya ndiyo yaliyo tokea kwa Salva na Tido Kama mifano.Kukubali post katika mazingira ya utawala unabidi uukubali ufisadi na kupoteza heshima yako au ujitoe na kulinda heshima yako .MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Thanks Superman kwa maelezo mazuri. Nafikiri Mheshimiwa Mkuchika ingekuwa vema angekuomba umsindikize katika kuelezea hii hoja. Jazba ilimtawala kiasi kwamba ilikuwa ngumu kumuelewa anachosema nini, nikafikiri amejisahau kama Busanda ilishapita ile ni issue tofauti
 
Safi sana Mkuu,

Naamini una uelewa mkubwa wa haya mambo maana ulivyoiweka umeiweka kitaalamu kabisa kusaidia wengi humu. Hoja hapa si kuuzwa kwa TBC ya utangazaji.

Kama ulivyosema mwenyewe hapa kwamba

Katika Digital Broadacsting, kuandaa content na kuzirusha kutatenganishwa. Anyaeandaa content hataruhusiwa kuzirusha ili kutoa room kwa fair competition kwa wale wengine watakoataka kuanzisha TV na Radio.

Kwa hiyo TBC kama TV ya Taifa nayo haitaruhusiwa kurusha na hivyo mrushaji atakuwa Star Media Tanzania Limited ambayo ni ubia kati yake na kampuni ya Kichini ambayo imepewa 65%. Hapa itabidi ueleze vyema kama TBC haitakuwa na mamlaka ya kurusha matangazo na haya masafa ya public - Public Multiplexer Operator- kama ulivyoeleza vyema hapa kwanini yasiwe mikononi mwa Watanzania? Kwanini serikali isianzishe yenyewe kampuni ikamiliki 100% na kutoa fedha? Ni kiasi gani hicho ambacho hao Wachina wamewekeza ambacho serikali haina? Je, kwanini serikali isiwekeze ama Watanzania kupitia soko la hisa wawekeze au taasisi ya umma isiwekeze halafu wakatafuta sasa Wachina/wazungu/waarabu/waafrika kwa tenda ya wazi wenye utaalamu wakawalipa? Bado panahitajika maelezo. Yale yale ya NBC, TTCL, ATC etc. Baadhi ya watu TCRA wanaijua mifano hiyo kwa vitendo.

Katika Digital Braodacsting masafa yatakuwa mengi na wengi wanaweza kuomba leseni na kufungua vituo vyao vya habari.

Hao wengi watalazimika kuchukua kutoka kwa Star Media (wachina wenye hisa kubwa); Basic Transimission Limited ya Mengi (ITV), Nyala (Star TV) na Mhanika (MOAT); na Agape Associates ya mashirika 11 ya Kikristo (hakuna Waislamu wala Wahindu) ambako watalipia.

Katika mfumo wa Fair Play huwezi kuwa Refa na kisha Mchezaji. Hivyo Makampuni yote ya Utangazaji hayakutakiwa kuomba kuwa Multiplexer Operator.

Basicaly hataomba lakini tayari TBC walikuwa na nafasi kama public broadcaster na wangeizisha kampuni ikaitwa TBC Transimission Limited ambayo Msajili wa Hazina angekuwa na asilimia 100 ya hisa.

Basically kulikuwa kunatakiwa makampuni matatu:
1. One - Public Multiplexer Operator
2. Two - Private Multiplexer Operator.

Hapo napo kuna mchemsho sana. Watanzania walikuwa hawajajiandaa kwa hili jambo zito na nyeti ndio maana hata TBC, ITV/Star/MOAT nao wamejitokeza wenyewe bila Channel Ten, C2C, TVZ, Mlimani TV, Abood TV etc japo hao wote wana nafasi ya kulipia hisa na kujiunga na kampuni ya Basic lakini hawataruhusiwa kuingia Star Media (hata TVZ) kama utakuwa umesoma MEMAT kama tulivyoweka hapo juu.

Defintely kimikakati ingefaa TBC waunde kampuni nyingine ya kurusha matangazo ya Public Broadcastors. So, hii inaweza ikawa sababu ya wao kufanya expression ya kufanya hiyo kazi pamoja. However, this has got nothing to do with CONTENT ambayo ndiyo Core activity ya TBC.

Hapa naungana na wewe 100% ndio nasema TBC wangeunda wao kampuni wakamiliki 100% na si kuachia Wachina 65% eti kwa sababu tu sheria ya TCRA inawaruhusu!!!???? HAPANA maana serikali sasa inaangalia uwezekano wa kuunda sera ya kuhakikisha sekta ya habari wageni wasimiliki hisa zaidi ya 35% sasa huu si mfano mzuri hata kidogo kwa TBC yetu jamani.

Katika Expression of Interest iliruhusiwa kuwa na partners na katika partners local partner lazima alitain 35% minimum.

Utaona kuwa kampuni kama ITV na StarTV yameungana kuunda kampuni ya Basic Transmission.

Hata kama wanaruhusiwa wageni kumiliki 65% ina maana hapa wageni wangeruhusiwa 98% TBC ingebaki na 2% hii haingii akilini (japo kwa sasa).

Na vile vituo vya kidini kuunda Agape associates Limited

Hapa hakuna vituo vya kidini ni vya Kikiristo na TCRA hapa wamechemsha japo naamini hawakukusudia.

Na TBC na partners kuwa StarMedia Tanzania Ltd.

Sasa hapa kuuzwa kwa TBC kunakujaje wakuu.

[/QUOTE]

Kuuzwa ni kwamba core bussiness ya utangazaji ni minara na si studio. Unaweza kuwa na studio ya kajichumba kamoja na kwa gharama ndogo sana, lakini huwezi kuwa na minara ya matangazo. Hapa tutafakari kwa makini zaidi.

Jambo la msingi hapa ni kwamba TCRA kama mamlaka husika haijafanya makosa yoyote kwa kuwa imefanya kazi yake vyema kwa kuwashirikisha wadau wote ikiwamo TBC, TV binafsi na zile za kidini hata za Waislamu na hivyo kwa Agape kuchukua jukumu ni matatizo nje ya TCRA kwa kuwa waliweka deadline na waliowahi ndio hao.

Tatizo la Waislamu ni kwamba walizidiwa ujanja na kina Agape na si TCRA na hivyo pingamizi lao limelenga zaidi Agape na kwa hao wengine ikiwamo TBC kwa kuwa wanaamini hawawezi kupitisha matangazo hao huko bali wanataka nao wapewe masafa yao ama Agape ijivunje ili nao waingie upya.

TUJADILI KWA KUANGALIA UTAIFA ZAIDI NA SI KUHAMISHA HOJA KWENDA KWENYE USHINDANI KAMA ALIVYOFANYA MKUCHIKA NA TIDO WAKE ambao wamejielekeza kulijibu MWanaHalisi zaidi na si kuangalia Taifa mbele yao.

Naomba kuwasilisha.
 
nilipomuona anaongea mheshimiwa waziri jana na ameshika gazeti lile nikajua analirudisha kwenye kifungo tena,tushukuru haikutokea hivyo,ila kwa jinsi alivyowasilisha ujumbe wake ilikuwa ngumu kujua anakoelekea,kwakweli kajazba kalimtawala sana mh.
 
Asante Kamanda;

Angalia majibu yangu kwa hoja zako:

Kwa hiyo TBC kama TV ya Taifa nayo haitaruhusiwa kurusha na hivyo mrushaji atakuwa Star Media Tanzania Limited ambayo ni ubia kati yake na kampuni ya Kichini ambayo imepewa 65%. Hapa itabidi ueleze vyema kama TBC haitakuwa na mamlaka ya kurusha matangazo na haya masafa ya public - Public Multiplexer Operator- kama ulivyoeleza vyema hapa kwanini yasiwe mikononi mwa Watanzania? Kwanini serikali isianzishe yenyewe kampuni ikamiliki 100% na kutoa fedha? Ni kiasi gani hicho ambacho hao Wachina wamewekeza ambacho serikali haina? Je, kwanini serikali isiwekeze ama Watanzania kupitia soko la hisa wawekeze au taasisi ya umma isiwekeze halafu wakatafuta sasa Wachina/wazungu/waarabu/waafrika kwa tenda ya wazi wenye utaalamu wakawalipa? Bado panahitajika maelezo. Yale yale ya NBC, TTCL, ATC etc. Baadhi ya watu TCRA wanaijua mifano hiyo kwa vitendo.

TBC ni moja tu kati ya Public Content Providers. Upo uwezekano wa kuwa na Public Content Providers wengine. Mfano, Halamshauri ya Jiji la DSM wameomba leseni ya Content hivyo matangazo yao pia yatapitia katika hawa Multiplexer Operator (Public na siyo Private). Pia kuna distric Councils zingine ambazo zina ama radio ama TV. So kisheria TBC hawakuwa na jinsi yoyote zaidi ya kuunda chombo huru. lakini pia haikuwa lazima TBC kushiriki katika Expression of Interest kwa kuwa mchakato wote ulikuwa ni wa kibiashara. Kulikuwapo hata na arguments kwamba iweje serikali ijiingize katika mchakato wa kibiashara na kuwa haki itatendeka vipi? Hata havyo baada ya kugundulika kuwa siyo TBC wanaoomba leseni bali ni LTD company hilo likawa limetulia.

Hao wengi watalazimika kuchukua kutoka kwa Star Media (wachina wenye hisa kubwa); Basic Transimission Limited ya Mengi (ITV), Nyala (Star TV) na Mhanika (MOAT); na Agape Associates ya mashirika 11 ya Kikristo (hakuna Waislamu wala Wahindu) ambako watalipia.

Mkuu kama nilivyosema huu ulikuwa ni mchakato wa kibiashara ambao ulialika makampuni mbalimbali ya ndani na nje yenye uwezo. Sasa kwa nini hao wengine hawakuomba kwa kweli sijui. Ninachojua TCRA imerudia huu mchakato karibu mara 3 kwa muda wa miaka miwili. Katika Mchakato wa kwanza yaani expression Interest ya kwanza TBC hawakuwepo. Pia si makampuni yote yaliyoomba yalikuwa short listed.

Pia kumbuka pia kuomba leseni TCRA si kupewa. Ila katika hali halisi TBC na wabia wake wanaweza kupewa kwa kuwa serikali lazima iwakingie kifua. Hakuna jinsi. Ukiacha matangazo ya TBC yakapitia kwa Private Multiplexer basi kuna uwezekano wa gharama kuwa juu na hata kuburuzwa katika Media politics.

Basicaly hataomba lakini tayari TBC walikuwa na nafasi kama public broadcaster na wangeizisha kampuni ikaitwa TBC Transimission Limited ambayo Msajili wa Hazina angekuwa na asilimia 100 ya hisa.

Mkuu sina pingamizi na hilo. Cha kujiuliza ni kuwa sheria ya TBC inaruhusu wao kuanzisha kampuni nyingine tena Ltd? Mimi si mtaalamu wa sheria lakini hii ilikuwa ni moja ya hoja za kiushindani katika mchakato ule ili haki itendeke vizuri.

Hapo napo kuna mchemsho sana. Watanzania walikuwa hawajajiandaa kwa hili jambo zito na nyeti ndio maana hata TBC, ITV/Star/MOAT nao wamejitokeza wenyewe bila Channel Ten, C2C, TVZ, Mlimani TV, Abood TV etc japo hao wote wana nafasi ya kulipia hisa na kujiunga na kampuni ya Basic lakini hawataruhusiwa kuingia Star Media (hata TVZ) kama utakuwa umesoma MEMAT kama tulivyoweka hapo juu.

Mkuu hapa ndiyo shida yetu Watanzania ilipo. karibu miaka 3 TCRA wanalizungumza hili lakini bado wa TZ wengi hawalijui. Expression of Interest imetoka mara 2 au 3 kwa miaka miwili. makampuni yamealikwa yalete Proposals zao, wanaojitokeza ni wachache tena mengi makampuni ya nje sasa ni nini kifanyike? Pili hili suala linahitaji utaalamu na experience ya hali ya juu kwa kuangalia nchi ambazo zina mfumo huo wa Digital tayari. So si suala la TBC kujitegemea tu, je inao wataalamu kwa kusupport hiyo infrastructure nchi nzima? Hii ni mbali ya mtaji unaotakiwa ambao kwa makisio ya chini unaweza kuwa si chini ya USD 10 Million (Dola Million Kumi).

Ni dhahiri kuwa wale ambao wana vituo vya TV na baadye Radio wote watapitisha Content zao kwa Multiplexer Operators. Vituo binafsi kwa Private Operators na vile vya Public kwa Public Operators.

Hapa naungana na wewe 100% ndio nasema TBC wangeunda wao kampuni wakamiliki 100% na si kuachia Wachina 65% eti kwa sababu tu sheria ya TCRA inawaruhusu!!!???? HAPANA maana serikali sasa inaangalia uwezekano wa kuunda sera ya kuhakikisha sekta ya habari wageni wasimiliki hisa zaidi ya 35% sasa huu si mfano mzuri hata kidogo kwa TBC yetu jamani.

Mkuu; mimi bado naamini Core Business ya TBC ni CONTENT na si Transmission vinginevyo. lakini hili wacha niwaachie wataalamu waliongelee.

Hapa hakuna vituo vya kidini ni vya Kikiristo na TCRA hapa wamechemsha japo naamini hawakukusudia.

TCRA hawajachemsha. Agape na wabia wao walichofanya ni kuungana ili kuwa na Multiplexer Operator yao. Swali ni kuwa kwa nini Waislamu hawakufanya hivyo? Je waislamu wanaweza kuruhusu matangaza yao yapitie katika Multiplexer Operator inayomilikiwa na Wakristo? Mimi sijui. lakini kama wana hoja ya msingi ya kupinga, kupitia PUBLIC NOTICE niliyoambatanisha katika post yangu hapo juu, wanaweza kuweka pingamizi TCRA.
 
Asante Superman na Halisi, nina swali nadhani ni la kisheria Zaidi

Star Media ni 65% Chinnese and 35% TBC,

Je Kwa Wachina kuwa na majority of share katika hiyo kampuni, je Star Media ni Private Company au ni Kampuni ya Umma ( Public)

Kama ni Kampuni ya Binafsi ( Private), je Ni sahihi kwa Kampuni Binafsi kuwa Public MUX Operator?

Asante
 
Mkuu majibu yako hapa chini.

Public Multiplexor Operator ni kampuni yoyote ama binafsi ama ya umma ambayo itarusha matangazo ya digital ya taasisi za umma.
attachment.php
 
Attachments

  • TCRA Public Notice.jpg
    TCRA Public Notice.jpg
    117.3 KB · Views: 727
TCRA huko nyuma walitangaza Expression of Interest kualika makampuni kwa ajili ya kutoa huduma za Multiplexxer Operator for Digital Broadcasting. Hii ni Terrestrial transmission Technology ambayo itamfanya mtumiaji wa TV na baadaye radio kupata matangazo yake kwa njia ya Digital. Faida yake ni kuwa matangazo yanakuwa na ubora wa juu na pia masafa yanayotumika (spectrum) ni ndogo kuliko ilivyo sasa kwa Analogue Transmission.

Katika Category ya sasa ya License kuna Content License, katika category hii kuna Radio na TV na Vituo vyote vya Radio na TV wana leseni hii. Leseni hii inawawezesha wenye vituo kuandaa Content na Kuzirusha.

Katika Digital Broadacsting, kuandaa content na kuzirusha kutatenganishwa. Anyaeandaa content hataruhusiwa kuzirusha ili kutoa room kwa fair competition kwa wale wengine watakoataka kuanzisha TV na Radio.

Kwa taarifa tu ni kuwa kwa DSM sasa hivi masafa ya Radio yamejaa na kwa hiyo huwezi kuanzisha Radio Mpya. TV masafa yamebaki machache. Katika Digital Braodacsting masafa yatakuwa mengi na wengi wanaweza kuomba leseni na kufungua vitua vyao vya habari.

Sasa basi katika Digital Broadcasting, Technolojia ya transmission ni tofauti na ya sasa hivi na zaidi ya hayo kujenga Miundombinu (Infrastructure) za transmission ni gharama kubwa sana kwa NCHI NZIMA, hii ni mbali na uendeshaji wake. Ni dhahiri kuwa inahitajika kampuni yenye uwezo mzuri wa kiufundi na kiutendaji.

Katika mfumo wa Fair Play huwezi kuwa Refa na kisha Mchezaji. Hivyo Makampuni yote ya Utangazaji hayakutakiwa kuomba kuwa Multiplexer Operator. Basically kulikuwa kunatakiwa makampuni matatu:
1. One - Public Multiplexer Operator
2. Two - Private Multiplexer Operator.

Defintely kimikakati ingefaa TBC waunde kampuni nyingine ya kurusha matangazo ya Public Broadcastors. So, hii inaweza ikawa sababu ya wao kufanya expression ya kufanya hiyo kazi pamoja. However, this has got nothing to do with CONTENT ambayo ndiyo Core activity ya TBC.

Katika Expression of Interest iliruhusiwa kuwa na partners na katika partners local partner lazima alitain 35% minimum.

Utaona kuwa kampuni kama ITV na StarTV yameungana kuunda kampuni ya Basic Transmission.

Na vile vituo vya kidini kuunda Agape associates Limited

Na TBC na partners kuwa StarMedia Tanzania Ltd.

Sasa hapa kuuzwa kwa TBC kunakujaje wakuu.

Mkuu ndo maana niliweka hii thread baada ya kusoma aliyoyasema mkuchika na sikumuelewa, pengine hajui alichokuwa anakieleza kwa wanahabari.

Asante sana nimeelimika ila kama kuna zaidi usione taabu kutuelimisha zaidi.

Wabheja sana nkhoi
 
Hawa watu wasitudanganye kabisa na vijisentence vya ajabu,hapa iko wazi kuwa tbc imeuzwa.Kamahujauza hizo sharing za kazi gani 65% ni ya wachina na mchezo umekwisha.Na wadanganyika wataendelea kudanganyika una 35% halafu unasema hujauza.Ndio yaleyale Celtel ni mtoto wa TTCL sasa yako wapi.
You can full people sometimes but not all times-Bob Marley
 
Sitaongelea suala la kuuzwa ama kutouzwa kwani jana waziri mwenye dhamana katoa maneno makali kukanusha, nguvu aliyotumia jana hakika isingehitajika kama taarifa hizi zingewekwa wazi, ikumbukwe tu kuwa TBC si ya 'watanzania ' pekee bali ni taasisi ya umma wa watanzania na kwa chochote kinachoendelea basi ni vizuri umma ukahabarishwa.

Suala jingine ni namna ambavyo chombo hiki kimegeuka kuwa mdomo mchafu uliojaa uongo na usiotafuta ukweli wa upande mwingine, nitaonesha mfano wa taarifa kuhusu nia ya ZEC kumshtaki Maalim Seif, mwandishi aliyekuwa akimuhoji mtndaji wa ZEC alionesha kana kwamba tayari seif ana hatia na hata maswali aliyouliza yalikuwa ni ya kijinga sana, na kwa kuwa aliwakilisha tbc, sitaki kuesma kuwa tbc ina waandishi wasiotafuta ukweli kwa pande zote. ukirejea suala la habari ya viongozi wa chadema kuwasuta ccm na nec yao kuingilia mamlaka ya spika, mwandishi aliyeripoti taarifa ile hakufanya jitihada za kutengeneza taarifa iliyokuwa na maoni ya pande zote matokeo yake taarifa ya mwenezi wa ccm ikaonekana kama ndo msingi na ukweli halisi. Waandishi wa Tz na hasa hawa wa TBC wanapaswa watambue kuwa habari ni biashara na ni jukumu la TBC kuhabarisha kiusahihi na sio kwa kama redio uhuru ama gazeti la mzalendo.

Mfumo sahihi wa habari hujengwa na umma na kamwe hakuna kichaa atakayedanganya umma hata kama amevaa suti
 
Hawa watu wasitudanganye kabisa na vijisentence vya ajabu,hapa iko wazi kuwa tbc imeuzwa.Kamahujauza hizo sharing za kazi gani 65% ni ya wachina na mchezo umekwisha.Na wadanganyika wataendelea kudanganyika una 35% halafu unasema hujauza.Ndio yaleyale Celtel ni mtoto wa TTCL sasa yako wapi.
You can full people sometimes but not all times-Bob Marley

Malindi, sidhani mambo nia kama hivyo unavyosema.
Hii 35:65 share haihusu TBC, na sio kwamba TBC imeuzwa. Ni kitu kipya ambacho kinaanzishwa na hawa wachina watakua wanauza set-top-boxes ambazo zitakuwa zinatumika kwa ajili ya kudecode broadcasted digital signals. TBC1 ni moja ya channels ambazo zitakuwa available, pamoja na TBC2 ambayo itafunguliwa hivi karibuni kwa ajili ya entertainment (kama Channel 5 hivi). Pia channel nyingine za Asia zitakuwepo pia.

Watakachokuwa wakifanya hawa wachina, na hasa ndio ambapo hiyo 35:65 share ina apply ni ku supply technology (everything including set-top-boxes, broadcasting equipments etc) kwa wateja na TBC.

Sehemu nyingine ni kwenye collection ya fees. Ni vyema kujua kwamba hii huduma haitakuwa bure, utakuwa unalipia kama vile Dstv, isipokuwa rate yake itakuwa ni ndogo sana. So tegemea in the future almost every channel itakuwa ina cost something.

This chinese guys will be suppling scratch cards (like voucher cards). You scratch the card and send hidden codes to a specific short code say 15010 to recharge your account.

TBC is looking into another way to boost their revenue, and that's it.

Kusema kuwa TBC imeuzwa hapa, si kweli! I have worked with TBC since Sep 08, and also with Star Mobile to work out the short code thing and this is what I can say.

I don't mean I am employed at TBC, nonetheless!
 
Back
Top Bottom