Tido Mhando, amtaja Rais Mstaafu Jakaya Kikwete mahakamani

MKURUGENZI Mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando, amedai mchakato wa kulitoa shirika hilo kutoka mfumo wa analogia kwenda mfumo wa dijitali ulitokana na maelekezo ya rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete.

Tido amesema hayo leo Alhamisi Septemba 20, 2018 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, alipokuwa akijitetea kuhusu tuhuma zinazomkabili.

Mtuhumiwa huyo akiongozwa na Wakili wake, Dk. Ramadhani Maleta, amedai TBC kutoka analojia kwenda dijitali, ilitokana na uamuzi wa Kikwete na kwamba alimtaka alibadilishe shirika hilo liwe na hadhi inayostahili na kwamba mchakato huo ulifanywa na bodi ya shirika hilo na kupata baraka za bodi ya zabuni.

Tido anakabiliwa na mashtaka manne yakiwemo ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia serikali hasara ya TSh milioni 887.1.
Kiukweli mgosi yuko poasana kawasaidia watu wengi sana kufika Bbc london,ningekuwa mimi ni Tido nigefungua kituo changu cha habar maana mpaka wkt huo wote kama mtahi jamani alikuwa nao na uzoef ndio usiseme,angefungua kampuni yake cjui kwa nn anapenda kuajiriwa hili jambo ndio lina mcost sana.
 
Kama kikwete alivyotaka kummaliza balozi Mahalu wa Italy kule mahakamani mpk Mkapa akaenda Mahakamani kumtetea then itakua ni zamu ya Kikwete kwenda mahakamani kumtetea tido.

Karma is watching you.
Mahalu maji yashafika shingoni.. ngoja nayeye tumuone
 
MKURUGENZI Mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando, amedai mchakato wa kulitoa shirika hilo kutoka mfumo wa analogia kwenda mfumo wa dijitali ulitokana na maelekezo ya rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete.

Tido amesema hayo leo Alhamisi Septemba 20, 2018 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, alipokuwa akijitetea kuhusu tuhuma zinazomkabili.

Mtuhumiwa huyo akiongozwa na Wakili wake, Dk. Ramadhani Maleta, amedai TBC kutoka analojia kwenda dijitali, ilitokana na uamuzi wa Kikwete na kwamba alimtaka alibadilishe shirika hilo liwe na hadhi inayostahili na kwamba mchakato huo ulifanywa na bodi ya shirika hilo na kupata baraka za bodi ya zabuni.

Tido anakabiliwa na mashtaka manne yakiwemo ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia serikali hasara ya TSh milioni 887.1.
duh!!
 
Kama kikwete alivyotaka kummaliza balozi Mahalu wa Italy kule mahakamani mpk Mkapa akaenda Mahakamani kumtetea then itakua ni zamu ya Kikwete kwenda mahakamani kumtetea tido.

Karma is watching you.
Tafadhali naomba kumuelewa uyo balozi kwa maelezo marefu mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom