Tido Mhando, amtaja Rais Mstaafu Jakaya Kikwete mahakamani

Ketoka

JF-Expert Member
Sep 23, 2015
1,087
1,913
MKURUGENZI Mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando, amedai mchakato wa kulitoa shirika hilo kutoka mfumo wa analogia kwenda mfumo wa dijitali ulitokana na maelekezo ya rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete.

Tido amesema hayo leo Alhamisi Septemba 20, 2018 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, alipokuwa akijitetea kuhusu tuhuma zinazomkabili.

Mtuhumiwa huyo akiongozwa na Wakili wake, Dk. Ramadhani Maleta, amedai TBC kutoka analojia kwenda dijitali, ilitokana na uamuzi wa Kikwete na kwamba alimtaka alibadilishe shirika hilo liwe na hadhi inayostahili na kwamba mchakato huo ulifanywa na bodi ya shirika hilo na kupata baraka za bodi ya zabuni.

Tido anakabiliwa na mashtaka manne yakiwemo ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia serikali hasara ya TSh milioni 887.1.
 
Patamu hapa..... Atakayefahamu tarehe ya Muheshimiwa Rais mstaafu J M Kikwete kupanda kizimbani kwa ushahidi anitonye niende mie nikajionee.
 
Screenshot_20180920-192859.jpg

Zaidi soma hapa.... http://www.mwananchi.co.tz/habari/Tido-amtaja-Kikwete-mahakamani/1597578-4769282-82kuyy/index.html
 
Back
Top Bottom