TID awekwa jela mwaka mmoja

Mpiganaji

Member
Oct 10, 2007
15
0
Breaking news: the famous musician in town TID has been jailed for one year after being convicted on charges of assault.
 
Pole bw.TID
Lakini wakati mwingine hawa vijana wenzangu wanamuziki wa bongo ya fleva wanapenda makuu mno.
Hata kufikia kufanya mambo kienyeji sana.Nawashuri vijana wenzangu wana bongo ya fleva muwe makini sana, msipende kufanya vitu bila kutumia busara.
Anyway bw.TID pamoja na kukupa pole, nakuombea ustahimilivu huko ukonga.
 
Breaking news: the famous musician in town TID has been jailed for one year after being convicted on charges of assault.
....Niliwahi kusoma kwenye gazeti moja kuwa dogo alimtembezea mkono mtu si unajua mastaa wetu wa uswazi!!! akivuma kidogo basi watu hawasemi kitu juu yao acha akaonje joto kidogo huenda adabu itakuja....
 
Belo,
kwani huelewi maana ya assault?
Kama huelewi nisamehe kwa kukupa pole lakini kwa tafsiri yangu ya 'kiingereza cha ugoko' ametiwa hatiani kwa kosa la 'shambulio la mwili' au kudhalilisha.
Hata hivyo hakijaharibika kitu, hapa JF tena!kuna wajuvi wa lugha wamejaa watasaidia kutafsiri hiyo habari kwa lugha mama, lugha adhim ya kiswahili.
 
Dah...

Talent might not get wasted over a year...anaweza toka huko na more conscious music... ila mali zake nyengine ndio utata...

Mwaka ukonga... Hivi siku za Gerezani zinahesabiwa kama siku za kila siku humu Duniani?
 
Belo,
kwani huelewi maana ya assault?
Kama huelewi nisamehe kwa kukupa pole lakini kwa tafsiri yangu ya 'kiingereza cha ugoko' ametiwa hatiani kwa kosa la 'shambulio la mwili' au kudhalilisha.
Hata hivyo hakijaharibika kitu, hapa JF tena!kuna wajuvi wa lugha wamejaa watasaidia kutafsiri hiyo habari kwa lugha mama, lugha adhim ya kiswahili.

I know it but nilikuwa nataka kujua ni wapi na lini
Jamaa kuna wakati alikuwa na kesi ya kubaka akashinda ,inaonekana jamaa alikuwa na usongo wa kwenda jela
 
Duu, TiD.
Nimekuwa nasoma vituko vya jamaa. Huku kapiga picha na Wema Sepetu na kuziweka mtandaoni, hakulipa hela ya MINIBAR huko alikolala, kapigana, katukana nk. Naona alikuwa anaitafuta sena JELA. Naona hadi JELA imesema " ehh, kijana ngoja nikuruhusu uingie kwangu maana umesota sana kutaka kufika humu ndani.."
USIPOZIBA UFA, UTAJENGA UKUTA. Sijui akitoka huko atakuwa kajenga ukuta au ataamuwa kwa hasira kuwa HOMELESS.....
 
Mpiganaji
Hujamalizia hii habari,isije ikawa kama ile kesi ya Wilfred Lwakatare bukoba kwamba afungwa jela,kumbe si kile cha keko wala segerea bali kifungo cha nje.
 
Amefungwa jela Mwaka mmoja na Mahakama moja ya Mwanzo Kariakoo baada ya kutiwa hatiani kwa kumshambulia mkazi mmoja wa Dar Khalid Mohamed.

Haijulikani kama amekwenda Jela ama atalipa faini, lakini kwa kawaida Kosa kama hili mfungwa hupewa nafuu ya adhabu kwa kulipa faini na hasa kama utendaji wake wa kosa ni Mara ya Kwanza.

Lakini kama rekodi ndivyo inavyotaka kuoneshwa,atakuwa amekwenda jela maana anasifa ya kupiganapigana na aliwahi kuonywa, hata wakati wa Kili alitoa sambusa za makonde.

Ila kwa kawaida mahakama, huwa haioni umuhimu wa kumfunga mtu kwa kosa kama hili
 
Nimekupata Belo.
Nadhani mpiganaji atupe habari timilifu, kama alivyouliza Belo.
Au kama kuna mtu yeyote mwenye taarifa kamili za hiyo kesi na hatimaye hukumu aimwage hapa jamvini.
 
breaking News: The Famous Musician In Town Tid Has Been Jailed For One Year After Being Convicted On Charges Of Assault.

Kaka Malizia Hiyo Story Utupunguzie Maswali, Kifungo Cha Nje Au Ndani.?.

Au Source Wako Hakukueleza Zaidi.
 
ni kwamba huyu bwana amefungwa jela Mwaka mmoja na Mahakama moja ya Mwanzo Kariakoo baada ya kutiwa hatiani kwa kumshambulia mkazi mmoja wa Dar.

Haijulikani kama amekwenda Jela ama atalipa faini, lakini kwa kawaida Kosa kama hili mfungwa hupewa nafuu ya adhabu kwa kulipa faini na hasa kama utendaji wake wa kosa ni Mara ya Kwanza. ila kwa rekodi yake anasifa ya kupiganapigana na aliwahi kuonywa.

Ila kwa kawaida mahakama, huwa haioni umuhimu wa kumfunga mtu kwa kosa kama hili
 
Habari nilizozipata Punde toka chanzo cha uhakika inadai kuwa uyu bwana alishitakiwa kwa tendo la kushambulia.. sasa taarifa ilivyokuja mwanzo ilisema amehukumiwa Kifungu cha mwaka mmoja au Kiasi flani cha Pesa kama faini..kwa hiyo anahaki ya kuchagua..watu wakapumua wakijua jamaa atatoa hela tu kama faini mziki utaendelea kama kawaida..sasa habari nilizozipata Punde nizakusikitisha..Jamaa hajapewa option ya faini wala nini ni kwenda kunyea ndoo mwaka mzima..... !!!! maskini bishoo yule..!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom