TID awekwa jela mwaka mmoja

hiyo ndio faida ya kubwia unga..huyu nae si teja bana watu wanajua..yeye na kile kidada Ray c wanakula unga kama hawana akili nzuri
 
kumbe kweli?????????

TID afungwa jela mwaka mmoja


Na Rehema Maigala

MSANII mahiri wa muziki wa kizazi kipya nchini Khalid Mohammed a.k.a TID (26), mkazi wa Kinondoni, Dar es Salaam, amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la shambulio.

Msanii huyo maarufu nchini alijikuta akishika kichwa ghafla jana baada ya kumsikia Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Hamisa Kalombola akisoma hukumu hiyo ambayo haikuwa na faini wala fidia.

Baada ya hukumu hiyo, msanii huyo alishikwa kwa umakini na askari magereza kwa ajili ya kupelekwa chumba cha mahabusu ili kusubiri safari ya kwenda gerezani.

Muda mfupi baadaye TID, alitolewa nje ya chumba cha mahabusu, huku akiwa ameshikwa mkono na ndugu zake wakisaidiana kumvua shati, kwani ilionekana kama amepata presha ya ghafla kutokana na hukumu hiyo, ambapo ndugu zake pamoja na marafiki walionekana na nyuso za huzuni.

Mlalamikaji katika kesi hiyo, Ben Mashibe alileta mashahidi wanne katika Mahakama hiyo, ambao wote kwa pamoja walielezea jinsi mshitakiwa alivyompiga mlalamikaji na kumsababishia maumivu makali kichwani.

Mshitakiwa alidai yeye ana shahidi mmoja, hata hivyo alishindwa kumleta mahakamani kwa kuwa alikuwa safari, ambapo jana kabla ya kutoa hukumu, Hakimu Kalombola alimtaka mshitakiwa ajitetee ili mahakama impunguzie adhabu na katika utetezi wake alidai ana familia inayomtegemea hasa mama yake mzazi.

Awali ilidaiwa mahakamani hapo kuwa Julai mwaka jana, mshitakiwa alimshambulia mlalamikaji kwa kumpiga na trei ya bia kichwani walipokuwa Masaki Slip Way jijini Dar es Salaam na kumsababishia maumivu makali.
 
Sawa Mkuu Field
Labda Kwa Kuongezea Kituko Kingine Cha Huyu Bwana\

Siku Moja Nilikuwa Naenda Misri..nikapitia Nairobi,tukiwa Tunakaribia Kushuka Tukagongana Folen Ya Chooni
Jamaa Wkatuambia Aiwezekani Muda Umeisha Saa Ya Kufunga Mikanda Jamaa Akanganagania Sana Alipoingia Chooni Amini Usiamini Wakati Anatoka Alipakaza Mavi Kwenye Ndege Kule Chooni,,alivo Mshenzi Akapaka Mpaka Sehemu Ya Kukalia...kutokana Na Kuzidiwa Ikawa Wakwanza Kwenda Nkamuuliza Muhudumu Akasema Ametoka Yule Kaka ,,,duh Jamani Mavi Yote Yalirudi Ndani Mpaka Airport Toilet....nafikiri Hii Itamfundisha
Big Up Akim
Pole
Wema Sepetu Ndio Maisha Ulikuwa Namnyama
 
Anatoka Alipakaza Mavi Kwenye Ndege Kule Chooni,,alivo Mshenzi Akapaka Mpaka Sehemu Ya Kukalia...kutokana Na Kuzidiwa Ikawa Wakwanza Kwenda Nkamuuliza Muhudumu Akasema Ametoka Yule Kaka ,,,duh Jamani Mavi Yote Yalirudi Ndani Mpaka Airport Toilet....nafikiri Hii Itamfundisha

kwi! kwi kwi! kwi!
Basi kule anaenda kukibeba sasa kwenye ndoo au kufukua mitalo ya nnyaa iliyoziba.Alafu naomba wampe nguo za wafungwa zile zilizo chakaaaa mpaka huku kwenye makalio si iwa unaona wafungwa wengine wana jezi zimechakaa sana sasa huyu jamaa hapewi mpya kutokana na ubishoo wake atapewa chakavu tu tena kwa maksudi yeye si superstar jmosi/jpili nenda segerea kamwangalia utaona wiki tu atakuwa kanyoloswa huyu anaenda kukutana na wanaume wababe bora asipokee ugali wa mtu maanake atakacho pata sijui kama atamsimulia huyo Siwema.
 
Amefungwa jela Mwaka mmoja na Mahakama moja ya Mwanzo Kariakoo baada ya kutiwa hatiani kwa kumshambulia mkazi mmoja wa Dar Khalid Mohamed.

Khalid Mohamed ndiye TID umesababisha nianze weekend mapema maana nimecheka sana, kwani ni nadra sana mtu kujishambulia mwenyewe halafu akajipeleka mahakamani na kuhukumiwa.
 
Dalili za huyu msanii kuishia pabaya zilionekana kitambo kidogo!! Alilewa sifa na kusahau kwamba yeye ni kioo cha umma. Hukumu ya ke ni sawa ila imechelewa, Angeanza Dudu Baya kabisaaa kipindi kile.

In addition, nadhani ana maadui wengi ndio maana hata hukumu yake ikawa ya haraka bila mswalie mtume

Bado Mafisadi, Vijoo kwekwe na wengine wengi
 
Kwanza nampa pole sana huyu kijana. Pili, adhabu aliyopata ni nafasi nzuri ya kumkumbusha jukumu lake la kujichunga mwenendo wake na tabia yake, aache visingizio visivyokuwa na mantiki vya kudai alikuwa amelewa. Kulewa sio hoja inayoweza kuhalalisha kitendo chochote cha kudhalilisha utu wa mwingine. Lakini la tatu na muhimu sana ni huu msongamano wa wafungwa magerezani. Nadhani huu ni mfano mmojawapo wa aina za kesi zinazotujazia wafungwa magerezani wakati adhabu mbadala zipo. inafaa kurejea na kutazama upya mazingira ya matumizi ya aina mbalimbali za adhabu kwa wanaotiwa hatiani, na kutafuta suluhisho la kupunguza msongamano magerezani bila kuathiri haki za waathirika wa uhalifu.
 
huyu jamaa hapewi mpya kutokana na ubishoo wake atapewa chakavu tu tena kwa maksudi yeye si superstar jmosi/jpili nenda segerea kamwangalia utaona wiki tu atakuwa kanyoloswa huyu anaenda kukutana na wanaume wababe bora asipokee ugali wa mtu maanake atakacho pata sijui kama atamsimulia huyo Siwema
Sasa unafurahia nini? wabongo kwa kuombeana mabaya hatujambo.....
 
Angeanza Dudu Baya kabisaaa kipindi kile.
Hili lijamaa jela ndio mahala pake pa kuishi......kuna wale wanaojiita magangsta Kikosi cha Mizinga wale nao ovyoooo!
 
mimi namsikitikia sana TID, japokuwa wengi wako against him sijui ni wivu ama nini, lakini alikuwa mwanamziki mzuri ambaye in one way or another alitangaza nchi kwa miziki yake mizuri.namuombea amalize kifungo chake haraka akiwa mzima wa afya na atoke aendelee na nyota yake.
on the contrary, ni vizuri kuona majaji wa bongo hawana upendeleo kama majaji wa ulaya,kwahiyo iwe fundisho kwa bongo stars kuwa na adabu wakiwa mitaani.
 
Hili lijamaa jela ndio mahala pake pa kuishi......kuna wale wanaojiita magangsta Kikosi cha Mizinga wale nao ovyoooo!

Bora akaanzishe bendi nyingine huko Jela. Kikosi cha mizinga hovyo sana wale bado zamu yao. wasanii wetu hawa wakipata vihela kidogo tu basi ukorofi kibao. hii ndo fundisho kwao. Mapozi yote ya TID kwishaaaaaaaaaa kazi
 
mwisho wa siku eti anadai "oooh naomba mnisamehe coz nina mama mzee ananitegemea"...
sasa kabla hajafanya huo uharo wake hakujua kuwa kuna bi mkubwa anamtegemea?
kweli wahenga wanasema starehe ya siku moja hukupa majuto ya daima.
 
Hili lijamaa jela ndio mahala pake pa kuishi......kuna wale wanaojiita magangsta Kikosi cha Mizinga wale nao ovyoooo!

kikosi wanakuwa hovyo kwa sababu gani?
unaweza kunipa sababu?
au kwa vile hawabani pua?
 
Mara nyingi makosa ya jinai yatokanayo na ulevi yakishajirudia huhukumiwa kifungo cha moja kwa moja ikiwa namna moja ya kumfundisha mkosaji aachane na ulevi. Ni afadhali bwana mdogo huyu angesema kuwa alipatwa na hasira za ghafla baada ya kuvunjiwa heshima hadharani na mlalamikaji.
 
kikosi wanakuwa hovyo kwa sababu gani?
unaweza kunipa sababu?
au kwa vile hawabani pua?
Mkuu unawajua Kikosi kweli? na kiongozi wao Kala Pina?........bora ya wabana pua(Marlaw,Ali kiba,matonya etal) wanaingiza pesa kwa kubana pua zao kuliko hao wanajifanya magangsta kwa kuiga enzi za west coast na east....hailipi hiyo....

Sikiliza kibao cha Madee(Hip hop hailipi)....wakati naandika haya nasikiliza Cinderela toka kwa Ali kiba
 
Mkuu unawajua Kikosi kweli? na kiongozi wao Kala Pina?........bora ya wabana pua(Marlaw,Ali kiba,matonya etal) wanaingiza pesa kwa kubana pua zao kuliko hao wanajifanya magangsta kwa kuiga enzi za west coast na east....hailipi hiyo....

Sikiliza kibao cha Madee(Hip hop hailipi)....wakati naandika haya nasikiliza Cinderela toka kwa Ali kiba

kwa hiyo unawashauri wanaume wabane pua coz ndo dili?
je unamjua jim reeves, au hata don williams? au ulikuwa mdogo enzi zao?
hawa jamaa hawakuwahi kubana pua na still dunia inawakumbuka.
ok na je mbona prof J, FA, AY hawabani pua na wanaingiza $ kuwashinda wao?
na ni wabana pua wangapi ambao nyimbo zao ni uharo na hata hawasikiki ambao mauzo yao yamepitwa hata na ya kikosi?

kumbuka wahenga wanasema debe tupu ndo linalopiga kelele.
wasalimie wabana pua wenzio
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom