Ticha gani wa twisheni ulikuwa unamkubali sana

Kati ya walimu niliopata kuwakubali basi Marehemu Kazibure alikuwa anawashinda wote! Alinifanya nione Physics ya Advance sio somo gumu kabisa. Kizuri zaidi alikuwa anakupa mwanafunzi nafasi ya kufikiri sio kukulisha tu. Kwakweli alikuwa mwalimu bora wa Physics kwa wanafunzi wanaojiandaa kusoma Engineering.

Mwl Kazibure alikuwa hatari kwa Physics Tanzania nzima. Maprifessor wengi wa Engineering vyuo vikuu na hasa UDSM walifundishwa naye Kibaha. Pia Edgar Tenga ( Mechanical Engineer na Rais Mstaafu wa TFF ) alifundishwa Physics na Kazibure Kibaha miaka ya 70 !
 
Nilikutana na mwehu mmoja wa economics *(jina nalihifadhi) kaishia kunitamani na kunitogoza. Nilimwahidi nitakupa baada ya likizo kuisha nikasepa. Hadi leo sitaki hata kunwona

Uliahidi kumpa nini? Hela za tuition au!
 
sh
Katika historia yangu nilisoma tuition advance tu tena advance math sababu mwalimu wetu alikuwa kilaza na internet ilikuwa tatizo

Mwaramy nampata ndio wa mwanzo kusoma kwake ,jamaa anashuka ile mbaaaya

Ila kwa mwara nilisoma mara moja tu

Kwa math kuna mtu anaitwa engineer huyo nampa salute zangu zote ,jamaa hakunaga anakushukia complex,differential nk kutoka kichwani ,mpelekee swali lolote anakushukia na uzuri mnaweza kuwa wawili au 3 au prkee yako tu kwahiyo upo free kumuuliza na kujadiliana ,yupo zake nje na meza yake ..kama unatatizo lako la mechanics, physics ,pure mtafute hiki kichwa anakushukia kutoka kichwani

Watabe wa Advance math

Engineer ,mwara ila engineer namuweka mwanzo
shaharani?
 
Kila mwanafunzi lazma kuna ticha wa twit anaye au aliyemkubali kinoma!..wakati wa analogy kulikuwa na akina mkandawile,kazibure na mama shija! Digitali nayo ina wakali kama muddy physics 'kamshana'

huyu jamaa nilikuwa namkubali sana kuanzia o level had a level hebu na wewe tiririka matcha wa twit uliowakubali either wa analogy or digital era! g!
Sintasahau ule upaja wa yule mwalimu anayeitwa ... Na kale kasauti kake.Juzi mwaka Jana nimekutana nae ila ...
 
Kuna bwana mmoja pale mchikichini alikua anaitwa yasini, MZEE WA KISWAHILI, naona humu kila mtu anajifanya kasoma physics.
 
Back
Top Bottom