TIC, TAN-TRADE, EPZA, TTB & BRELA: Mrundikano wa Taasisi zinazofanya kazi zinazofanana

Andrew123

JF-Expert Member
Jun 2, 2012
6,988
8,497
Nimekaa nikafikiri hapa TZ tuna taasisi nyingi za Serikali kuanzia
1. Tanzania Investment Centre (TIC) vs EPZA vs BRELA,
2.Tanzania Tourist Board (TTB) Vs TANTRADE,
3. Tanzania Employment Services Agency (TaESA) vs Public Service Recruitment Secretariat

Nyingi ya hizi taasisi zinafanya kazi almost sawa na sioni logic ya kuwa nazo zote. Ningependekeza zipunguzwe katika kubana matumizi na kuongeza ufanisi. Vinginevyo kuifanya Tanzania Middle Income country by 2025 itakuwa ni ndoto.
 
Acheni hizo jamani mnataka sisi tukale wapi? kila mwaka tunapiga safari si chini ya 5 nje ya Tanzania (Kujifunza, semina na makongamano) kila baada ya miaka 3 tunapata mgao wa magari mapya, kasha tunauziana hayo ya "Zamani" ukitaka ufanisi kafungue kampuni wewe na mkeo si huku TIC wala TAN-TRADE.
 
andreakalima

Tanzania ni mwendo wa kuchuma, baadae ndo wanavutagana wenyewe kila mmoja anataka awe juuvya mwingine!

Kuna TFDA, TBS, Mkemia mkuu, pharmacist association nini sijui nao walishakuwa na mgogoro na TFDA kwa mwingiliano wa kazi. kuna mwingiliano wa kimaslahi kati ya Shirika la petrol na Eruwa hiii nayo ilitakiwa kuunganishwa na kuongeza idara badala ya sasa kuwa na mrundikano wa taasisi ambao mwisho wa siku ni mzigo tu.
 
Nyingine ni Tanzania Commission for Universities (TCU), National Accreditation Council for Technical Education (NACTE) & Vocational Education & Training Authority (VETA).Wote na-deal na post-secondary education lakin wazee wakaona ngoja waunde sehemu za kutafuna posho za safar na vikao mfano VC wa Ardhi University, Member wa bodi TCU, NACTE & VETA. Tanzania Oyeeeeeee.
 
Jamani kuwa na taasisi nyingi siyo jambo baya. Kwanza inaleta ufanisi na pili inaongeza ajira. Baba zenu, kaka na dada zenu, wadogo zenu n.k wanafanya kazi huko. Kama zisingekuwepo wangepata kazi wapi? Pili kazi ya serikali siyo kupunguza matumizi.

Sasa ipunguze matumizi ili iweje. Kazi ya serikali ni kuhakikisha pia wananchi wake wabapata kipato cha kuspend ili mzunguko wa fedha uendelee na maisha yaendelee.

Serikali leo ikisema inaelekeza fedha zote kwenye muradi ya elimu na afya tu watu kibao wataathirika hata waliojiajiri na walioko kwenye private sector
 
Dar es Salaam Institute of Technology, Arusha Techinical College, National Institute of Transport, Mbeya Tech (sijui sasa inaitwaje) nazo hizi zinafanya kazi inayofanana zingefanywa taasisi moja
 
Jamani kuwa na taasisi nyingi siyo jambo baya. Kwanza inaleta ufanisi na pili inaongeza ajira. Baba zenu, kaka na dada zenu, wadogo zenu n.k wanafanya kazi huko. Kama zisingekuwepo wangepata kazi wapi? Pili kazi ya serikali siyo kupunguza matumizi. Sasa ipunguze matumizi ili iweje. Kazi ya serikali ni kuhakikisha pia wananchi wake wabapata kipato cha kuspend ili mzunguko wa fedha uendelee na maisha yaendelee. Serikali leo ikisema inaelekeza fedha zote kwenye muradi ya elimu na afya tu watu kibao wataathirika hata waliojiajiri na walioko kwenye private sector

Wewe unafurahia kodi yote iishie kwenye mishahara badala ya kutuletea maendeleo?
 
Mbona ya kawaida tu hayo Wakuu. Hebu geuzieni macho kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii: PSPF, GEPF, PPF, LAPF, NSSF na mwingine nimeusahau .... Juu ya wote hao kuna "Mama yao Mlezi" SSRA!

N.b: Huko Nchi jirani ya Zanzibar hakuna ka-Mfuko ka Hifadhi ka Jamii kengine kanakopiga mihela vilevile kama hawa Dada zake hapo juu?
 
Tanzania ni mwendo wa kuchuma, baadae ndo wanavutagana wenyewe kila mmoja anataka awe juuvya mwingine!

Kuna TFDA, TBS, Mkemia mkuu, pharmacist association nini sijui nao walishakuwa na mgogoro na TFDA kwa mwingiliano wa kazi. kuna mwingiliano wa kimaslahi kati ya Shirika la petrol na Eruwa hiii nayo ilitakiwa kuunganishwa na kuongeza idara badala ya sasa kuwa na mrundikano wa taasisi ambao mwisho wa siku ni mzigo tu.

Kiukweli issue ya TBS na TFDA ni michanganyo...!
 
Kwenye Elimu nako vipi? Waalimu wanaajiriwa serikali na local Gov. at the same time
 
Hapo hapo kuna DUCE, MUCE na UDSM School of Education wote wanatoa/wanafundisha walimu but kila taasisi ina mkuu na ana entitlement zote kuanzia V8/Vx mpya, posho na kuwekwa kwenye bodi kibao za kutafuna pesa safari kila kukicha
 
Hapo hapo kuna DUCE, MUCE na UDSM School of Education wote wanatoa/wanafundisha walimu but kila taasisi ina mkuu na ana entitlement zote kuanzia V8/Vx mpya, posho na kuwekwa kwenye bodi kibao za kutafuna pesa safari kila kukicha
Tunakoelekea Huko mtashauri hata shule za msingi na secondari ziunganishwe na Kuwe na shule moja tu Tanzania nzima.

Point yangu iko pale pale, taasisi moja Kubwa is un manageable na inakuwa na ukiritimba. Moja ya Njia ya kuondoa ukiritimba na kuleta ufanisi ni kuvunja na kutengeneza multiple organization Amazon zitashindana zenyewe kwa zenyewe na hi yo kuleta ufanisi.

Nafikiri mnaona minis sasa hivi jinsi mifuko ya jamii inavyo chacharika.
 
Huu ni ujanja ujanja wa kupeana vyeo sidhan hata kuna Performance Review baada ya kipindi kupima utendaji wao
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom