Tibu magonjwa mbalimbali kwa kutumia ukwaju

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,907
6,700
Ukwaju ni tiba ya magonjwa mbalimbali, leo tujaribu kuona faida zake

Majani ya ukwaju yanatibu fangasi, kusafisha kibofu cha mkojo na kutibu maumivu ya viungo.

Magome na mizizi yanatibu tatizo la kukosa choo, matatizo ya tumbo na tumbo kujaa gesi.

Tunda la ukwaju huondoa kemikali sumu, lehemu mwilini na kutibu tatizo la mmeng'enyo, pia inaua bacteria na kuzuia wadudu wasikae katika ngozi.

Ukwaju hutibu homa za mara kwa mara

MATUMIZI

Kunywa juice ya ukwaju usiweke kabisa sukari wala juisi yako usiisage kwa blenda

Kwa ajili ya kuunga sehemu iliyovunjika fanya kuchukua juisi ya ukwaju changanya na mafuta ya ufuta weka jikoni ipate uvuguvugu kisha toa jikoni, chukua dawa uliyoiandaa kandia sehemu iliyovunjika asubuhi na jioni kwa muda wa siku saba utapata matokeo mazuri.

Kutibu Ngiri
Chemsha majani ya ukwaju kunywa kutwa mara tatu kwa siku sita utaona matokeo

Kutibu maumivu ya sikio
Weka vitone viwili vya juisi ya ukwaju maumivu yatakata.

Kuwashwa mwili au vipele mwilini
Pondaponda majani ya ukwaju, pakaa sehemu yenye matatizo utapata nafuu mapema

Mwili kutoa harufu mbaya
Chukua ukwaju ulainishe vizuri kisha pakaa kwapani, sehemu za siri na sehemu zozote zinazoa harufu kwenye mwili wako

Kupunguza uzito na unene
Kunywa glass mbili za juisi ya ukwaju kila asubuhi nawe utapunguza uzito na unene.

Upungufu wa nguvu za kiume
Kunywa juisi ya ukwaju asubuhi na jioni ndani ya siku 14 utaanza kupata raha ya tendo la ndoa

Kuteguka
Chukua juisi ya ukwaju changanya na chumvi ya mawe kisha pakaa sehemu iliyoteguka ndani ya siku tano utapata nafuu kubwa inshaallah.

Ukwaju una faida nyingi sana ndani ya mwili wa binadamu kwa hiyo tunashauriwa kutumia juisi yake bila sukari, majani yake na mizizi yake mara kwa mara sababu ukwaju unatukinga na magonjwa mbali mbali.

Pia kwa watu wa imani wanaamini ukwaju huondoa nuksi.

KAMA UNA TATIZO LA VIDONDA VYA TUMBO JUISI YA UKWAJU HAIKUFAI

ANGALIZO: Ukwaju naouzungumzia hapa ni ukwaju asilia sio ukwaju wa Azam wa kwa Bwana Bakhresa! Hakikisha unatumia ukwaju asilia.

FB_IMG_1622749703652.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom