Tibaijuka unafiki atupendi kesi kibao ziko ofisini kwako unazikimbia za viwanja ..acha unafiki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tibaijuka unafiki atupendi kesi kibao ziko ofisini kwako unazikimbia za viwanja ..acha unafiki

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Dec 15, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, amewarejeshea wamiliki halali nyumba ya Wakfu wa Msikiti iliyoporwa na wajanja wachache kwa miaka 21 iliyopita, huku akiwataka watu wanaojimilikisha nyumba na viwanja kwa njia za utapeli, kuacha tabia hiyo mara moja, vinginevyo watashughulikiwa bila kuangaliwa usoni.
  Nyumba hiyo ambayo ilitolewa Wakfu na marehemu Hajati Aziza Omar kwa Msikiti wa Mwinyi, ulioko Ilala, iko kwenye Kitalu namba 77, Kiwanja namba 32, Mtaa wa Somali, Kariakoo, jijini Dar es Salaam.
  Profesa Tibaijuka alitoa onyo hilo wakati akikabidhi hati ya kiwanja cha nyumba hiyo kwa wadhamini wa msikiti huo jijini Dar es Salaam jana, ambao walisaini hati hiyo mbele yake katika hafla fupi ya makabidhiano ya hati hiyo.
  Alisema matatizo ya watu kujimilikisha nyumba na viwanja kwa njia za utapeli, yamekuwa mengi nchini na kwamba, aliyejimilikisha kiwanja cha nyumba hiyo, alitumia mwanya huo kutokana na ucheleweshaji wa umilikishaji.
  Aliwataka viongozi wa dini kuwa macho na kulinda mali za misikiti na makanisa dhidi ya uporaji unaoweza kufanywa na matapeli hao.
  “Tusipokuwa macho, watu hao watajimilikisha, kwani tatizo hili haliko hapa tu, lipo sehemu nyingi,” alisema Profesa Tibaijuka, ambaye katika hafla ya makabidhiano ya hati hiyo jana, aliongozana na Kamishna wa Ardhi, Anna Mdemu na Msajili wa Hati, Subira Sinda kutoka wizara hiyo.
  Aliongeza: “Watu hao kama wapo waache. Mchezo umekwisha. Wizarani hatuangalii usoni, tunaangalia haki.”
  Kabla ya kuhutubia na baadaye kukabidhi hati hiyo, Profesa Tibaijuka, aliwaomba viongozi wa Kiislamu, waumini na watu wote waliohudhuria hafla hiyo, kusimama kwa dakika moja kumkumbuka marehemu Hajat Aziza aliyetoa nyumba hiyo itumike kwa maslahi ya msikiti huo. Awali, Imamu Mkuu wa Msikiti huo, Sheikh Abeid Maulid, alisema kiwanja cha nyumba hiyo kiliporwa mwaka 1991 ikiwa ni siku chache baada ya Hajat Aziza kufariki dunia.
  Alisema baada ya hapo walianza jitihada mbalimbali kukomboa kiwanja hicho, ikiwa ni pamoja na suala hilo kulifikisha kwa Rais Jakaya Kikwete, ambaye aliwarudisha kwa Profesa Tibaijuka.
  Sheikh Abeid alisema wanamshukuru Profesa Tibaijuka kwa ukarimu na uadilifu wake uliowezesha kurejeshewa nyumba hiyo.
  Naye Imamu Mkuu wa Msikiti wa Idrisa, ulioko Kariakoo, Maalim Ali Bassaleh, alisema tatizo hilo lisingetokea kama Waislamu wangekuwa na Mahakama ya Kadhi, ambayo hushughulikia pia masuala ya Wakfu.
  CHANZO: NIPASHE


  0 Maoni | Kuwa wa kwanza kutoa maoni
   
 2. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #2
  Dec 15, 2011
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mkuu pamoja na heshima nyingi, unafiki hapa uko wapi?
   
 3. k

  kajunju JF-Expert Member

  #3
  Dec 15, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 986
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Aliyepost habari hii ana chuki na prof tiba..
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  Mkuu nimeona nikuwekeeee hili
  binafsi yumefatilia sana kesi moja ya kiwanja kama si mahakama kutupa ushindi kwa mara ya pili juzi nilichoka kabisa...kuna mtu anamjua alimpelekea docs zote akaambiwa washenzi wake huyu na huyu wamesaini hiyo akutaman hata kuuliza kinachoendelea/......mbaya zaid ******* huyu aliechukua kiwanja ameshindwa mahakamani anatufwata ati anaomba kama tunaweza kumuuzia kiasi chochote leo hii karandinga imeenda kushusha ka gorofa mshenzi chake natumaini anawaza mara saba

  kuna wengi wanazulumiwa na wafanyakazi wa ardhi huyu mama anajua hakak kamchezo anakaa kimya anaendelea kuwalea ndio mana hii ya gazeti nimemwita mnafiki amejaa unafiki mkubwa aende aulize waatu wake wa chini kuna kesi ngapi za ardhi tatizonini unakaa kufanya kazi na magazeti ..sio njema kwa upande wangu
  ingawaa namtakia kila la kheri wizara aliopewa ni majarizu zaid ya shetani
   
 5. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #5
  Dec 16, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Nimesikitishwa na hotuba ya Maalim Ali Baassaleh: badala a kuishukuru serikali kwa kushughulikia tatizo la nyumba hiyo yeye anawabeza kwa kutowapatia mahakama ya kadhi?!, kwa hiyo mahakama ya kadhi iliwepo waislam hawta hitaji uwepo wa waziri? Ama mawaziri?.
   
 6. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #6
  Dec 16, 2011
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mkuu nimekuelewa, nilidhani unafiki uliouzungumzia ni kutokana na story iliyokuwa kwenye gazeti kumbe unazungumzia matukio unayoyajua kuhusiana na huyo mama-shukrani kwa kutoa upande wake wa pili, mimi nilikuwa namchukulia kama mmoja wa mawaziri makini ndani ya baraza la JK
   
 7. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #7
  Dec 16, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Anna Tibaijuka anachukua mambo mengi ambayo akianza hayamalizi; mfano kampeni alioanzisha ya kuvunja nyumba zilizojengwa kwenye open spaces, pia wale waliojenga na kuziba barabara huko Jangwani beach imefikia wapi?
   
Loading...