Tibaijuka: MAYFAIR PLAZA nayo nitaivunja!

friendsofjeykey

Senior Member
Aug 12, 2010
129
13
Hayo ndio maneno ya waziri wa ardhi jana jioni.

Habari toka ndani kabisa wizarani ni kwamba mama keshapewa file la ujenzi pale na watu waliofanya environmental impact assessment kumbe walikuwa pesa hivyo bado kuna mambo ya verification on who did what lakini either way mama keshasema kuwa ujenzi not only wa pale Mayfair Plaza si halali bali anasema kuwa hata Mheshimiwa Rais alishasema kuwa ujenzi ule ni at the expense of walalahoi ambao wanaishi Msasani pale jirani na shoppers plaza ambako wakati wa masika mkondo wote wa maji umeelekezwa kwao na wajenzi wa Mayfair Plaza.

Hoja kubwa ya mama ni kuwa tayari rais alishatoa agizo kuwa jengo lile livunjwe hivyo atakacho kifanya ni kutekeleza amri tuu ya bosi wake

Na si hivyo tuuu Mama Tibaijuka amesema mto wake ni huo huo kama alioanza nao na akina Taher Mucadam hivo hao wenye Mayfair plaza kama wana mawakili waweke stand by kabisa kwani matinga tinga yake yako tayari.

ninachojiuliza je atavunja na zile nyumba / apartments mpya nyuma ya Tanesco jirani na hapo hapo Mayafair plaza ambazo inasemakana ni za Mkulu mmoja huko sirikalini? kwa sababu zile nazo wanasema zinachangia kadhia kubwa wakati wa masika kama Mafair Plaza kwa walalahoi waishio msasani.
 
Sasa kweli huyu mama wa kihaya mbona ni zaidi ya Magufuli? Nampa big up kama uzi utakua ni huu huu! Mama pia usisahau kwenda na kule Kariakoo kwenye yale magorofa waliojenga Wapemba nina wasiwasi nayo pia hayakujengwa kwenye kiwango kinachotakiwa kama utakumbuka .

kuna magorofa huwa yanaanguka yenyewe kutokana na kutokuwa na ubora wa ujengaji.
 
maana hawezi kuvunja Mayfair Plaza na kuziacha zile apartments za Mkulu nyuma yake kwani zote apparently watu wa EIA katika original reports zao zilisema hapafai kujengwa structures zile!!
 
Mama Tiba Wape wapeee vidonge vyao,wakimeza wakitema ni shauri lao. Hahaha!
 
Baada ya huko nenda kabomoe TANESCO Ubungo Morogoro Road,

Kisha hamishia Hasira zako LandMark Hotel Mandela Raod

zilijengwa ndani ya hifadhi ya barabara, ziko ndani ya hifadhi ya Barabara
 
Hiyo ni ndoto.
Kamwe hawezi kuvunja Mayfair, nyie subirini mjionee.

Social_network_film_poster.jpg


Napenda watu wenye mawazo na mitazamo tofauti kama wewe...sio bendera fuata upepo tuu

hawa mkulu hebu tupe sababu kwa nini hawezi kusubutu kupavunja pale?
 
Hiyo ni ndoto.
Kamwe hawezi kuvunja Mayfair, nyie subirini mjionee.

Hili nalo neno.

Tumerekodi maneno yako na tutafuatilia kwa ukaribu. Ila ukweli ni kuwa ukitaka kubomoa majengo yote yaliyojengwa kinyume na taratibu utaigeuza Dar es salaam kuwa kama mji ulioshambuliwa na mabomu wakati wa vita. Kama Mogadishu vile. Kwa maana kuna majengo lukuki yaliyojengwa pasipotakiwa.
 
Wakti anaendelea na katikati ya mji mi nnamuomba aje na huku kwetu Bonyokwa ambako hakujaendelezwa sana atusaidia kuupanga mji.Usipoziba ufa utajenga ukuta.Sio wanaacha mji uanjiotea tu hakuna viwanja vya michezi hakuna mitaa inayoeleweka hakuna maeneo ya kujenga hospitali au shule halafu baadae ndo eti wanakuja kuvunja na kuingiza hasara kwa taifa.Kumbuka pia kuvunja ni gharama
 
Back
Top Bottom