Tibaijuka kwa hili la kupinga adhabu ya kifungo kwa kukosa risiti umeonesha uzalendo wa hali ya juu

jembe2015

Senior Member
Sep 21, 2014
118
71
Sheria ya kifungo cha miaka 3 kwa mtu atakayepatikana hana risiti au ameipoteza ni kuwakomoa wananchi na wala sio kuwasaidia.

Sikubaliani nayo kabisa,ni bora kuweka utaratibu mbadala amabo utawasaidia wananchi na kuwahimiza umuhimu wa kuchukua lisiti mara wanapo pata huduma .

Sheria ya kifungo cha miaka 3 kwa mtu atakayepatikana hana risiti au ameipoteza ni kuwakomoa wananchi na wala sio kuwasaidia.Sikubaliani nayo kabisa,ni bora kuweka utaratibu mbadala amabo utawasaidia wananchi na kuwahimiza umuhimu wa kuchukua lisiti mara wanapo pata huduma .
https://youtu.be/NXVtvYQRrtw
Kwani unadhani hawajui nini kifanyike, ni kuwa wanaambiwa nini cha kufanya na wenye Chama! Tibaijuka ni Prof mzuri tu, ni huo ufisadi wa system alikuja kuwekwa. Uzalendo ulimshinda. Watu wanaiba, na wewe iba! Ni Nyerere tu na Sokoine walishinda vishawishi
 
Wakichangia mchango wa Mama Tibaijuka baadhi walisema walimjua tu kama mama wa Mboga lakini sasa wamemkubali. Ni vizuri hatimaye wengi wameliona hilo.

Hiyo kauli ya mboga ilikuwa propaganda kumchafua huyu mama ili kuwaficha waliokwapua fedha za ESCROW hapo STANBIC. Yeye alisema alipewa fedha na ndugu yake Rugemalira akiamini ziko halali akazipeleka shuleni kwake ambapo anawafadhili watoto wengi masikini kusoma katika viwango vya juu.

Huyu mama aliitisha press conference na alimtaka Rais Kikwete na Serikali yake wathibitishe kama fedha ya Rugemalira siyo halali ili wazirejeshe Kikwete akasema ni halali siyo za Serikali. Lakini Kikwete huyo huyo ambaye Rais Magufuli amesema alimkabidhi kila kitu hewa akamfukuza uwaziri huyu mama peke yake tena hadharani pale Diamond. Kwa hiyo mama huyu alitumbuliwa bila kosa lolote.

Huyu mama mimi niliamini amekwisha lakini wapi? Akakaa kimya na kurudi jimboni kwao akagombea ubunge tena na kushinda pamoja na hila zote alizofanyiwa asirudi Bungeni.

Kumbe wananchi wake wamemuelewa kabla ya sisi wana mitandao kufanya hivyo kwa sababu humu jamvini tunalishwa propaganda za mafisadi halisi waliomchafua huyu Mama kwa sababu wanasema katika vikao ni mkweli haogopi kusema analoamini ni sahihi.

Kumbe hili ndilo lilimkera Kikwete akamfukuza kwenye vikao vyote alivyochaguliwa kihalali ikiwemo Kamati Kuu ya CCM. Kikwete alikuwa anaogopa ukweli wa Tibaijuka. Unauma.

Sasa angalia mchango wake mkubwa Bungeni kuwasaidia Watanzania na pia Serikali ya Magufuli wasitunge sheria mbovu.

Kaokoa wangapi ambao tungefungwa tu kwa kuwa tumeipoteza risiti. Kumbuka sheria ikishatungwa ndiyo basi. Hata Rais hawezi kukusaidia maana naye sharti atawale kwa mujibu wa sheria.

Ni rushwa ngapi zingetafunwa na watu wa TRA katika kutishia watu wasipowalipa watawapeleka gerezani. Kadhia ya polisi wa trafiki sasa ingelikuwa pia ya vijana wa TRA kuvizia watu kwenye migahawa na maduka wakikagua risiti za kielektroniki.

Kweli nimejifunza kwamba wananchi vijijini ni makini katika kuchagua viongozi kuliko sisi mijini. Hawatawaliwi na jazba au fitna. Wanampima mtu.

Imagine tungelipoteza hazina hii hivi hivi katika uchaguzi mkuu.

Hata Rais Magufuli ana sifa ya kupenda ukweli na ndiyo maana wajumbe wa CCM waliamua ndiye apeperushe bendera yao baada ya jina la Lowassa kukatwa tena na huyo Rais ambaye sasa wote tunajua kutoka kwa mrithi wake kuwa alikabidhi kila kitu hewa.

Naamini ndiyo maana hata hawa akina Mama Tibaijuka sasa wanasema ukweli ndani ya Bunge la CCM bila kuogopa maana angelikuwa ni Kikwete huyu mama angerudi matatani. Kwa kuwa Magufuli amesema mara nyingi msema kweli ni mpenzi wa Mungu basi hatutarajii huyu mama kusumbuliwa tena kwa ukweli wake. Ameokoa jahazi.

Na ninampongeza Waziri wa Fedha Dr Mpango ambaye naye alikubali hoja za Mama Tibaijuka ukweli wake ulipodhihirika. Ni dalili nzuri.
 
Ni upuuzi mtupu kupigwa fine kwa sababu huna receipt, hapa ninapoishi receipt inatumika kama kisibitisho (1) ownership rights, (2) kukucover kwa warranty, halafu tuna ile traditional kama hukupewa receipt inamaanisha hicho kitu ni Bure, usilipe.
Jamani msibumburuke na sharia za kiajabu ajabu fanyeni research muwe mnawatuma watu kwenye hizi nchi wasome watu wanadeal vipi na hizi issue,
Professor hovyo kabisa, ccm wanakuja na idea za stone age
 
Hilo litakuwa deal zuri la mapolisi na maafisa wa TRA.
Mkuu hapa ni swala la wana nchi kuwa proactive. Nadhani Takukuru wakijipanga hawa polisi wa vizia wananchi wasio na risiti wataishia jela. Tunataka jamii yetu ibadilike, tulipe kodi itakayotuletea maendeleo siyo kuwanufaisha wachache tu. Ushauri wangu ni Takukuru kujipanga, kutoa elimu kwa wananchi na namna wananchi wanaweza kuaccess huduma zao kwa urahisi. Kama kweli serikali ina nia ya kukomesharushwa hasa kwa waendaji wake, Takukuru ikiwezeshwa litawezekana. Kuna mifumo yaka ile ya polisi. Takukuru wawe na emergence response unit, kuwe na namba maalumu ya kutrigger kuonyesha sehemu fulani kuna uharifu, wa rushwa hivyo wataweza kufika sehemu ya tukio mara moja.
 
Ndugu yangu, hivi Tukukuru inaongozwa na malaika?
 
Wakichangia mchango wa Mama Tibaijuka baadhi walisema walimjua tu kama mama wa Mboga lakini sasa wamemkubali. Ni vizuri hatimaye wengi wameliona hilo.

Hiyo kauli ya mboga ilikuwa propaganda kumchafua huyu mama ili kuwaficha waliokwapua fedha za ESCROW hapo STANBIC. Yeye alisema alipewa fedha na ndugu yake Rugemalira akiamini ziko halali akazipeleka shuleni kwake ambapo anawafadhili watoto wengi masikini kusoma katika viwango vya juu.

Huyu mama aliitisha press conference na alimtaka Rais Kikwete na Serikali yake wathibitishe kama fedha ya Rugemalira siyo halali ili wazirejeshe Kikwete akasema ni halali siyo za Serikali. Lakini Kikwete huyo huyo ambaye Rais Magufuli amesema alimkabidhi kila kitu hewa akamfukuza uwaziri huyu mama peke yake tena hadharani pale Diamond. Kwa hiyo mama huyu alitumbuliwa bila kosa lolote.

Huyu mama mimi niliamini amekwisha lakini wapi? Akakaa kimya na kurudi jimboni kwao akagombea ubunge tena na kushinda pamoja na hila zote alizofanyiwa asirudi Bungeni.

Kumbe wananchi wake wamemuelewa kabla ya sisi wana mitandao kufanya hivyo kwa sababu humu jamvini tunalishwa propaganda za mafisadi halisi waliomchafua huyu Mama kwa sababu wanasema katika vikao ni mkweli haogopi kusema analoamini ni sahihi.

Kumbe hili ndilo lilimkera Kikwete akamfukuza kwenye vikao vyote alivyochaguliwa kihalali ikiwemo Kamati Kuu ya CCM. Kikwete alikuwa anaogopa ukweli wa Tibaijuka. Unauma.

Sasa angalia mchango wake mkubwa Bungeni kuwasaidia Watanzania na pia Serikali ya Magufuli wasitunge sheria mbovu.

Kaokoa wangapi ambao tungefungwa tu kwa kuwa tumeipoteza risiti. Kumbuka sheria ikishatungwa ndiyo basi. Hata Rais hawezi kukusaidia maana naye sharti atawale kwa mujibu wa sheria.

Ni rushwa ngapi zingetafunwa na watu wa TRA katika kutishia watu wasipowalipa watawapeleka gerezani. Kadhia ya polisi wa trafiki sasa ingelikuwa pia ya vijana wa TRA kuvizia watu kwenye migahawa na maduka wakikagua risiti za kielektroniki.

Kweli nimejifunza kwamba wananchi vijijini ni makini katika kuchagua viongozi kuliko sisi mijini. Hawatawaliwi na jazba au fitna. Wanampima mtu.

Imagine tungelipoteza hazina hii hivi hivi katika uchaguzi mkuu.

Hata Rais Magufuli ana sifa ya kupenda ukweli na ndiyo maana wajumbe wa CCM waliamua ndiye apeperushe bendera yao baada ya jina la Lowassa kukatwa tena na huyo Rais ambaye sasa wote tunajua kutoka kwa mrithi wake kuwa alikabidhi kila kitu hewa.

Naamini ndiyo maana hata hawa akina Mama Tibaijuka sasa wanasema ukweli ndani ya Bunge la CCM bila kuogopa maana angelikuwa ni Kikwete huyu mama angerudi matatani. Kwa kuwa Magufuli amesema mara nyingi msema kweli ni mpenzi wa Mungu basi hatutarajii huyu mama kusumbuliwa tena kwa ukweli wake. Ameokoa jahazi.

Na ninampongeza Waziri wa Fedha Dr Mpango ambaye naye alikubali hoja za Mama Tibaijuka ukweli wake ulipodhihirika. Ni dalili nzuri.
hivi lazima umtaje lowassa?
 
Nhnnn...just a little comment on this! I feared to be jailed/penalized nikaomba lists za mzingo wangu..... Uwezi kusinda vita ya rushwa kama hutoi adhabu kwa mtoa na mpokeaji hata kama adhabu hizo zitatofatiana kidogo. That really makes sense and balanced of responsibilities and commitments. Lakini kwa kuwa nchi yetu inaendeshwa kwa hisia za kisiasa hoja ya huyo mama ndugu yangu itaonekana kubeba maji.
 
Alternative B.... wananchi wapewe zawadi pale wakireport duka ama huduma ambazo hutolewa bila risiti.
 
Inawezekana ikawa ni technique ya kushinda uchaguzi 2020, kama nusu ya raia watakuwa gerezani na wafungwa waruhusiwe kupiga kura.
Kumbe unajua kuwa chadema wengi ni wahalifu wanastahili kuwa jela bali ni huruma ya serikali. Bungeni wanasema uongo ambao ni utamaduni wao. Kusema uongo ni kosa.
 
Back
Top Bottom