Tibaijuka ashushwa cheo UN | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tibaijuka ashushwa cheo UN

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Game Theory, Mar 4, 2009.

 1. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #1
  Mar 4, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,572
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Kuna habari kuwa huyu mama kashushwa cheo kule HABITAT je kuna ukweli gani kuhusu hili?

  wana JF mliopo karibu na UN huko hebu tupeane updates kulikoni?

  mniwie radhi sina source wala link ya hii info
   
 2. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #2
  Mar 4, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,864
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Ni kweli kuna thread ingine tayari GT!

  Sijui kwa nini Moon kampiga chini!
   
 3. J

  Jafar JF-Expert Member

  #3
  Mar 4, 2009
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwani kafanya nini tena?
   
 4. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #4
  Mar 4, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hiyo habari iko kwa Gazeti la The Citizen, isome chini:

  UN replaces Tibaijuka
  By Citizen Correspondent, Dave Opiyop, Nairobi

  Prof Anna Tibaijuka has been replaced as the Director General of the United Nations Office in Nairobi.

  The position has consequently been taken over by Mr Achim Steiner, who is also the United Nation�s Environmental Programme Executive Director.

  Prof Tibaijuka however retains her post as the Executive Director of UN Habitat.

  The changes, which were effected on March 1, were done by UN Secretary General Mr Ban Ki Moon.

  However, on Tuesday, a section of the UN staff led by their Union President Mrs Rhoda Atana, protested at the move to replace Mrs Tibaijuka terming this as unfair.

  And they took issue with process to replace Mrs Tibaijuka saying it lacked respect for �gender and diversity� principles within the UN system.

  "Where is that gender and geographic balance where the only UN headquarter duty station headed by a woman is transferred to a man with no justification?" she posed.

  Added Mrs Atana: "Where does the Secretary General's report on improvement of the status of women in the UN system, discussed at the 63rd of the General Assembly, take us?"

  "We have nothing against Mr Steiner, but are disturbed by the process followed in the replacement of Mrs Tibaijuka," said Mrs Atana.

  She went on: "We have high confidence in the Office of Secretary General (Ban Ki-moon) but we would like to express our utmost confidence in Mrs Tibaijuka"s performance."

  Mrs Atana, who was addressing the media at the Unep Complex in Gigiri, expressed concern with the criteria used in replacing her as Director General of the UN Nairobi office.

  The timing of her replacement, she added, was wrong coming at a time when the UN Habitat Governing Council was scheduled to meet at the end of the month.

  "This does not augur well for her... she has worked hard to reform Unon and would have concluded her term with even greater reforms," said Mrs Atana.
   
 5. Companero

  Companero Platinum Member

  #5
  Mar 4, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Kwa mujibu wa gazeti la leo la The Citizen, wafanyakazi wa UN huko Nairobi wameandamana kupinga kitendo hicho. Waandamanaji hao wanasema sio haki. Pia wanalalamika kuwa uamuzi huo unapingana na ripoti ya UN kuhusu maendeleo ya usawa wa kijinsia katika shirika hilo. Hali kadhalika uamuzi huo unaharibu uwiano wa kijiografia.
   
 6. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #6
  Mar 4, 2009
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,185
  Likes Received: 2,747
  Trophy Points: 280
  At times nawashangaa hawa mama zetu ma-activist. Hivi kama mwajiri wako anaona hufanyi kazi..analazimika kuku-retain hata kama hufanyi kazi aliyokupa kwa minajili ya GENDER? These people must be kidding!

  To me hii ni demotion (imekuwa short ya kumfukuza tuu) kwa sababu kwa seniority hata elimu huyu mama yuko juu sana ya huyu Mjeremani anayemreplace (mkurugenzi wa UNEP). (Huyu Mjeremani is just a young white man..hana experience kubwa sana atleast kulinganisha na mama Tibaijuka). Well siwezi kumuhukumu mama yetu lakini kuna kitu kavuruga tuu.. Asingekuwa demoted just like this.

  By the way, the fact that Migiro yuko jikoni na hii issue imetokea..I smell fish hapa..either mama kashindwa kumsaidia (maana kwa kumbukumbu zangu huyu mama ameshakuwa accused mambo mengi sana dhidi ya utendaji wake wa kazi-wanaojua watakuja hapa watumwagie dataz) au ilikuwa aondoke jumla ndo Rose akampigania atleast amalizie kipindi chake UN-HABITAT. Yote yanawezekana.

  Ila make no mistake..wenzetu wazungu wanaenda kwa dataz..hapa wameshafanya uchunguzi wao kwa kina..na wameonelea wamuondoe.

  Ila to me ni aibu...maana atleast wangeleta mtu mwingine (after all UNON ilikuwa na separate Director tangu mwanzo..ni juzi tuu Kofi Anan aliamua kubadilisha....kitendo cha kumchukua Mjeremani aliyeingia UNEP anamkuta mama Tibaijuka akiwa Boss tayari....It sends wrong signal! Sijui ni wapi... ila mama kaharibu some where-big time!
   
 7. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #7
  Mar 4, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,864
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  May be ni ule mradi wa nyumba HABITAT aliopeleka Muleba kule kwake kwa upendeleo!

  Hebu tuambiane..ni kigezo gani alitumia kupeleka ule mradi wa nyumba Muleba ktk wilaya zaidi ya 131 Tanzania?
   
 8. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #8
  Mar 4, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,837
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Huyu Mama wala mimi binafsi nilivyopata kumjua na shule yake ile ya Babro si-mfagiliii kabisa. Ni kafisadi tuu. Nakumbuka ameanzisha shule yake hiyo kwa madai anasaidia maskini lakini ikaja gundulika amefanya commercial na iko very expensive. Watoa msaada wa-swedish kama sio wadanish wakagundua ikawa tifu sana alafu sijui ikaishia wapi. So kwa hili la shule simkubali kabisa.
   
 9. Companero

  Companero Platinum Member

  #9
  Mar 4, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Kwani amefukuzwa kazi na "mzungu"? Kwa mujibu wa hao waandamanaji wa UN unaosema wameshika bango la jinsia tu, huyu mama alikuwa analeta mapinduzi/mabadiliko hapo UN. Kumbuka hawa waandamanaji ni Jumuiya ya Wafanyakazi (Trade Union). Na walitaka amalizie kuleta mapinduzi. Hizi taasisi sote tunazijua jinsi zilivyo na mawazo mgando haya yaliyoelemea kwenye Umagharibi/Uropa-Umarekani. Mimi binafsi simfahamu wala simfagilii huyo mama ila nachojua aliwahi kujaribu kuleta mapinduzi fulani kupitia BAWATA Sirikali ikaishughulikia BAWATA. Usawa wa Kijinsia nayo ni mapinduzi pia.
   
 10. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #10
  Mar 4, 2009
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Campanero,

  Ningefurahi kujua specifically alijaribu kuleta mapinduzi gani BAWATA na "Sirikali ikaishughulikia BAWATA" vipi.
   
 11. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #11
  Mar 4, 2009
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,185
  Likes Received: 2,747
  Trophy Points: 280

  Mkuu hizi sweeping statements sidhani kama zinatusaidia hapa.

  HEBU TUELEZEE NI MAPINDUZI GANI HAYO ALIYOKUWA ANAYALETA? NA NI AKINA NANI WALIMPINGA? Clearly hao wafanyakazi wamesema kwamba hii decision ya kumuondoa mama Tibaijuka iko against GENDER POLICY ya kuwainua wanawake katika UN. Au sikusikia vizuri? hilo mimi ndo nimeelewa. hayo ya mapinduzi kikazi..nadhani yapo tuu..hata wewe ungepewa hiyo kazi..lazima utaingia na work style tofauti. NA AFTER ALL LAZIMA UWE NA NEW IDEAS..ILA HAITAMZUI MWAJIRI WAKO "KUKUACHA UPUMZIKE" kama hayo mapinduzi yako hayaleti tija.

  Yes, kaondolewa na mzungu, kwani BAN Ki Moon ni mswahili? Yes anayechukua nafasi yake ni mzungu, kwani Achim ni mswahili?

  Jamani tusitake kuweka visingizio hapa. Personally mama Tibaijuka nimewahi kumuona MARA MOJA na I always admire her tenacity in defending what she believes in. Especially ile kesi yake ya BAWATA..She rocks! LAKINI kwa hili naamini kabisa hajaonewa. na kama unabisha..subiri kuna wazee wa ze DATAZ watakuja hapa wamwage.

  Hakuna anayemchukia mbongo mwenzetu..ila sasa wengine tuko tofauti..ukichemka..inabidi uwajibike! Infact hata mama Mongella alivyokula hela ya AU ingebidi afukuzwe kazi (tatizo hapa AU ni shirika la waafrika, kwa hiyo busara za spika zilitumika). UN hakuna busara za speak huko baba! You break it, you own it!

  By the way mi nadhani hapa hakuna cha mawazo mgando ya wazungu wala nini..Hivi nani analipa Bill ya UN? Tanzania tunaweka kiasi gani kwenye ile account ya UN pale New York? Anayemlipa mpiga zumari ndo anachagua wimbo mkuu..au umesahau? Hili lipo globally..kuanzia kwa mtu binafsi mpaka kwa Obama!
   
 12. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #12
  Mar 4, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,099
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  hii issue naona kuna mambo yameingilianaa...nimesoma hayo maandamano ya Nairobi kupinga MAMA kuondolewa HIYO nafasi ila nahisi ni hisia zaidi zilitawala huo ushawaishi.

  afterall hiyo nafasi alipewa na same boss position amempatia mtu mwingine.
  labda tujadili mama kwa muda aliokaa UN ameisadia vipi nchi yake katika anga za kimataifaaa...kuanzia muleba mpaka mpanda.

  Pia watz kwenye anga za kimataifa hatujaweza kukamata sana post nyingi hasa za utekelezaji... je tuna tatizo gani??? maana hata east africa community i heard kenyans are more, followed by upcoming rwandans....

  SISI KAMA TAIFA KIPAUMBELE CHETU NI NN??
  RWANDA NASIKIA WAO WAMEFOCUS RASILIMALI WATU (HUMAN RESOURCE DEVPT)....NA MATUNDA WAMEANZA KUONJA KWA KASII TUUUU...

  UWOGA WETU WOTE KATIKA PROTOCAL YA EAC NI KUKOSA RASILIMALI WATU WATAKAOLETA MAPINDUZI KIUCHUMI NA KISIASA...TUFANYEJEEEE???
   
 13. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #13
  Mar 4, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 854
  Likes Received: 399
  Trophy Points: 80
  Wana Jamvi
  Habari za Prof Tibaijuka zimesikika kwa mwezi mmoja kuwa atabadilishwa. Na nyingine zinatonya kuwa hata Dr. Migiro yuko njiani. Yaelekea kuna bifu huko UN kuwa ama Wabongo/Waafrika wamekuwa wengi na soga zimezidi. Kwamba kuna kau-fagio ka Ban-Kimoon kuondoa baadhi ya watu wa Kofi Annan.

  Sasa kuhusu Prof Tiba kama ni fisadi, mara sijui nini - niseme wazi namfahamu huyu, amenifundisha. Kama hajabadilika, ni mama mwadilifu na anayejiamini. Watu wasiojiamini watapata taabu naye, na hasa wanaume wanaodhani kwa sharubu zao wataogopwa na wanawake, na si kwa hoja zao. Kwa hiyo mara nyingi utasikia watu wa namna hiyo wakisema huyu mama anajidai, ni nshomile, n.k.

  Kuhusu shule ya Barbro Johanson Model Girls secondary school, si yake kwa hakika. Ni shule inayoendeshwa na mfuko wa Joha Trust, ulioundwa kutokana na fedha/estates ya hayati Mama Barbro Johanson, Msweed, aliyefanya kazi Bukoba kama mmisionari, na akawa Mbunge wa Taifa kwa kuteuliwa na JKN. Mama yule kwa passion juu ya elimu ya wasichana aliacha trust kwa ajili ya kuwasaidia wasichana wenye vipaji maalum. Church of Sweden na SIDA waka-top up kuendeleza vision hiyo. Kila mwaka kuna fundraising inayofanyika hapa Sweden kwa ajili ya shule hiyo. Yeye prof Tiba ni mjumbe wa trust fund, na mwenyekiti ni balozi Rupia.

  Sasa what happens on the ground in Dar siyo suala la Prof Tiba. Lakini ile shule siyo yake hata kidogo, na kweli watoto wa kike wenye vipaji na maskini wanapata scholarship pale shuleni.

  Suala la BAWATA walio wazee humu walieleze vizuri. Ni refu linaibua feelings nyingi kuhusu serikali yetu. Walio wepesi huwa wanahusisha hata kifo cha mmewe Prof. Ana (Hayati Balozi Tibaijuka au Mulokozi?!) na manyanyaso aliyoyapata Prof Ana wakati wa kupambana na serikali kuitetea BAWATA. Wakili wake alikuwa Prof Shivji.
   
 14. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #14
  Mar 4, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,837
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hapo Mkuu wewe utulie tu huna data kuhusu hilo just go there ujioonee ni watoto wa aina gani wako kwenye hiyo shule and how this Mama is involved. You will learn how selfish she is.
   
 15. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #15
  Mar 4, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 854
  Likes Received: 399
  Trophy Points: 80
  ======

  Ndugu yangu data ninazo. Nimedumu kwenye bodi miaka 4. Nimesikiliza malalamiko kama yako na kuyafanyia kazi. Nina orodha ya watoto wote walioko pale na kuhakiki kama críteria zinafuatwa za admission ambazo ni kipaji cha taaluma. Akiishapata admission, tunaangalia criteria za kumpa scholarship. Karo ni milioin 2.5, lakini based on parents income, wapo wanaolipa kuanzia milioni 2 hadi wasiolipa kitu. Asilimia 80 ya wanafunzi wanalipa laki 5.

  Uselfish unaoutaja ni upi? Kama ni wa 50% ya student watoke Kagera, hilo siyo lake ni la mtoa wosia (Mama Barbro) badala ya shule kujengwa Kagera.

  Prof hufika shuleni once a year wakati wa graduation. Nimemsikia mara kadhaa akilalamika kuwa angependa jukumu hili akabidhiwe mtu mwingine kwa sababu ya kazi nyingi. And I think it is happening soon. Anafanya in honor ya yule mama kwa mchango wake wa kuinua wanawake Tanzania. Ndiye aliyejenga shule ya wasichana ya Kashasha na Vision hiyo hiyo ndiyo alitaka iwe ya taifa zima.

  Nakuomba umwage hapa selfshness yake tuione.
   
 16. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #16
  Mar 4, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,864
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  baija bolobi,

  Na ile project ya UN ujenzi wa nyumba aliopeleka kwake Muleba kwa upendeleo je unasemaje?
   
 17. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #17
  Mar 4, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 854
  Likes Received: 399
  Trophy Points: 80
  ====

  Mzalendo Halisi

  Hiyo project niliisikia kwenye vyombo vya habari. Sina cha maana cha kuisemea. Lakini pia nilisikia iliyo kubwa zaidi ya UN HABITAT itakayofanyika eneo lote la Mbagala DSM. Sasa nani anaamua project iende wapi, mimi sijui. Nilichotolea malelezo ni shule ya Barbro ambayo naifahamu kwa TZ na hapa Sweden.
   
 18. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #18
  Mar 4, 2009
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,839
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Mama huyy kaleta projects nyingi hapa tanzania sasa kama muleba waliomba project hiyo awakatalie kwa sababu gani kwanza ni TZ nyumbani .hivi mnataka watu wawe malaika.Omba kwa mungu labda atakuteremshia mwanaadamu asiyejali kwao
   
 19. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #19
  Mar 4, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 854
  Likes Received: 399
  Trophy Points: 80
  ======

  Na ninadhani ni nafuu akapeleka kwao Muleba kuliko kuufisadi mradi na kujenga mahekalu binafsi au kuwa na vijisenti vya kuiweka serikali mfukoni.
   
 20. I

  Ilongo JF-Expert Member

  #20
  Mar 4, 2009
  Joined: Feb 25, 2007
  Messages: 292
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  Wewe ulitaka huu mradi upelekwe wapi ili ufurahi?
   
Loading...