Tibaijuka aombwa kuwatimua maofisa ardhi Kinondoni

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Tibaijuka aombwa kuwatimua maofisa ardhi Kinondoni

na Andrew Chale

B436B0E0-479F-4DEC-A231-8D21D76FA5D3.jpeg

MBUNGE wa Kawe, Halima Mdee (CHADEMA), amemtaka Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Anna Tibaijuka kuwafukuza kazi maofisa ardhi wa Manispaa ya Kinondoni kwa kushindwa kumaliza migogoro ya ardhi inayoikabili manispaa hiyo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana Mdee alidai kuwa suluhisho pekee la kuondokana na migogoro ya ardhi katika manispaa hiyo ni kuwafukuza maofisa hao na kuajiri wataalamu wapya.

Alisema kuwa maofisa hao ndiyo wamekuwa chanzo cha migogoro huku wizara ikishindwa kuwachukulia hatua kutokana na utendaji mbovu.

Namuomba Waziri Tibaijuka awafukuze watendaji wasio waadilifu na kuajiri wapya kwani huko mitaani wako wataalam wengi walio na uwezo tofauti na hao ambao wanachakachua ardhi ya wananchi wanyonge, alisema.

Mdee aliwataka viongozi wanaohusika na masuala ya ardhi, barabara na mazingira kuhakikisha wanafuatilia kwa karibu suala la uharibifu wa uchimbaji kokote unaofanywa na mwekezaji mmoja na kusababisha uharibifu wa mazingira.

Kuna taarifa nimezipata ambazo zinadai kuwa kigogo mmoja wa manispaa wa Kinondoni anapelekewa milioni mbili kila wiki, hivyo kwa kushirikiana na kamati yangu tunafuatilia suala hilo ili kuweza kunusuru ardhi hiyo, alisema.
 
MBUNGE wa Kawe, Halima Mdee (CHADEMA), amemtaka Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Anna Tibaijuka kuwafukuza kazi maofisa ardhi wa Manispaa ya Kinondoni kwa kushindwa kumaliza migogoro ya ardhi inayoikabili manispaa hiyo.

Hivi kuanzia lini Waziri amekuwa mtendaji na kuweza kuwafukuza watendaji serikalini? Wako wapi DED na ma-MEYA?
 
Hivi kuanzia lini Waziri amekuwa mtendaji na kuweza kuwafukuza watendaji serikalini? Wako wapi DED na ma-MEYA?

Hao ndio wanapitisha "dili" zote za ufisadi wa ardhi; hivyo hawawezi kuwafukuza maafisa ardhi hata siku moja. ... They are partens in this vice.
 
Hivi kuanzia lini Waziri amekuwa mtendaji na kuweza kuwafukuza watendaji serikalini? Wako wapi DED na ma-MEYA?

Hapo umekosoa nini? Au ndo umechefua?!, anayeweza kuwawajibisha watumishi wa hmashauri ni waziri mwenye dhamana ya local gvt- kama hujui usiendelee kukosoa hovyohovyo unatujazia upupu humu janvini.
 
Back
Top Bottom