Tibaijuka ‘ang’ata’ usiku | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tibaijuka ‘ang’ata’ usiku

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 22, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, aliposema atahakikisha watu waliojenga kwenye maeneo ya wazi na yasiyoruhusiwa wavunje wenyewe majengo yaliyopo, hakuwa anatania na wale waliokuwa wakimvimbishia kichwa, watakuwa wamekosea.

  Hali hiyo ilidhihirika jana jioni wakati tingatinga la Halmashauri ya Manispaa ya Ilala mkoani Dar es Salaam, lilipofanya kazi ya kuvunja maeneo ambayo yameanza kujengwa majengo kinyume cha utaratibu na ambayo inaaminika kuwa ni ya wazi au hayaruhusiwi majengo hayo.

  Jana majengo mawili katika Jiji la Dar es Salaam, kiwanja kilichopo karibu na Hoteli ya Palm Beach, ambacho ndio kwanza kilikuwa kimepandishwa ukuta pamoja na ukuta mwingine uliojengwa jirani na Hospitali ya Aga Khan katika Barabara ya Ocean Road, vilivunjwa jana jioni na askari wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.

  Licha ya mmiliki wa kiwanja cha jirani na Hoteli ya Palm Beach, Taher Muccadam kutoa notisi ya siku saba kwa Waziri Profesa Tibaijuka amuombe radhi na kumlipa fidia ya Sh bilioni mbili kwa madai kwamba alimvunjia heshima kwa jamii vinginevyo atamfikisha mahakamani, agizo hilo limepuuzwa.

  Badala yake, umma wa wakazi wa Dar es Salaam waliokuwa wakirejea majumbani mwao jana jioni, walishuhudia tingatinga la Manispaa ya Ilala, lenye namba SM 3937, chini ya ulinzi mkali, likifanya kazi ya kuangusha ukuta huo saa moja jioni kabla ya kuhamia ukuta wa jirani na Aga Khan nusu saa baadaye.

  Kazi hizo mbili zilifanywa na tingatinga hilo chini ya ulinzi wa askari zaidi ya 50 waliokuwa katika magari mengine manne, Isuzu; Toyota Land Cruiser Hard Top, Toyota Double Cabin na Toyota Nissan Patrol yenye namba za usajili SM 3096, SM 4360 na STJ 5662, mali ya Manispaa ya Ilala.

  Mara baada ya kazi hiyo kukamilika katika eneo la Palm Beach, wananchi waliokusanyika kushuhudia tukio hilo, baadhi yao walisikika wakisema, “huyu ndiye Waziri, siyo viongozi wababaishaji. Watu wanamtisha eti wana vibali kutoka Ikulu, yeye aliwambia hatishiki na vibali vyao.”

  Mwingine alisema, “huyu mama (Profesa Tibaijuka) hana mchezo, kama fedha anazo za kutosha, hasumbuliwi na vijisenti…tunahitaji viongozi wenye kusimamia sheria nchini mwetu.”

  Mmoja wa viongozi waliosimamia kazi hiyo, hakutaja kutaja jina lake wala kueleza hatua hiyo imefikiwa na nani, akisema, “hatupo hapa kuongea na vyombo vya habari. Kazi mnaiona.”

  Kiwanja hicho cha Palm Beach ambacho ni namba 1006 ni kati ya viwanja ambavyo Profesa Tibaijuka alidai kuwa ni cha wazi na kwamba hakiruhusiwi kuwa makazi.

  Hivi karibuni, Profesa Tibaijuka akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam aliwataka wananchi waliopora viwanja na maeneo ya wazi nchini na kujenga, wajisalimishe kwa mazungumzo, kwa sababu huenda wakaokoa hata matofali kabla hatua zaidi hazijachukuliwa.
   
 2. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #2
  Dec 22, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Saaaaafiiii
   
 3. N

  Ninkwenda Member

  #3
  Dec 22, 2010
  Joined: Nov 10, 2010
  Messages: 39
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkubwa atishiwi nyau!
   
 4. Jeremiah

  Jeremiah JF-Expert Member

  #4
  Dec 22, 2010
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 642
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Good start tibaijuka. Keep it up Come Geita as well.
   
 5. Wa mmoja

  Wa mmoja Member

  #5
  Dec 22, 2010
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Good mama Tibaijuka....kilichobaki tusubiri yatakayojiri!
   
 6. m

  matawi JF-Expert Member

  #6
  Dec 22, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Welldone jamani lakini isije ikawa kama dowans tunaambiwa tuilipe kwa pesa ya kodi
   
 7. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #7
  Dec 22, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Nimechukia sana huyo Ponjoro kumchimbia mkwara Waziri wa Serikali ati aombe radhi. We unapata kiwanja kwa njia za Panya halafu bado una jeuri ya kumtaka Waziri akuombe radhi. Si inasemekana hciho kiwanja cha Palm kina mkono wa RizOne? Ngoja tusubiri mchezo utakavyoendelela.Tuombe Mungu isiwe nguvu ya Soda. Miaka mitano iliyopita watu waliingia kwa mkwara mpaka wakavunja baraza za nyumba zilizokuwa zimetokezea barabarani. Miezi sita tu baadae kila kitu kikarudi kama kawa...
   
 8. kijoti

  kijoti Member

  #8
  Dec 22, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  viongozi wetu bwana wanaanza vizuri sana lakini utashangaa baada ya mwaka si yule tena, sijui wanakuwa wamelishwa nini jamani inakera sana. sasa huyu mama tumwangalieni kwa karibu sana. kama hicho kiwanja ni huyo riz moja...basi na shughuli kubwa sana
  keep it though mama TIba!!!
   
 9. Jungumawe

  Jungumawe JF-Expert Member

  #9
  Dec 22, 2010
  Joined: May 2, 2009
  Messages: 246
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  umesema kweli mwanza ilitokea wakavunja kituo cha mafuta, lakini hatimaye kodi za walalahoi zilimlipa mhindi na faida juu na kumpa kiwanja kingine. Ni aina nyingine ya ufisadi, mtashangilia lakini mwisho wa maneno itakula kwetu subirini myaone!!!!!!!!!
   
 10. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #10
  Dec 22, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  I hope amezingatia sheria .Tusije kuambiwa tumlipe mamilion ya fedha kama hao wengine wanavyodai. Lets wait and see.

  Je hati imefutwa au bado ni valid?
   
 11. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #11
  Dec 22, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kwa kuvunja iyo inarudisha heshima ya serikali.
   
 12. Mwenzetu

  Mwenzetu JF-Expert Member

  #12
  Dec 22, 2010
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 500
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Je? Gharama za kuvunja nani atalipa?
   
 13. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #13
  Dec 22, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Tibaijuka fanya kazi mama mpaka watu wakome...moto uliouanza usiuzime kabisa. Ukiuzima tutaamini kuwa ni nguvu za soda tu
   
 14. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #14
  Dec 22, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  wanshindana na ishomireee alieaga kwao asie na shida wala njaa

  kazi wanayo mama wikijayo nakuletea wengine mzazi anafikiri ni wale wapuuzi wakina chiligati aliowahonga
  akahonge ikulu walikompa kibali cha MAVI YAKE
   
 15. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #15
  Dec 22, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  hii picha ndio imeanza, hao wahindi si ndio wanachangia CCM wanapata kiburi, ndoja waone sasa mama katoka UN hajui mambo ya hongo za kijinga
   
 16. M

  Mundu JF-Expert Member

  #16
  Dec 22, 2010
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Heshima kwanza, mambo mengine baadaye. Bravo mama!!
   
 17. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #17
  Dec 22, 2010
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  ok, ngoja tuone hiyo swaga yake! Lakini mimi bado nasisitiza Mama anahitaji Ku-strategise kwanza. Anatakiwa ajipange vizuri...matatizo ya ardhi ni mengi sana na si dar tu. Hatutaki show za media nadhani tunataka mikakati madhubuti itakayoleta permanent solution.
   
 18. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #18
  Dec 22, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,838
  Likes Received: 2,000
  Trophy Points: 280
  Bado kuna maeneo mengi korofi, tunasubiri hayo
   
 19. W

  Womtindo Member

  #19
  Dec 22, 2010
  Joined: Dec 7, 2010
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  nafikiri mimi nataka niwe tofauti kidogo na wengi wa wachangiaji, kuna mmoja amesema isije ikawa kama Dowans, nami nachelea hivyohivyo. Maamuzi ya haraka ya viongozi wetu wakati mwengine matokeo yake yanatugharimu watanzania wote.
  Mimi nilifikiri ingekuwa vema kwanza kusettle hizo claims za mmiliki na kuhakikisha kuwa ameshindwa kabla ya kuchukua hatua ya kuvunja ukuta, tusije tukajikuta 'tunalipa fine ya maamuzi mabovu'
   
 20. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #20
  Dec 22, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,838
  Likes Received: 2,000
  Trophy Points: 280
  Hili ndilo la muhimu zaidi, tumeshashuhudia athari za maamuzi kama haya
   
Loading...