Tiba za asili: Manufaa ya asali na mdalasini

Nitafute Kwa wakati wako nipate kukutibia upate kupona.Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Herbalist Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe.fewgoodman@hotmail.com What's App +905344508169 Au Ni add Kwa Facebook tumia jina hili mzizimkavu. Au boonyeza hapa.Mzizi Mkavu
Habari kaka, naona Habbat Sawda na Mdalasini vyote kama vinaenda sawa na Asali, kwako kipi ni the best unachorecommend? Kwa upande wangu napenda sana mchanganyiko kama ni Unga tu nichanganye na Asali nilambe au kula basi, ikishakuwa kuchemsha sijui kupasha moto napataga shida. Nina tabia ya Kula kijiko cha asali kila nikiamka na nikitaka kulala, nimejikuta tu napendelea kufanya ivyo bila kujua nnachokitibu haswa! Now nataka add btn Mdalasini na Habbat Sawda Natanguliza Shukrani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari kaka, naona Habbat Sawda na Mdalasini vyote kama vinaenda sawa na Asali, kwako kipi ni the best unachorecommend? Kwa upande wangu napenda sana mchanganyiko kama ni Unga tu nichanganye na Asali nilambe au kula basi, ikishakuwa kuchemsha sijui kupasha moto napataga shida. Nina tabia ya Kula kijiko cha asali kila nikiamka na nikitaka kulala, nimejikuta tu napendelea kufanya ivyo bila kujua nnachokitibu haswa! Now nataka add btn Mdalasini na Habbat Sawda Natanguliza Shukrani

Sent using Jamii Forums mobile app
Tumia vyote hivyo sio mbaya chukuwa unga wa mdalasini kijiko 1 kidogo changanya na unda wa Habbat Sawda kijiko 1 kidogo tia katika Asali kijiko 1 kikubwa koroga vizuri kisha urambe asubuhi mcha na usiku kabla ya kula kitu.

ONYO KALI: Usije kuramba unga wa Mdalasini pasipo na kuchanganya na Asali utakuja kufa. Kwani Unga wa Mdalasini ukija kuramba unga mtupu utakwenda kuingia ndani ya Mapafu yako na kukuziba Pumzi na haitofika zaidi ya dakika 30 utafariki dunia shauri yako usijaribu kuramba Unga wa Mdalasini pasipo na kutia ndani ya Asali au kwenye Maji ya Moto.
 
Tumia vyote hivyo sio mbaya chukuwa unga wa mdalasini kijiko 1 kidogo changanya na unda wa Habbat Sawda kijiko 1 kidogo tia katika Asali kijiko 1 kikubwa koroga vizuri kisha urambe asubuhi mcha na usiku kabla ya kula kitu.

ONYO KALI: Usije kuramba unga wa Mdalasini pasipo na kuchanganya na Asali utakuja kufa. Kwani Unga wa Mdalasini ukija kuramba unga mtupu utakwenda kuingia ndani ya Mapafu yako na kukuziba Pumzi na haitofika zaidi ya dakika 30 utafariki dunia shauri yako usijaribu kuramba Unga wa Mdalasini pasipo na kutia ndani ya Asali au kwenye Maji ya Moto.
Ooh! Shukrani Kaka, na hii elimu ya Mdalasini hope umewafumbua macho na wengine. Uendelee Barikiwa kwa Msaada wako humu ndani kaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu nimekutana na makala hii nikaonelea nianzishe topic hapa ili tuweze kujadiliana na wataalam wetu na watufahamishe ukweli wake na uwongo wake au kutupa ushauri zaidi ya huu niuonao katika mada hii. Nimejaribu kwa kadiri ya uwezo wangu kuirekebisha kiswahili chake lakini nahisi hakiko sawa bado lakini naaminu ujumbe unafika.

Leo naanza na Manufaa ya Asali na Mdarasini:

MDALASINI NA ASALI

Asali inafahamika vema Duniani kote kama mojawapo ya silaha ya kiajabu katika kupigana na magonjwa na matatizo yatokanayo na uzee.

Sasa hivi, utafiti mpya umeonyesha kwamba uwezo wa asali unaweza kuongezwa maradufu kama itachanganywa na mdalasini wa kawaida.

Uchunguzi wa kina ufanywao kwa wiki na jarida la World News wa Tiba, wataalamu wa madawa yatokanayo na mimea pamoja na kijarida cha afya na lishe, imeonekana kwamba kuna dazani nyingi za umuhimu wa asali na mdalasini pamoja na michanganyiko {dawa} ya kusisimua iletayo afya bora.

Kama ifuatayo:
1. Ugonjwa wa Viungo/Maumivu na Uvimbe {ARTHRITIS}.
Wataalamu wa lishe wanapendekeza kuchukua kwa kutumia mchanganyiko wa sehemu moja ya asali pamoja na sehemu mbli za maji vuguvugu na kijiko kimoja {cha chai} chenye mdalasini - na kuchua sehemu zilizoathirika. Nafuu hupatikana katika muda wa dakika moja.


Vinginevyo tengeneza chai-kikombe kimoja chenye maji moto, weka vijiko vya chakula -viwili vya asali kwa kijiko cha chai cha mdalasini. Kunywa asubuhi na jioni ili kuondoa maumivu.

Katika tafiti iliyofanyika hivi karibuni na chuo kikuu kimoja huko Copenhagen, madaktari waliwapa wagonjwa 200, {syrup} mchanganyiko wa kijiko kimoja 'cha chai' cha asali na kimoja cha mdalasini kila asubuhi kabla ya kifungua kinywa. Asilimia 73% yao waliripoti nafuu kubwa ya maumivu yao na ongezeko katika kufanya shughuli kama kujongea na kutembea vyema.

2. Kukatika kwa nywele {HAIR LOSS}
Asali ikishachanganywa na mdalasini pamoja na mafuta vuguvugu ya olive, hutoa kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele kinachotumika katika dawa ya Dork. Mchanganyiko huo vuguvugu unapakwa kwa kusugua kichwani na kuachwa kwa dakika 15.


3. Ukungu wa miguuni {FUNGUS}
Changanya kijiko kikubwa cha mezani cha asali, vijiko viwili vya mdalasini {vya chai}. Pakaa sehemu zilizoathirika usiku kwa muda wa nusu saa, kisha safisha kwa sabuni na maji. Shida yako itakwisha kwenye kipindi cha wiki moja.


4. Maamhukizo kwenye kihofu cha mkojo {BLADDER INFECTION}
Bilauri ya maji vuguvugu yaliyochanganywa na vijiko viwili {vya chai} vya mdalasini na kijiko kimoja {cha chai} cha asali huondoa bacteria kwenye kibofu. Unaweza ukatumia juisi ya cranberry badala ya maji ikiwa ambukizo la kibofu linakuwa sugu.


5. Maumivu ya jino {TOOTHACHE}.
Changanya sehemu tano za asali, na sehemu moja ya mdalasini na tumia kwa maumivu ya jino.


Dondoshea kwenye jino au meno yaliyoathirika hadi maumivu yatakapotoweka.

6. Vidonda vitokanavyo kwa mgonjwa kulala kwa muda mrefu {CANKER
SORES}.
Saladi ya kupaka vidonda iliyochanganywa na asali pamoja na mdalasini kwenye chai ya raspberry nyekundu ni dawa nzuri ya kuondoa maumivu makali ya canker sores.


7. Helemu {CHOLESTERAL}
Kipimo cha helemu cha watu waliokuwa na afya nzuri {katika jaribio} kilishuka kwa wastani wa asilimia 10 katika muda pungufu ya masaa mawili baada ya kunywa bilauri moja {ounce 16} yenye vijiko viwili vikubwa vya mdalasini iliyochanganywa na chai ya moto. Kinywaji hiki kutwa mara tatu kilifanya kazi nzuri ya kushusha kiwango cha helemu mwilini.


Madhara yaletwayo na vyakula vyenye mafuta yanaweza kudhbitiwa kwa matumizi ya mara kwa mara ya chai hii pamoja na chakula chako. Hii imeripotiwa na mtafiti maarufu Dr Alexander Andreyed na Eric Vogelmann.

Ugunduzi wao uliyakinishwa kwenye jarida mashuhuri la kitiba la Denmark July 1994. vilevile/ aidha uchunguzi mwingine ulibayanishwa kutoa matumizi ya kila siku ya asali safi hupunguza viwango vya helemu.

8. Mafua {COLDS}
Mafua yameshaeleweka ya kwamba hupotea/huondoka baada ya masaa machache baada ya waathirika kutumia kijiko kimoja {cha mezani} cha asali vuguvugu iliyochanganywa na robo kijiko{cha chai} cha mdalasini, mchanganyiko huu ni mahususi katika kusaidia kuondoa chafya na kuvimba koo.


9. Ugumba {INFERTILITY}
Asali inaaminika kuamsha nyege na wapenzi wa jinsia zote mbili wanashauriwa kunywa angalau vijiko viwili {vya mezani} kila siku kabla ya muda wa kulala {usiku}.


Mdalasini umetumika kwa muda mrefu kwenye dawa za kihindi na kichina ili kuongeza uwezo wa uzazi ka kina mama wenye kuhitaji kuzaa.

Kiungo hiki {mdalasini} huchanganywa na kiasi cha asali na kufanya mgando {paste} ambao hupakwa kwenye fizi za meno na kunyonywa na kuingia mwilini taratibu.

Familia moja iliyokuwa haina watoto iltumia mgando huu kwa mafanikio na kupata mapacha wa kike baada ya kushindwa kwa muda wa miaka 14 kupata mtoto. Walikuwa wameshakata tamaa ya kupata mtoto hadi waliposikia kuhusu mchanganyiko huu wa asali na mdalasini.

10.Mchafuko wa tumbo {UPSET STOMACH}
Asali imetambuliwa kwa kipindi kirefu kama dawa ifaayo kuondoa mchafuko wa tumbo pamoja na kichefuchefu. Ongeza kiasi kidogo cha mdalasini na hii tiba ya kimaajabu vilevile itapunguza maumivu yaletwayo na vidonda vya tumbo.

ikopoa sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba tutumie huu uzi kutaja tiba za asili tunazozijua kwani ni wazi kuwa yapo magonjwa yasiyo na tiba muafaka hospitalini lakini kuna watu wanajua tiba za asili.

Lengo ni kuweka kumbukumbu kwani maandishi uliyoweka hapa yanaweza kuja kuwa na manufaa miaka hata 50 ijayo, huwezi kujua.

Najua wengi hatujui majina kwa lugha ya kiswahili, au kisayansi ya mimea mingi tunayoijua ni tiba. Naomba tu uitaje kwa jina la lugha unayoifahamu, inawezekana akatokea mdau anajua jina la mmea huo kwa lugha nyingine tunayoweza kuielewa wengi. Kama unaweza weka picha kabisa ya mmea au tiba unayoongelea.

Binafsi nitaanza na kutaja mimea ya tiba zifuatazo katika posts zitakazofuata, na nitajitahidi kuweka picha pale ninapoweza. Pia nitaandika "tiba" au "tambiko" kwa mujibu wa wazee wangu niliobahatika kukua nao (ingawa kwa sasa sifanyi hizo), kwa lengo tu la kuweka kumbukumbu kwani inawezekana miaka mingi ijayo watoto au wajukuu zetu wakaja kusoma huu uzi katika kujifunza mila na desturi zao.
Baadhi ya tiba nitakazotaja hapa ni zile ambazo niliwahi kuona wazee wangu wakizitumia, zile nilizowahi kutumia mwenyewe, zile nilizowahi kuhadithiwa, na hata zile nilizosoma sehemu mbali mbali ikiwemo humu JF...

Baadhi ya nitakazoweka kwenye posts zinazofuata ni;

1. Mimea inayotibu maumivu ya tumbo (la kuharisha)
2. Mimea inayotibu maumivu ya tumbo (sio la kuharisha)
3. Mimea inayotibu vidonda
4. Mimea inayotibu kiungulia
5. Mmea unaotibu athma (mara moja tu)
6. Mimea inayoongeza nguvu za kiume
7. Mmea unaotibu maumivu ya meno (pamoja na kutoboka)
8. Tiba ya maumivu ya sikio (sio mmea)
9. Mimea inayofunga kizazi kwa wanawake
10. Mmea unaotibu jipu (bila kupasuliwa)
11. Dawa ya kusaidia kutoa kondo la nyuma la ng'ombe
12. Mmea unaotibu minyoo (kwa binadamu na mifugo)
13. Mmea unaotibu mastitis kwa ng'ombe
14. Kadhalika

Pia zipo tiba vyingine ambazo zinahusiana na imani ambazo nitazitaja baade kwa mfano
1. Jinsi ya kumkinga au kumtibu mtoto mchanga dhidi ya "kijicho"
2. Jinsi ya kujizuia "kufanyiwa mchezo" kwa chakula unachokula hadharani au kwenye sherehe
3. Jinsi ya kuzuia mvua isinyeshe siku kuna tukia kama sherehe au mkutano
4. Tambiko ya kuomba mvua
5. Kadhalika

Nawaombeni wanaJF mposti kwenye huu uzi tiba zozote za asili mnazozijua au mlizowahi kusikia. Huwezi jua miaka mingi ijayo akatokea kijana wetu mtafiti akasoma bandiko lako, akafanya utafiti akaibuka na dawa matata ambapo utakuwa umesaidia vizazi na vizazi...
Mkuu tunakusubiri sana huku
 
...mmmm, ila hili la Mayai SABA kila siku kwa Siku 30 kwa ajili ya Mambo yetu yalee...inataka Moyo!
Hii maana yake ni Maya 210 kwa Mwezi!!
Kuna Usalama hapo kula mayai 210 kwa Siku 30?
Nahisi hata hizo Nguvu unazotafuta ndio zitapotea zaidi!!
Ndio maana mara nyingi matibabu haya ni hizo dawa nyingine zinazotangazwa humu mitandaoni...ni vigumu sana kupata feedback kutoka aliyezitumia na kufanikiwa!!!
 
...Mkuu, lakini hii sio Dawa ya Matibabu. Hii ni solution ya tatizo lako la muda uliopo. Ina maana kila ukiwa na tatizo hilo Unajpaka!
Sio kwamba ukiisha ipaka mara moja ama mbili tu basi tatizo lako la chuma kutosimama vizuri limekwisha! No!
Hii ukijizoesha sana inaweza ikakufikisha mahali bila kuipaka mkulunge hausimami.
Vumbi halifai kwa kweli...!!
Kuna dawa inaitwa vumbi la kongo ni balaa hio. Kwa uchache lisaa kiunoni. Kuna jamaa anauza ni pm nikupe namba ukachukue anakaa tabata
 
...Mkuu, lakini hii sio Dawa ya Matibabu. Hii ni solution ya tatizo lako la muda uliopo. Ina maana kila ukiwa na tatizo hilo Unajpaka!
Sio kwamba ukiisha ipaka mara moja ama mbili tu basi tatizo lako la chuma kutosimama vizuri limekwisha! No!
Hii ukijizoesha sana inaweza ikakufikisha mahali bila kuipaka mkulunge hausimami.
Vumbi halifai kwa kweli...!!
Vumbi la Kongo ni mtu anachelewa kufika kileleni tu, haligusi uwezo wa mashine kusimama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nami pia ningependa kufahamu tiba ya asili ya macho hasa kwa mtu anayesumbuliwa na myopia( Short sightedness)
 
38 Reactions
Reply
Back
Top Bottom