Tiba ya tatizo la kiwango kidogo cha mbegu za kiume

kichakaa man

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
5,479
5,064
Kwanza kabisa naomba mods hii makala msiunganishee na makala zingine. Huu uzi nataka niweke niseme niwekee ufumbuz kwa njia za asili kwa mtindo wa vyakula vya asili ili kuweza kutibu tatizo hili la low sperm count ( kwa kusadia tu nilikuwa mhanga wa hili tatizo lilinitesa sana lakin baada ya kupata ushauri wa kitaalum kutoka kwa Dr flan pale hospital ya Rufaa mbeya na kupona na mungu kasadia wife kajifungua dume tena nimefanana naye balaa

Mbinu naweka hapa na kuna mambo mengine wataalamu zaid yangu wataongezea .

Ila ushauri wangu ni vyema kwenda hospital kubwa ufanye vipimo ili Dr aweze kujua nin tatizo lako na jinsi ya kuweza kukusadia kulingana na tatizo lako maana sio wote matatizo yanafanana hasa ukubwa wa tatizo

UPUNGUFU WA UZALISHAJI WA MBEGU ZA KIUME (LOW SPERM COUNT)

Upungufu katika uzalishaji wa mbegu za kiume inahusiana na kutokuwepo kwa mbegu za kiume kwenye manii au uwepo wa mbegu kidogo sana katika manii.

Mbegu za kiume huwa zinachunguzwa kwa kutumia kifaa maalum au darubini katika
maabara, kwa kawaida mwanaume ili aweze kumpa mwanamke mimba anatakiwa atoe kiasi cha mbegu kati ya milioni ishirini hadi milioni mia nne kwa tendo, chini ya milioni ishirini huwezi kumpa mimba mwanamke.

Endapo kiwango cha mbegu zitakuwa kidogo kitaalam hali hiyo huitwa ‘Oligospermia’ na kama huna kabisa mbegu hali hiyo huitwa
‘Azoospermia.Dalili za kutokuwa na mbegu za kiume Hakuna dalili za moja kwa moja kusema kwamba utaumwa kitu fulani, lakini dalili
zifuatazo huambatana na tatizo hili;
=kwanza ni kukaa katika mahusiano kwa kipindi
kisichopungua mwaka mmoja lakini mwenzi wako hapati mimba, =kushindwa kufanya
tendo la ndoa kwa uume kukosa nguvu’ Low
sex Drive’ na
=ukisimama unashindwa
kuendelea na kumalizia tendo ‘Erectile dysfunction’ pamoja na kuwahi kumaliza tendo la ndoa.
=Maumivu na uvimbe wa korodani, =kupungua kwa vinyweleo na ndevu kutoota pia ni dalili inayoashiria matatizo ya uzazi kwa mwanaume kwani ni ishara ya upungufu wa
Kromozomu au homoni za kiume.
Hizo zote ni dalili kuu za matatizo ya uzazi kwa mwanaume.

Kipindi au Wakati gani wa kumuona daktari au mtaalamu?
Endapo umekaa na mwenzio mwaka mmoja au zaidi, mnafanya tendo la ndoa bila kinga yaani kizuizi chochote wakati wa kupangilia ujauzito lakini mimba haipatikani. Kama una matatizo ya nguvu za
kiume au unawahi kumaliza tendo la ndoa. Unakosa hamu ya kufanya tendo la ndoa au uume unalegea wakati wa tendo pia ni mojawapo ya chanzo.

Unakuwa na maumivu ya korodani au korodani kuvimba, maumivu ya uume na maumivu wakati wa kukojoa au uwepo wa kivimbe katika uume.

Chanzo cha tatizo Uzalishaji wa mbegu za kiume unafuatana
na ubora wa korodani kama haina tatizo lolote na kiwango bora cha mfumo wa homoni mwilini mwako. Homoni zinadhibitiwa katika ubongo na kuimarisha korodani zizalishe mbegu. Mbegu zikishazalishwa,
husafirishwa na mirija midogo sana na laini hadi katika tezi dume ’Prostate gland’ ambayo kazi yake kubwa ni kuzalisha manii. Matatizo katika mbengu za kiume ni kutokuwepo kwa mbegu kunakosababishwa na hitilafu au matatizo kwenye korodani, kuzalisha mbegu zenye kasoro, mbegu zisizo na kiasi na mbegu chache.

Matatizo ya korodani husababishwa na joto kali katika korodani, maambukizi katika korodani na uume na kuumia korodani. Mishipa ya damu kulalia korodani ‘Variocele’ pia ni mojawapo ya tatizo kubwa la kuziba
kwa mirija ya usafirishaji mbegu hizo.

Zipo pia sababu za kimazingira zinazoathiri uzalishaji wa mbegu za kiume mfano kemikali za viwandani, rangi za viwandani
au majumbani, dawa za mashambani na za kuua wadudu, mionzi ya X- Ray, kukaa kwenye joto kali, kuvaa nguo za kubana na
kukaa mahali kwa muda mrefu, kupakata kompyuta ‘(Lap top)’ kwa muda mrefu, matumizi ya sigara, bangi na madawa mengine ya kulevya kwa muda mrefu na
ulevi uliokithiri. Uzito mkubwa wa mwili na matatizo ya akili.

Uchunguzi wa tatizo hili hufanyika katika hospitali za mikoa na wilaya kwa madaktari wa masuala ya uzazi. Vipimo vya damu kuangalia mwenendo wa mfumo wa homoni mwilini Kipimo cha Ultrasound kuangalia korodani yako kwa
ndani. Uchunguzi hufanyika kisayansi hospitali tu, hakuna vifaa vingine vya kuchunguza kwa
kubahatisha, unatakiwa utolewe damu, na utoe mbengu zako za kiume baada ya kupumzika kufanya tendo la ndoa angalau
kwa siku tatu.

Matibabu na ushauri hufanyika baada ya uchunguzi ambapo
daktari atatoa dawa kuzingatia na tatizo lililopo. Kama hakuna mbegu zipo chache au kuna maumivu au kasoro zozote. Uwepo wa kasoro
za viungo vya uzazi pia ni tatizo mfano, uume mfupi, kutokuwa na korodani au kuwa na korodani moja.

Upande mwingine wanaume anaweza kuwa anazalisha mbegu za kutosha lakini anashindwa kumpa mweza wake ujauzito kutokana na matatizo aliyonayo mwenza wake kama
=kuwa na acidic katika uzazi ambapo huuwa mbegu za kiume zikifika ndani ya kizazi
=kuzalisha yai ambalo halijakomaa kwa wanamke
=kuhalibika kwa kuta za kizazi 'uterus' au kuwa zaifu na kushindwa kuhimili au kubeba ujauzito.
=upande mwingine wanaume kuzalisha mbegu mbovu au zenye matatizo.

Kwa maelezo zaidi unaweza kutembelea page zetu Facebook kwa jina la *afya kwa wanaume* na *afya ya wanawake* pia unaweza kiwasiliana nasi kwa ushauri na tiba ya uhakika.



SHARE NA LIKE ELIMU HII IWAFIKIE WENGINE ILI WAJIFUNZE NA KUELIMIKA ILI KUPUNGUZA MATATIZO YA UZAZI NDANI YA JAMII ZETU.

Hiyo hapo ni makala nimeona kwa Facebook

Vyakula ambavyo mim nilitumia kutibu tatizo langu la low sperm count (alinishaur nitumie miez 3 na kipind chote hiki niliambiwa nisifanye mapenz ili mbegu ziweze kukomaa na kukusanyika na mambo mengine ambayo ni ya kitaalamu zaid ).na bado naendelea kula pia kufanya mazoez ya kukimbia Mara kwa Mara mim nilikuwa nafanya karibia kila siku.

Dozi yangu ilikuwa ni hii

Mbegu za maboga ( naloweka na chumvi kias tu ili kupata radha na kuanika zinakauka ila alisema nisikarange) Kula mbegu 300 kwa siku kwa kipind chote cha dozi yangu
kula ugali wa dona na mboga za majani kwa wingi pamoja na matunda
Asali mbichi vijiko 3 kwa siku kila siku
kutumia karanga,mayai ya kienyeji ,

Na zingine ntawapatia baadaye



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaan huu uzi umenifanya ni summarize na kubold point yangu kuwa LiFE STYLE yetu siku izi wanaume pia imebadilika sana utakuta mtoto wa kiume anakula chips zege kama kidemu cha ambiansi yaan mtoto wa kiume ata ngogwe hajawai kula therefore kuliepuka ili janga natoa RAI vijana Punguzeni ulaji wa chips yai utakimbiwa na mkeo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom