'Tiba ya malaria ibadilishwe'

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,584
2,000
'Tiba ya malaria ibadilishwe'

Imeandikwa na Hellen Mlacky; Tarehe: 16th December 2010 @ 06:13

TAASISI ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), imependekeza dawa ya Artesunate inayotengenezwa nchini China, iwe dawa mbadala ya kutibu malaria kali ili kuokoa maisha ya watoto 100,000 barani Afrika dhidi ya vifo vitokanavyo na malaria kali kila mwaka.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Dk. Julius Massaga, aliyasema hayo jana katika warsha ya siku moja ya kujadili utafiti wa miaka mitano wa matumizi ya dawa hiyo kwani ina uwezo mkubwa wa kutokomeza malaria kali kuliko dawa ya Quinine na hivyo kuchangia kupunguza idadi ya vifo vya watoto na watu wazima vitokanavyo na ugonjwa huo.

Dk. Massaga alisema, mwaka 2006, NIMR kupitia kituo chake cha Tanga ilifanya utafiti chini ya ushirikiano ujulikanao kama “African Quinine Artesunate Malaria Trial” (AQUAMAT) ili kubaini ubora wa Artesunate katika kutibu malaria kali na kugundua kuwa dawa hiyo ni rahisi kutumia na haina madhara kwa mtumiaji.

Alisema, utafiti huo ulifanywa kwa ushirikiano na Kitivo cha Magonjwa ya Ukanda wa Joto cha Chuo Kikuu cha Mahindo kilichopo Bangkok, Thailand na kufadhiliwa na Taasisi ya Welcome Trust ya Uingereza.

“Ikilinganishwa na tiba rasmi ya Quinine, dawa ya sindano ya Artesunate ilipunguza vifo kwa takriban robo kwa watoto wenye malaria kali. Kutokana na matokeo haya, Artesunate inapaswa kutumika badala ya Quinine kama tiba rasmi duniani kote,” alisema.

Alisema malaria inayosababishwa na vimelea vya Falciparum inaongoza kwa vifo vya watoto Afrika na ni moja ya sababu zinazosababisha watoto kulazwa na vifo vingi hutokea nyumbani au karibu na nyumbani.

Alisema, kwa wanaobahatika kufikishwa hospitali wakiwa na malaria kali huanzishiwa dawa ya Quinine ambapo utafiti umebaini kuwa mmoja kati ya watoto sita hupoteza maisha ambapo pia imebainika kwamba huchangia kuleta madhara mbalimbali kwa wagonjwa waitumiayo.

“Kutokana na utafiti wenye mafanikio ujulikanao kama South East Asian Quinine Artesunate Malaria Trial (SEAQUAMAT), dawa ya Artesunate ilibainika kuchangia kupunguza vifo vya watu wazima wanaougua malaria Kusini Mashariki mwa Bara la Asia hatimaye kuweza kufikia asilimia 14, kutoka asilimia 23 ya vifo wakati wa matumizi ya Quinine,” alisema Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIMR.

Dk. Massaga alisema utafiti huo ulifanyika kwenye vituo 11 katika nchi tisa za Afrika ikiwemo Tanzania ambapo ilikuwa na vituo viwili vilivyohusisha Hospitali ya Wilaya ya Korogwe (Magunga) na Hospitali Teule ya Wilaya ya Muheza, zote kutoka mkoa wa Tanga, chini ya uratibu wa Kituo cha Utafiti cha Tanga.
 

Masika

JF-Expert Member
Sep 18, 2009
723
195
Did they perform resistance research? How artesunate and quinine resisted by mixed malaria parasites?
Does it mean the trial conducted to seriously ill patients without their consent and check whether they could respond to artesunate or quinine? this should be bad
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom