Tiba ya madonda ya tumbo kwa muda mfupi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tiba ya madonda ya tumbo kwa muda mfupi

Discussion in 'JF Doctor' started by schlumberger, Jul 28, 2012.

 1. s

  schlumberger JF-Expert Member

  #1
  Jul 28, 2012
  Joined: Jun 15, 2012
  Messages: 635
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Madonda ya tumbo ni ugonjwa unaowasumbua watu wengi: Mimi nimekuwa muathirika mara mbili. Hii hapa stori yangu:

  Niliugua ugonjwa wa madonda ya tumbo tokea mwaka 1999 - 2007. Wakati ule nilikuwa Tabora Boys. Hali ilikuwa mbaya hata kufikia kutokwa na damu wakati wa kujisaidia haja kubwa. Nilikuwa nikitumia dawa mbalimbali za Hospitali na za Kisunna. Ziliweza kupunguza maumivu lakini tatizo lilibaki palepale. sikuwa naweza kufunga Mwezi wa Ramadhani kwa miaka yote tisa. Baada ya kumaliza chuo kikuu nilipata kazi na nikawa natibiwa Pale AGAKHAN bila mafanikio. Doctor akashauri nifanye kipimo fulani cha kuingiza mpira tumboni (sikumbuki jina la kitaalamu). Ilikuwa ni siku ya Ijumaa na kipimo kilikuwa Alhamisi wiki inayofuata. Siku ya jumapili nikakuta na bwana mmoja anitwa Sheikh Mbonde (0784375259/719279675) na katika mazungumzo nikamweleza tatizo langu na appt ya doctor. Akaniambia "Jihesabu umepona". Skuelewa! Jioni yake akanipa dawa na jumatatu nikaanza kuitumia.

  Alhamisi nikafanya hicho kipimo na doctor alikuwa Prof. Othman (Marehemu). Wakati ule mpira unaingia tumboni kwa kweli hakuna kilichoonekana. Doctor akasema sina vidonda vya tumbo. Nikajibu "Doctor siamini". Akasema "Huamini kipimo? au huniamini mimi? au una matatizo kichwani!. Asingenielewa! Miaka tisa? Mhh!!

  Taratibu nikaanza kula vyakula vilivyoungwa ndimu, maharage, chai ya rangi, ugali wa dona n.k. Pia nikaanza kufunga mwezi wa Ramadhani bila shida yoyote.

  Hali hii iliendelea hadi mwaka 2011 mwezi wa 10. Kulitokea nikapata stress nyingi na pia nikawa nafanya kazi kwa muda na nachelewa kula. Kwa muda wa kama siku tatu au nne hivi nikaanza kusikia maumivu.

  Ohh! Hali ikarudi kama mwanzo. madonda yakaanza tena.

  Mfungo ulipokaribia nikamtafuta Bw. Mbonde na kumweleza tatizo langu tena akaniahidi kunipa dawa lakini kutokana na kutingwa na kazi (ni - mwajiriwa) hakufanikiwa mpaka siku moja kabla ya Ramadhani.

  Siku ya kwanza nikafunga na pia nikatoa sadaka kwa maskini. kwa kweli siku iliisha vibaya. Nilipata maumivu sana. Nikajipa moyo na siku ya pili nikafunga na huku nikilisha maskini. Maumivu yakapungua kidogo. Siku ya tatu nakaweza kufunga bila shida sana.

  Leo ni siku ya nane Ramadhani na tumbo limetulia kabisa. Namshukuru Mwenyezi Mungu na namshukuru Doctor wangu Bwana Mbonde.


  Pia nashukuru kwa kuwa watu wengi ambao wamekuwa wanasumbuliwa na tatizo hili nimewaunganisha na huyu bwana na wananipigia simu kunishukuru. kwa maneno yake anasema "ANASAIDIA UMMAH". KWA TZS 60,000/= KWA DOZI. Ni "mchaMungu".

   
Loading...