Tiba ya Machinga Dar na Mwanza Yaweza kutibiwa Hivi

DSN

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,837
1,674
Mikoa ya Dar es Salaam na Mwanza ni mikoa ya Majiji ambayo kwa kiwango kikubwa huduma zitolewazo na Machinga ni muhimu sana kwa maisha ya Watanzania kwa huduma wazipatazo na pia ni muhimu sana kwa Machinga wenyewe kwa kuwa shughuli wanazo ziendesha hugeuka kuwa Ajira za kuendesha maisha yao na kumudu kulipa kodi muhimu kwa ujenzi wa Taifa lao kupitia shughuli mbalimbali za maisha yao ya kila siku.

Machinga [Marching Guy or Marching Market] ni mfumo wa uendeshaji biashara ambao unafanywa na Mataifa mengi tu mbalimbali Duniani yakiwemo yale yalioendelea kama Uingereza [UK] na Marekani [USA]
A Street.hawker.in.rome.arp.jpg

NINI KIFANYIKE ILI KUEPUKANA NA VUTA NI KUVUTE HIZI.

A: WAJIBU WA SERIKALI YA WILAYA, MKOA NA SERIKALI KUU.
1: KUUNDA KIKOSI KAZI CHA KUSIMAMIA SHUGHULI ZA MACHINGA.

Kuunda Vikosi kazi [taskforce] ndani ya maeneo husika ya Wilaya, Mkoa, Jiji na Taifa ambayo yatakuwa na kazi moja rasmi kusimamia shughuli na mienendo ya wafanyabiashara wadogo wadogo na machinga hawa kwa ukaribu sana wakishirikiana na viongozi wanaochaguliwa na vikudi vya wafanyabishara wadogo na machinga katika maeneo yao.

2: KUANDAA NA KUTENGA MAENEO YENYE TIJA KWA WAFANYABIASHARA.
Kuandaa maeneo ambayo yatakuwa mahususi na yenye tija [Convenient] kwa ajili ya kusaidia wafanyabishara wadogo wadogo na hawa machinga kufanya biashara zao bila kuvunja sheria na kuepeuka kuwa kero dhidi ya watumiaji wengine wa miundombinu ya umma.Hivi sasa kumekua na sombasomba hamisha hamisha isiyo na Tija kwa kuwa Wafanyabiashara hao hutolewa maeneo yenye tija kwao na kupelekwa kusiko na Tija.Hata kama maeneo hayo watakayopewa wafanyabiashara hao kwa muda mfupi basi yawe na Tija kwao na hata kwa watumiaji wa huduma hizo za machinga hao.

3: MIFUMO YA MAWASILIANO NA MAHUSIANO.

Kuwe na mifumo ya kupokea Taarifa za wafanyabiashara hao na hata taarifa za wateja [umma] wa wafanyabiashara hao kwa kutumia njia rafiki [Friendly Communications Means] ambazo zitatoa fursa kwa watumiaji wa masiliano kuona sauti zao zinasikika na kufanyiwa kazi juu ya kero na matatizo wanayokumbana nayo katika huduma husika.

4: ULINZI NA USAFI KATIKA MAENEO HUSIKA YA BIASHARA HIZO.
Kusimamia na kuratibu usafi na Ulinzi, Usalama wa mali za Wananchi kwenye shughuli zote hasa kwenye misongamano kwa kufunga camera za CCTV na pia kufanya kazi hiyo kwa kushirikiana na viongozi wa Wafanyabishara hao kwa kuwa wao wana ufahamu wa watu waovu, wezi, vibaka katika maeneo yao wanayofanyia biashara hizo. Mfano mzuri wa zoezi la kuwahusisha viongozi ni jiji la Mwanza [japo lilingia dosari mwaka 2015, baada ya viongozi wao baadhi kuanza kupokea rushwa kila wanapomkamata mfanyabishara anaye fanya biashara maeneo yasiyo rasmi kama walivyokubaliana na jiji.Kwa Serikali kuwa mdau na kutumia vyombo vyake vya dola itawafanya Viongozi wa Wafanyabishara hawa kuogopa kujihusisha na rushwa kwa kuwa watajua jicho la Dola liko kwao pia.

5: MIPANGO NA MIUNDO MBINU ENDELEVU [SUSTAINABLE PLANS].
Kutengeneza mipango [Procedures] na Sera {Policy] na miundo mbinu [Infrastructures] yenye kusudio la kuwaandalia mifumo endelevu na ya maendeleo [Sustainable Plans] dhidi ya wafanya biashara kwa kuwa kama Taifa ambalo kabla ya Uhuru watanzania walikua milioni kumi [10 Million] leo hii miaka hamsini na tano [55] Watanzania wako Millioni Arobaini na tano [45] hiyo ni ishara kuwa Watanzania wanaongezeka lakini Eneo la Kariakaoo Dar es salaam na Makoroboi Mwanza ni lile lile babu yangu Mzee Maganga alipita na mimi mjukuu wake na uzao wake wote tunalipita hivyo hivyo kwa Watanzania wengine na familia zao.

Hii na sawa na kusema unaitaji ubunifu mwingine mpya ambao bado utaleta maana ile ile na pengine kuvutia zaidi na kufanya watanzania wa miaka hamsini ijayo kufurahia huduma za eneo husika kama ambavyo watu hujikuta wanavutika kutafuta huduma za Kariakoo ama Makoroboi. Hiyo ni sawa na kusema kama Taifa tunaitaji mazungumzo kupitia Task Force kuongea na umma kwenye mijadala ya wazi kupata maoni yao ni maeneo gani wao wanaona ni bora kwa Wananchi kujengwa masoko yenye hadhi ya kuvuta huduma kama yanavyovuta watu haya ya Karikoo, Makoroboi au Kilombero Arusha.Think Tankers wanaweza kutoa viasharia vya maeneo lakini umma ukapewa nafasi ya kudigest maeneo tajwa ili japo kuona impact kubwa itakuwa imeelekezwa kwenye eneo gani kwa mujibu wa umma [mass].

6: KUTAMBUA NA KURASIMISHA HUDUMA HIZI ZA WAMACHINGA.
Ni kwa fursa hiyo ya Serikali kwa kushirikiana na viongozi wa Machinga, itapata mwanya wa kumfikia kila mmachinga na kumpa nafasi ya kushirikiana naye na kumtambua kwa nafasi [level] ya uwezo wa biashara yake na kumsajili na akapata namba ya utambulisho kama Mfanyabiashara wa kiwago cha Umachinga [Marching Guy] na hivyo hata pale Serikali inapokuwa na fursa za kumsaidia na kuboresha uwezo wake mfanyabishara huyu inakuwa inajua ina idadi kiasi gani cha wanohitajika kusaidia kupanua biashara zao na hata kunapotokea kupatikana kwa eneo rasmi ambalo Serikali inalikabidhi kwa Wamachinga hao inakuwa inajua idadi ya Wafanyabiashara hao.

B: WAJIBU WA MACHINGA
1: KUWA NA UONGOZI NGAZI HUSIKA.

Ni wajibu wa wafanyabiashara wadogo wadogo hawa kuwa na uongozi maalumu utakaofanya kazi kwa niaba yao, kuwasemea na kuwakilisha mahitaji yao kwenye vikao muhimu vya kimashauri kati yao na Serikali iwe ya Wilaya, Mkoa, Jiji ama Taifa.

2: KUANDAA DAFTARI LA IDADI YA WAFANYABIASHARA NGAZI HUSIKA.

Hii nayo itasaidia uongozi kuwa na idadi ya Wafanyabishara hizi ndogo ndogo wa aina zote za biashara iwe ni wauza vitu vidogo vidogo, kama viatu, nguo, vyakula, matunda, vitabu, Saa, Vifaa vya Magari, Vifaa vya Umeme na Biashara zingine nyingi. Ni jukumu la Uongozi wa Wafanyabishara hao kuwaandalia mazingira ya utambulisho kwa kuwapa vitabulisho vya kuwatambua rasmi.

3: KUWA NA KANUNI, TARATIBU NA MISINGI YA KUJIONGOZA
Wafanyabiashara hao wadogo wadogo wanapaswa kuwa na kanuni, taratibu na Misingi ya kujiongoza kwa daraja husika [level] ili kuleta tija kwao wao Wafanyabiashara na Wateja wao ambao ni umma wa Watanzania, na pia kuwa na utii kwa Serikali yenye mamlaka juu ya Biashara yao kuwepo maeneo hayo ama kutokuwepo maeneo hayo.Kwa wao kujiundia miongozo hiyo na uratibishaji wa shughuli zao za kila siku kutawajengea wigo wa kurasmisha huduma hiyo ya Biashara ndogo ndogo na kuwapa heshima kuwa Mwajiri mwenye kutambulika kokote kule aendako na kwa lolote atakalo lifanya kwa kuzingatia sheria za Nchi.

4: UONGOZI WA WAFANYABIASHARA KUWA NA MIKAKATI ENDELEVU

Uongozi wa ngazi husika toka wilaya mpaka Taifa unapaswa kuwa na malengo yenye tija kwa wanachama wake ambao ndio watumishi wa sekta husika ya biashara hizo ndogo ndogo. Wanapaswa kuwa na maono [Vision] ya kuwaongoza Wafanyabishara hao kuwa taasisi yenye heshima ya kibiashara kwa kuwa na fursa za kutoa semina, mikutano na mafunzo mbalimbali kwa wanachama ama ushirika wa Wafanyabiashara hao wadogowadogo ili wawajenge kuziona fursa za maendeleo mbalimbali pia kuwa daraja kati ya Wafanyabiashara na Serikali yao na pia kwa Umma ndio walaji wa huduma zao wanazo zitoa.

5: KUSIMAMIA NA KUHAMASISHA ULINZI NA USAFI WA BIASHARA ZAO:
Kwa Viongozi kuwa sehemu ya wahamasisha ulinzi na usafi wa maeneo yao ya biashara ni na mna njema ambayo itachangia kuwa alama ya mafanikio ya biashara ndogo ndogo kwenye miji mikuu.Kwa Serikali kuwapa fursa viongozi kutembelea maeneo ya kujifunza na wao kuja kutumia elimu walioyopata kuimiza wenzao waifuate ni ushawishi utakao leta Tija na mafanikio kwa pande zote.

C: HATUA ZA HARAKA KUONDOA MTAFARUKU WA MAENEO YA MACHINGA

1: JIJI LA DAR ES SALAAM
NEW KARIAKOO MARKET -DAR.

Kulingana na mwanga wa ushauri alioutoa Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano kuhusu kubadirisha matumizi ya baadhi ya maeneo ambayo ni mali ya umma. Nami binafsi likaja wazo hivi kuna haja gani ya kuwa na nyumba za polisi pale Msimbazi. Kama inawezekana kwanini zile Kota za Polisi zisiamishwe na kujengwa mahali pengine pale pakajengwa jengo la MSIMBAZI MACHINGA MALL..ushauri kusijengwe ghorofa kwa kuwa Watanzania hawana utamaduni wa kufanya manunuzi kweye ghorofa [Cultural Factors] ili isije likawa halina maana kama Machinga Complex karume.

Lijengwe jengo Kubwa Pana kusijenngwe kuta ndani bali wazi kiasi cha kuweza kuwakatia vizimba vya kupanga bidhaa zao kwa mifumo ya kistaarabu.Kwenye eneo hilo kunaweza kuwa kunapatikana vyombo vya nyumbani tu [Home Appliance].

Kisha kuna Shule ya Serikali pale pembeni ya barabara ya Uhuru nayo si Mbaya inaweza Kutafutiwa eneo jingine wale vijana wakaamishwa pale eneo lile likawa UHURU MACHINGA HUB na ikibdi kujengwe Walking Flyovers ili Watu wawe wanavuka toka upande mmoja kwa kutembea kwenda upande mwingine.Yani kuwe na uwezo wa mtu kuvuka kwa juu toka Mtaa wa Kongo Karikakoo akaenda upande wa pili barabara ya Uhuru.

Kama kuna Majengo ya Msajili wa Majumba maeneo ya Mtakaa wa Kongo Karikakoo si mbaya pia Serikali kuwaomba National Housing kuona ni kwa namna gani wanaweza kupata plan ya kujenga Majengo ambayo yatawahifadhi Machinga wengi na kukidhi madhari nzuri yenye ubunifu wa kisasa na kuzidi kuipendezesha Kariakoo ili iendelee kuwa HUB ya Biashara kusini mwa jangwa la Sahara ikiwahudumia Malawi, Msumbiji, Kongo, Rwanda, Burundi, Sudani, Somaria, etc.

MITAA YA KARUME, LUMUMBA NA SAMORA POSTA
Hii mitaa inaweza kuwa na utaratibu ambao umeshaanza kuonekana wa kufungwa siku za jumamosi hasa Karume na Lumumba na wakienda hivyo wafike kuufunga mtaa wa Samora siku ya Jumapili ambayo wenye maduka yalio mtaa huu uwa wanafunga siku za Ijumapili hivyo nao unaweza kutumika kuwa mtaa mzuri kwa machinga wauza vitu vidogo vidogo.

2: JIJI LA MWANZA
Jiji la Mwanza kuna lile eneo lilo mbele ya Ofisi ya Mabasi ya Zamani ya Tanganyika yani [Stand ya Mabasi ya Zamani] eneo hili kwangu naona zile shughuri za baadhi ya mabasi kwenda mikoani kufanyika pale zingesitishwa pale na kuperekwa sehemu zingine na eneo lile ligeuzwe kuwa eneo ambalo machinga wanalitumia na kule kwenye kituo cha Taxi na Daladala kinachoangaliana na duka la Vunja bei napo kiwanja kile kinaweza kutumiwa na Wamachinga na kuboreshwa. Kwa hatu hizo hata Msongamano wa Magari maeneo hayo utapungua kama si kuisha kabisa.Ni swala la Mkoa na Wilaya kubuni eneo gani ligeuzwe kituo ambalo liko nje kidogo na vituo vunjwa.

Pia sio mbaya ile shule Kongwe pale mjini ya Pamba nayo kwa umri wake na kuongezeka kwa watu ni vyema nayo ikatoka pale yale majengo yake yakabuniwa vizuri na kuwa PAMBA MACHINGA HUB ..Uwepo wa shule ile pale mjini kati [City Centre] unachangia sana kushindwa kwa wanafunzi wengi sana wanaosoma shule hiyo...kwa kuwa na mazingira ambayo sio rafiki kwa vijana wetu wanaosoma hapo upelekea wengi kuanguka mitihani. Kwangu mimi kwa umri wa shule ile pale ni vyema sasa yakatafutwa maeneo tulivu wale vijana wakatolewa pale na kupisha eeo lile kuwa la Mikakati ya Shughuri za kibiashara jijini Mwanza.

MTAA WA MAKOROBOI
Huu pia unaitaji maboresho sana kuangalia namna ambayo ikibidi Mkoa husika unaweza kugharimika kuuboresha mlima unao hifadhi baadhi ya vibanda vya Wafanyabiashara hao kwa kupanua na kutegeneza mitalo ya kupitisha maji na kuweka Pavement ili kulifanya eneo hilo wakati wa masika liendelee kuwa zuri na la kuvutia. Kipindi cha Masika eneo la Makoroboi linatia Kinyaaa kwa kuwa ueguka kuwa na tope na miundo mbinu yake ya kupita sio iliyoboreshwa bali ni vijichochoro ambavyo ugeuka kuwa rojorojo la tope na kuvuluga kabisa eneo hilo zuri kwa huduma ya biashara ndogo ndogo ambazo mamilioni ya Watanzania ufaidika na hudma za eneo hilo.

HITIMISHO:
Machinga ni raia Watanzania ,wanaitaji fursa kama ambavyo wengine wanazo..Dunia nzzima inatambua uwepo wa Machinga ambao upewa majina mengi kama [Marching Guys, Street Hawkers, Vendors, Pedestrians etc.] hivyo kunaitajika ubunifu ikibidi kubadili mandhari ya umma tuliyoyazoea ili kuleta Mapinduzi ya Mandhari mpya ili Watanzania wengine nao wajione ni sehemu ya Taifa kufanyike Mapinduzi hayo.

Kulikua na tetesi wakati fulani Nyamagana miaka hiyo ya Nyuma kuna mtu alitaka apewe..ili afanye investment kwani Wananchi wa Mwanza Wakiulizwa watoe maoni yao kati ya kuwa na kiwanja cha Mpira na kuwa na Soko jipya eneo lile ushauri wao nini? Wananchi wataongea na kutoa maoni yao.

Machinga wanachopaswa kufanya ni kutii sheria, taratibu na kannuni zilizowekwa na mamlaka huku zile ambazo zinaonekana kuwa msumeno kwao zikiboreshwa ili nao kwa mujibu wa mazingira [FACTS] ziweze kuwafaha [Accomodate] na wao wafikie malengo yao ya kujenga Taifa lao kama Watanzania ambao ndio wenye Nchi na hayo maendeleo ni kwa faida yao.

Kazi kubwa watakuwa nayo viongozi wa Serikali ngazi ya Mtaa, Kata, Tarafa, Wilaya, Mkoa na Taifa kuwa na ubunifu [Creativity] ambao lengo lake ni kujenga na kuepuka migongano kwa kuangalia wapi majibu yasiyo na mawaa yanaweza kupatikana. Kwa Mkoa kuwa na watu maalumu wanao tizama njia za majibu wakiwa kama timu [Think tank] ya Mkoa ama Wilaya kupata majawabu ya maswala mazito ni suruhu njema ya kuboresha matatizo ya umma kwennda kuwa mafanikio ya umma.

A Steert Market .jpg
 
Attachments

  • A Steert Market .jpg
    A Steert Market .jpg
    30.4 KB · Views: 74
mmmh ni kweli lakini sijui kama ngazi husika wamekusikia.
Lengo nni mimi na wewe kupeana kile ambacho wote tuona kinaonekana kama basi kikifikilika na kupewa nafasi ya kutathimiiwa basi kwa majadiliano yetu sote tunaweza tukafika sehemu tukasema ili linatufaha sote
 
Naunga Mkono Mkuu, Kwanza, Ni Lazima shughuli ya Machinga irasimishwe rasmi na kutambulika kama kazi zingine, hili litafanyika kwa kutunga sheria rasmi ya kuwatambua, inaweza kuitwa The Marching ACT, hii itaainisha Maana ya Machinga, Chombo kitakachowasimamia, Maeneo yao rasmi nchi nzima nk.

Kwa Mwanza, Kila Mtaa ni lazima uwe na aneo rasmi la Machinga, eneo la Machinga kwa kila mtaa, linaweza kujengwa ndani ya soko husika, ikibidi, Kila mkoa Ukope au Uombe fedha au utumie Fedha zao za ndani kwa kibali cha serikali kuu, Fedha hizo zijenge Jengo la Ghorofa moja, yaani upande wa chini utakuwa ni kwa ajili ya Machinga au kwa juu ni akina mama wanaouza bidhaa zao.

Kwa mfano, SOKO la NYAMANORO AU PASIANSI, lijengwe Jengo lenye Ghorofa Moja, Upande wa Chini watakaa Machinga na wa Juu mama wauza bidhaa mbalimbali, na Vizimba vya kutosha vijengwe kwa kila hall.

Ni matumaini yangu, wataalamu wa Michoro wanaweza kuchora vizuri tu hii michoro ya majengo haya,
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Hatimae Shukrani kwa Serikali kusikia Kilio hiki...Cha Machinga kuwa sekta iliyo lasmi
 
Naunga Mkono Mkuu, Kwanza, Ni Lazima shughuli ya Machinga irasimishwe rasmi na kutambulika kama kazi zingine, hili litafanyika kwa kutunga sheria rasmi ya kuwatambua, inaweza kuitwa The Marching ACT, hii itaainisha Maana ya Machinga, Chombo kitakachowasimamia, Maeneo yao rasmi nchi nzima nk.

Kwa Mwanza, Kila Mtaa ni lazima uwe na aneo rasmi la Machinga, eneo la Machinga kwa kila mtaa, linaweza kujengwa ndani ya soko husika, ikibidi, Kila mkoa Ukope au Uombe fedha au utumie Fedha zao za ndani kwa kibali cha serikali kuu, Fedha hizo zijenge Jengo la Ghorofa moja, yaani upande wa chini utakuwa ni kwa ajili ya Machinga au kwa juu ni akina mama wanaouza bidhaa zao.

Kwa mfano, SOKO la NYAMANORO AU PASIANSI, lijengwe Jengo lenye Ghorofa Moja, Upande wa Chini watakaa Machinga na wa Juu mama wauza bidhaa mbalimbali, na Vizimba vya kutosha vijengwe kwa kila hall.

Ni matumaini yangu, wataalamu wa Michoro wanaweza kuchora vizuri tu hii michoro ya majengo haya,
Naona tunaelekea kwenye mawazo yako taaratibuuu...safi sana kwa hatua hizo zilizochukuliwa ahadi sasa/
 
Mikoa ya Dar es Salaam na Mwanza ni mikoa ya Majiji ambayo kwa kiwango kikubwa huduma zitolewazo na Machinga ni muhimu sana kwa maisha ya Watanzania kwa huduma wazipatazo na pia ni muhimu sana kwa Machinga wenyewe kwa kuwa shughuli wanazo ziendesha hugeuka kuwa Ajira za kuendesha maisha yao na kumudu kulipa kodi muhimu kwa ujenzi wa Taifa lao kupitia shughuli mbalimbali za maisha yao ya kila siku.

Machinga [Marching Guy or Marching Market] ni mfumo wa uendeshaji biashara ambao unafanywa na Mataifa mengi tu mbalimbali Duniani yakiwemo yale yalioendelea kama Uingereza [UK] na Marekani [USA]
View attachment 443470

NINI KIFANYIKE ILI KUEPUKANA NA VUTA NI KUVUTE HIZI.

A: WAJIBU WA SERIKALI YA WILAYA, MKOA NA SERIKALI KUU.
1: KUUNDA KIKOSI KAZI CHA KUSIMAMIA SHUGHULI ZA MACHINGA.

Kuunda Vikosi kazi [taskforce] ndani ya maeneo husika ya Wilaya, Mkoa, Jiji na Taifa ambayo yatakuwa na kazi moja rasmi kusimamia shughuli na mienendo ya wafanyabiashara wadogo wadogo na machinga hawa kwa ukaribu sana wakishirikiana na viongozi wanaochaguliwa na vikudi vya wafanyabishara wadogo na machinga katika maeneo yao.

2: KUANDAA NA KUTENGA MAENEO YENYE TIJA KWA WAFANYABIASHARA.
Kuandaa maeneo ambayo yatakuwa mahususi na yenye tija [Convenient] kwa ajili ya kusaidia wafanyabishara wadogo wadogo na hawa machinga kufanya biashara zao bila kuvunja sheria na kuepeuka kuwa kero dhidi ya watumiaji wengine wa miundombinu ya umma.Hivi sasa kumekua na sombasomba hamisha hamisha isiyo na Tija kwa kuwa Wafanyabiashara hao hutolewa maeneo yenye tija kwao na kupelekwa kusiko na Tija.Hata kama maeneo hayo watakayopewa wafanyabiashara hao kwa muda mfupi basi yawe na Tija kwao na hata kwa watumiaji wa huduma hizo za machinga hao.

3: MIFUMO YA MAWASILIANO NA MAHUSIANO.
Kuwe na mifumo ya kupokea Taarifa za wafanyabiashara hao na hata taarifa za wateja [umma] wa wafanyabiashara hao kwa kutumia njia rafiki [Friendly Communications Means] ambazo zitatoa fursa kwa watumiaji wa masiliano kuona sauti zao zinasikika na kufanyiwa kazi juu ya kero na matatizo wanayokumbana nayo katika huduma husika.

4: ULINZI NA USAFI KATIKA MAENEO HUSIKA YA BIASHARA HIZO.
Kusimamia na kuratibu usafi na Ulinzi, Usalama wa mali za Wananchi kwenye shughuli zote hasa kwenye misongamano kwa kufunga camera za CCTV na pia kufanya kazi hiyo kwa kushirikiana na viongozi wa Wafanyabishara hao kwa kuwa wao wana ufahamu wa watu waovu, wezi, vibaka katika maeneo yao wanayofanyia biashara hizo. Mfano mzuri wa zoezi la kuwahusisha viongozi ni jiji la Mwanza [japo lilingia dosari mwaka 2015, baada ya viongozi wao baadhi kuanza kupokea rushwa kila wanapomkamata mfanyabishara anaye fanya biashara maeneo yasiyo rasmi kama walivyokubaliana na jiji.Kwa Serikali kuwa mdau na kutumia vyombo vyake vya dola itawafanya Viongozi wa Wafanyabishara hawa kuogopa kujihusisha na rushwa kwa kuwa watajua jicho la Dola liko kwao pia.

5: MIPANGO NA MIUNDO MBINU ENDELEVU [SUSTAINABLE PLANS].
Kutengeneza mipango [Procedures] na Sera {Policy] na miundo mbinu [Infrastructures] yenye kusudio la kuwaandalia mifumo endelevu na ya maendeleo [Sustainable Plans] dhidi ya wafanya biashara kwa kuwa kama Taifa ambalo kabla ya Uhuru watanzania walikua milioni kumi [10 Million] leo hii miaka hamsini na tano [55] Watanzania wako Millioni Arobaini na tano [45] hiyo ni ishara kuwa Watanzania wanaongezeka lakini Eneo la Kariakaoo Dar es salaam na Makoroboi Mwanza ni lile lile babu yangu Mzee Maganga alipita na mimi mjukuu wake na uzao wake wote tunalipita hivyo hivyo kwa Watanzania wengine na familia zao.

Hii na sawa na kusema unaitaji ubunifu mwingine mpya ambao bado utaleta maana ile ile na pengine kuvutia zaidi na kufanya watanzania wa miaka hamsini ijayo kufurahia huduma za eneo husika kama ambavyo watu hujikuta wanavutika kutafuta huduma za Kariakoo ama Makoroboi. Hiyo ni sawa na kusema kama Taifa tunaitaji mazungumzo kupitia Task Force kuongea na umma kwenye mijadala ya wazi kupata maoni yao ni maeneo gani wao wanaona ni bora kwa Wananchi kujengwa masoko yenye hadhi ya kuvuta huduma kama yanavyovuta watu haya ya Karikoo, Makoroboi au Kilombero Arusha.Think Tankers wanaweza kutoa viasharia vya maeneo lakini umma ukapewa nafasi ya kudigest maeneo tajwa ili japo kuona impact kubwa itakuwa imeelekezwa kwenye eneo gani kwa mujibu wa umma [mass].

6: KUTAMBUA NA KURASIMISHA HUDUMA HIZI ZA WAMACHINGA.
Ni kwa fursa hiyo ya Serikali kwa kushirikiana na viongozi wa Machinga, itapata mwanya wa kumfikia kila mmachinga na kumpa nafasi ya kushirikiana naye na kumtambua kwa nafasi [level] ya uwezo wa biashara yake na kumsajili na akapata namba ya utambulisho kama Mfanyabiashara wa kiwago cha Umachinga [Marching Guy] na hivyo hata pale Serikali inapokuwa na fursa za kumsaidia na kuboresha uwezo wake mfanyabishara huyu inakuwa inajua ina idadi kiasi gani cha wanohitajika kusaidia kupanua biashara zao na hata kunapotokea kupatikana kwa eneo rasmi ambalo Serikali inalikabidhi kwa Wamachinga hao inakuwa inajua idadi ya Wafanyabiashara hao.

B: WAJIBU WA MACHINGA
1: KUWA NA UONGOZI NGAZI HUSIKA.

Ni wajibu wa wafanyabiashara wadogo wadogo hawa kuwa na uongozi maalumu utakaofanya kazi kwa niaba yao, kuwasemea na kuwakilisha mahitaji yao kwenye vikao muhimu vya kimashauri kati yao na Serikali iwe ya Wilaya, Mkoa, Jiji ama Taifa.

2: KUANDAA DAFTARI LA IDADI YA WAFANYABIASHARA NGAZI HUSIKA.
Hii nayo itasaidia uongozi kuwa na idadi ya Wafanyabishara hizi ndogo ndogo wa aina zote za biashara iwe ni wauza vitu vidogo vidogo, kama viatu, nguo, vyakula, matunda, vitabu, Saa, Vifaa vya Magari, Vifaa vya Umeme na Biashara zingine nyingi. Ni jukumu la Uongozi wa Wafanyabishara hao kuwaandalia mazingira ya utambulisho kwa kuwapa vitabulisho vya kuwatambua rasmi.

3: KUWA NA KANUNI, TARATIBU NA MISINGI YA KUJIONGOZA
Wafanyabiashara hao wadogo wadogo wanapaswa kuwa na kanuni, taratibu na Misingi ya kujiongoza kwa daraja husika [level] ili kuleta tija kwao wao Wafanyabiashara na Wateja wao ambao ni umma wa Watanzania, na pia kuwa na utii kwa Serikali yenye mamlaka juu ya Biashara yao kuwepo maeneo hayo ama kutokuwepo maeneo hayo.Kwa wao kujiundia miongozo hiyo na uratibishaji wa shughuli zao za kila siku kutawajengea wigo wa kurasmisha huduma hiyo ya Biashara ndogo ndogo na kuwapa heshima kuwa Mwajiri mwenye kutambulika kokote kule aendako na kwa lolote atakalo lifanya kwa kuzingatia sheria za Nchi.

4: UONGOZI WA WAFANYABIASHARA KUWA NA MIKAKATI ENDELEVU
Uongozi wa ngazi husika toka wilaya mpaka Taifa unapaswa kuwa na malengo yenye tija kwa wanachama wake ambao ndio watumishi wa sekta husika ya biashara hizo ndogo ndogo. Wanapaswa kuwa na maono [Vision] ya kuwaongoza Wafanyabishara hao kuwa taasisi yenye heshima ya kibiashara kwa kuwa na fursa za kutoa semina, mikutano na mafunzo mbalimbali kwa wanachama ama ushirika wa Wafanyabiashara hao wadogowadogo ili wawajenge kuziona fursa za maendeleo mbalimbali pia kuwa daraja kati ya Wafanyabiashara na Serikali yao na pia kwa Umma ndio walaji wa huduma zao wanazo zitoa.

5: KUSIMAMIA NA KUHAMASISHA ULINZI NA USAFI WA BIASHARA ZAO:
Kwa Viongozi kuwa sehemu ya wahamasisha ulinzi na usafi wa maeneo yao ya biashara ni na mna njema ambayo itachangia kuwa alama ya mafanikio ya biashara ndogo ndogo kwenye miji mikuu.Kwa Serikali kuwapa fursa viongozi kutembelea maeneo ya kujifunza na wao kuja kutumia elimu walioyopata kuimiza wenzao waifuate ni ushawishi utakao leta Tija na mafanikio kwa pande zote.

C: HATUA ZA HARAKA KUONDOA MTAFARUKU WA MAENEO YA MACHINGA

1: JIJI LA DAR ES SALAAM
NEW KARIAKOO MARKET -DAR.

Kulingana na mwanga wa ushauri alioutoa Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano kuhusu kubadirisha matumizi ya baadhi ya maeneo ambayo ni mali ya umma. Nami binafsi likaja wazo hivi kuna haja gani ya kuwa na nyumba za polisi pale Msimbazi. Kama inawezekana kwanini zile Kota za Polisi zisiamishwe na kujengwa mahali pengine pale pakajengwa jengo la MSIMBAZI MACHINGA MALL..ushauri kusijengwe ghorofa kwa kuwa Watanzania hawana utamaduni wa kufanya manunuzi kweye ghorofa [Cultural Factors] ili isije likawa halina maana kama Machinga Complex karume.

Lijengwe jengo Kubwa Pana kusijenngwe kuta ndani bali wazi kiasi cha kuweza kuwakatia vizimba vya kupanga bidhaa zao kwa mifumo ya kistaarabu.Kwenye eneo hilo kunaweza kuwa kunapatikana vyombo vya nyumbani tu [Home Appliance].

Kisha kuna Shule ya Serikali pale pembeni ya barabara ya Uhuru nayo si Mbaya inaweza Kutafutiwa eneo jingine wale vijana wakaamishwa pale eneo lile likawa UHURU MACHINGA HUB na ikibdi kujengwe Walking Flyovers ili Watu wawe wanavuka toka upande mmoja kwa kutembea kwenda upande mwingine.Yani kuwe na uwezo wa mtu kuvuka kwa juu toka Mtaa wa Kongo Karikakoo akaenda upande wa pili barabara ya Uhuru.

Kama kuna Majengo ya Msajili wa Majumba maeneo ya Mtakaa wa Kongo Karikakoo si mbaya pia Serikali kuwaomba National Housing kuona ni kwa namna gani wanaweza kupata plan ya kujenga Majengo ambayo yatawahifadhi Machinga wengi na kukidhi madhari nzuri yenye ubunifu wa kisasa na kuzidi kuipendezesha Kariakoo ili iendelee kuwa HUB ya Biashara kusini mwa jangwa la Sahara ikiwahudumia Malawi, Msumbiji, Kongo, Rwanda, Burundi, Sudani, Somaria, etc.

MITAA YA KARUME, LUMUMBA NA SAMORA POSTA
Hii mitaa inaweza kuwa na utaratibu ambao umeshaanza kuonekana wa kufungwa siku za jumamosi hasa Karume na Lumumba na wakienda hivyo wafike kuufunga mtaa wa Samora siku ya Jumapili ambayo wenye maduka yalio mtaa huu uwa wanafunga siku za Ijumapili hivyo nao unaweza kutumika kuwa mtaa mzuri kwa machinga wauza vitu vidogo vidogo.

2: JIJI LA MWANZA
Jiji la Mwanza kuna lile eneo lilo mbele ya Ofisi ya Mabasi ya Zamani ya Tanganyika yani [Stand ya Mabasi ya Zamani] eneo hili kwangu naona zile shughuri za baadhi ya mabasi kwenda mikoani kufanyika pale zingesitishwa pale na kuperekwa sehemu zingine na eneo lile ligeuzwe kuwa eneo ambalo machinga wanalitumia na kule kwenye kituo cha Taxi na Daladala kinachoangaliana na duka la Vunja bei napo kiwanja kile kinaweza kutumiwa na Wamachinga na kuboreshwa. Kwa hatu hizo hata Msongamano wa Magari maeneo hayo utapungua kama si kuisha kabisa.Ni swala la Mkoa na Wilaya kubuni eneo gani ligeuzwe kituo ambalo liko nje kidogo na vituo vunjwa.

Pia sio mbaya ile shule Kongwe pale mjini ya Pamba nayo kwa umri wake na kuongezeka kwa watu ni vyema nayo ikatoka pale yale majengo yake yakabuniwa vizuri na kuwa PAMBA MACHINGA HUB ..Uwepo wa shule ile pale mjini kati [City Centre] unachangia sana kushindwa kwa wanafunzi wengi sana wanaosoma shule hiyo...kwa kuwa na mazingira ambayo sio rafiki kwa vijana wetu wanaosoma hapo upelekea wengi kuanguka mitihani. Kwangu mimi kwa umri wa shule ile pale ni vyema sasa yakatafutwa maeneo tulivu wale vijana wakatolewa pale na kupisha eeo lile kuwa la Mikakati ya Shughuri za kibiashara jijini Mwanza.

MTAA WA MAKOROBOI
Huu pia unaitaji maboresho sana kuangalia namna ambayo ikibidi Mkoa husika unaweza kugharimika kuuboresha mlima unao hifadhi baadhi ya vibanda vya Wafanyabiashara hao kwa kupanua na kutegeneza mitalo ya kupitisha maji na kuweka Pavement ili kulifanya eneo hilo wakati wa masika liendelee kuwa zuri na la kuvutia. Kipindi cha Masika eneo la Makoroboi linatia Kinyaaa kwa kuwa ueguka kuwa na tope na miundo mbinu yake ya kupita sio iliyoboreshwa bali ni vijichochoro ambavyo ugeuka kuwa rojorojo la tope na kuvuluga kabisa eneo hilo zuri kwa huduma ya biashara ndogo ndogo ambazo mamilioni ya Watanzania ufaidika na hudma za eneo hilo.

HITIMISHO:
Machinga ni raia Watanzania ,wanaitaji fursa kama ambavyo wengine wanazo..Dunia nzzima inatambua uwepo wa Machinga ambao upewa majina mengi kama [Marching Guys, Street Hawkers, Vendors, Pedestrians etc.] hivyo kunaitajika ubunifu ikibidi kubadili mandhari ya umma tuliyoyazoea ili kuleta Mapinduzi ya Mandhari mpya ili Watanzania wengine nao wajione ni sehemu ya Taifa kufanyike Mapinduzi hayo.

Kulikua na tetesi wakati fulani Nyamagana miaka hiyo ya Nyuma kuna mtu alitaka apewe..ili afanye investment kwani Wananchi wa Mwanza Wakiulizwa watoe maoni yao kati ya kuwa na kiwanja cha Mpira na kuwa na Soko jipya eneo lile ushauri wao nini? Wananchi wataongea na kutoa maoni yao.

Machinga wanachopaswa kufanya ni kutii sheria, taratibu na kannuni zilizowekwa na mamlaka huku zile ambazo zinaonekana kuwa msumeno kwao zikiboreshwa ili nao kwa mujibu wa mazingira [FACTS] ziweze kuwafaha [Accomodate] na wao wafikie malengo yao ya kujenga Taifa lao kama Watanzania ambao ndio wenye Nchi na hayo maendeleo ni kwa faida yao.

Kazi kubwa watakuwa nayo viongozi wa Serikali ngazi ya Mtaa, Kata, Tarafa, Wilaya, Mkoa na Taifa kuwa na ubunifu [Creativity] ambao lengo lake ni kujenga na kuepuka migongano kwa kuangalia wapi majibu yasiyo na mawaa yanaweza kupatikana. Kwa Mkoa kuwa na watu maalumu wanao tizama njia za majibu wakiwa kama timu [Think tank] ya Mkoa ama Wilaya kupata majawabu ya maswala mazito ni suruhu njema ya kuboresha matatizo ya umma kwennda kuwa mafanikio ya umma.

View attachment 443508

Hongera sana, wazo limeshiba vya kutosha, ningekuwa mimi ningefanyia jaribio hata kwenye halimashauri moja kama role model baadaye nika excel kwingine
 
Back
Top Bottom