Tiba ya Loliondo: Tumekula nyama ya mtu tutawezaje kuacha? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tiba ya Loliondo: Tumekula nyama ya mtu tutawezaje kuacha?

Discussion in 'JF Doctor' started by KAMBOTA, Apr 4, 2011.

 1. K

  KAMBOTA Senior Member

  #1
  Apr 4, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  ….dhambi ya ubaguzi haina mwisho ni kama kula nyama ya mtu mkila hamtaacha…

  Haya ni maneno ya baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere wakati akituasa kuhusu athari za ubaguzi katika jamii yetu ambayo aliisema mwaka1995, kwake Nyerere ubaguzi ni sawa na dhambi ya kula nyama ya mtu ambayo anadai mtu akilifanya hili hawezi kuacha kamwe.
  Tangu kuibuka kwa mchungaji Ambilikile Mwasapile wa kanisa la KKT kule Loliondo kumejitokeza hali mbaya ya ubaguzi wa kidini, makabila, kanda na hata kimikoa. Pengine hata wewe msomaji wangu utashangazwa ubaguzi wenyewe uko wapi? Juzi nilipigiwa simu na msomaji wangu ambaye ni mtanzania kutoka nchini Uingereza Bw Awadh ambaye katika maelezo yake kuhusu tiba ya loliondo maarufu kama ‘kwa Babu’ hakusita kuweka wazi jinsi tiba hiyo inavyochangia kututafuna kama sio kudhihirisha hali ya ubaguzi wa kutisha miongoni mwa watanzania.
  Babu alipoanza kutibu, baadhi ya viongozi wa kanisa la KKT walijitokeza na kumuunga mkono lakini hawakuwahi kuwalazimisha watanzania kwenda huko bali watu wenyewe walianza kumiminika kwenda Loliondo sasa tatizo moja lilijitokeza kwa maaskofu wa mjini wapenda hela wakahofia kukosa waumini wa kuchangia sadaka wakaanza kumshambulia babu wa watu ambayye aalishaweka wazi kuwa tiba hiyo ni ya kiimani kwa hivyo wale waliotayari waende na kama mtu haamini basi asiende, sasa najiuliza kwanini maaskofu waanze kumtukana mzee yule? Au wanataka tuamini hawatosheki na fedha?
  Lakini wakati serikali ilipoadi kujenga barabara kwenda kwa babu huyo huko kijijini Samunge ambayo imechangiwa na baadhi ya viongozi mbalimbali kufika kwa babu na kupata kikombe cha dawa, ahadi hii ya serikali ndiyo haswa imetudhihirishia waziwazi kuwa Tannzania haipo salama kama wengi wetu tunavyodhani.
  Tangu ahadi hiyo itolewe kila kona ya nchi sasa kumeibuka wagawa vikombe kabla hata serikali haijasaini hiyo fedha ya kujenga barabara kukaibuka mgawa kikombe mwingine huko Mbeya na kabla masaa 24 hayaisha akaibuka mwingine huko Tabora na kabla huyu hajapata wateja wa kutosha tayari huko Morogoro akaibuka mwingine na kabla watu hawajajiuliza yupi zaidi sasa kaibuka mwingine huko Magu mkoani Mwanza na sasa nimepata taarifa kuna mwingine tena huko Songea, wote hawa kama Babu wanadai kuoteshwa na Mungu tena kwa staili ileile ya ila tofauti yao ni kiwango cha malipo huku baadhi wakiwataka watu kulipa 1,000 na wengine 700 tofauti na Babu ambaye anataka watanzania kulipa 500 na watu wa mataifa ya kigeni kulipa dola moja.
  Kuna hali ya hatari imejitokeza ambayo tunapaaswa kuwa nayo makini vinginevyo tunaua nchi yetu, mavuguvugu yote haya ya manabii yametokea baada tu ya serikali kuridhia kujenga barabara huko Samunge kwa babu je tujihoji hii ina ashiria nini? Je kwanini haya yote yaje mara baada ya ofa ya serikali kujenga barabara? Je huu sio ushahidi kuwa ‘manabii’ hawa wengine kupigania fursa za kimaendeleo tena kwa mbinu za kitoto? Madai yangu haya yanapewa nguvu kwa jinsi viongozi mbalimbali huku baadhi yao wakiwa wa serikali kwenda kupata vikombe kwa manabii hawa, je hatuoni hii inalenga kuifanya serikali itupie jicho huko? Kisha ipeleke fursa pia za kimaendeleo kama barabara na maji?
  Ndani ya kuibuka kwa manabii lukuki kuna hali ya udini wa baadhi ya watu kuzuiwa kuzuiwa kwenda Loliondo kwa vile Babu ni mkristo tena vilevile kuna malumbano ya madhehebu ya kikristo ambapo kama nilivyosema kuna baadhi ya ‘mabingwa wa miujiza ya kuponya’ wamewakataza waumini kwenda huko llakini sioni mantiki ya katazo lao hilo iwapo wao wameshindwa kuwapona na baadhi yao walikuwa wakwanza kwenda Loliondo kwa Babu, vilevile watu wa kila mkoa wanatamani kuwa na nabii wao kuliko kwenda Loliondo, huku nako watu wa kila kabila na kila kanda hawataki kwenda kanda ya kaskazini kwa wamasai na wachagga ingawaje Mwasapile si mchagga lakini yuko miongoni mwa wasonjo na wamasai kila kabila na kanda hawataki kujishusha wala kusalimu amri kwa Babu Mwasapile na wao wanataka wawe na manabii wao kwanini isiwezekane?
  Ndio maana nasema kuwa kwangu mimi nafurahi kuona kuwa sasa watanzania wanaonyesha tabia zao za ukweli , naona yaliyokuwa gizani yameletwa kwenye mwanga na yale yaliyokuwa chini yameletwa juu ili yaonekane waziwazi na katika migawanyo hii yote sioni matumaini upande wa serikali ambayo bilashaka sasa imezidiwa katika kushughulikia kuibuka kwa manabii kila uchao….Naam! hizi si zama za vikombe pekee bali pia ni zama za ubaguzi wa kidini, madhehebu, kanda na makabila, nini kitafuata? Serikali ifanye nini? na sisi wananchi tuchukue hatua gani kuponya mipasuko hii? …Tafakari!

  Kitendawili si deni ukishindwa nipe mji,
  Naam! Naandika ili nitukanwe nishaandika sasa nangoja kutukanwa!
  Nova Kambota Mwanaharakati,
  Nipigie; 0717-709618 au 0766-730256,
  Niandikie; novakambota@gmail.com
  Nitembelee; www.novatzdream.blogspot.com
  Tanzania, East Africa,
  Jumatatu April 04 , 2011.
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Apr 4, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kwani serikali iliyoahidi kujenga barabara huko ni ya dini gani? Vipi ndugu yangu na wewe unafikiria tumbo kama mwana UVCCM? Think before you leap! Sidhani dhana ya kujenga bara bara ya Samunge ilijikita kwenye udini au ubaguzi wowote ila kwenye ku-ease pressure ya mambo makubwa kama ya Dowans na hali ngumu ya maisha kwa ujumla kwa wananchi bila kujali dini na kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa kwani hata media karibu zote zimeweka loliondo kama their top priority! kanda au vyovyote vile! Sijui haya mawazo ya ubaguzi umeyakokotoa vipi, hebu tueleze tukuelewe!
   
Loading...