Tiba ya Kitoweo tembe yake munyu

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,794
Ni nani anataka kutibua tope la utelezi kwenye kidimbwi cha Ma J papa na Ma J kamongo? Kuna nyakati jina linaweza kuingia kwenye mgogoro mpaka unaweza kudhani limetupiwa kimavi kifurushi cha buku.

Ripoti ya awali imetoka. Hii sio ile ya wahishimiwa wanasiasa, hii ni ya wanataaluma, wasomi wa kaliba wenye weledi wao! Sasa sijui majaliwa ya Ma J zote mbili itakuwaje! Ile kubwa nzito na ile ndogo nyepesi... Je tutarudi kwenye vioo vya makamera na kusema tulipotoshwa halafu tukapotoka;? Tuupe muda wakati ni hakimu wa haki

Anyway tuachane na hayo maana uongo hupanda lift na kufika haraka lakini ukweli hukwea ngazi na kufika kwa kuchelewa! Lakini hufika! Ya Majaliwa zote mbili yanaanza kuwa masahibu! Ni nani huyo kazisagia kunguni hizi herufi zenye tarakimu 8? Mbona hizi ni shufwa na si witiri? Hivi kulikuwa na coincidence kwenye mfanano ama ni conspiracy ya kupangwa kama magazijuto? Kwamba lile dubwana litataga majini halafu mwokozi atakawa wajina? Lisemwalo lipo.

Kuna ya blaza Kakurwa, katibua kidimbwi. Kile kile ambacho kiliwahi kutibuliwa na mndewa half ray taratibu. Radio mbao za ushushushu wa kiswahel zinasema hawa wote ni kaka watatu na MaJ. Pengine kweli au sikweli. Sasa ni vikao kutwa kucha. Kidimbwi kinatokota maana kimeshaanza kukorogeka hasa.

Mboga ikiumwa dawa yake ni chumvi, sasa chumvi ikiumwa dawa yake ni ninini? Tabibu hajitibii wala kinyozi hajinyoi labda za chini. Sasa chumvi inaumwa yatakuwa maajabu ya mwaka kama itajitibu ama itapata tiba!

Juhudi zinafanyika za hali ya juu bro aliyeshikilia mkononi ripoti ya uchunguzi wa mali za chama chawala asikose koromeo akataka kumwaga mboga! Tutatafutana mpaka vilingeni.

Kuna vitenge vilivyogeuka mashuka
Kuna umeme wa vimulimuli
Kuna maji kama ya Kandoro(rip)
Kuna mwanangu yule yeye ni kukopa kwa kwenda mbele, dhamana ni mimi na wewe na vilembwe vyetu...!
sasa kumbe hata dona sio letu ni la jirani

Kwakweli sijui nilikuwa nataka niandike nini.. nimeshindwa kumalizia
Majaliwah keshaanza kozi na kapokewa na mkuu wa mkoa na ripoti ya awali ya ajali ya kitaalam nayo imetoka!

Kama huamini katika nyota hasa ya jaha.. Basi utakuwa na wivu mkali sana. Lakini isiwe nyota ya mchongo.
 
Ndege ya Air Tanzania inazunguka tu hapa Mwanza na inaonekana kama umeshindwa kutua.

20221123_143608.jpg
 
Kuna ya blaza Kakurwa, katibua kidimbwi... Kile kile ambacho kiliwahi kutibuliwa na mndewa half ray taratibu.. Radio mbao za ushushushu wa kiswahel zinasema hawa wote ni kaka watatu na MaJ.. Pengine kweli au sikweli.. Sasa ni vikao kutwa kucha.. Kidimbwi kinatokota maana kimeshaanza kukorogeka hasa..!
.
 
Majaliwa alikuwa wa kwanza kufika hapo na ndiye aliyefungua mlango kwa kutumia kasia na kuanza kuokoa watu.

Nimemnukuu katelefoni Ila hiyo ya hao watoa ripoti itakuwa wamekuja na chuki zao binafsi kwa W M
Wana wivu sana hawa wachunguzi wa kitaaluma
 
Kumbuka nguvu ya Hawa hata kwenye misahafu.. Ndiye kiumbe pekee aliweza kubonga na nyoka.. Labda huyu awe wa mchongo
Asije akawa kama mke wa Ayubu maana huo Utatu ni kama uko na extra power kama ilivyo kwa Mtumishi wa Bwana Ayubu.
 
Kuna watu wapo nje ya mchezo ndio wachezeshaji. Wanawaangalia tuu. Mwisho wa siku utasikia tuu kuna watu Wamejaa kwenye mtego ambao umeshawekwa. Tuupe muda wakati kujiandaa kupokea majibu.
 
Delilah anapangua safu ya 4:4:2 Ya Aliyekuwa mwenye Kanda yenye kidimbwi kikusanyicho maji ya Nile ya kimisri
 
Kuna watu wapo nje ya mchezo ndio wachezeshaji. Wanawaangalia tuu. Mwisho wa siku utasikia tuu kuna watu Wamejaa kwenye mtego ambao umeshawekwa. Tuupe muda wakati kujiandaa kupokea majibu.
Tuupe muda wakati kujiandaa kupokea majibu.
 
Back
Top Bottom