Tatizo la Gonjwa la Sukari (Diabets Mellitis): Fahamu chanzo, aina na ushauri wa tiba ya tatizo hili

S Sulayman,
mkuu umeeleza vyema sana ila wanga kwa mgonjwa wa sukari si chakula kimfaacho kabisa mpaka tuwe na uwezo wa kurekebisha kongosho lake liwe na uwezo wake wa awali,
Yote kwa yote ni elimu yako nzuri ni ipongeze na ni wakati wa wote kuishikilia na kuuishi ila tuboreshe yale yalopelea
 
Sawa Kaka, nimekuelewa vizuri. Una maoni gani kwa waliokuwa wanamkubali na wanakubali tiba zake, ili walikuwa wanapinga gharama zake kwamba ni kubwa sana?
Wanaompinga Dr.Sebi kuwa gharama zake ni lakini dawa zake zinaponyesha sio kutuliza mimi pia dawa zangu zina gharama na zinaponyesha kabisa sio kutuliza ugonjwa.Watu wamezoea kwenda Hospitali na kupewa dawa za kutuliza maradhi sio kuponyesha kwani dawa za Hospitali haziponyeshi bali zinatuliz amaradhi unapo tumia Vidonge au sindano zinakupa unafuu fulani lakini maradhi bado unakuwa nayo.Tofauti na dawa zangu za asili unapotumia unapona kabisa.
 
Wanaompinga Dr.Sebi kuwa gharama zake ni lakini dawa zake zinaponyesha sio kutuliza mimi pia dawa zangu zina gharama na zinaponyesha kabisa sio kutuliza ugonjwa.Watu wamezoea kwenda Hospitali na kupewa dawa za kutuliza maradhi sio kuponyesha kwani dawa za Hospitali haziponyeshi bali zinatuliz amaradhi unapo tumia Vidonge au sindano zinakupa unafuu fulani lakini maradhi bado unakuwa nayo.Tofauti na dawa zangu za asili unapotumia unapona kabisa.

Unauza bei gani dawa mzeee
 
HAMNA DAWA YA KISUKARI MKUU NI MATEPELI TU WATAKULA HELA ZENU. SANA SANA WATAKUPA MATAKATAKA YAO AMBAYO YATAENDE KUMALIZA FIGO KWA KUCHUJA HIYO SUMU YA HAYO MATAKATAKA WANAYUKUPA ,MWAKA JANA NILIMPOTEZA JIRANI YANGU KWA KUACHA KUTUMIA METROFOMIN NA INSULIN AKAWA ANATUMIA HAYO MATAKATAKA YA HAO MATAPELI MWISHONI ILE SUMU IKAUA FIGO ZOTE MBILI ,CHA MSINGI FUATA USHAURI WA DR NA DIET PIA MAZOEZI .KAMA UNAKUNYWA BEER ACHA KABISA. Nkingwamh,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mkuu, kisukati ni tatizo sana kwa mazingira na ulaji wetu, ajitahidi kushusha kiwango cha sukari, kiwe single digit, chini ya 10, atumie atibiotic kali ili kuua hao bacteria, na awe anatumia asali kama dawa kwenye kidonda ili kuwafanya bacteria wasisambae mwilini, asali ikiweka kwenye kidonda itawafanya bakteria wajikusanye kwenye kidonda na kupunguza uwezekano wa wao kusambaa mwilii, pole sana. Mm nimepoteza wadogo zangu wawili kwa kisukari n i m diabetic as well

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu k
Habari zenu wakuu?
Leo nimeenda kumuangalia Aunt yangu ambaye anasumbuliwa na kisukari,ana hali mbaya sana wakuu!
Ana kidonda kikubwa sana mguuni,usiku hapati usingizi kabisa.
Naombeni maoni yenu wakuu,ni namna gani naweza kumsaidia Aunt yangu?
Anateseka sana wakuu.
Kidonda chake ndio kinanipa wasiwasi sana.
Mkuu kidonda hicho chaweza pona kwa;
1.Kupunguza kiwango Cha sukari
2. Mpeleke hospitali ya karibu akoshwe kwa sprit VEMA na apakwe IODINE TINCTURE
 
Daah umenikumbusha my Mom (Rip) alipata kidonda kwenye Ankle( Enka) cha kisukari masikin tuliangaika hatimaye ya Mungu Mengi!! Namkumbuka sana mama na ni pengo kubwa kila nikilifikiria naumia sana.
 
Pole kwa kuuguza,zingatieni tu masharti ya wataalam.Mama yangu alianza kupata malengelenge mguuni Kisha kikawa kidonda,kidonda kilikua na hakikupona hadi akakatwa mguu,kabla hata ya kuruhusiwa kutoka hospital sukari ilipanda akafariki
Sent using Jamii Forums mobile app
Dah,pole sana Kiongozi...
Hata Aunt yangu kidonda chake kiliaanza kama malengelenge..!
 
Pole sana mkuu, kisukati ni tatizo sana kwa mazingira na ulaji wetu, ajitahidi kushusha kiwango cha sukari, kiwe single digit, chini ya 10, atumie atibiotic kali ili kuua hao bacteria, na awe anatumia asali kama dawa kwenye kidonda ili kuwafanya bacteria wasisambae mwilini, asali ikiweka kwenye kidonda itawafanya bakteria wajikusanye kwenye kidonda na kupunguza uwezekano wa wao kusambaa mwilii, pole sana. Mm nimepoteza wadogo zangu wawili kwa kisukari n i m diabetic as well
Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana mkuu...
Asante kwa ushauri wako pia..!
 
Pole Sana ndugu Mimi dingi yangu alikufa Kwa ugonjwa wa kisukari mwishoni mwa 1997 pia alipataga kidonda kama Hicho mguuni . Kidonda hakikuponaga ingawa alikuwa na mkwanja mrefu Ila Kwa sasa mtu ukiwa na cash unatravel kwenye developed countries kupata tiba Kwa bongo bado technology yetu ndogo

Sent using Jamii Forums mobile app
Am sorry for your loss.
 
Wapendwa hebu tujadili.Nilipima mwezi January nilikua na 1,22 g /L,nikapima February ikawa 1,16g/L,nikapima mwezi March ndani ya kila siku kumi na tano kwa mwezi nilikuwa 1,25g/L na 1,20 g/L respectively.Na pia nilipima mkojo wakakuta sukari .

Ila vipimo vyote hivyo nilichukua nikiwa nimefunga kula,inamaanisha kama napima kipimo kesho,leo kuanzia saa tatu usiku sili wala kunywa chochote mpaka nitakapochukuliwa kipimo kecho yake asubuhi.

Nilipoenda kumwona Dr alipoona kipimo cha mwisho akasema"Una kisukari"Nilimbishia maana mimi naona nipo kwenye limit.

Ila tokea kipimo cha kwanza nimeshaacha kabisa kula sukari,ingawa bado nakula wanga ,nafanya mazoezi.

Kiukweli hii stuation inaniumiza sana maana hata miaka 40 sijafika ingawa nimeshavuka miaka 30.

Sitaki kufa mapema kwa kisukari.
Tujadiliane wananzengo.

==============
Duniani takwimu zinaonyesha kila sekunde 10 mtu mmoja mwenye kisukari hufariki na zaidi ya watu 40,000 wenye kisukari Tanzania hukatwa miguu pia zaidi ya watu milioni 422 wana kisukari duniani hivyo kupelekea ugonjwa huu kushika nafasi ya 5 kama kisababishi cha vifo duniani. Ugonjwa wa kisukari ni moja ya ugonjwa unaowahangaisha watu wengi duniani kwani mtu anaweza akaishi na ugonjwa huu kwa muda mrefu takribani miaka 5 na kuendelea bila hata ya kujijua kuwa anatatizo la kisukari, kwa kiwango kikubwa hutokana na mfumo wa maisha wa mtu atakavyoamua kuishi, hivyo huu ugonjwa unaweza ukampata kila mtu mtoto kwa mtu mzima

Ugonjwa wa kisukari ni nini? ni ugonjwa unaotokana pale insulin inaposhidwa kubalansi sukari, ambayo homoni ya insulin hutengenezwa kwenye kongosho(pancreas) na kongosho inaposhindwa kufanya kazi vizuri hupelekea homoni ya insulin kupungua au kuongezeka na ndo hapo hutokea utofauti wa kisukari, pia ugonjwa huu hauambukizwi kutoka kwa mtu kwenda kwa mtu. Ikumbukwe kuwa kisukari huwapata mpaka watu wasio wanene(wembamba) na mama wajawazito

VISABABISHI VINAVYOPELEKEA MTU APATE UGONJWA WA KISUKARI.

Vyanzo vinavyopelekea mtu aweze kuwa mwathirika wa ugonjwa wa kisukali endapo asipovizingatia kwa umakini vyazo vikuu vipo vya aina mbili ambazo ni mfumo wa maisha na kurithi.

Mfumo wa maisha. Hii imekuwa sababu kubwa ya kuathiriwa na ugonjwa wa kisukari kwa haraka zaidi kuliko chochote na hii inatokana na ulaji (vyakula na vinywaji), kutokana na uandaaji wa vyakula kutoka vinalimwa hadi kuja kuingia kinywani mwa binadamu imekuwa ni changamoto kwa sababu ya kemikali zinazotumika kutunzia vyakula lakini pia na mtu yeye mwenyewe kama anapenda kula vitu vitamu vitamu ni kirahisi zaidi mtu huyo kuathirika kwa ugonjwa huu, uchunguzi uliofanyika huko marekani unasema kuwa mtu anaependa kula vyakula vyenye sukari nyingi au vitamu kuwa anakiwango kikubwa cha bacteria wabaya mwilini na hao bacteria hupendelea kula vitu vitamu kwahiyo inakuwa ni kirahisi sana kuchochea homone na kushidwa kwa kongosho kubalansi kiwango cha sukari mwilini.

Unene (obesity). Uzito uliopitiza kiwago ni moja ya sababu zinazopelekea mtu kuugua ugonjwa wa kisukari kwa sababu mwili wa mtu mnene unakuwa na sukari nyingi au kuwa na glucose nyingi

Kazi za ofisini. Mtu anaefanya kazi za kukaa kwa muda mrefu bila kufanya mazoezi anakuwa na hatari ya kuwa na kiwango kingi cha sukari kwa sababu anakuwa hafanyi zoezi lolote la kuweza kuunguza mafuta na sukari mwilini mwake hii ni tofauti na miaka ya 1980’s miaka hiyo watu wengi shughuri zao zilikuwa siyo za ofisini knazi zao nyingi zilikuwa za kuushughurisha mwili na hivyo ilikuwa ni kirahisi zaidi kuunguza mafuta bila hata ya kufanya mazoezi hii ni tofauti na sasa.

Kurithi. Haijafahamika kuwa nini sababu inayopelekea kurithi huu lakini kama kwenye ukoo kulikuwa na mgonjwa wa kisukari hivyo ugonjwa usishangae mtu kuugua kisukari bila hata ya hizo visababishi vya juu.

Baada ya kujifunza juu ya visababishi vinavyopelekea kuadhirika kwa ugonjwa wa kisukari hivyo ni muhimu kufahamu kuwa mtu anapokuwa na kisukari anakuwa na dalili zipi, zifuatazo ni dalili za mtu alie na ugonjwa wa kisukari.

DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI

Unapoona hizi dalili siyo kwamba ni moja kwa moja tayari una ugonjwa wa kisukari ni vema zaidi ukafika hospital ukachukua vipimo pale unapoona baadhi ya dalili ili kupata uhakika wa afya ya mwili wako japo dalili za mtu mwenye kisukali ni kama zifuatazo;

i. Kukojoa mara kwa mara. Mtu mwenye kisukari hukojoa mara kwa mara ni pamoja na insulin kushidwa kubalansi sukari mwilini na kufanya sukari iwepo kwenye damu nyingi ndo maana huchochea kukojoa mara kwa mara.

ii. Kiu isiyoisha. hii ni kwa sababu mwili wako unapoteza maji mengi kwa njia ya mkojo na hivyo husababisha mwili uhitaji mengi isivyo kawaida.

iii. Njaa kali. Ni kwasababu insulin yako haiwezi kubeba glucose mwilini mwako au hauna insulin ya kutosha ambayo husaidia kubeba lishe zilizomo kwa vyakula na kukufanya upate vitamin vya kutosha.

iv. Kuongezeka uzito. Hii inatokana na dalili ya kusikia njaa kali na hivyo humfanya mtu kula vyakula vingi na kwenda kuchochea homoni mwilini kufanya kazi pasivyo kawaida na ndio hapo unamkuta mgonjwa wa kisukali ananenepa tu.

v. Kupungua uzito. Hupungua uzito hasa pale mgonjwa wa kisukari anapokosa hamu ya kula na hivyo mwili wake hukosa lishe au virutubisha na kupoteza madini mengi mwilini mwake na seli zake hukosa chanzo cha chakula.

vi. Kukojoa mkojo na wadudu kama sisimizi na nzi kuuzingira. Kama nilivyosema hapo mwanzo kuwa bacteria wabaya wanapenda vitu vitamu hivyo na wadudu nao hivyo hivyo mgonjwa wa kisukari huwa anatoa mkojo wenye sukari nyingi na ndio maana huo mkojo unakuwa rafiki na wadudu.

vii. Kuchoka. Ili mtu awe na nguvu za kutosha ni lazima sukari ibadirishwe kutoka kwenye vyakula kwenda kwenye misuri, hivyo basi mgonjwa wa kisukari, sukari yake hubaki kwenye damu na siyo kwenye misuli na ndo maana huchoka bila hata kufanya kazi yoyote anaweza kuamka asubuhi kutoka kitandani na anakuwa kachoka.

MADHARA KWA MGONJWA WA KISUKARI NA BAADHI YA VIUNGO VINAVYOATHIRIKA ZAIDI.

Kupenda vitu vitamu hususani jamii ya sukari huwa ni tamu sana kwenye ulimi lakini changamoto inakuja kule inakoelekea kwa ajili ya kutunzwa na kutumika, hapo ndo husababisha changamoto mbalimbali mwilini hasa kwenye baadhi ya viungo vya mwili. Yafuatayo ni madhara ya sukari inapozidi mwili na kiwango sahihi cha sukari inayotakiwa mwili pale unapokuwa umekula chakula:

·vidonda vya miguuni (diabetes foots). Ugonjwa wa kisukari huathiri miguuni hasa pale unapopata ganzi inapelekea kushidwa kuhisi maumivu hivyo hata ukipata jeraha au mchubuko unakuwa huhisi maumivu ya aina yoyote unakuwa hauna tofauti na aliechomwa sindano ya ganzi kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji,
vidonda vya mtu mwenye kisukari ni vigumu sana kupona kwa sababu damu inakuwa haifiki ya kutoshakwenye kidonda na asilimia kubwa bacteria wabaya
huanza kukishambulia kwa kasi kwa sababu kinakuwa ni kitamu

diabetes6

kwa bacteria na kinaonekana kuwa na malengelenge ya mafuta na hao bacteria hushambulia kwa kasi hivyo kusababisha kuongezeka kwa kidonda na mwishoe kukatwa endapo hatawahi huduma mapema ya kujikinga.

Kutokuona vizuri au mtoto wa jicho. Mishipa ya kwenye macho huwa ni midogo midogo sana na iko laini sana ukiliganisha na mishipa ya sehemu zingine za mwili hivyo inapoingiliwa na sukari damu hushidwa kupita ya kutosha sehemu za macho na kumfanya mtu awe anaona ukungu ukungu au kutokuona kabisa.

Madhara ya figo. Figo inapokuwa imezidiwa na kiwago kingi cha sukari hulazimika kupunguza maji ya ziada na utengenezaji wa calcium kwa ajili ya kulinda mifupa hivyo sukari nyingi kukimbilia kwenye damu na baadaye huwa sumu mwilini.

Kiharusi (stroke). Kwa kuwa madhara ya sukari mojawapo ni kudhoofisha mishipa kwenye mwili hivyo mtu wa kisukari ana hatari kubwa ya kupata stroke kwa sababu baadhi ya mishipa kwenye ubongo huathiriwa na kukosa uwezo wa kupitisha damu ya kutosha na mwishoe kupasuka na kusababisha kiharusi.

Maradhi ya moyo. Vyanzo vya mishipa huanzia kwenye moyo na kusambaa pande zingine za mwili, moyo huathiriwa na ugonjwa wa kisukari kwa sababu sukari hudhoofisha mishipa na kumfanya mtu kuwa dhaifu hivyo kama damu haipiti ya kutosha kwenye mishipa inakuwa ni kirahisi kupata magonjwa ya moyo kama vile moyo kupanuka, moyo kuwa na tundo pamoja na kuongezeka kwa mapigo ya moyo.

·Kwa wanaume kuishiwa nguvu za kiume. Hili ni tatizo kubwa kwa wanaume kwa sababu mfumo wa uzazi wa mwanaume umeundwa kwa mishipa na misuli, kama patakuwa hakupati ujazo mzuri wa damu inakuwa ni rahisi sana kushidwa kushiriki tendo ndoa na wengi wao wanapopatwa na hali kama hii huigiwa na presha au msongo wa mawazo na kuibuia matatizo mengine tena.

Hayo ni baadhi ya madhara anayopatwa mtu mwenye kisukari japo anaweza kupatwa na changamoto zingine nyingi kwenye mwili wake na kumpelekea kupata shida awe mtoto au mtu mzima, lakini jinsi kwa kukosa uelewa na umakini zaidi kundi la watu wengi huishia kukatwa baadhi ya viungo na mwishoe kifo.

Lakini ujue kuwa kama ugonjwa siyo wa kuambukizwa itashidikanaje kuuzuia ili usiendelee kukudhuru usipatwe na madhara makubwa ya kiafya , moja ya suluhisho ambalo limesaidia watu kadha wa kadha linalotokana na mimea, mitishamba mboga mboga ambazo husaidia kurudisha ubora wa mwili kama mwanzo na badae unakuwa na afya njema jifunze kuhusu hii program inavyofanya kazi.


Changamoto ya kisukari inaweza kabisa kuepukika endapo tu ukiwa na nia ya kujiimarisha bila kukata tamaa ya kuitumia hii program, kama wengine imeweza kuwaimarisha na wakawa vizuri kwanini isiwe kwako pia. Kuna ubora gani kwa hii program.
  • Inasaidia kuogeza uwezo wa kinga mwilini na kukupa nguvu hivyo kuondoa uchovu wa bila sababu
  • Inaimarisha uwezo wa tendo la ndoa kwa pande zote kwa wanaume na kwa wanawake, pia inaimarisha tezi dume kwa wanaume.
  • Inaondowa hatari ya kupata kiharusi kwani hewa(oxygen) na damu vitakuwa inapita vyema kwenye ubongo
  • Inasaidia kuondoa sumu mwilini na kubalansi kiwango cha sukari mwilini kama imepanda zaidi huishusha na kama imeshuka zaidi huipandisha.
  • Inasaidia kuondoa bacteria wabaya na kuwapandisha uwezo wa utendaji kazi wa bacteria wazuri.
  • Inasaidia kuhakikisha mzunguko wa damu uko sawa na ujazo ulio sawa kwenye mishipa
  • Endapo kama tayari mwathirika anavidonda sehemu yoyote ya mwili hufanya kazi kukausha vidonda na kuondoa bila kuonyesha makovu.
  • Inaisaidia kongosho utoaji wa insulin kufanya kazi vizuri
  • Inamchanganyiko wa mbogamboga ambazo hufanya kazi ya kukupa damu na nyuzi nyuzi ili kusaidia upataji wa choo usiwe wa shida.
  • Inasaidia kuondoa matatizo ya macho na kuondoa mtoto wa jicho bila kukwanguliwa kwa kutumia vifaa
Hakuna changamoto ya kudumu chini ya jua vyote vina suluhisho, amuwa kuwa wa tofauti kwa kutafuta suluhisho kwa matendo. Wasiliana nasi ili kujua zaidi kuhusu kisukari na suluhisho lake kwani hatukuumbwa ili tuteseke na kisukari bali tuishi wenye afya tele.

=====

Magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni magonjwa ambayo hayasambazwi kwa mtu mwingine kwa kuwa hakuna vimelea mwilini vinavyohusiana na magonjwa hayo. Magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni kama ya moyo na mishipa ya damu, figo, saratani, kifua sugu, kisukari, magonjwa ya akili na mengine ya kurithi kama vile ugonjwa wa selimundu (Sickle Cell Disease).

Ripoti ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) ya 2013, inadai magonjwa yasiyo ya kuambukiza ndio chanzo kikubwa cha vifo ulimwenguni, yakifanya asilimia 63 ya vifo vyote kwa mwaka. Magonjwa yasiyo ya kuambukiza huua watu zaidi ya milioni 36 kila mwaka. Asilimia 80 ya vifo vinasababishwa na magonjwa hayo hutokea nchi zinazoendelea, Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi hizo. Inakisiwa kuwa mwaka 2020 magonjwa haya yasiyo ya kuambukiza yatasababisha asilimia 73 ya vifo vyote duniani na asilimia 60 ya ukubwa wa tatizo la magonjwa duniani.

Nchini Tanzania, katika mpango wa upimaji wa afya kwa magonjwa yasiyoambukiza jijini Dar es Salaam, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umebaini kuwa idadi kubwa ya wanaume wanapatwa na magonjwa hayo kuliko wanawake. Uchambuzi huo umeonyesha magonjwa yasiyoambukiza kama kisukari, shinikizo la damu na saratani zote ambazo zimekuwa chanzo cha vifo hivyo, huku serikali ikisema imeamua kuongeza juhudi za makusudi kupambana nayo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mfuko wa Bima ya Afya, athari ya magonjwa yasiyoambukiza ni mara nne zaidi ya watu waliopo mijini kuliko vijijini, huku asilimia 12.8 ya wanaougua wakiwa wako mijini na asilimia 3.1 wako vijijini kutokana na mfumo wa maisha.

Uchunguzi mwingine uliofanywa na jopo la madaktari bingwa kuanzia mwaka 2011 hadi 2014 ulibaini asilimia 79 ya watanzania wazee waligundulika kuugua magonjwa ya kisukari, macho na shinikizo la damu. Pia walidai magonjwa hayo yamekuwa kikwazo cha maendeleo kutokana na kuwasumbua wazee na hata wenye umri wa kati ya miaka 40 na 50.

Kisukari ikiwa ni moja ya muuaji wa kimya kimya katika kundi hili la magonjwa yasiyo ya kuambukiza. Watu milioni 285 duniani kote wameathiriwa na kisukari ambayo ni sawa na asilimia 6.6 ya idadi ya watu wote ulimwenguni pia ikishika nafasi ya 5 kwa kusababisha vifo duniani.

Nchi zinazoongoza kwa idadi kubwa ya watu wenye kisukari ni China wagonjwa milioni 43.2, India wagonjwa milioni 40.9, Marekani wagonjwa milioni 25.8, Urusi wagonjwa milioni 9.6 na Brazil wagonjwa milioni 6. Nchi zenye idadi kubwa ya watu wazima wenye kisukari ni Nauru kwa asilimia 30, Bahrain kwa asilimia 25.5, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kwa asilimia 25, Saudi Arabia kwa asilimia 23.7 na Mauritius kwa asilimia 20.

KISUKARI NI NINI HASWA?

Sukari mwilini hutokana na vyakula pamoja na vinywaji tunavyotumia kila siku na hutumika kuupa mwili nguvu. Glukosi ni aina ya sukari ambayo huzipa chembe za mwili nishati. Hata hivyo ili glukosi iingie ndani ya chembe hizo inahitaji insulini. Insulini ni kemikali (Homoni) ambayo hutokezwa na kongosho (Pancrease).

Kisukari ni ugonjwa unaotokana na mtu kuwa na sukari nyingi kupita kiasi kwenye damu. Ugonjwa huo huvuruga utaratibu wa kuingiza sukari ndani ya chembe kutoka kwenye damu kwa kuwa chembe huhitaji sukari ili kupata nishati.

Ugonjwa wa Kisukari hutokea pale ambapo tezi ya kongosho inaposhindwa kutengeneza kichocheo (Homoni) aina ya insulin au pale mwili unaposhindwa kutumia vizuri kichocheo hicho na kusababisha kuongezeka kwa sukari (Hyperglycemia) au kushuka kwa kiwango cha sukari (Hypoglycemia). Ugonjwa wa kisukari unaweza kusababishwa na kuwa na kiwango kidogo cha insulin mwilini, mwili kutosikia kichocheo hicho au yote mawili.

TAKWIMU MBALIMBALI ZA UGONJWA WA KISUKARI

Kulingana na ripoti mbalimbali karibu watu milioni 316 ulimwenguni pote wana kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu, ingawa wengi wao hawajui wana kiwango hicho. Kwa mfano, nchini Marekani pekee asilimia 90 ya watu wenye sukari nyingi kwenye damu hawatambui kama wana tatizo hilo. Ingawa asilimia 8.3 ya watu watu wa Marekani wana Kisukari ambayo ni sawa na watu milioni 25.8 na kufanya Kisukari cha 7 kusababisha vifo vya watu Marekani.

Mamilioni ya watu wana ugonjwa huo lakini hawana habari! Ni ngumu zaidi kutibu ugonjwa wa kisukari kwa kuwa mtu anaweza kuishi nao kwa muda mrefu kabla haujagunduliwa. Hiyo ndiyo sababu watu husema kwamba ugonjwa huo huua kimyakimya.

NINI CHANZO HASA CHA KISUKARI?

Ili kuelewa vyema ugonjwa wa kisukari ni muhimu kwanza kuelewa namna chakula kinavyovunjwa vunjwa na kutumiwa na mwili ili kuzalisha nguvu. Wakati chakula kinapoyeyushwa matukio kadhaa hutokea. Moja ni sukari inayoitwa glucosi ambayo ni chanzo cha nishati/nguvu mwilini huingia katika damu. Tukio la pili ni kiungo kinachoitwa kongosho (Pancrease) kutengeneza kichocheo cha insulini. Kazi ya insulini ni kuondoa glucosi katika damu na kuingiza katika misuli, seli za mafuta na ini, ambako hutumika kama nishati.

Watu wenye kisukari huwa na kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu kuliko inavyotakiwa kwa sababu miili yao haiwezi kupeleka sukari kwenye seli za mafuta, ini na misuli ili ihifadhiwe kwa ajili ya kuzalisha nguvu. Hii ni kutokana na moja ya sababu zifuatazo, huenda kongosho zao haziwezi kutengeneza insulini ya kutosha au seli za mwili wao haziathiriwi na insini kama inavyotakiwa au sababu zote hizo mbili.

Main Symptoms of Diabetes FikraPevu.com
Kama wewe ni mnene kupita kiasi, hufanyi mazoezi kwa ukawaida au una watu wa ukoo walio na kisukari, huenda tayari una kiwango cha juu cha sukari kwenye damu. Ongezeko la sukari kwenye damu mbali na kuwa kisababishi cha kisukari, hali hiyo inahusianishwa na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa akili uitwao 'DEMENTIA'.

Kula sukari nyingi sio sababu ya ugonjwa wa kisukari. Lakini lazima tuseme kwamba kula sukari nyingi si nzuri kwa afya yako kwani utaongeza uzito wa kuweza kuathiri uwezo wa mwili wako kujikinga na maradhi tofauti. Ugonjwa wa kisukari umeitwa kwa kufaa "ugonjwa unaoathiri kiini cha nishati ya mwili". Mwili unaposhindwa kutumia glukosi, mifumo mbalimbali ya mwili inaweza kuacha kufanya kazi au hata kusababisha kifo.

Ugonjwa wa Kisukari kitaalamu hujulikana kama 'DIABETES MELLITUS'. Jina 'Diabetes Mellitus' linatokana na neno la Kigiriki linalomaanisha 'kunyonya' na neno la Kilatini linalomaanisha 'tamu kama asali'. Maneno hayo yanafafanua vizuri sana ugonjwa huo, kwani maji hupita mwilini mwa mtu aliye na ugonjwa wa kisukari kana kwamba yananyonywa na mdomo na kupitia kwenye njia ya mkojo kisha kutoka nje ya mwili. Isitoshe mkojo huwa na ladha tamu kwa kuwa una sukari. Ndiyo sababu kabla ya kuvumbua njia bora za kupima ugonjwa huo, mbinu moja ya kutambua kama mtu ana ugonjwa wa kisukari ilikuwa kumwaga mkojo wa mgonjwa karibu na kichuguu cha sisimizi. Ikiwa sisimizi wangevutiwa na mkojo huo basi hilo lilimaanisha kwamba mkojo una sukari.

NI NANI ANAWEZA KUWA NA UGONJWA WA KISUKARI?

Watu walio katika makundi yafuatayo wana uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa wa kisukari:-

– Wenye uzito uliozidi,

– Wenye historia ya kuwa na wagonjwa wa kisukari katika familia zao,

– Wanawake waliozaa watoto wenye kilo 4 au zaidi,

– Watu wasiojishughirisha au wasiofanya mazoezi,

– Wenye shinikizo la damu,

– Wenye msongo wa mawazo na

– Wenye matumizi makubwa ya pombe na sigara.

Watu hawa wanashauriwa kupima sukari yao kila mwaka wakiwa na umri wa miaka 45 na kuendelea.

Kuna hatari kubwa ya kuugua ugonjwa huo ikiwa mtu ana mafuta mengi katika tumbo na kiuno chake kuliko katika mapaja yake. Mafuta katika kongosho na ini huvuruga uwezo wa mwili wa kudhibiti kiasi cha sukari kwenye damu.

Wavutaji wa sigara wanakabiliwa na hatari kubwa zaidi kwani zoea hilo hudhuru moyo na mfumo wa mzunguko wa damu na kubana mishipa ya damu. Kitabu kimoja kinasema kwamba asilimia 95 ya watu wanaougua kisukari ambao hulazimika kukatwa viungo ni wavutaji wa sigara.

DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI

~ Kunywa maji mengi kuliko kawaida na kusikia kiu kila wakati.
~ Kwenda haja ndogo mara kwa mara. Watoto kukojoa kitandani.
~ Kuwa dhaifu, kukosa nguvu na kujisikia mchovu kila wakati.
~ Kupungua uzito au kukonda licha ya kula vizuri.
~ Kusikia njaa kila wakati na kula sana.
~ Wanawake kuwashwa ukeni.
~ Kutoona vizuri.
~ Kupungua nguvu za kiume au hamu ya kujamiiana kwa wanawake.
~ Ganzi, kuchomwachomwa au kutohisi unapoguswa sehemu za miguu, viganja na vidole.
~ Miguu kuoza na hata kupata gangrini.
~ Kukaukwa na ngozi na pia kupata aina ya ngazi katika miguu.
~ Vidonda au majeraha sehemu yoyote ya mwili kutopona haraka.
~ Majipu mwilini.

Wenye dalili hizi wanashauriwa kupima sukari ili kubaini kama wana kisukari.
----------------------------
Ugonjwa wa Kisukari ni miongoni mwa magonjwa sugu yanayoendelea kuathiri afya za mamilioni ya watu wa nchi nyingi duniani ikiwamo Tanzania.
Ugonjwa huu hutokea pale ambapo tezi ya kongosho inaposhindwa kutengeneza kichocheo aina ya Insulin au pale mwili unaposhindwa kutumia vizuri kichocheo hicho na kusababisha kuongezeka au kushuka kwa kiwango cha sukari kwenye damu au hyperglycemia.

Aina za kisukari
Kisukari kimeanishwa katika makundi yafuatayo:

Kisukari Namba Moja
Hii ni aina ya kisukari inayowaathiri zaidi watoto na vijana. Aina hii hutokea iwapo seli maalum zinazotengeneza homoni ya insulin zijulikanazo kama beta cells of Islet of Langerhans. Iwapo tezi kongosho zitakosekana au zitaharibika kwa sababu yeyote ile, na hivyo kusababisha ukosefu kabisa au upungufu wa kichocheo hicho kwenye damu.

Mambo yanayoweza kusababisha uharibifu wa seli hizi katika tezi kongosho ni pamoja na kushambuliwa kwa tezi hiyo.
Mashambulizi katika kongosho huweza kufanywa na magonjwa yanayosababisha upungufu wa kinga ya mwili. Uharibifu katika tezi kongosho hupelekea kukosekana kabisa kwa wa tezi ya insulin au huifanya tezi hiyo kuzalishwa kwa kiwango kidogo.

Wagonjwa wa aina hii ya kisukari huhitaji kupewa dawa za insulin kwa njia ya sindano katika maisha yao yoteili waweze kuishi. Ndiyo maana aina hii ya kisukari huitwa pia kisukari kinachotegemea Insulin au Insulin Dependent Diabetes Mellitus (IDDM)

2. Aina ya Pili ya Kisukari
Hii ni aina ya kisukari inayotokea zaidi ukubwani. Aina hii ya kisukari husababishwa na kupungua kwa ufanisi utendaji kazi wa homoni ya insulin.

Hali hii husababishwa na unene uliopitiliza yaani obesity, au hali ya kutofanya mazoezi kabisa (physical inactivity).
Kwa vile, katika aina hii ya kisukari, insulin huzalishwa katika kiwango cha kutosha isipokuwa tatizo lipo kwenye ufanisi wa utendaji kazi wake.

Wagonjwa wa aina hii ya kisukari hawahitaji kupewa insulin kwa njia ya sindano. Ndiyo maana aina hii hujulikana pia kama kisukari kisichotegemea insulin au Non-Insulin Dependent Diabetes Mellitus (NIDDM)

3. Kisukari cha Ujauzito
Ni aina ya kisukari kinachotokea pindi kunapokuwa na ongezeko la kiwango cha sukari katika damu (hyperglycemia) wakati wa ujauzito. Aina hii ya kisukari huathiri karibu asilimia 2-5 ya wanawake wajawazit, ingawa wengi wao hupata nafuu na kupona kabisa mara tu baada ya kujifungua.

Hata hivyo, karibu asilimia 20 mpaka 50 ya wanawake wajawazito wanaopata aina hii ya kisukari huweza kuendelea nacho hatimaye kuwa aina ya pili ya kisukari maishani.

Kisukari husababishwa na nini?
Visababishi vya kisukari hutofautiana kulingana na aina husika ya kisukari.

1. Visababishi vya aina ya kwanza ya kisukari
Aina ya kwanza ya kisukari ina uhusiano mkubwa sana na kurithi. Aidha aina hii pia husababishwa na maambukizi ya Coxsackie virus type B4.

Visababishi vingine ni pamoja na sumu inayotokana na kemikali za baadhi ya vyakula (food borne chemical toxins), na kwa baadhi ya watoto wachanga maziwa ya ng’ombe yanaweza kuchochea kinga ya mwili wa mtoto kuushambulia mwili wenyewe (autoimmune reaction) na hivyo kupelekea uharibifu katika tezi kongosho.

2. Visababishi vya aina ya pili ya kisukari
Kwa ujumla aina hii ya kisukari husababishwa zaidi na mfumo wa maisha na matatizo ya kurithi. Aidha vitu kama kuongezeka uzito na unene kupita kiasi (obesity) nayo pia huchangia kutokea kwa aina hii ya kisukari.
Sababu nyingine ni pamoja na Kuongezeka umri, maisha ya kivivu na kutofanya mazoezi (physical inactivity).
 
Mkuu Cha kufanya hapo Ni kufuata ushaur wa daktar tu,,, punguza kula vitu Kama nyama kula Sana mboga mboga,, fanya mazoezi kwa Sana,,, kula ugali wa Dona au muhogo,, Kama unatumia bia inabidi uache kabsa,,,
Harafu punguza mawazo mkuu,,, huo Ni ugonjwa wa kawaida Kama utafuata vizur ushaur wa daktar,,, na ukaweza kuumantain,,,
 
Mkuu Cha kufanya hapo Ni kufuata ushaur wa daktar tu,,, punguza kula vitu Kama nyama kula Sana mboga mboga,, fanya mazoezi kwa Sana,,, kula ugali wa Dona au muhogo,, Kama unatumia bia inabidi uache kabsa,,,
Harafu punguza mawazo mkuu,,, huo Ni ugonjwa wa kawaida Kama utafuata vizur ushaur wa daktar,,, na ukaweza kuumantain,,,
Asante sana mate.
 
Kikubwa hapo ni kufuata ushauri Wa tabibu, mazoezi yanaluhusu na punguza sn vyakula vyenye sukari, bia soda acha nakuhakikishia ndani ya miezi 2 mpk 3 utashangaa kabisa!
 
Ke,jinsia ina uhusiano na kisukari au?
Kuna uhusiano sana, wanawake wenye umri wako huwa na kisukari.

Sababu ni hizi,
Moja, wanawake wengi hampendi kazi za kutoka jasho, kama kutembea au mazoezi yenye kutoa jasho.

Pili, wanawake wengi mnapenda sana kula vyakula vyenye protini kama nyama, mayai nk..hivi vitu ndo vinaongoza kusababisha kisukari.

Tatu, wanawake wengi kutokana na sababu hizo juu, wanawake wengi mmetumia sana dawa za hospitali, ambazo sasa zimeharibu mfumo wa utoaji sumu mwilini na hivyo mnaugua kisukari mapema.

Nne, wanawake wengi mmepunguza kuzaa sana na kunyonyesha sana, zoezi la kunyonyesha ni zuri maana huurekebisha mwili kiwa katika mfumo sahihi, wengi wanaonyonyesha huwa na uzito wa kawaida wa mwili na kutokana na kunyonyesha, wamama wengi hula vizuri ili kupata maziwa.

Nilijua tu kuwa wewe ni ke, ndo maana nikitaka co confirm.

Na kwa kuwa umenijibu kwa ujeuri sitakuambia njia rahisi ya kuondokana na tatizo lako hadi uniombe radhi hapa hapa.
Ili uende kwa hao madakatari wako waendelee kukutesa na tiba zao.
Amina.
 
Back
Top Bottom