Tiba ya Babu: Sababu za serikali kujikanyaga hapo awali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tiba ya Babu: Sababu za serikali kujikanyaga hapo awali

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Zak Malang, Mar 14, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0


  WanaJF:

  Nimejaribu sana kutafuta sababu kwa nini hapo awali Serikali ilijikanyaga kuhusu tiba ya babu wa loliondo – kwanza kusitisha utoaji huduma hiyo kwa kupitia Waziri wa Afya Dr Mponda kwamba dawa hiyo haijafanyiwa tathmini ya kisayansi, haijapata ruhusa ya TFDA et etc..

  Masaa 24 baadaye serikali hiyo hiyo kupitia Waziri wa ncvhi ofisi ya waziri mkuu Lukuvi alitengua amri hiyo ya awali kwamba Babu aendelee na serikali itamsaidia kwa gari na kuhusu masuala ya usafi wa mazingira ya eneo lile.

  Nilijiuliza sana kwa nini serikali ilikuja na kauli mbili tofauti kabisa katika masaa 24 tu kuhusu suala moja? Hatimaye nimepata jibu.

  Gazeti moja leo limeandika kwamba kumbe vigogo wengi wa serikali wakiwemo karibu nusu ya mawaziri walikwenda kupata kikombe – tena mwanzoni mwanzoni kabisa – kabla ya hali kuwa mbaya kutokana na umati mkubwa wa watu!

  Halafu pia tulisikia kwamba naye Bwana Mkubwa alipata kikombe akiwa sehemu moja la maeneo ya huko akiangalia nyayo za kale za binadamu kama kivutio cha utalii.

  Inavyoelekea Dr Mponda hakuwa anajua ya vigogo hao kupata vikombe na alitoa amri ya kusitisha tiba kutokana na msukumo wa kisheria na kimajukumu ya kikazi kama waziri wa afya na yeye mwenyewe akiwa Daktari. Hata sababu alizotoa ziliashiria hivyo kwamba tiba haijatestiwa (haijafanyiwa uchunguzi wa kitaalamu) kufuatana na sheria na kanuni zilizowekwa.

  Sasa amri ya Dr Mponda ilikuwa inakinzana moja kwa moja na imani ya Bwana Mkubwa na vigogo waliokwenda kunywa dawa hiyo – yaani amri ya waziri isingesitishwa, basi vigogo hawa wangejikuta wanasutwa na kuumbuka kwa kukumbatia dawa za ki-imani.

  Yaani fikiria hivi: Iwapo ije kuthibitika kwamba JK na vigogo wengine walikwenda kupata vikombe na huku serikali yake imepiga marufuku dawa hiyo hadi kwanza ithibitishwe ki-daktari. Hii ingekaa vipi machoni mwa raia?

  Hivyo mara moja agizo likabadilishwa na kwa mtazamo wangu – lilifanyika kisiasa zaidi kwa lengo la ‘kuwafariji’(ku-mitigate) hatua ya vigogo hao na JK mwenyewe kwamba wasionekane wapumbavu kwenda Loliondo kupata kikombe – kwani serikali yao pia naunga mkono.

  Ni mtizamo wangu.


   
 2. Mjanga

  Mjanga JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2011
  Joined: Feb 13, 2011
  Messages: 1,246
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145
  MTAZAMO WAKO UKO WAPI??? MBONA KAMA UNARIPOTI YALIYOJIRI KWENYE VYOMBO VYA HABARI MKUU??? SIKUSHAMBULII LAKINI!!!:ballchain:


   
 3. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,934
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Ukichanganya na kauli za maaskofu na vuguvugu la cdm..... kisiasa ilikuwa ni lazima watengue amri. Hii ndio Tanzania!
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Mar 14, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Kama ina-make sense vile! Hii serikali kila mkuu anatoa statement kivyake pale linapotokea suala kuu muhimu la nchi. Wakuu wangekaa pamoja na kujadili hili suala, wangekuja na msimamo mmoja tangu mwanzo. Lakini tatizo lingezuka -- waziri Mponda angelazimishwa tu kutoa taarifa ambayo ki-taaluma haiamini?

  Na ndiyo maana alitumiwa Lukuvi kutoa agizo la kutengua na siyo kutoka Wizarani. Nchi hii inaendeshwa ki-hovy hovyo, Mungu atusaidie.
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Mar 14, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Mimi nadhani ilionekana ni vigumu kuendelea kuficha kwenda Loliondo kwa vigogo hao kwani yangejulikana tu, na ndiyo maana wakaamua amri ya Wizara ya Afya itenguliwe kwa haraka isije -- kama unavyosema, hao vigogo walionekana kupata dawa huku kumbe imepigwa marufuku na serikali!
   
 6. Tekelinalokujia

  Tekelinalokujia JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 353
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hii ndio bongo yani kwanza unawahi then unaangalia sheria inasemaje ila kwa habari za babu imekaa kama national emergancy kwahiyo ndio hivyo, usicheze na life kabisaaaaaa, huku wengine wanawashauri waislam wenzao wasiende, huku si kutafutiana ubaya?
   
Loading...