Tiba ya Babu Loliondo: Wanasiasa tuliingizwa mkenge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tiba ya Babu Loliondo: Wanasiasa tuliingizwa mkenge

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mhabarishaji, Jun 23, 2011.

 1. M

  Mhabarishaji JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2011
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 1,001
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Tiba ya mchungaji wa Kainsa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Ambikile Mwasapile, imeingia dosari baada ya kuanza kupoteza umaarufu na idadi ya watu wanaokwenda kupata kikombe hicho kuanza kupungua kwa kasi, Sauti Huru limebaini.


  Tiba hiyo iliyodaiwa kutibu aina zote za magonjwa yakiwemo magonjwa sugu, ilianza kutolewa kwenye kijiji cha Samunge, miezi mitatu iliyopita na watu mbalimbali kumiminika kupata kikombe hicho kilichopigiwa mbiu na vyombo vya habari, viongozi wa dini na wanasiasa waandamizi.


  Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa, hivi sasa idadi ya watu wanaokwenda kupata tiba hiyo hivi sasa imepungua tofauti na iliyokuwa hapo awali, na inaelezwa hali hiyo imechangiwa na utata uliogubika tiba hiyo.
  Imebainika kuwa idadi kubwa ya watu ambao walikuwa wakienda kupata 'Kikombe' hicho hawajapona na wengine wamepoteza maisha muda mfupi tu baada ya kunywa dawa hiyo, na wapo ambao hali yao imezidi kuwa mbaya baada ya kunywa dawa hiyo; tofauti na imani iliyokuwa imejengwa kupitia matangazo ya vyombo vya habari kwamba tiba hiyo imetoka moja kwa moja kwa Mungu na haishindwi kitu.


  Mashaka zaidi kwenye dawa hiyo ni ukimya wa mamlaka husika ikiwemo taasisi ya utafiti wa madawa (NIMRI) ambayo zaidi ya kuthibitisha kwamba dawa hiyo haina madhara kwa binadamu anayeitumia imeshindwa kuweka wazi kama ni kwei inatibu magonjwa yanayotangazwa na mchungaji Mwaisapile.


  Aidaha imeelezwa kwamba wengi wa waliopata kikombe hicho hawakupona na badala yake magonjwa yao yameendelea kuwatesa na huku wengine wakipoteza maisha.


  Mkazi mmoja aishie Tabora Mjini aliyeongea na gazeti hili ambaye alikwenda na familia yake kunywa dawa hiyo amesema hakuona mabadiliko pamoja na kuwa na imani na dawa hiyo.


  "Naomba niwahakikishieni kwamba mimi nilienda Loliondo na mke wangu pamoja na wanangu mi nikiwa nasumbuliwa na sukari , mke wangu pumu na wanangu wawili wlikuwa wamepooza lakini hadi sasa niongeapo na wewe hali imerudi pale pale na labda tunaumwa zaidi", alisema Jumanne Mwanasali na Kuongeza; "Yaani tunajuta gharama kubwa tulizotumia kwenda Loliondo kusema kweli Serikali lazima ilaumiwe kwa kutuhamasisha kupitia vyombo vya habari lakini hakuna kilichotokea."


  Naye kiongozi mmoja wa siasa ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini amekiri kutopona kutokana na kikombe cha babu wa Loliondo na kudai walidanganyika.
  "Yani kama kuna wakati wanasiasa tumeingizwa mkenge basi ni katika tiba ya Loliondo. Nilienda na mke wangu, nimechoma mafuta kwenye gari langu nimekaa kwenye foleni siku tatu kwa maisha ya tabu nikajua nitapona kisukar, leo hali yangu ni mbaya zaidi hata kabla ya kwenda, ama kweli wajinga ndio waliwao", alisema mwanasiasa huyo wa upinzani mwenye ushawishi mkubwa nchini.


  Naye kijana mmoja anayeishi Mwananyamala amesema walimpeleka mama yao aliyekuwa anasumbuliwa na tatizo la kupooza upande mmoja kulikotokana na mshtuko wa moyo (stroke) lakini tangu walipotoka Loliondo, hali ya mama huyo imekuwa mbaya sana na hivi sasa wanahangaika sana ili kuokoa maisha yake.


  Habari zaidi kutoka maeneo kadhaa ya kuelekea Loliondo ikiwemo Mto wa Mbu zinasema biashara imeshuka sana kwenye maeneo hayo, pamoja na Samunge kwenyewe na kwamba hata nauli ya kuelekea huko nayo imeshuka.


  Nauli ya kwenda Loliondo ambayo kuna wakati ilikuwa ni kuanzia shilingi laki moja na hamsini elfu kwa mtu mmoja, hivi sasa imeshuka mpaka thelathini elfu na kuna uwezekano ikarudi kwenye bei yake ya kawaida ya shilingi elfu kumi na tano.


  Nayo bei ya chakula huko Samunge ambayo kuna wakati ilifikia shilingi elfu tano kwa sahani moja ya wali, hivi sasa imeshuka mpaka elfu moja na mia tano.


  Hata idadi ya wanasiasa waliokuwa wakimiminika kuelekea Samunge kila siku, wakiwemo wale waliokuwa wakitumia tiba hiyo ya babu kama mtaji wao wa kisiasa, hivi sasa hawaonekani tena kwa babu na wengine ambao licha ya kupata kikombe hawakupona wameanza kuhangaika kutafuta tiba nyingine zikiwepo za maombezi na waganga wa kawaida wa kienyeji.


  Mkazi mmoja wa Samunge alipoulizwa kama helikopta za mbunge wa Moshi mjini, Philemon Ndesamburo zinaendelea kwenda kijijini humo alisema hakumbuki ni lini aliiona helikopta hizo kwa mara ya mwisho.


  Itakumbukwa siku chache baada ya tiba hiyo kutangazwa na baadhi ya wataalamu wa tiba kuitilia shaka, walijitokeza watu maarufu katika jamii waliotumia lugha za kuilazimisha serikali iikubali, ukiwemo uongozi wa kanisa la KKKT jimbo la Arusha uliodai tiba hiyo ni mradi maalum wa kanisa hilo.


  SOURCE: Sauti Huru, Juni 22-28, 2011
   
 2. MANI

  MANI Platinum Member

  #2
  Jun 23, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,861
  Trophy Points: 280
  Ngoja PJ aje atupe maelezo maana alikuwa mstari wa mbele kupigia debe.
   
 3. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Sauti huru?!, unataka wanasiasa waendelee kumiminika huko?!, si uliambiwa kikombe ni mara moja?!, unataka waka- basti?!, unataka watu waendelee kumiminika huko hujui kama wagonjwa wanapona hivyo kupungua?!, biased anyway.
   
 4. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #4
  Jun 23, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Wewe kama huamini ni tatizo lako nina ndugu zangu karibia kumi wameenda na wamepona akiwemo mama yangu kaka na bibi na wengine,
   
 5. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #5
  Jun 23, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,738
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  How objective is the source?
  Magazeti mengine huwa always yako biased...
  Changanya na zako....
   
 6. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #6
  Jun 23, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mimi nina ushahidi wa dada yangu amepona kisukari na kansa ya mguu,niko tayari kuwaonyesha ni pm mtamuona na kuongea naye,alikuwa anajinyea hawezi kutembea sasa hivi ukimuona jamani acheni,wacha Mungu aitwe Mungu
   
Loading...