Tiba ya Babu Loliondo: Wanasiasa tuliingizwa mkenge

Mungu aliumba kifo na kila mwenye pumzi ataonja mauti ni makosa kudhani kuna dawa ya babu itatuepusha na mauti, kama ni hivyo Mungu asingeumba kuugua na hadi kufa..mimi naona suala hapa sio kupona au kufa kwa wagonjwa waliokwenda kwa babu bali ni uhakika wa tiba hiyo na uhusika wa Mungu kwenye tiba hiyo. Walikujaa duniani mitume wa Mungu wakafa ndio itakuwa sisi binadamu tuamini moja kwa moja kuwa Mungu katelemsha dawa hiyo ili tusife au tusiugue............. A BIG NOOOOOOOOOOOOOOOOO
 
suala la tiba ya babu sio la kanisa la KKKT tu kwani waliokwenda huko ni watu wa dini zote( Waislamu, wakristo, wahindu, budha nk), kama ni suala la imani basi dini zote ziliwakilishwa kupata kikombe cha babu.....
 
nilishawahi kut6oa taadhari juu ya babu na tiba yake na wengi walinielewa wengine waliniporomoshea matusi,ukweli watanzania hafikir vyema kabla ya kutenda
 
Mungu atakusaidia tu ipo siku
Nimehangaika na ninaendelea kuhangaika tu. Atakuwa amechelewa kunisaidia. Wewe tengeneza mbinguni yako hapahapa duniani basi. Ukishakufa ni kuoza tu. Hakuna watu wameivuruga na kuigawa dunia hii kama YESU na Mtume MOHAMAD S.A.W.
 
Hii imekaa hivi:

Mtu ana tatizo la kiafya, kubwa, dogo, la muda mrefu, linaloleta maumivu makali, linalokuzuia kufanya shughuli zako, nk
Umehangaika weee, hospitali, kwa waganga, kwa lusekelo, kwa lwekatare, kwa maalim fulani pemba, nk

Kakuna nafuu,

Unaamua kwenda kwa babu kupata kikombe,

Umepata nafuu, umepona unashukuru unasonga mbele,

La unaendelea kutafuta.

Ya babu ni tiba mbadala tuu,

Zipo nyingi kama hizo.

Gharama ni sehemu ya tiba, haiepukiki.
 
Wapo wanaosema Mungu hayupo ni haki yao kwani vitabu vitakatifu vimetueleza kuwa kuna wapagani au makafri ni watu wasiotambua kuwepo kwa Mungu. Werevu wanasema ni heri ukamtambua ili siku ya kiama uwe mmoja ya watakaookoka na adhabu ya Mungu kwani kuabudu hakuna gharama yoyote zaidi ya kuamini tu. Ni kama unavyoweza kuamini kwamba bila mimi au wewe kujua mumeo au mkeo anaweza kuvunja uaminifu pasipo mwenza kujua kwani ndio mapungufu ya binadamu.
 
Nimehangaika na ninaendelea kuhangaika tu. Atakuwa amechelewa kunisaidia. Wewe tengeneza mbinguni yako hapahapa duniani basi. Ukishakufa ni kuoza tu. Hakuna watu wameivuruga na kuigawa dunia hii kama YESU na Mtume MOHAMAD S.A.W.
.

Dini zimechangia sana kuivuruga dunia hilo halina ubishi na baadhi wanatabiri kwamba hata kama Mungu yupo kwa tunaoamini lakini dini zitaendelea kupoteza umaarufu na waumini wa kweli kadri tunia inavyosonga mbele. Dini zimekuwa chanzo cha machafuko, vita, mifarakano na migongano katika jamii kila dini ikijipa haki ya kutawala duniani na pengine kufuta haki ya dini zingine. Sina hakika kama ubnafsi huu ni uumbaji wa Mungu ambaye kama hakufanya makusudi kuumba dini nyingi angeweza kuifanya dunia kuwa ya dini moja bila sisi kuhangaika kwa naiba yake. Mambo haya ndio baadhi ya watu hawaamini kama Mungu yupo na ana nguvu zenye kuweza yote.
 
Sheikh Yahaya alikuwa mnajimu na kutiba wagonjwa na hapohapo mwanazuoni maarufu wa dini ya Kiislamu bado wenye kuamini kuna Mungu hawakuona taabu kwenda kwake bila kujali dini zao ni matokeo hayo hayo tukajikuta tunakwenda tena kwa babu wa dini ya kikristo loliondo kupata tiba kwa jina la Mungu.
 
Sasa watu waendelee kwenda wanini tena wakati walishapona kwani tz yote ilikuwa na ugonjwa! Halafu hilo gazeti lako ni udaku tu wamepungua sababu wamepona !
 
Sheikh Yahaya alikuwa mnajimu na kutiba wagonjwa na hapohapo mwanazuoni maarufu wa dini ya Kiislamu bado wenye kuamini kuna Mungu hawakuona taabu kwenda kwake bila kujali dini zao ni matokeo hayo hayo tukajikuta tunakwenda tena kwa babu wa dini ya kikristo loliondo kupata tiba kwa jina la Mungu.
Hata Osama bin Laden aliua kwa kutumia jina la Mungu na DINI yake. Aliungwa mkono na wengi tu.
 
Mungu aliumba kifo na kila mwenye pumzi ataonja mauti ni makosa kudhani kuna dawa ya babu itatuepusha na mauti, kama ni hivyo Mungu asingeumba kuugua na hadi kufa..mimi naona suala hapa sio kupona au kufa kwa wagonjwa waliokwenda kwa babu bali ni uhakika wa tiba hiyo na uhusika wa Mungu kwenye tiba hiyo. Walikujaa duniani mitume wa Mungu wakafa ndio itakuwa sisi binadamu tuamini moja kwa moja kuwa Mungu katelemsha dawa hiyo ili tusife au tusiugue............. A BIG NOOOOOOOOOOOOOOOOO

wewe hujaelewa...
Lini babu kasema ile tiba ya kikombe ni kinga ya magonjwa au kinga ya kifo?!!!
 
Nimehangaika na ninaendelea kuhangaika tu. Atakuwa amechelewa kunisaidia. Wewe tengeneza mbinguni yako hapahapa duniani basi. Ukishakufa ni kuoza tu. Hakuna watu wameivuruga na kuigawa dunia hii kama YESU na Mtume MOHAMAD S.A.W.

Hujachaguliwa bado na Mungu,..siku akikuteua huna jinsi,utanena lugha moja na waumini... kwa sasa hao unaoona wanaomuabudu amewateua,si wao waliomchagua bali kawachagua yeye! ni kwa rehema tu ! Wapo watu walokuwa na kashfa na dharau mara 1000 ya hayo maneno yako,lakini ilipofika Mungu akasema njoo unitumikie ikawa!
 
Hakuna aliyevunja record yake popote duniani,amenywesha watu millioni 4.8 kwa miezi mitatu hii ni record ya kuingia guiness book of records,na kwa maana hiyo aliwafika asilimia 10 ya watanzania wote katika kipindi hicho kifupi,kwa maana nyingine wote waliojihisi wagonjwa kawa maliza wanaokwenda sasa hivi wanaenda kufanya utalii
 
Ishu sio mti anaotumia ishu ni tiba yake. Ni kama vile Mmea wa Bangi una matumizi mengi tu, lakini ubaya na uzuri wake upo katika matumizi hivyohivyo mmea wa coke, usipindishe hoja, hoja si mmea, hoja ni tiba ya babu
 
Sheikh Yahaya alikuwa mnajimu na kutiba wagonjwa na hapohapo mwanazuoni maarufu wa dini ya Kiislamu bado wenye kuamini kuna Mungu hawakuona taabu kwenda kwake bila kujali dini zao ni matokeo hayo hayo tukajikuta tunakwenda tena kwa babu wa dini ya kikristo loliondo kupata tiba kwa jina la Mungu.

Uislamu uko wazi kabisa na unasema muislamu ni nani na anatakiwa afanye nini, yupi ataacha kuwa muislamu atakapofany nini? Uislamu si jina kuitwa Yahaya au Mrisho, uislamu ni matendo ndio maana uislamu hauna kiongozi mmoja duniani na wala hawasubiri kupokea amri ya kiongozi yeyote, waislamu wana amini katika Muongozo wa Quran. Katu usihusishe mtu fulani na uislamu kwa vile tu ana jina la kiislamu au kwa vile ni kiongozi wa BAKWATA, mjue muislamu kwa kujua Quran inasema muislamu ni nani. Hili ni rahisi kweli siku hizi quran ipo katika mtandao soma tafsiri yake, utamjua muislamu wala hutapata shida kama uliyonayo sasa
 
Nimehangaika na ninaendelea kuhangaika tu. Atakuwa amechelewa kunisaidia. Wewe tengeneza mbinguni yako hapahapa duniani basi. Ukishakufa ni kuoza tu. Hakuna watu wameivuruga na kuigawa dunia hii kama YESU na Mtume MOHAMAD S.A.W.

Bado hajachelewa, kwani unajua utakufa lini wewe hadi useme amechelewa kukusaidia!!!!!!!!!!!! Nahisi unahitaji maombi and am one of those people wataokuombea ili umjue Mungu na matendo yake makuu. Ipo siku neema itakuangukia tu, usikate tamaa
 
"Katengeneze mambo ya nyumbani kwako, maana utakufa leo hii, na hautapona ugonjwa wako" haya ni maneno yaliyoko kwenye maandiko matakatifu ya biblia. sasa huyo jamaa wa tabora gazeti linamnukuu peke yake, watu zaidi ya milioni 20 wameshakunywa kikombe cha babu, inakuwaje gazeti linamnukuu yeye peke yake?
Isije kuwa ni yule jamaa aliyepelekwa na Rostam kupata kikombe na Rostam baadaye akadai dawa ya babu haiponyeshi. Itaponyeshaje wakati bado hajajisafisha kiimani?
Hata Ngurumo ya Upako alipokwenda kunywa ile dawa alikataliwa kunywa kwa kuwa ilionekana hayuko safi!

Kwa maelezo yako hata watoto wadogo wanamaradhi sugu Tanzania. 20 millioni ni karibu nusu ya Watanzania nafikiri tungekuwa na mashuhuda humu wengi tu. Ikiwa ni kweli hesabu zako basi Gazeti liko sahihi na ndio maana walioingizwa mjini hawataki kujitokeza kukubali uzembe wao.
 
.

Dini zimechangia sana kuivuruga dunia hilo halina ubishi na baadhi wanatabiri kwamba hata kama Mungu yupo kwa tunaoamini lakini dini zitaendelea kupoteza umaarufu na waumini wa kweli kadri tunia inavyosonga mbele. Dini zimekuwa chanzo cha machafuko, vita, mifarakano na migongano katika jamii kila dini ikijipa haki ya kutawala duniani na pengine kufuta haki ya dini zingine. Sina hakika kama ubnafsi huu ni uumbaji wa Mungu ambaye kama hakufanya makusudi kuumba dini nyingi angeweza kuifanya dunia kuwa ya dini moja bila sisi kuhangaika kwa naiba yake. Mambo haya ndio baadhi ya watu hawaamini kama Mungu yupo na ana nguvu zenye kuweza yote.

Kama unakusudia dini za haki zilizoletwa na Mwenyezi Mungu umekosea sana. Hakuna dini za haki zilizochafua dunia lakini ni kinyume chake.
Uzaifu wa binaadamu haujaletwa na dini bali na vitendo vya kishetani na vitendo vizuri kamwe haviwezi kuiharibu dunia.
Tafuta mtu anaefuata maelekezo ya dini yake na umuweke pamoja na watu wenye sifa ambazo zimekatazwa na dini kama ulevi, uzinifu, fitina, uchoyo ,ukatili, ufisadi na vyenginevyo halafu uangalie wepi wana sifa za kuchafua dunia. Mtu anapoitumia dini kwa maslahi na hamu yake dini haiwezi kubebeshwa msalaba.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom