Tiba ya Babu Loliondo: Wanasiasa tuliingizwa mkenge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tiba ya Babu Loliondo: Wanasiasa tuliingizwa mkenge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mhabarishaji, Jun 23, 2011.

 1. M

  Mhabarishaji JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2011
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 1,001
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135

  Tiba ya mchungaji wa Kainsa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Ambikile Mwasapile, imeingia dosari baada ya kuanza kupoteza umaarufu na idadi ya watu wanaokwenda kupata kikombe hicho kuanza kupungua kwa kasi, Sauti Huru limebaini.


  Tiba hiyo iliyodaiwa kutibu aina zote za magonjwa yakiwemo magonjwa sugu, ilianza kutolewa kwenye kijiji cha Samunge, miezi mitatu iliyopita na watu mbalimbali kumiminika kupata kikombe hicho kilichopigiwa mbiu na vyombo vya habari, viongozi wa dini na wanasiasa waandamizi.


  Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa, hivi sasa idadi ya watu wanaokwenda kupata tiba hiyo hivi sasa imepungua tofauti na iliyokuwa hapo awali, na inaelezwa hali hiyo imechangiwa na utata uliogubika tiba hiyo.
  Imebainika kuwa idadi kubwa ya watu ambao walikuwa wakienda kupata 'Kikombe' hicho hawajapona na wengine wamepoteza maisha muda mfupi tu baada ya kunywa dawa hiyo, na wapo ambao hali yao imezidi kuwa mbaya baada ya kunywa dawa hiyo; tofauti na imani iliyokuwa imejengwa kupitia matangazo ya vyombo vya habari kwamba tiba hiyo imetoka moja kwa moja kwa Mungu na haishindwi kitu.


  Mashaka zaidi kwenye dawa hiyo ni ukimya wa mamlaka husika ikiwemo taasisi ya utafiti wa madawa (NIMRI) ambayo zaidi ya kuthibitisha kwamba dawa hiyo haina madhara kwa binadamu anayeitumia imeshindwa kuweka wazi kama ni kwei inatibu magonjwa yanayotangazwa na mchungaji Mwaisapile.


  Aidaha imeelezwa kwamba wengi wa waliopata kikombe hicho hawakupona na badala yake magonjwa yao yameendelea kuwatesa na huku wengine wakipoteza maisha.


  Mkazi mmoja aishie Tabora Mjini aliyeongea na gazeti hili ambaye alikwenda na familia yake kunywa dawa hiyo amesema hakuona mabadiliko pamoja na kuwa na imani na dawa hiyo.


  "Naomba niwahakikishieni kwamba mimi nilienda Loliondo na mke wangu pamoja na wanangu mi nikiwa nasumbuliwa na sukari , mke wangu pumu na wanangu wawili wlikuwa wamepooza lakini hadi sasa niongeapo na wewe hali imerudi pale pale na labda tunaumwa zaidi", alisema Jumanne Mwanasali na Kuongeza; "Yaani tunajuta gharama kubwa tulizotumia kwenda Loliondo kusema kweli Serikali lazima ilaumiwe kwa kutuhamasisha kupitia vyombo vya habari lakini hakuna kilichotokea."


  Naye kiongozi mmoja wa siasa ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini amekiri kutopona kutokana na kikombe cha babu wa Loliondo na kudai walidanganyika.
  "Yani kama kuna wakati wanasiasa tumeingizwa mkenge basi ni katika tiba ya Loliondo. Nilienda na mke wangu, nimechoma mafuta kwenye gari langu nimekaa kwenye foleni siku tatu kwa maisha ya tabu nikajua nitapona kisukar, leo hali yangu ni mbaya zaidi hata kabla ya kwenda, ama kweli wajinga ndio waliwao", alisema mwanasiasa huyo wa upinzani mwenye ushawishi mkubwa nchini.


  Naye kijana mmoja anayeishi Mwananyamala amesema walimpeleka mama yao aliyekuwa anasumbuliwa na tatizo la kupooza upande mmoja kulikotokana na mshtuko wa moyo (stroke) lakini tangu walipotoka Loliondo, hali ya mama huyo imekuwa mbaya sana na hivi sasa wanahangaika sana ili kuokoa maisha yake.


  Habari zaidi kutoka maeneo kadhaa ya kuelekea Loliondo ikiwemo Mto wa Mbu zinasema biashara imeshuka sana kwenye maeneo hayo, pamoja na Samunge kwenyewe na kwamba hata nauli ya kuelekea huko nayo imeshuka.


  Nauli ya kwenda Loliondo ambayo kuna wakati ilikuwa ni kuanzia shilingi laki moja na hamsini elfu kwa mtu mmoja, hivi sasa imeshuka mpaka thelathini elfu na kuna uwezekano ikarudi kwenye bei yake ya kawaida ya shilingi elfu kumi na tano.


  Nayo bei ya chakula huko Samunge ambayo kuna wakati ilifikia shilingi elfu tano kwa sahani moja ya wali, hivi sasa imeshuka mpaka elfu moja na mia tano.


  Hata idadi ya wanasiasa waliokuwa wakimiminika kuelekea Samunge kila siku, wakiwemo wale waliokuwa wakitumia tiba hiyo ya babu kama mtaji wao wa kisiasa, hivi sasa hawaonekani tena kwa babu na wengine ambao licha ya kupata kikombe hawakupona wameanza kuhangaika kutafuta tiba nyingine zikiwepo za maombezi na waganga wa kawaida wa kienyeji.


  Mkazi mmoja wa Samunge alipoulizwa kama helikopta za mbunge wa Moshi mjini, Philemon Ndesamburo zinaendelea kwenda kijijini humo alisema hakumbuki ni lini aliiona helikopta hizo kwa mara ya mwisho.


  Itakumbukwa siku chache baada ya tiba hiyo kutangazwa na baadhi ya wataalamu wa tiba kuitilia shaka, walijitokeza watu maarufu katika jamii waliotumia lugha za kuilazimisha serikali iikubali, ukiwemo uongozi wa kanisa la KKKT jimbo la Arusha uliodai tiba hiyo ni mradi maalum wa kanisa hilo.


  SOURCE: Sauti Huru, Juni 22-28, 2011

   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,449
  Likes Received: 22,365
  Trophy Points: 280
  mkome kushoboka ovyo na vitu viogeni. Babu saa hizi ni bilionea, bonge la mbunifu
   
 3. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Kafanye utafiti upya. Babu hakuanza kutoa tiba miezi mitatu iliyopita. Na utakapopata majibu uje utuambie majibu kuhusu tafiti zilizofanywa juu ya mti unaotumiwa na babu kwenye tiba.
   
 4. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #4
  Jun 23, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Babu aulizwe kwa nini watu hawaponi? Imani hapa si ishu tena
   
 5. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #5
  Jun 23, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Hilo gazeti gani tena
   
 6. Bundewe

  Bundewe JF-Expert Member

  #6
  Jun 23, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 401
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Madaktari wanaulizwa watu wanaofia hospitali?
   
 7. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #7
  Jun 23, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  nanyi mkiijua KWELI, hiyo KWELI itawaweka huru

  mbarikiwe na Bwana
   
 8. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #8
  Jun 23, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Babu ni mjasiriamali ameshatoka kimaisha sasa hivi. wale mliofikiria babu alitumwa na mungu imekula kwenu!
   
 9. T

  Technology JF-Expert Member

  #9
  Jun 23, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 733
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 60
  We told you!
   
 10. L

  LAT JF-Expert Member

  #10
  Jun 23, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  Sauti Huru ni gazeti gani hili? la udaku nini?
   
 11. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #11
  Jun 23, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,849
  Likes Received: 474
  Trophy Points: 180
  Ulienda kufanya nini???? ni kiherehere chako ukome.Cardinal pengo aliwahi kuhojiwa akatoa msimamo kuwa: watuwatakuwa wanapona kwa illusion na si tiba itokanayo na miujiza ya mungu kama ambavyo dawa ile ilitangazwa.Asiyesikia la mkuu sasa kaota tende
   
 12. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #12
  Jun 23, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Gazeti lenyewe sauti .Hizo ni isiha tu.UKUONYESHA UTAFITI WA HILO UNALOSEM
   
 13. T

  The GreatMwai Member

  #13
  Jun 23, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbona hata yeye anasema tuombe kupitia Bikira Maria anaponyesha lakini watu bado wanaugua na wanakufa na yenyewe ni illusion.
   
 14. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #14
  Jun 23, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  "Katengeneze mambo ya nyumbani kwako, maana utakufa leo hii, na hautapona ugonjwa wako" haya ni maneno yaliyoko kwenye maandiko matakatifu ya biblia. sasa huyo jamaa wa tabora gazeti linamnukuu peke yake, watu zaidi ya milioni 20 wameshakunywa kikombe cha babu, inakuwaje gazeti linamnukuu yeye peke yake?
  Isije kuwa ni yule jamaa aliyepelekwa na Rostam kupata kikombe na Rostam baadaye akadai dawa ya babu haiponyeshi. Itaponyeshaje wakati bado hajajisafisha kiimani?
  Hata Ngurumo ya Upako alipokwenda kunywa ile dawa alikataliwa kunywa kwa kuwa ilionekana hayuko safi!
   
 15. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #15
  Jun 23, 2011
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Huyo Ngurumo ya Upako ni nani kwani? Wewe ulikuwa unaamini kwamba kile anachofanya babu ni mpango wa Mungu aliye hai? Basi umekosea sana. By the way kuna miungu mingi sana lakini Mungu aliyehai ni mmoja tu,anayestahili kuabudiwa na kutukuzwa! kikombe cha babu ulikuwa mpango wa shetani juu ya wanadamu period!
   
 16. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #16
  Jun 23, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  sijasema ni mpango wa mungu au ni mpango wa shetani, kwa sababu sijui, nilichokuwa nasema ni kwamba watu wamekunywa dawa ya babu zaidi ya milioni 20, lakini gazeti limemquote mtu moja tena kutoka tabora, ambapo tokea mwanzo walishapinga kuwa babu ni mchawi.
   
 17. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #17
  Jun 23, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Ukweli utabaki kuwa ukweli! Fatilieni taratiiiibu mtajua kama kweli inatibu au la. Mwenzenu sijui na wala sitaki kujua, ila nikitaka nitajua ukweli
   
 18. w

  wanan Senior Member

  #18
  Jun 23, 2011
  Joined: May 11, 2011
  Messages: 143
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  imekula kwako angalia maandiko matakatifu sio kila jambo ni la heri usiku mwema jalribu kutafuta mchana upo wapi
   
 19. L

  LAT JF-Expert Member

  #19
  Jun 23, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  watu wameshapona na wengine hawajapona sasa unataka waendelee kwenda kwenda Loliondo kufanya nini

  au unawombea watu waendelee kuugua maradhi
   
 20. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #20
  Jun 23, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  "MAOMBEZI". Nadhani hiyo ndiyo driving force ya kuandikwa hii stori.
   
Loading...