Tiba ya Babu Imeleta Maafa - Chama Cha Madaktari

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,809
Tiba ya Babu Imeleta Maafa - Chama Cha Madaktari

Babu1%2813%29.jpg

Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapila

Chama cha Madaktari nchini (MAT) kimesema tiba inayotolewa na Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Masapila, kwa njia ya "kikombe" kwa ajili ya kutibu magonjwa sugu, imeleta maafa makubwa kwa wagonjwa.

Makamu wa Rais wa MAT, Dk. Primus Saidia, alitoa tamko hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana suala zima la magonjwa yasiyoambukiza na tiba mbadala.

Alisema wagonjwa wengi baada ya "kunywa kikombe cha Babu" waliacha kunywa dawa za magonjwa yaliyokuwa yakiwasumbua na kusababisha wengi wao kupooza, kufa na wengine hali zao kuzidi kuwa mbaya, “Ni vyema wananchi walio wagonjwa wa shinikizo la damu, kisukari, anemia na magonjwa mengine wakafuata ushauri wa madaktari badala ya kulaghaiwa na wachache,” alisema Dk. Saidia.

Alisema umma wa Watanzania umekuwa ukilaghaiwa kwa tiba mbadala na kuacha kutumia dawa za hospitali hivyo kuongeza ukubwa wa tatizo na wanapokimbilia hospitali tayari hali zao zinakuwa mbaya.

Dk. Saidia alisema ili dawa iweze kutumika hufanyiwa utafiti kwa kati ya miaka 10 hadi 15.

Naye Katibu Mkuu wa MAT, Dk. Richard Kabangira, ambaye ni daktari bingwa ya tiba wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando, alisema, “Serikali yetu haisikilizi wana taaluma, mfano Babu wa Loliondo utafiti uliofanyika pale ni wa dawa kutokuwa na madhara kwa binadamu na sio kutibu magonjwa.” alisema Dk. Kabangila na kuongeza, “Hospitali ya Rufaa ya Bugando ilipokea wagonjwa wengi wa kisukari baada ya kutoka Loliondo kufuatia wagonjwa hao kuacha kunywa dawa walizopewa hospitalini.”

Alisema waliwasiliana na wanachama wao nchini kote kufuatilia hali za wagonjwa waliokuwa wamekwenda "kwa Babu kupata kikombe" na waligundua kwamba waliokuwa wanatumia dawa (ARV) za kufubaza virusi vya UKIMWI, shinikizo la damu, kisukari na hata saratani waliacha dawa baada ya kunywa kikombe cha Babu.

Alisema pamoja na watu kadhaa kutoa ushahidi kuwa wamepona kwa dawa hiyo, utafiti uliofanywa na MAT, umegundua kuwa hakuna hata mtu mmoja aliyepona baada ya kunywa dawa ya Babu.

Alisema watumiaji wa ARV walipungua kama ilivyo kwa hao wengine, lakini baada ya muda hali zao zilikuwa mbaya wengine walikimbilia hospitalini lakini kwa kuwa walikuwa wamevuruga mtiririko wa tiba, walipata madhara makubwa.

Dk. Kabangira alisema MAT ilimwandikia barua Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii juu ya hatari ya tiba ya Babu, na kutoa ushauri wao, lakini ulipuuzwa kwa sababu za kisiasa.

Kufuatia hali hiyo, MAT imetoa wito kwa Serikali na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuwaeleza wananchi ukweli ili wasiangamie huku wakieleza kusikitishwa kwao kutokana na tiba hiyo kutumika kisiasa.

Chama hicho leo kinafanya mkutano wao mjini Mwanza, suala la tiba ya Babu linatarajiwa kuibuka katika mkutano huo unaowakutanisha wanachama wake.

source: ippmedia
 
Hilo tamko la chama cha madaktari linatakiwa kusambazwa kwa nguvu na vyombo vyote vya habari ili kuwaokoa watu ambao bado wanaenda kwa huyo babu.

kwa hakika serikali si ya kutegemewa kuokoa hali hii kwa haraka.
 
Bongo kila kitu politiki tu.... Uku wananchi wana angamia.
 
Ukiyaangalia kwa makini macho ya huyu Babu yamekaa kitapeli tupu. Dawa kaonyeshwa na Baba yake, naye anatutapeli eti kaoteshwa na Mungu. Du hili ni tapeli la uhakika.

Kweli babu anaweza au aliwahi kuuza hata Unga.
 
mhhh hii kali nilidhani kikombe kina chemical content za hatari. Kumbe ni maafa ya wagonjwa kuacha kuenelea na dawa.

Anyway sikubalian na Tiba ya babu lakini na hao wataalam maelezo yao hayatoshi.

Kama wako serious pia wasema Dini zinazopingana na matuzmizi ya condom zinasababisha maafa kuwazuia waumini wao hasa viajana kutumia condom.

BTN

Hivi hicho kikombe kina chemical content gani ??? mbona wataaalma wanaongea alakini hawatoi scietific data za content za hiyo dawa na inafanya nini kwenye mwili wa binadamu . yaaani Maelezo ya watalamu na wanasiasa hayana tofauti.

Ukiyaangalia kwa makini macho ya huyu Babu yamekaa kitapeli tupu..........

Na wewe na babu hamna tofauti unaleta utaabiri wa nyota usiokuwa takwimu za kisayansi . eti macho ya kitapeli......... teh teh teh teh
 
Wanasayansi wa Tanzania ni hypocrites. Kwa nini hawaku protest toka mwanzo? Maana wanasema dawa mpya huwa zinachukua miaka 15 kuthibitishwa, hivyo walijua wazi mmea wa babu haukuwa na proven pharmaceutical ingredient. Too late, thanks but no thanks.
 
Wanatoa tamko baada ya maafa. Au walikuwa beasy na shughul.
 
Tamko linaonyesha wazi kwamba katibu mkuu anatakiwa awajibike

alas, we dont have that culture
 
Wanatoa tamko baada ya maafa. Au walikuwa beasy na shughul.
<br />
<br />
hakuna ubusy wowote ulikuwa mfumo kristo kila mtu alimtetea babu eti kaoteshwa mara kaongea na mungu nadhani huyo mungu mwenyewe ana matata naye adhibitishwe na tbs
 
Babu aandaliwe mashtaka pamoja na wanasiasa na magazeti yote yaliyotoa promo kwa mtabibu fake kwa kisingizio cha dini na kanisa lake pia lilimbeba na kuwapa imani wananchi kuumia.

Kesi iwajumuishe na watoa vikombe wote, watu walitoa mpaka helcopta kutafuta easy political win.
 
<br />
<br />
hakuna ubusy wowote ulikuwa mfumo kristo kila mtu alimtetea babu eti kaoteshwa mara kaongea na mungu nadhani huyo mungu mwenyewe ana matata naye adhibitishwe na tbs

Hata kama huna imani na Mungu ingekuwa vema usichukua risk ya Jehanam kwa kumkashifu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom