Tiba ya Asthma,Nimonia kwa mtoto mdogo

1800

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
2,215
603
Wadau naombeni msaada wenu wa kiushari na kitabibu pia,

Nina mwanangu anasumbuliwa sana na kifua muda mrefu,ni mtoto wa miaka miwili,leo nimempeleka kwa speacilist amempima na ametoa majibu kua anasumbuliwa na nimonia,asthma pamoja na allergy,kuna dawa wamenipa ili aanze kutumia.

Ninachoomba ni ushauri wenu. Je, ni tiba gani ambayo ni ya uhakika kuweza kutibu gonjwa ili bila kujirudia,dawa hiyo iwe ya mitishamba au lah yote sawa,kikubwa ni uponyeshaji wa uhakika kabisa.
 
Athma haina dawa ni kutuliza tuu!pneumonia ni antibiotic kali kama duracef ya siku 10
 
Pole na kuuguza.... Mungu akuwekee wepesi mtoto apone. Huwa inachanganya saana mtoto mdogo anapokuwa anaumwa na ujui kitu gani.

Sijui tiba, tusubirie wataalam. Ila nimeguswa na magonjwa anayo umwa, pneumonia na Asthma zoote hizi husukumwa na moja ua sababu common ya baridi. Kama anaumwa mara kwa mara, jaribu kutafakari umakini wako katika kumhifadhi na kuhakikisha kuwa baridi haimpati. Lingine inaweza kuwa sio wewe moja kwa moja wamlea bali una msaidizi... Pia napo kuwa makini na fuatilia kama mtoto anajaliwa na kuhifadhiwa vizuri pale unapokuw haupo (hasa kama mwaishi sehemu ya baridi kama ninavyofikiria).

Niliona nigusie hayo... Kila la kheri katika kupata matibabu bora na ushauri wa dawa una eleweka, pamoja na mtoto kupona.
 
Mtoto wa miaka 2, dah pole sana, zingatia ushauri wa AshaDii hapo juu. Unaishi mkoa gani hapa tz?. Subiri atakuja jamaa mmoja anaitwa mzizimkavu ​atakuandikia dozi, tumsubiri.
 
Pole sana ndugu yangu, kwa mtoto wa miaka 2 is very sad.

Inasikitisha sana. Kiukweli mimi sifahamu dawa nyingine ya Asthma kwa watoto ila kwa watu wazima Cannabis is the only cure. Usishangae ndio ukweli and nina rafiki ambaye ana medical legality ya Cannabis for Asthma, Canada. THC ina tabia ya kufanya damu izunguke mwilini kwa kiwango kizuri na kufanya mapafu kupanuka na hewa kupita vizuri.

SOURCE:

WARNING:

You don't have to SMOKE marijuana. the best way to consume it for people suffering breathing problems would either be edibles, or vaporizing.
Pia kuna some people haiwasaidii but they are few.

NB: Ni wataalam wachache sana hapa Tanzania ambao wanaujuzi katika medical marijuana, most of them hawajasomea. I wish one day nianzishe taasisi ya tiba za kutumia Hemp, i know kuna magonjwa mengi can be cured. Ondoa dhana ya kukariri it is bad, but remember is safer than Cocacola and Caffeine. Take care.
 
Asanteni sana wakuu kwa michango na mawazo yenu yenye tija,naamini nitaondoka na mawazo chanya yatakayoweza kumsaidia dogo,asanteni sana,Mungu awabariki sana
 
Pamoja na ushauri mzuri wa wadau hapo juu hasa Ashadii juu ya kumhifadhi kutokana na baridi, ushauri wa pili ni kufanya "allergy test". Hii itakusaidia kujua ni nini kunaleta hiyo Ashtma = Allergy reaction na kuviepuka, baada ya muda atakuwa ok. Pneumonia inatibika kwa hizo dawa za hospitali na "kumhifadhi"= Kuhakikisha hapatwi na ubaridi iwe mchana au usiku, hivyo hakikisha anatiwa haraka hiyo. Usisahau maombi kwa Mungu katika jina la Yesu yanaweza kufanya mambo makubwa kuliko tuyawazayo au tujuayo.
 
1800, Pole..

Ningependa kuanza kwa kusema kuwa ni ugonjwa wa Pneumonia(Homa ya mapafu) na si "Nimonia".

Pili, ningependa kusema tiba ya Homa ya mapafu ni dawa za Antibiotics, lakini dawa hizi hutegemea vijidudu(bacteria) waliosababisha Homa hii, Umri wa mgonjwa..nikiwa na maana Bacteria mbalimbali huweza kuleta tatizo hili katika umri tofauti(mf. wazee, watoto, watu wenye magonjwa ya upungufu wa kinga, na kwa baadhi ya magonjwa ya kurithi).Hivyo kwa kutegemeana na takwimu, vipimo alivyopimwa mwanao antibiotics husika hutolewa.

Asthma(Pumu), Kuna mengi yalikwisha ongelewa kuhusu hili katika thread za hapa JF Doctor, ingekuwa vizuri kupitia(ukijielimisha na kuongeza ufahamu kuhusu hili) lakini pamoja na hayo ningesema, Ugonjwa wa Pumu ni ugonjwa wa muda mrefu, hutibika(KUPUNGUZWA TATIZO), kutegemeana na number ya/za mashambulizi(attack) zinazotokea ikiwa ni kwa wiki/mwezi..Hivyo umwelezapo daktari, mara ngapi mtoto anashambuliwa("banwa na pumzi", anashindwa kupumua, n.k) huweza kukupa tiba inayofaa.

Ni vizuri kujua kuna baadhi ya vitu vinavyopelekea/vinavyochochea hali hii ya "kubanwa" (Asthmatic attacks) kutokea zikiwepo baridi, allergy n.k.

Allergy(pia kama tatizo la Asthma lilikwisha elezwa hapa), hata hivyo ni vizuri kuepuka allergens(vitu vinavyosababisha/chochea) tatizo mf. vumbi, marashi, baridi, manyoya ya wanyama, maua na baadhi ya mimea hasa ikianza kuchavua(kutoa pollen) n.k.

Hivyo basi ni muhimu, kuepuka mazingira hatarishi yanayoweza kusababisha attacks.
 
Last edited by a moderator:

Daktari, sasa hivi 'Nimonia' ni kiSwahili rasmi (official) cha 'Pneumonia', na si 'homa ya mapafu' wala 'kichomi' tena. Nimeshiriki katika mchakato wa kutengeneza IEC materials kwa ajili ya ujio wa chanjo mpya dhidi ya kuhara (rotavirus vaccine) na Nimonia (Pneumococcal vaccine) zitakazozinduliwa wiki ijayo, na kulikuwa na debate kubwa sana kuhusu jina gani linaeleweka kirahisi na jamii. Na katika utafiti uliofanyika, ilionekana wazazi na walezi wanajua Nimonia kuliko homa ya mapafu au kichomi...hivyo guidelines zote sasa ninaita Nimonia.
 
Ahsante kwa taarifa mkuu.
 
Mkuu 1800 Pole sana kwa huyo mtoto kuumwa na hayo maradhi. Dawa Ya Kifuwa Kwa Watoto Na Watuwazima.

Kwa Uwezo Wa Mwenyeezi Mungu Inshaallahu Atujaalie Shifaa Aamin

Chukuwa Asali Weka Kitunguu Maji Kikatekate Kichanganye Kwenye Asali Kiweke Masaa 12 Halafu Tumia Kiasi Kama Kipimo Cha Hospitali.

Inshaallahu atapona mtoto wako usikose kuleta feedback.
 
1800, Pole..

Ningependa kuanza kwa kusema kuwa ni ugonjwa wa Pneumonia(Homa ya mapafu) na si "Nimonia".

Pili, ningependa kusema tiba ya Homa ya mapafu ni dawa za Antibiotics, lakini dawa hizi hutegemea vijidudu(bacteria) waliosababisha Homa hii, Umri wa mgonjwa..nikiwa na maana Bacteria mbalimbali huweza kuleta tatizo hili katika umri tofauti(mf. wazee, watoto, watu wenye magonjwa ya upungufu wa kinga, na kwa baadhi ya magonjwa ya kurithi).Hivyo kwa kutegemeana na takwimu, vipimo alivyopimwa mwanao antibiotics husika hutolewa.

Asthma(Pumu), Kuna mengi yalikwisha ongelewa kuhusu hili katika thread za hapa JF Doctor, ingekuwa vizuri kupitia(ukijielimisha na kuongeza ufahamu kuhusu hili) lakini pamoja na hayo ningesema, Ugonjwa wa Pumu ni ugonjwa wa muda mrefu, hutibika(KUPUNGUZWA TATIZO), kutegemeana na number ya/za mashambulizi(attack) zinazotokea ikiwa ni kwa wiki/mwezi..Hivyo umwelezapo daktari, mara ngapi mtoto anashambuliwa("banwa na pumzi", anashindwa kupumua, n.k) huweza kukupa tiba inayofaa.

Ni vizuri kujua kuna baadhi ya vitu vinavyopelekea/vinavyochochea hali hii ya "kubanwa" (Asthmatic attacks) kutokea zikiwepo baridi, allergy n.k.

Allergy(pia kama tatizo la Asthma lilikwisha elezwa hapa), hata hivyo ni vizuri kuepuka allergens(vitu vinavyosababisha/chochea) tatizo mf. vumbi, marashi, baridi, manyoya ya wanyama, maua na baadhi ya mimea hasa ikianza kuchavua(kutoa pollen) n.k.

Hivyo basi ni muhimu, kuepuka mazingira hatarishi yanayoweza kusababisha attacks.

Asante sana ndugu,ushauri wako ni mzuri na wenye kutoa mwanga,tutauzingatia ili kupata matokeo chanya!asante mkuu
 
Last edited by a moderator:
Mkuu 1800 Pole sana kwa huyo mtoto kuumwa na hayo maradhi. Dawa Ya Kifuwa Kwa Watoto Na Watuwazima.

Kwa Uwezo Wa Mwenyeezi Mungu Inshaallahu Atujaalie Shifaa Aamin

Chukuwa Asali Weka Kitunguu Maji Kikatekate Kichanganye Kwenye Asali Kiweke Masaa 12 Halafu Tumia Kiasi Kama Kipimo Cha Hospitali.

Inshaallahu atapona mtoto wako usikose kuleta feedback.

Asante kwa ushauri juu ya dawa hii ya asili,ila labda unisaidie kitu,je asali ni kiwango gani na mchanganyiko wa kitungu uwe kwa kiwango gani!ahsante sana ndugu
 
Pamoja na ushauri mzuri wa wadau hapo juu hasa Ashadii juu ya kumhifadhi kutokana na baridi, ushauri wa pili ni kufanya "allergy test". Hii itakusaidia kujua ni nini kunaleta hiyo Ashtma = Allergy reaction na kuviepuka, baada ya muda atakuwa ok. Pneumonia inatibika kwa hizo dawa za hospitali na "kumhifadhi"= Kuhakikisha hapatwi na ubaridi iwe mchana au usiku, hivyo hakikisha anatiwa haraka hiyo. Usisahau maombi kwa Mungu katika jina la Yesu yanaweza kufanya mambo makubwa kuliko tuyawazayo au tujuayo.

Asante sana kwa ushauri wako mkuu,hii ya allergy test nimeipenda na nitaifanyia kazi,asante mkuu
 
Madactory wengi hutoa sababu ya ugonjwa kwa kukisia.Mi mwanangu akiwa na miaka 3 alikua anakohoa sana.Nikaenda kwa mtaalamu wa kifua akasema ni pumu inamsumbua.Aliniandikia dawa mfuko wa Rambo ulijaa.Nilipofika home nikazisoma moja baada ya nyingine then nikazitundika.Nikaenda Dukani nikatafuta dawa ya kikohozi ya maji yenye mchanganyiko wa kupunguza mziho (BENYLIN ya watoto).Baada ya siku tatu akapona kabisa.Baadae nikagundua mtoto anakunywa sana maji ya baridi,then nikapiga marufuku.Kuhusu Nimonia,kuna dawa inaitwa Augment ya UK ni nzuri sana au Clavam
 
mkuu pole sana kwa kuuguza, ninachoweza kukusaidia mimi ni namba ya huyu mdingi ambaye anatengeneza dawa ya miti shamba ya pumu, kiukweli wengine niliowai kuwapa namba wanasema dawa yake imewasaida, dawa yake inarange kwenye 35000 mpaka 40000 kwa chupa, wewe mpigie maeelezo mengine atakupa yeye mwenyewe anaitwa mzee Pongwe 0715242033
 
Asante sana mkuu,mwanao alikua anakohoa na kutapika au alikua anakohoa tu?maana wangu anakohoa na kutapika mbali ya kifua kubana!
 
mkuu pole sana kwa kuuguza, ninachoweza kukusaidia mimi ni namba ya huyu mdingi ambaye anatengeneza dawa ya miti shamba ya pumu, kiukweli wengine niliowai kuwapa namba wanasema dawa yake imewasaida, dawa yake inarange kwenye 35000 mpaka 40000 kwa chupa, wewe mpigie maeelezo mengine atakupa yeye mwenyewe anaitwa mzee Pongwe 0715242033

Asante sana mkuu,ngoja nicheck nae sasa hivi!nashukuru sana
 
Asante kwa ushauri juu ya dawa hii ya asili,ila labda unisaidie kitu,je asali ni kiwango gani na mchanganyiko wa kitungu uwe kwa kiwango gani!ahsante sana ndugu
Mkuu 1800 Asali iwe asali mbichi safi ya nyki kiwango chake fanya kiwe kama kikombe cha kahawa na kitunguumaji kiwe kimoja tu Kikatekate Kichanganye Kwenye Asali Kiweke Masaa 12 Halafu Tumia Kiasi Kama Kipimo Cha Hospitali. tumia kwa muda wa siku 3 kisha uje hapa utupe maendeleo ya Mwanao yanakwendaje? Give me feedback.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom