Tiba na ponyo la maradhi yasiyoonekana hospitali

Rakims

Rakims

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2014
Messages
3,086
Points
2,000
Rakims

Rakims

JF-Expert Member
Joined Jun 4, 2014
3,086 2,000
MARADHI YASIYOONEKANA HOSPITAL

images-jpg.1114764
Katika mada hii nitakufundisha ni yapi maradhi ya sehemu za mwili ambapo mashetani wakikukumba wanaanza kusumbua na kukutesa kisiri siri kwa kujua au bila kujua. Maradhi haya kwa maana nyingine hujulikana kama kukumbwa na Mapepo au kukumbwa na nuksi au uchawi wenye kuleta magonjwa, Haya tunayajua vipi?

Kutoka kwenye hadithi maarufu ya Mtoto wa Mfalme Suleiman Bin Daud au (King Solomon Son of David) mfalme huyu katika hadithi za zama zake aliwahi mtoto wake kuugua maradhi haya ya kichawi na inahadithiwa kuwa maradhi hayo aliyowahi kuwa nayo yalikuwa yanamletea mateso ya kuhama hama, maradhi ya kuhama au ketembea mwilini ni maarufu sana zama hizi na huunganishwa na uchawi na hujulikana kama uchawi wa kumtesa mtu aliyekwenda kinyume na matakwa ya mashetani au shetani aliyemvaa.

Maradhi haya yanapomkumba mtu huwa yanatembea mwilini kwake na kusababisha sehemu nyingi sana matatizo katika mwili wake kama ni kwenye macho basi kuna kipindi unakuwa huoni au unaona giza na ndio yalimkumba huyo mwana wa Suleiman aliyekuwa nabii wa mwenyezi Mungu,ugonjwa huo ulikuwa ukihamia kwenye macho basi anashindwa kuona,ukitibiwa macho unaenda kwenye maskio anakuwa hasikii,ukitibiwa maskio,unaenda kwenye mdomo anakuwa haongei na ukitibiwa mdomo unahamia kwenye kichwa anakuwa kama kichaa,ukitibiwa hapo unahamia kwenye mgongo ana kuwa hawezi kukaa, ukitibiwa hapo unahamia sehemu za siri anakuwa hawezi kukojoa anakuwa kajifunga mkojo,na muda mwingine ukiwa hapo anashindwa kutembea. Sasa aina hii ya maradhi aliwahi kuumwa pia mwana wa Suleiman Nabii wa Mwenyezi Mungu japokuwa baba yake alikuwa nabii wa Mwenyezi Mungu. Suleiman alipoona madaktari wake wote wameshindwa kumtibu mwanae madaktari bingwa wa zama hizo waganga na wanasayansi hakuna aliyeweza kumsaidia maradhi hayo hadi pale ambapo alishuka malaika Jibril (Gabriel) ambaye alimuamuru Suleiman kumuita Malkia wa Shayk aliyekuwa akiitwa Serobat.

01-jpg.1115426
Serobat alipofikishwa haraka kwa Suleiman kwa woga na hofu zaidi akamwambia Nabii Suleiman "ewe Suleiman nisamehe anayemfanya hivi mwanao ni mjukuu wangu na hajaweza hayo isipokuwa kwa kukubaliwa na mwenyezi Mungu" Shetani huyo alikuwa na jina tofauti ndipo na alikuwa ni katika falme za mashetani ikabidi ugonjwa huo moja kwa moja upewe jina la Ugonjwa wa Serobat kwa kuwa ulikuwa ni ugonjwa mpya na haukupewa jina uchawi huo zaidi ya hilo na dawa zake ikabidi ziwe ni za kitofauti. kila sehemu ya mwili alitumwa shetani kwenda kusumbua kiasi cha kwamba akitolewa mmoja mwingine anajidhihirisha sehemu nyingine ya mwili

Haya sasa ndio maelekezo ya kila dawa na sehemu zilizotumika kuponya, dawa hizi zinaweza kuponyesha ugonjwa wowote sehemu hiyo unayokusumbua hata kama umeshakuwa ni ugonjwa wa mazoea kwenye mwili wako: na kila sehemu hiyo basi kulikuwa kuna uchawi wa shetani mmoja anaesimamia

1. Ubongo,
Hapa shetani aliyekuwa anasimama na kucheza na akili pamoja na fikra za huyo mtoto alikuwa akiitwa Mina, Mina ni aina ya jini mwenye uchawi wa kuvuruga akili ya mtu na kumfanya akawa kama kichaa na wote wenye kuumwa kichaa, Shetani huyu list yao huwa anayo
dawa iliyotumika na kuelekezwa kumtoa uchawi wa Mina cha kwanza ilikuwa ni Kisomo(Maombi) ya nabii Suleiman baada ya kufanyika maombi, ilitumika majani ya kitunguu maji,maganda ya chenza,ikachanganywa na bobo,patchouli na chumvi kisha vikasagwa na kubaki laini na baada ya hapo vikachemshwa kisha akapakaliwa kama massage ya kichwani, shetani huyo hakujaribu tena kugusa kichwa hicho na hawezi kugusa kichwa cha mtu aliyefanyiwa hivyo tena, na katika mzunguko wa maradhi ya kuhama ukifanya hivyo basi hayawezi tena kuhamia kichwani.

2. Mwili, Jina la shetani aliyekuwa akisumbua hapa ni Roin huyu hudeal na kuumiza mwili wa mtu kumchosha kumfanya kuisha nguvu na kumtilia joto kali na baridi vyote kwa pamoja na ili kumuondoa au kumuua dawa zake ni jani la bibo lililo karibu sana na tunda,kitunguu maji, tangawizi yenye unjano, limao la kupikia,mdalasini,chumvi na magome ya bibo unaweka yakauke kisha unatia maji ya *********** unamwagia mwili mzima hapo hapo jini huyo akichelewa kudondoka na kujihisi umetua mzigo basi huungua na kufa sijataja maji hayo kwa sababu sioni haja ya kuelekeza kuuwa mashetani maana tutazalishwa wachungaji wapya hapa

3. Maskio, Shetani anaesumbua hapa huitwa Hubbi huyu aliweza kuondolewa kwa dawa ambazo ni jani la tunguja,sungusungu na chumvi ikawekwa kwenye kikombe kisha kuchemshwa akapakaliwa maskioni. dawa hii kwa mtu anaesumbuliwa na shetani aliyemtia kiziwi au kwa matatizo ya maskio basi hupona kabisa

4. Mdomoni, pia shetani aliyemsumbua hapa alikuwa akiitwa Malani, Nae dawa zilizotumika ilikuwa ni mafuta ya zaituni ambapo hupakaliwa mdomoni mara kwa mara basi hawezi mtu kusumbuliwa tena na maradhi ya kinywa.

5. Macho, Jina la Shetani aliyekuwa akimsumbua hapo na uchawi wake ni Duhri, dawa yake kuwa ni Ubani makka na majani ya maua nyota, yanachanganywa pamoja na kusagwa vyote hadi kuwa unga kisha vinalowekwa kwenye maji ya vuguvugu ya Zamzam halafu baada ya hapo yanazungushiwa jirani na macho yaani kwenye duara za macho kisha inaachwa ikaukie hapo kama ni maradhi ya kichawi au jini basi hupona hapo hapo lakini kama ni maradhi ya kawaida ya macho huchukua muda kidogo.

6. mkono, jina la shetani wa hapa kwa uchawi wake ni Wahitu.

7. Shingo, jina la shetani wa hapa kwa uchawi wake ni Bayuh

8. Moyo, jina la shetani wa hapa kwa uchawi wake ni Baliyun

9. Tumbo na Mgongo, jina la shetani wa hapa kwa uchawi wake ni vijakazi wa Zoba

10. Hips na makalio, jina la shetani wa hapa kwa uchawi wake ni Malitung

11. kiuno, jina la shetani wa hapa kwa uchawi wake ni Hamun

12. mapaja, jina la shetani wa hapa kwa uchawi wake ni Kadung

13. kidevu, jina la shetani wa hapa kwa uchawi wake ni Kanif

14. mwili, jina la shetani wa hapa kwa uchawi wake ni Calf

15. sehemu za siri, jina la shetani wa hapa kwa uchawi wake ni vijakazi wa Phul

16. sehemu ya nyuma ya siri,au kuingiliwa kinyume jina la shetani wa hapa kwa uchawi wake ni Dalungah

17. utumbo, jina la shetani wa hapa kwa uchawi wake ni Dubur

18. tumbo, jina la shetani wa hapa kwa uchawi wake ni Poku kijakazi wa Ophiel


Zote hizi ni dawa ambazo pia hutibu hata kwa kula au kunywa. Baada ya malikia huyo kumfundisha tiba hii Nabii Suleiman basi aliamua kumuweka kama mmoja kati ya mashetani ambao walikuwa vijakazi wake.

Kila sehemu nilizotaja hapo na zinginezo ambapo maradhi yana hama basi huwa kuna shetani mwenye kusimamia maradhi hayo yanayomtesa mtu na ambapo akijitahidi kufuatilia maradhi hayo basi huwa hapati majibu ya kueleweka hospitali je unasumbuliwa na moja ya sehemu hizo nilizotaja na umeshazunguka hospitali bila majibu weka majibu hapo chini ili kuweza kuupdate maelekezo ya sehemu uliyochagua.


ANGALIZO:

Usiwe mwepesi wa kutumia dawa zinazoandikwa mitandaoni bila kupata uhakika wa anayeandika na kadhalika ikiwa unahitaji kutumia moja ya dawa zitakazo elezwa hapa jamii forum basi jitahidi kupata uhakika wa dawa hizo kabla ya matumizi kutoka kwa wahusika na maelekezo yenye kujitosheleza

Rakims
 

Attachments:

napendamovie

napendamovie

Member
Joined
Apr 24, 2015
Messages
74
Points
125
napendamovie

napendamovie

Member
Joined Apr 24, 2015
74 125
Duh majina mengne ndo naskia Leo ahsante kwa elimu
 
Ivonovsky da White

Ivonovsky da White

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2012
Messages
214
Points
225
Ivonovsky da White

Ivonovsky da White

JF-Expert Member
Joined Aug 23, 2012
214 225
dawa ya tumbo na mgongo
 

Forum statistics

Threads 1,304,178
Members 501,290
Posts 31,505,441
Top