Tiba asili isigeuzwe biashara ya Wahindi au hisani ya Wamarekani

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,053
28,245
Niwapongeze wizara ya afya na Ustawi wa jamii kwa kutambua mchango wa TIBA ASILI (SIO MBADALA) kama sehemu ya mfumo wa afya Tanzania na nia yao ya kuonesha kuwa tiba zetu za asili ambazo zimekuwepo miaka mingi zinaweza kuwa sehemu ya ubunifu na msaada mkubwa nyakati za milipuko na nyakati za kukabiliana na magonjwa kwa ujumla.

Timu ya wizara ya Afya leo hii imejitokeza katika kuelezea umuhimu wa tiba zetu za asili ambazo zilianza pengine hata kabla ya tiba hizi za kisasa.

Ujuzi huu ni wa Kitanzania na inawezekana uliwahi kuibiwa enzi hizo tunatawaliwa na pia inaeezewezekana unaendelea kuibiwa hadi sasa kwa kuwa tu masikini katika uwekezaji katika tasnia ya utafiti na uendelezaji wa dawa.

Nikitolea mfano wa kujifukiza, kuchua, kutumia muarubaini n.k ni wazi kila mtanzania wa miaka ya 80 na kurudi nyuma alikutana na tiba hii ingawa ilipuuzwa miaka ya hivi karibuni.

Pia ukifuatilia historia ya tiba utakutana na mabadiliko kadri muda unavyoenda yaani kutoka kwenye mizizi hadi dawa za kisasa na kurudi kwenye mizizi chakula (concotion).

Kila mtanzania anapaswa kutambua kuwa tiba ni biashara kubwa duniani ndio maana leo hii kila nchi inapigania kuwa na dawa au chanjo ya corona, na wanafanya hivyo ili waweze kuuza na kuinua uchumi wao.hivyo ni vyema wizara ya afya ,taasisi za kiusalama na wadau wote kutambua hili.

Leo hii tumeoneshwa kuwa kuna local remedies zinazoweza kutumika kwa usalama kabisa ili kutukinga dhidi ya maradhi mbalimbali ikiwemo corona.

Wito wangu kwa Mh. Rais ni mmoja na muhimu, kamwe tusije ruhusu wasanii, walaghai, wala rushwa, wezi na watumia fursa kuingilia muelekeo na ubunifu uliowasilishwa leo.

YAANI NI UHUNI NA AIBU KUBWA TUKISIKIA ETI TIBA ASILI YA CORONA IMEVUMBULIWA NA MUHINDI,MWARABU, MCHINA AU MZUNGU ILI AJIPIGIE HELA. Huu utakuwa ni uhuni wa kutupwa na wahusika wote wanafaa kusekwa lupango mara moja.

TIBA ASILI IWE IMEGUNDULIWA NA MMASAI KAMA LAIZER alivyoibua TANZANITE kule Mererani...Tiba asili igunduliwe na Mshana Jr kutoka upareni, hapo ndipo tutakapoongea lugha sahihi dhidi ya wanaotaka kutumia afya zetu kama mtaji.

SITARAJII KUSIKIA TIBA ASILI KWA HISANI YA MAREKANI BALI TIBA ASILI KWA HISANI YA TANZANIA.

KITENGO CHA TIBA ASILI PALE MUHIMBILI KIAMKE,NIMR WAAMKE ,SUA WAAMKE n.k .

HII NI
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!

Aione:
1-Field Marshal Gwajima
2-Dr Molel
3-Bingwa wa Tiba Asili wizara ya Afya
4-Waganga wa Tiba asili(Sio mbadala) Tanzania.
 
Waziri anaziita "bidhaa za asili" haziiti dawa sijui kwanini.
 
Ni sahihi unachokinena lakini hili jambo lisigeuzwe kuwa agenda ya kisiasa hapo tutafaulu kwa kiwango cha kushangaza sana
Kama wairan wameweza basi hata sisi tutaweza lakini ni mpaka pale tutakapoziweka siasa kando
 
Kwa mara ya kwanza tunakubaliana
 
Back
Top Bottom