Thread ya Show ya "I am Zuchu": Kutoa Tsh. million 5 kumuona Zuchu kwenye VVIP inaitaji uwe na utajiri wa Bakhresa

AlphaMale

JF-Expert Member
Oct 26, 2019
613
1,404
Elf 50 au laki 1 kumuona Zuchu kwenye VVIP inaeleweka, ila million 5 aise kwani naenda kumuona Niki Minaj au?

Zuchu yuko overpriced


Mauzo ya Ticket
From Diamond Platnumz bingwa wa promotion.

"Mwanzoni tuliweka kwa watu 500 ticket zikaisha tukaongeza ukumbi hadi watu 1000 jana usiku zikaisha tena ikabidi tutanue ukumbi hadi watu 2000 na kuset upya stage usiku wa manane nazo zimeisha."

My take; chenye thamani usipokithamini, hakithaminiki.

View attachment 1510288


Mapato kutokana na Mauzo ya Ticket
Kwa hesabu ya haraka haraka kama kiingilio cha wastani kilikua mil.1 basi haina shaka show ya Zuchu imeingiza kiasi cha Tsh Bil.2

Mechi ya Simba na Yanga mapato yao makubwa kuwahi kutokea nazani si zaidi ya mil. 600. Sijui watu wa Football tunafeli wapi?


Tathmini ya Show
Kwanza niwape pongezi Sana Wasafi namna walivyopamba ukumbi ulikuwa very nice na pia setting up ya jukwaa ilikuwa zuri Sana ikiwemo graphics zilizotumika on scene wakati msanii anaperfomance ilikuwa Ni fire Sana.WCB wanajua how to brand msanii na hii ndio tofauti yao na wasanii wengine I believe after hiyo show itapandisha value ya Zuchu Mara dufu.

Perfomance

Performance ya mboso dah was amazing kwa kweli amefanya wonders performance na ana deserve zile hela nyingi alizotuzwa.I think mbosso ndio msanii aliyetunzwa hela nyingi Sana.

Combination performance ya mboso & Zuchu

Moja Kati ya performance iliyonikosha kweli kweli nilipenda chemistry walionayo.

Combination ya Zuchu & Jide commando

Kumekuwa namsemo kwamba wanawake wanachukiana Sana lakini ushirikiano wa Jide na zuchu unaweza kutengeneza kitu kwenye Huu mziki.Walifanya something special as if Kama walikuwa na ngoma ya pamoja hapo kabla.Honestly nimependa Sana performance yao ya pamoja kiasi ambacho mashabiki wakataka warudie kuperform Mara 3.

Performance ya Zuchu

Kwanza kabisa ana confidence yake kaperform as if ana muda mrefu kwenye game I did like dress code yake ila nimependa zaidi performance ya wimbo wake wa "Nisamehe" nimependa alivyo calm na hisia kubwa aliyotumia Kama wimbo ulivyo, ukichanganya na voice yake ilivyo mzuri you get something good.Pia ametuonesha uwezo wake pia wa kudance huku aliimba kwa baadhi ya wimbo zake was amazing.

Combination ya mama yake na Zuchu

Waliua Sana aisee mama na mtoto.

performance ya Lavalava

Katika show zake zote za Lavalava hii ndio best show kuliko zote nilizowahi kuona kutoka kwake mzee aliua.


Ushauri wangu kwa baadhi ya udhaifu

Kuna watu wengi walibaki nje ambao walikosa tickets Wasafi wangejitahidi kuweka scene kubwa nje ya Ukumbi walau waone Nini kinajili ndani kuliko walivyowaacha.

La pili hili Ni moja Kati ya tatizo kubwa la watanzania wengi na nilichoona Jana watu kutokuja kwenye tukio kwenye muda uliopangwa watu hawapendi kuzingatia muda wasafi walipanga tukio nzima lianze saa 1 usiku Cha ajabu hata Diamond mwenyewe na Zuchu walikuja saa 2 usiku badala ya saa 1 usiku.

Last Saturday Zuchu alitambulishwa rasmi katika ulimwengu wa Muziki. Huu ni ulimwengu uliojaa vitimbwi na vioja vya kila aina ya ushetani. Huwezi kupata unachokitaka bila kukubali kuishi maisha ya kumtumikia shetani.

Ni lazima ukubali yafuatayo:- Kudhalilisha mwili wako kwa kuvaa nusu uchi, kujirekodi picha za utupu, kutukanana na wenzako mitandaoni, kuishi na mabeef,kufeki maisha ya uongo na kurogana.

Kuimba mziki mzuri pekee havijawahi kumsaidia msanii kudumu kwenye hicho mnachokiita "Game". Ukiingia kwenye fani ya mziki ni kuchagua moja kwa moja kumtumikia shetani. Najua wengi hawapendi kusikia haya lakini huo ndo ukweli. Sawa utamiliki magari,majumba,n.k ila kwa gharama ya kuuza nafsi na utu wako.

Jiulize kwanini V- Money kakimbia huko, huku akikiri wazi Secular music imejaa ushetani! The likes of Ray C, na Mzee Yusufu. Umaarufu wa kimuziki kamwe hautompa mtu furaha zaidi ya msongo wa mawazo na majuto.Shetani ni mjanja sana. Anajua mwanadamu anatamani vitu vya thamani km majumba na pesa. Naye amevitanguliza vitu hivyo machoni kama beit or Trap . Ni kama anakuambia," Take these and serve me". Ila hakuonyesha maumivu yaliyo nyuma ya hivo vitu anavyokupa.

Wengi wanazani wasanii wakubwa wana furaha na kuinjoy maisha si kweli!! Mfano Diamondi mi naona mziki umempa majanga mengi zaidi kuliko kabla ya kuwa mwanamziki.Ni heri angeendelea kuuza mitumba angeishi kwa amani kuliko ilivyo sasa. Mnazani anapenda kuishi na uadui na baba yake? No! That is a Satanic attack which he doesn't know!. Very sad to say that.

Sipo hapa kueleza majanga ya Diamondi ila kwa ufupi thamani ya chozi la furaha ulilolitoa Zuchu wakati ukikabidhiwa gari ya kutembelea, ni mwanzo wa maumivu makubwa ya kiroho na kifikra utakayoyapitia japo kimwili utaonekana umenona. Kama huamini muulize Rachel aliyezaniwa kuwa Ray C mpya bongo atakuambia.Mikel Jackson pamoja na mapesa yake alikufa akiwa hana furaha, Whitney Huston vile vile. Muziki uliharibu kabisa maisha yao.

Muziki ni nyenzo muhimu kwa Shetani kuharibu maisha ya vijana. Kwa watoto wa kike mziki umepelekea wengi kuzalishwa na kushindwa kuolewa. Wengi wameingizwa kwenye utumwa wa ngono na madawa ya kulevya bila kupenda na pindi umaarufu unapoisha ndio hugundua kuwa wamepotea. Wachache sana wanaobahatika kutoka salama.

Ni mbinu hiyo hiyo ndio iliyowasambaratisha Bongo movie na sasa wamechoka hata hawajulikani walipo.Wengi mnawajua si vema kuwataja.

Karibu sana mdogo wangu Zuchu kwenye ulimwengu wa wasanii uliojaa ushetani.

Mahudhurio ya Wasanii tofauti tofauti
 
Kuna ule msemo wa "usiseme watu hawana hela semea nafsi yako kuwa huna hela."

Wewe waache wenye hela zao wataenda,wewe kama huna hela na kama unataka kuangalia lipia king'amuzi chako angalia na vile kama hutaki UNAWEZA UKALALA UKA-ASSUME KAMA HAMNA KINACHOENDELEA HAMNA UTAKACHO PUNGUKIWA.

Ila waache wenye hela zao wakazitumie ndio maisha hayo,kuna wengine uwezo wao V8,wengine PRADO,PAJERO,wengine VITZ,IST ,wengine BAJAJ,wengine PIKIPIKI,wengine TZ 11 cha msingi pambana na hali yako.
 
Yule Mo ana hela ya urithi...Waliotafuta wenyewe hawana muda huo..Rostam au Bakhresa watasikiliza nachomeka kwenye tope kuwa serious kidogo
Mkuu million 5 unaona ni nying? Kwa mtu mweny pesa hiyo ni hela mbuzi tu

Alaf kwa Mo mbna umeenda mbal..naongelea madogo tu wa mtaan hizo million 5 wapo wanaingiza kwa lisaa na wanskiza bongo flavour vzr tu... Mkuu Dunia ya sasa sio Kama ya zaman..hiyo 5M nying kama unasubr mshahara
 
Back
Top Bottom