Thomas Sankara (1949-1987) - Muasisi wa taifa la Burkina Faso

Ukiwa kama sankara utakufa na miaka 39


quote-i-want-people-to-remember-me-as-someone-whose-life-has-been-helpful-to-humanity-thomas-sankara-86-93-66.jpg
 
"lets us consume what we can control " Ukomboz wa mwafrika halisi ulikuwa hapa ACHA REMMY ONGALA aseme WEMA****** maana miamba mingi Ya africa imesalitiwa na watu wa karibu ambao iliwatendea wema
 
Thomas Sankara alizaliwa desemba 21 mwaka 1949 kwenye nchi ya Burkina Faso, ikitambulika Kama Upper Volta kwa wakati huo. Thomas Sankara alikuwa kiongozi mwenye maono makubwa na siasa za mrengo wa kushoto, anatambulika sana kama "Che of Africa"-‘Che wa Afrika’ akifananishwa na Ernesto Guevara ambaye alikuwa mwanamapinduzi huko Amerika Kusini.
Wakati wa mafunzo ya kijeshi alikutana na kapteni Blaise Compaoré, wakawa marafiki wakubwa. Hivyo mwaka 1983, waliongoza mapinduzi yaliyoiondoa serikali ya kidhalimu madarakani na kuiweka serikali mpya yenye mitizamo ya kijamaa. Sankara alikuwa raisi mpya lakini Octoba 15 mwaka 1987, Blaise Compaoré alimpindua kisha kuchukua madaraka.
Inaweza kuwa ndiye rais pekee Afrika Magharibi ambaye anakumbukwa zaidi. Thomas Sankara, akiwa Kama raisi ndani ya miaka minne tu aliibadilisha Burkina Faso kutoka kuwa nchi masikini na inayotegemea misaada mpaka kuwa taifa imara linalojitegemea kiuchumi na kujamii.
Thomas Sankara alianza kwa kupambana ili kung’oa mizizi ya urasimu na rushwa iliyokuwa imekithiri huko Burkina Faso. Alipunguza mishahara ya mawaziri na kuuza maghari yote ya kifahari yaliyotumiwa ikulu, kisha akanunua gari la bei ndogo tu, Renault 5. Mshahara wake ulikuwa dola 450 sawa na shilingi 958,005 za kitanzania. Pia alikataa kutumia viyoyozi (air conditioning) kwani alijiona kama mwenye hatia, hii ni kwa sababu ni watu wengi katika nchi yake hawezi kununua wala kuvitumia.
Alibadili jina la nchi lililoachwa na wakoloni la Upper Volta na kuiita Burkina Faso yaani nchi ya ‘waburkinabe’ ikimaanisha ‘Ardhi ya watu wenye misimamo’
Maendeleo aliyoyaleta Thomas Sankara kwa nchi ya Burkinafaso hayaelezeki kwa maelezo mafupi. Mwaka mmoja tu wa utawala wake, Sankara aliongoza utolewaji wa chanjo kwa watoto milioni mbili na nusu wa nchi hiyo. Vifo vya watoto wanaozaliwa vilikuwa ni vya kutisha. Kati ya watoto 1000 waliozaliwa zaidi ya 280 walifariki chini ya miaka mitano, mpaka kufikia vifo 145 kwa kila watoto 1000 waliozaliwa ndani ya mwaka mmoja.
Sankara alisisitiza nchi ‘kujitegemea’, alipiga marufuku uingizwaji wa bidhaa toka nje ambazo zingeweza kutengenezwa Burkina Faso. Hii ilisaidia ukuaji wa viwanda vidogovidogo, haikuchukua muda wabukinabe walianza kuvaa nguo zilizotokana na pamba iliyolimwa ndani ya nchi yao. Pia alizuia uingizaji wa mchele na nafaka zingine toka Ulaya.
Makabaila waliojimilikisha ardhi kubwa walipokonywa na ikagawanywa upya kwa wakulima wadogowadogo. Miundo mbinu ya umwagiliaji na miradi ya usambazaji wa mbolea iliisaidia nchi hiyo kuwa na chakula cha kutosha ndani ya miaka mitatu. Ndani ya miaka miwili aliyoingia madarakani maudhurio ya wanafunzi mashuleni yalipanda toka asilimia 10 mpaka asilimia 90.
Miezi 12 ya utawala wake aliongoza upandwaji wa miti milioni 10 ili kupunguza madhara yaliyokana na kuongezka kwa jangwa la sahara. Sankara alisisitiza wanawake kupewa hadhi wanayostahili hata katika jamii zilizokuwa na mfumo’DUME’, wanawake wengi waliajiriwa hata kwenye zile nafasi nyeti. Ili kujenga mshikamano alitangaza siku maalumu ambayo wanaume walipaswa kuwasaidia kazi zote za nyumbani wake zao.
Hakuwa raisi ‘legelege’, Sankara alitaka wananchi wake kufanya mazoezi. Haikushangaza alipoonekana mara kwa mara asubuhi katika mitaa ya jiji la Ouagadougou akifanya mazoezi.
Mwaka 1987, wakati wa kikao cha viongozi wa umoja wa nchi za Afrika, Thomas Sankara alijaribu kuwashauri viongozi wenzake kukataa mikopo ya kifedha toka mataifa ya magharibi. Alisisitiza kuwa mikopo na misaada ya kifedha inarudisha ukoloni barani Afrika.
‘mikopo inatufanya kila mmoja wetu kuwa mtumwa wa fedha za magharibi’, sera na masharti ya mikopo na fedha za misaada inatufanya tutengane, inatudhalilisha na kutupora uwezo wetu wa kuwajibika ili kujiimarisha kiuchumi, kisiasa na hata kiutamaduni. Inahatarisha juhudi zetu katika kujitegemea ili kupata maendeleo endelevu. Hatuwezi kuendelea Kwa misaada ya kifedha!
Alilaumiwa kwa kutumia nguvu kubwa kuhakikisha sera zake na matamko yake yanatekelezwa. Inaelezwa alikuwa mtu wa maamuzi ambayo ni magumu, lakini pia mara nyingi alifokea hata mawaziri na wafanyakazi wazembe. Baada ya mapinduzi ya 1987, Blaise Compaoré alifuta sera zote za utaifishaji na kukubali masharti yaliyowekwa na mashirika ya kimataifa ya fedha. Kwa namna hii ndio maana Blaise Compaoré anaelezwa Kama kibaraka aliyetumwa kumuondoa rafiki yake wa siku nyingi ili tu kufungua njia za unyonywaji wa rasilimali za nchi ya Burkina Faso.
Mpaka sasa Blaise Compaoré anakabiliwa na mashtaka ya mauaji ya Thomas Sankara mara baada ya kuondolewa madarakani.
Maono ya Thomas Sankara yalikuwa ni Waafrika wawe pamoja ili kujiletea maendeleo yao. Alipinga bila uoga udhalimu waliofanyiwa watu wa Afrika ya kusini ambao kwa kipindi hicho walikuwa chini ya serikali ya makaburu waliotekeleza sera ya ubaguzi wa rangi. Alimuambia wazi raisi wa Ufaransa wa kipindi hicho Jacques Chirac kuwa anakosea kuiunga mkono serikali ya kikaburu pindi raisi huyo alipotembelea Burkina Faso. Sankara alijikuta anakuwa adui mkubwa wa Ufaransa kwani sera zake zilipingana na ubepari. Alikuwa mjamaa na mwafrika mwenye uchungu na hali ya wananchi wake, mpaka anauliwa na kupinduliwa alimiliki gari, Jokofu, magitaa matatu na akiba ya dola 400 tu.
Wiki moja kabla ya kupinduliwa, katika kumbukumbu ya Che Guevara, Sankara alisema ‘Wanamapinduzi wanaweza kuuwa lakini mawazo yao mazuri hayatakufa kamwe’. Leo anakumbukwa Kama mtu mwenye uadilifu mkubwa, mkweli na mwenye msimamo wa kueleweka tofauti na viongozi wengi wa Afrika wa sasa.
Ni vijana wachache wa wakati huu wamepata kusikia juu ya Thomas Sankara, ambaye mauaji yake si tu yalipelekea kuchukua uhai wake bali yameondoka na mitizamo chanya juu ya Afrika na waafrika wenyewe. Inaaelezwa mabepari na ‘vijibwa’ wao wanatumia nguvu kubwa kuhakikisha Sankara na mawazo yake yanafutika Afrika. Kwa kufanya hivyo vizazi vijavyo vitakuwa vimetengwa bila daraja litakalowawezesha kujua hali ilivyokuwa na mashujaa wao.

Imeandaliwa na FRANCIS DAUDI
0768035253
Makala hii ni kipande tu ya kitabu ninachokiandaa
‘Greatest Sons of Africa’
 

Attachments

  • 1452875202440.jpg
    1452875202440.jpg
    18.1 KB · Views: 126
Ahsante ndugu kinyangesi kwa kutuletea history inayozalizimishwa ifutike ili tuendelee kuwa na mawazo mgando juu ya mabeberu wanaoinyonya Africa kwa sura ya kutusaidia, na inasemakana hata kaburi lake halijulikani lilipo.
Inashangaza kuona mtu aliyetumwa na hao waendesha mashtaka ya mauaji kumuua Thomas Sankara eti wanamshitaki.
 
Thomas Isidore Noël Sankara taa ya Afrika iliyozimika ghafla!

Na; Comred Mbwana Allyamtu

Andiko hili ni kwa mchango mkubwa kutoka kwa Martin Maranja Masese,

Mnamo august 1983, vijana wawili, makapteni wa jeshi na wanamapinduzi, Thomas Sankara na Blasius Compaore, waliipindua serikali ya Rais wa wakati huo katika nchi iliyokuwa ikijulikana kama Upper volta, rais huyu aliitwa Baptiste Ouedraogo...

Vijana hawa wakiwa katika fikra za Karl Max, wakiwa na ndoto nyingi za kuijenga Upper volta.., walibadili kabisa historia ya taifa hilo, walibadili jina la nchi na kuitwa Burkina faso, manake nchi ya watu, country of honorable citizen..

Uchapa kazi wa vijana hawa (Sankara na Compaore), Thomas sankara akiwa ndiye rais unaweza kufananishwa na ule wa Fider Castrol na Che Guavera, kabla haujachuja kule Cuba..

Haiyumkini Sankara alikuwa anatumia baiskeli kutembelea vijijini kuhimiza maendeleo, wakati pacha wake (Compaore) wakiwa kama pete na kidole..

Urafiki wa makapteni hawa wa jeshi la Burkinabe, ulikuwa mkubwa kiasi ambacho, wakati wanausalama walipomwambia Sankara kuwa Compaore ana mpango wa kumpindua na kumuua, yeye aliwajibu kuwa compaore asingeweza kufanya hivyo, labda mtu mwingine...

Blaise Compaore alikutana na Thomas Sankara mwaka 1976 katika mafunzo ya kijeshi Morocco na hapo walianza urafiki wao uliokuwa wazi kwa karibu watu wote waliokuwa wakiwafahamu nchini Burkina Fasso na nchi jirani.

Thomas Sankara alikuwa akiwaeleza wanausalama wake kuwa, hata kama Compaore angetaka kufanya hayo, hakuna wa kumzuia.

Ni wazi kuwa Kapteni Thomas Isidore Sankara alikuwa karibu sana na Blaise Compaore, kwa kiasi ambacho Blaise Compaore alikuwa sehemu ya maisha ya kila siku ya Sankara...

kama ilivyotabiriwa na watu wengi wa karibu wa Thomas Sankara, Blaise Compaore aliongoza mapinduzi yaliyosababisha kifo cha Sankara mnamo mwaka 1987, na yeye mwenyewe (Compaore), huku akishuhudia rafiki yake kipenzi Sankara akiuuwa, Akawa ndiye mrithi wa kiti cha Urais wa iliyokuwa Upper Volta baadaye Burkina Fasso..

Thomas Isidore Noël Sankara ni nani??

Isidore Noël Thomas Sankara alizaliwa tarehe 12.12.1949 Mjini YOKO katika nchi iliyokuwa ikiitwa Upper Volta (Volta ya juu) na kuuawa tarehe 15.10.1987 na wanajeshi wenzake wakiongozwa na rafiki yake Rais Blaise Compaore katika mapigano ya usaliti yaliyotokea Mjini Ouagadougou akiwa katika kikao cha utendaji wa kazi...

Thomas Sankara alipanda ngazi za kijeshi hadi cheo cha kaptenu pamoja na mwanajeshi Rafiki yake Blaise Compaore ANAYEJUA SIRI YA KIFO CHA CHA THOMAS SANKARA .

Kuna nyakati ambazo Blaise Compaore alipata kunena kwa kinywa chake katika shirika la kutetea haki za Binadamu duniani kwamba “kifo cha Thomasi Sankara kilikuwa ni ajali tu...

Mwaka 1981 Thomas Sankara alikuwa waziri wa mambo ya ndani katika serikali ya kijeshi ya Rais wa wakati huo wa Burkinabe ya zanani (Upper Volta) Jean Baptiste Major. Dr. na baadaye aliteuliwa kuwa waziri mkuu kwa kipindi cha kuanzia Mwezi Januari 1983 mpaka mwezi Mei alipokamatwa na kutiwa mbaroni na serikali ya Rais Major Jean Baptiste Dr kutokana na msimamo wake juu ya ukombozi kwa watu wote wa Volta ya Juu na kupendelea Marxist Revolution theories..

Thomas Isidore Noël Sankara alikuwa Rais wa Upper Volta (Volta ya Juu) kuanzia mwezi Agosti 4 1983 hadi mwezi Octoba 15 1987 baada ya mapinduzi ya kijeshi dhidi ya Major Dr Jean Baptiste yakiongozwa na Blaise Compaore na kuwa Rais wa TANO wa VOLTA YA JUU au BURKINA FASO baada ya kubadilishwa jina na Sankara.

Thomas Sankara aliyejulikana kama Che – Guevara wa Afrika alianzisha Program mbalimbali za kijamii na kiuchumi kuleta mabadiliko katika nchi za Afrika. Alibadilisha Upper Volta na kuwa Burkina Faso (land of Upright Men).

Alianzisha kampeni ya kuboresha Elimu na kutanua
Huduma za Afya kwa watu wa Burkina Faso maeneo ya vijijini hasa kwa watoto walio athirika na magonjwa ya Uti wa mgongo , Homa ya manjano, na surua.. na watoto karibu milioni 3 walipata tiba hizo..

Pia alianzisha kampeni ya upandaji wa miti kitaifa, na takribani miti Milioni kumi ilipandwa nchi nzima..

Pia alianzisha kampeni ya usafi nchini kote, kila mwananchi alipaswa kufanya usafi eneo alipo.. na Sankara mwenyewe alikuwa anashika fagio na kuingia barabarani kufanya usafi.. Hiyo ni kampeni iliyoitwa mfagio wa mwananchi (le balai citoyen).

Aliongeza idadi ya wanawake katika serikali yake, ikiwa ni kampeni yake nchi nzima kupinga tohara kwa wanawake, pia alianzisha kampeni na baadae utaratibu wa kisheria wa kuwataka wasichana waliopata mimba wakiwa mashuleni kuendelea na masomo... pia akaajiri wanawake jeshini, akawapa ajira katika sekta za umma.. ili kupunguza unyanyasaji wa kijinsia na kuleta uwiano na usawa nchini Burkina Fasso.

Pia ndoa za wasichana wadogo na za kulazimishwa haswa za kimila katika maeneo mengi ya Burkina Fasso zikapigwa marufuku..

Thomas Sankara ambaye hakutaka makuu kabisa na wananchi wa Burkina Fasso. Akiwa kama Rais wa nchi, alivaa nguo zilizotengenezwa Burkina Faso badala ya suti kutoka Paris na London.. mara nyingi alionekana akiwa kwenye gwanda la jeshi..

Pia.. Thomas Sankara alifuta matumizi ya magari ya kifahari kwa viongozi na watumishi wote wa umma, yeye kama Rais alikuwa akitumia baiskeli au miguu kwenda kwa wananchi vijijini kuhimiza na kusimamia shughuli za kimaendeleo..

Alijikita sana kwenye kusimamia na kukuza sekta ya afya katika Burkinabe, alihimiza watu kujihusisha na kilimo.. akiwapelekea zana za kilimo na pembejeo bure kwa watu wa vijijini na kugawa ardhi kwa wananchi ili wajihusishe na kilimo..

Kwa muda mfupi sana akiwa kama Rais wa Burikna Fasso, aliweza kuifanya nchi hiyo kuagiza chakula kutoka nchi za nje na kuifanya nchi hiyo kuanza kuuza vyakula vyake nje.. akaanza kuifanya Burkina Fasso kuwa imara kiuchumi.

Sankara aliwahimiza watawala wa Afrika waache kuwaibia wananchi, waache kutegemea sadaka kutoka nje.

Sankara akawaambia madeni ya Afrika hayana uhalali kwa vile yalitokana na mikataba mibovu.

Ndio maana hakuna maendeleo yaliyotokana na mikopo ya kigeni.

Sankara akataka Afrika iache kulipa madeni yasiyolipika.

Mwalimu Nyerere naye wakati huo alisema mtu hawezi kulipa madeni wakati watoto wanakufa njaa.

Thomas Sankara alisema ukitaka kujua maana ya ubeberu angalia sahani yako ya chakula, utaona kila aina ya chakula unachokula kinatoka nje. Ndipo akahimiza Afrika ijitegemee kwa chakula, akisema: "Anayekulisha anakutawala"

Thomas Isidoré Nöel Sankara ni wazi aliwakasirisha sana mabeberu wa kimagharibi, hasa ubeberu wa Kifaransa uliokuwa ukitawala kupitia vibaraka wake wa Afrika kama Rais Felix Houphouet- Boigny wa Ivory Coast...

Chini ya uongozi wake (Thomas Sankara), Burkina Faso ililima chakula chake badala ya kuagiza kutoka nje...

Kwa hatua hiyo, Thomas Sankara akawa amewaudhi wakubwa wa dunia (mabeberu) kwa kukataa kwake mipango ya kurekebisha uchumi ya Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha Duniani (IMF) huku hoja kubwa ya sankara ikiwa ni kwamba, mipango hiyo ni ya kinyonyaji.

Thomas Sankara aligawa ardhi kwa wakulima wadogo baada ya kuchukua kutoka kwa wawekezaji wa nje ambao walikuwa wameipora baada ya kupewa na uongozi uliopita..

Katika huduma za jamii alileta mabadiliko makubwa katika huduma za elimu, afya, maji na kuboresha miundombinu ya barabara kuunganisha sehemu mbalimbali za nchi hiyo.

Sankara katika kuhakikisha kuwa rasilimali za nchi zinahudumia wanachi wa kawaida, Sankara alipambana na rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma, huku akimtaka kila mwananchi kujituma kulijenga taifa.

Thomas Sankara alikuwa mtu anayechukia rushwa na ufisadi, uvivu, uzembe, dhuluma na unyonyaji wa wananchi na rasilimali zao. Alitaka kuona watu wake wakifaidika kwa rasilimali za nchi yake.

Huyu ndiye Thomas Sankara ambaye alipunguza mshahara wake hadi dola 450 kwa mwezi, ambaye alitembea kwa baskeli katika mitaa ya Ouagadougu bila ya kulindwa. Alipoulizwa kwanini hana walinzi alisema wananchi ndio walinzi wake, hivyo hahitaji kuambatana na wanajeshi wenye bunduki.

Washauri wake mara kwa mara walimshawishi aachane na matumizi ya baisikeli.

Akaamua kutumia gari lenye bei ya chini (Renault 5) badala ya msururu wa mashangingi kama tuonavyo leo katika Afrika...

Hata hivyo alibaki na baiskeli yake mpaka alipokutwa na mauti, na akaunti yake ya benki ilikutwa na akiba ya dola 400 ambayo ni sawa na Tsh 850, 550/= (laki nane elfu hamsini na tano namia tano hamsini), kwa sasa, badala ya mabilioni mengi kama wanayoficha huko Uswisi watawala wetu leo...

Kumbuka, Thomas Sankara amedumu kwenye uongozi kwa kipindi cha miaka 4 pekee kabla ya mapinduzi yaliyoongozwa na Rafiki yake kipenzi... Blaise Compaore.. ambayo yaliondoka ba uhai wake, lakini kwa kipindi hiko cha miaka 4 akihudumu kama Rais, alitengeneza mageuzi makubwa sana..

Ndoto kubwa ya kila siku ya Thomas Sankara, ilikuwa ni kuifanya Burkinafasso kuwa moja kati ya mataifa makubwa Afrika kiuchumi..

Thomas Sankara alikataa hata picha yake (yeye kama Rais) kutundikwa katika majengo, na taasisi za serikali.. alisema hataki kutukuzwa..

Sankara alikuwa akipokea mshahara wa dola 450 kwa mwezi, mshahara mdogo kuliko viongozi wote barani Afrika kwa wakati huo..

Huyu ndiye Thomas Isidore Noël Sankara anayejulikana kama Ernesto Che Guevara wa bara la Afrika (alikuwa akivaa mavazi kama Che Guevara, mwenendo, matendo na malengo yake yalifanana na Ernesto Che Guevara, pia walikuwa marafiki wakubwa).., aliyeiongoza nchi kwa muda wa miaka minne kabla ya kuuliwa na maadui wa mapinduzi wakiongozwa na kapteni Blaise Compaoré Aliuliwa nyakati za usiku na mara moja akazikwa kwa haraka. Ernesto Che Guevara naye alikuwa mwanamapinduzi wa Marekani Kusini aliyeuliwa na majasusi wa Marekani (CIA) na kisha kuzikwa kisirisiri.

Thomas Sankara aliyekuwa muumini wa fikra za kupigania Umoja wa Afrika au Pan Africanist mara nyingi alionekana kutopendwa na mataifa ya magharibi kutokana na fikra zake za kupinga dhuluma za wakoloni kunyonya watu wanyonge.

Mwaka 1985, Thomas Sankara alikaririwa akisema kuhusu falsafa yake kisiasa iliyokuwa maarufu, ilikuwa ikisema;

‘you cannot carry out fundamental change without a certain amount of madness’, yaani kwa tafsiri isiyo rasmi, hauwezi kuleta mageuzi ya msingi bila kuwa na kiasi fulani cha ukichaa... ndiyo maana mabeberu walieneza propaganda kwamba Sankara ni kichaa anayeingoza Burkina Fasso..

Pamoja na yote na mengi mazuri.., wapinzani ndani na nje ya nchi ya Burkinafasso, walisikika wakimlaumu Sankara kwa kupiga marufuku vyama huru vya wafanyakazi na vyama vya siasa.

Pia Sankara alianzisha Mahakama za wananchi ‘people’s revoluntionary tribunals’ ambazo zililenga kutoa hukumu kwa wapinga mapinduzi, wafanyakazi wazembe... Jambo ambalo lilileta hamasa ya watumishi wa umma kufanya kazi kwa nguvu wakiogopa hukumu..

Ila hatua hiyo ilipigwa vita saba na wapinzani wake..

Kumbukumbu kubwa ya wananchi wa Burkinabe (Burkina fasso), kuhusu Kapteni Thomas Sankara, ilikuwa ni wiki moja kabla ya kuuwawa kwake alitabiri, na alikaririwa akisema:

“Wanamapinduzi wanaweza kuuliwa, lakini fikra za kimapinduzi zitaendelea kuishi daima”

Hapo alikuwa akinukuu maneno ya Mwanamapinduzi maarufu Duniani, Ernesto Che Guevara ambaye aliwahi kusema..

“Revolutionaries and individuals can be murdered, but ideas never die.”

Thomas Sankara alifariki Oktoba 15 mwaka 1987 baada ya kupinduliwa na Blaise Compaore kuchukuwa utawala nchini Burkina Faso kwa muda wa miaka 27..

Inafahamika kwamba, kwa mara ya kwanza mwaka 1997, familia ya marehemu Thomas Isodoré Noël Sankara, ilifikisha ombi la kutaka mwili wa Sankara ufukuliwe ili ufanyiwe uchunguzi..

Taarifa zinafahamisha kuwa serikali ya Blaise Compaore ilitupilia mbali ombi kutoka familia ya Thomas Sankara la kutaka kufanyike uchunguzi kuhusu kifo cha Sankara.

Kwa mujibu ya ripoti ya kifo cha Thomas Sankara, serikali ilifahamaisha kuwa Thomas Sankara alifariki kifo cha kawaida.

Familia ilitaka kufahamu kama ni kweli katika kaburi hilo ndipo mwili wa Thomas Sankara ulipohifadhiwa..

Blaise Compaoré ni nani??

Compaoré alizaliwa katika mji wa Ziniaré, uliopo umbali wa kilomita 43 kutoka Jiji la Ouagadougou, ambao ndiyo mji mkuu wa Burkina Faso, alipitia mafunzo ya kijeshi akiwa amefikia cheo cha kapteni.

Ni mwanzilishi wa chama chake cha Congress for Democracy and Progress, akihusika katika mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 1983 na yale ya mwaka 1987. Miaka mitatu baada ya kufanya mapinduzi na kuingia Ikulu, alichaguliwa rasmi Rais wa Burkina Faso kwa kura mwaka 1991, katika uchaguzi uliosusiwa na upinzani na kisha alichaguliwa tena kwa njia hiyo ya kura katika chaguzi za mwaka 1998, 2005 na 2010.

Alikuwa gwiji wa kushiriki mapinduzi ya kung’oa na kupachika watu madarakani na katika kuthibitisha hilo, akiwa na umri wa miaka 33, Blaise Compaoré aliratibu mapinduzi ya kijeshi yaliyomng’oa madarakani Meja Jean-Baptiste Ouedraogo nchini Liberia, hiyo ilikuwa Agosti 4 mwaka 1983. Wakati huo Burkina Faso ilikuwa ikiitwa Upper Volta.

Mapinduzi hayo ya kijeshi yaliungwa mkono na Libya chini ya Muammar Gaddafi rafiki wa Compaore, kwa wakati huo, Libya ikiwa katika msuguano na Ufaransa kuhusu Chad.

Washirika wengine wa mapinduzi hayo ya Agosti 4, mwaka 1983 ni Kapteni Henri Zongo, Meja Jean-Baptiste Boukary Lingani na Kapteni Thomas Sankara— aliyetangazwa Rais kuwa katika mapinduzi hayo ya kijeshi.

Compaoré wakati huo alipofanya tena mapinduzi ya kijeshi mwaka 1987, alizungumzia mauaji ya rafiki yake wa jeshini zamani (Rais Sankara) ambaye alimsaidia kuingia Ikulu (mwaka 1983) akisema ilikuwa ajali tu.

Hata hivyo licha ya kuongoza mapinduzi ambayo si tu yalimng’oa rafiki yake huyo madarakani bali hata kumuua, licha ya kukaa kwake Ikulu kwa miaka 27, Compaore hakuwahi kuchunguza sababu za mauaji hayo ya Sankara, jambo linalozua hisia kwamba alishiriki kuhakikisha Sankara anauawa ili mapinduzi yatimie bila

Katika utawala wa rafiki yake (Sankara), ulioanza mwaka 1983 hadi mwaka 1987, Compaoré aliwahi kuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi, akiwa amepata kutumikia cheo cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Naibu Waziri wa Sheria..

BLAISE Compaoré aliyeitawala Burkina Faso kwa muda wa miaka 27 alilazimishwa na wananchi kuikimbia nchi hiyo tarehe 31-10-2014.. Amekimbilia Ivory Coast (Cote d’Ivoire) ambako anahifadhiwa na rafiki yake Rais Alassane Ouattara...

Hii ni baada ya wananchi wenye hasira walipojitokeza kwa maelfu mitaani katika mji mkuu wa Ouagadougou.

Tatizo lilianza pale Blaise Compaoré alipotaka kubadili Katiba ili aendelee kutawala. Bunge lilikuwa tayari kutii amri yake. Ndipo wananchi wakalichoma moto jengo la Bunge na ofisi za serikali pamoja na makao makuu ya chama tawala cha CDP (Congress of Democracy and Progress). Baadhi ya nyumba za wabunge waliokuwa mstari wa mbele katika kutetea Compaoré aongezewe muda nazo zilichomwa moto.

Mkuu wa majeshi ya ulinzi nchini Burkina Fasso Honoré Traore akajitangaza kuwa Rais mpya. Wananchi wakamkataa.

Baada ya muda Honoré Traore akapigwa kikumbo na Luteni Kanali Isaac Yacouba Zida akashika madaraka. Wananchi wakaendelea kudai serikali watakayoichagua wenyewe kidemokrasia, wakisema hawakumfurusha Blaise Compaoré ili jeshi lishike hatamu...

Wimbo mkubwa wa wananchi wa Burkinabe ni kwamba... Blaise Compaoré alimuua kipenzi chao.. na hivyo kusaliti mapinduzi ya haki ya awali yaliyoongozwa na Thomas Sankara dhidi ya serikali ya Jean Baptiste Ouedraogo.

Vyombo vya propaganda chini ya serikali ya Blaise Compaore wa kwamba Thomas sankara hakuwa muhimu sana katika uwepo wa taifa hilo,...

Hata mapinduzi ya wananchi wa Burkina Fasso dhidi ya Compare walihamasishwa na kumbukumbu za Kapteni Thomas Sankara. Ingawa watawala wanajaribu kufuta kumbukumbu zake lakini wananchi wa kawaida wangali wanamkumbuka.

Ni vizuri ikumbukwe kuwa hii ni mara ya tisa kwa majeshi kuvamia urais wa Burkina Faso tangu nchi hiyo kupata uhuru wa bendera kutoka Ufaransa mwaka 1960. Ni uhuru wa bendera kwa vile leo nchi hiyo inaendelea kukaliwa na majeshi ya Ufaransa, na utajiri unaporwa na wawekezaji.

Kwa sababu hata mapinduzi ya Blaise Compaore kumuondoa rafiki yake Thomas Sankara yaliongozwa na Compaore akisaidiwa na Ivory Coast, ufaransa na wakafanikiwa kumuua Sankara..

Wanamapinduzi na wana mageuzi wote Duniani, ni watu wanaojulikana kama wapinga ubeberu waziwazi na ndiyo maana wengi wao wamekumbana na ukatili wa mabeberu.

Wako wana mapinduzi na wana mageuzi waliouawa kama akina Thomas Sankara wa Burkina Fasso na Patrice Lumumba wa DR Congo na wengine kutumikia vifungo virefu na vya maisha maisha kama Nelson Mandela.

(Makala hii imeandikwa kwa msaada mkubwa wa mashirika mbalimbali ya habari ya kimataifa).
Pamoja na muogozo kutoka kwa kaka yangu mwanahistoria mahili nchini Martin Maranja Masese,


" Mungu bariki Tanzania Mungu bariki Afrika Mungu bariki kizazi chake"

Ndimi.
Comred Mbwana Allyamtu

+255765026057
+255679555526
mbwanaallyamtu990@gmail. Com
 
Asante mkuu! Nakubari makala zako, Wanaharakati Black Americans wanamkubari Sana huyu Sankala kuliko hata viongozi maarufu Africa, Leo nimejua kwa nini! Endelea kushusha vitu kadri ukipata nafasi!
 
Tujikumbushe kidogo kuhusu Kapteni Thomas Sankara,
Rais wa zamani wa Burkinafaso 1983-1987. Rais kijana kabisa aliyechukua nchi katika umri wa miaka 33 tu katika mapinduzi ya mwaka ule wa 1983 katika nchi ile ya koloni la zamani la Wafaransa, zamani ikijulikana kama Volta ya Juu! Upper Volta.

Sankara alikuwa na baiskeli moja na gari moja tu. Alipinduliwa na kuuawa jioni ya tarehe 15/10/1987. Aliyempindua alikuwa ni rafiki yake wa karibu sana. Kapteni Blaise Compaore. (your worst enemy could be your best friend, and your best friend your worst enemy) alipata kuimba Mwanamuziki Robert Nesta Marley.

Mara kadhaa watu wa usalama walimtahadharisha Sankara kuwa rafiki yake huyo anapanga mipango na kula njama za kutaka kumuua. Yeye alikuwa anawajibu kuwa kama Compaore anataka kuniua basi hawezi kushindwa kitu maana anajua kila kitu kunihusu mimi!
 
Huyo jamaa alikuwa dhaifu wa fikra kwahiyo mpk anaambiwa hakujua cha kufanya! ukiwa kama rais unashindwa kumdhibiti adui yako vipi adui wa nchi..? hatari hii
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom