Thomas Nyimbo aahidi kuijenga CHADEMA; apongezwa!

SG8

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
3,955
2,125
Leo asubuhi nimeongea na mmoja wa wasaidizi wa Mh. Nyimbo aliyekuwa mgombea ubunge wa Njombe magharibi kwa tiketi ya CDM na kuhujumiwa na CCM kwa maelekezo ya Anna Makinda na Pindi Chana (Viti maalum Njombe CCM) kuwa pamoja na dhamira ya kupinga matokeo mahakamani. Mh Nyimbo ameamua kufanya yafutayo.
1. kugharimia ufunguzi wa matawi ya CDM vijiji vyote 104 vya jimbo lake ndani ya wiki mbili toka sasa. Gharama kwa kiasi kikubwa atchangia yeye kwa kuwashirikisha wananchi wake.
2. Ameweka makadirio ya kuandikisha wanachama wasiopungua 5000 kwa kipindi hicho cha wiki 2 na kuunda safu imara ya uongozi toka msingi mpaka jimbo/Wilaya
NB.Mheshimiwa anastahili pongezi kwa sababu kwa miak yake ambayo ni zaid ya 60 ni wazi anatuandalia sisi vijana mazingira mazuri ya kupata fursa za kushiriki siasa sasa na baadae.
WITO: Wadau hasa chadema Makao makuu muwezesheni kwa vfaa kama vile kadi, katiba na bendera kwa watu wenye moyo kama ni wachache katika jamii. Aidha Cahdema mkoa wa Iringa kupitia kwa mbinge wa viti maalum na Mjumbe wa kamati kuu Bi Chiku Abwao mpeni tafum mzee huyu ili mwaka 2015 tuisambaratishe CCM Mkoa wa Iringa na Njombe
 
Nimeipenda hii, Nyimbo ni mtu makini akitumiwa vizuri anaweza kuikuza CHADEMA Iringa. Nitamushauri mbuge wangu Machemli na madiwani lukuki kufanya hivyo ili kuweka ngome imara ukerewe.
 
Jambo la kuigwa na wengi, huyo ni mzalendo, anapenda watu wake na nchi yake....kudhulumiwa hakujamkatisha tamaa. Watu kama hao ndio viogozi tunaowataka....chonde chonde vijana role model huyo....Mr. Nyimbo we are proud of you
 
hii ni akili ya mtu mwenye kujitambua, na si wale wakipewa tukamati huko bungeni basi
huanza kuvihujumu vyama baadae
 
Hii nimeipenda saaaaana. Mola akubariki Mh. Nyimbo and this is what we call legacy. Natamani ifanyike hivyo kwa mikoa yote yenye wabunge wa CDM na huu ni mfano wa mikakati tumekuwa tukihimiza wanaJF. 2015 yaweza kuonekana ni mbali lakini kufanya maandalizi ya mapema ndo jawabu. Wanasema "Jasho jingi wakati wa maandalizi, damu kidogo wakati wa Vita"
 
Kuna jambo muhimu mwandishi Lula waNzali amenikumbusha kwenye toleo la leo la Raia Mwema, ni vyema kufurahia matukio mazuri(kutangaza mipango mizuri ya kujenga chama kama alivyofanya Nyimbo) lakini ni bora maradufu kufurahia matokeo yanayofuatia baada ya tukio (kama kweli ametimiza mpango huo, wananchi wakatoa ushirikiano,kusogea karibu na wananchi kuchochea maendeleo,chama kuimarika,n.k)
 
Hawa ndio wana mageuzi wanatakiwa kwa sasa -sio viongozi tuu leteni contact zake tumpe shavu mwana mageuzi huyo, tunao uwezo kuchangia mambo haya zaidi ya harusi
 
Hii ndo njia ya kukataa matokeo, maana baada ya hiyo miaka mitano anakuwa na uhakika wa kubadili matokeo kama siyo muda mfupi baada ya nahakama kuridhia. Big Up Nyimbo!
 
Back
Top Bottom